KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Mama Vanessa Sehemu Ya Sita (6)

Katika kitu ambacho Lucas huwa kinamnyima raha ni kuona mwanamke akilia mbele yake. Yaani yeye mwanamke akijilIza basi huwa anamwamini kupita kiasi. Alimbembeleza mpaka Mama Vanesa akanyamaza. Kwikwi zilimkaba sana na alikuwa akiona kabisa kijana huyo ameonewa. Mwanzo hakuwa na ushahidi wa moja kwa moja lakini zile picha zinazomuonesha mme wake akiwa na mke wa Lucas zilimuuma kupita maelezo.

“Kwa hiyo haya yote yametokea nini sasa kifanyike” Lucas alihoji mara baada ya mama huyo kubembelezwa na kurudi katika hali yake ya kawaida.

“Ndo maana nimekuita hapa ili tupange mambo na ikibidi tumkomeshe”

“Wewe unataka tumfanyeje hili hali yeye ni boss mwenye fedha. Nikikuruka na kujifanya mjuaji sana ndo nafutwa kazi kabisa.”

“Siku zote usikubali kupoteza haki yako kisa kuogopa kufukuzwa kazi. Usikubali kunyang’anywa mke au hata uhuru wako kisa pesa. Nakuambia tukiungana mimi na wewe tutafanikiwa kwa hili. Dawa ya moto ni moto na hivi tunaushahidi, hiyo kazi huwezi kufukuzwa. Mimi ndo Emmy hilo jina la mama Vanessa ni la heshima tu.

“Sawa Emmy ingawa nitapenda kukuendelea kukita mama Vanesa ni jina zuri linatamika vizuri. Ingawa mtu anavuta taswira laba ni mama kweli”.

“Kila mwanamke ni mama maana hata kama bado hajazaa ipo siku atakuja kuzaaa”. Sio mbaya ukiiita hivyo maana hata Vanesa mwenyeewe anajua kuwa mimi ndo mama yake. Alifafanua mama huyo.

“Sawa lakini bado sijajua mpango mkakati ni upi?

“Ni mdogo tu ukitendwa tenda, ukipendwa pendwa”.

Maneno hayo yalikuwa bado yanamuacha njiapanda Lucas Manyama hakujua mwanamke huyo alikuwa akitaka nini hasa kutoka kwake. Maneno hayo kwake yalikuwa yakiahshiria kuwa mama huyo alikuwa akitaka alipe kisasi kwa wao kuwa wapenzi. Kuna vitu vilikuwa vikimtatiza kwanza kwa nini mama huyo alichagua njia hiyo ya kulipa kisasi kwa nini wasipeleke ushahidi a idara ya kazi na kueleza kuwa alikuwa akisimamishwa kazi kwa sababu ya hujuma za boss wake ambaye alitumia uboss kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe. Hili jambo lilimuumiza sana hasa akikumbuka ni mbali sana alipotoka. Alifikiria jinsi alivyomsomesha mke wake tena kwa tabu mpaka akafanikiwa kupata elimu na baadaye kazi. Alifikiria tukio la yeye kusimamishwa kazi na kuona kabisa haikuwa sawa. Wakati Lucas akiwaza na kuwazua mara simu ya mama Vanesaa ikaita.

Mama Vanesaa aliangalia na kusita kupokea maaana aliyekuwa akipiga ni baba Vanessa. Simu haikukukoma maana ilivyokata ikapigwa tena na safari hii mama Vanesaa alipokea.

“Upo wapi mke wangu maana ndo nimerudi kutoka Mwanza kwenye semina nimefika nyumbani sijakukuta?”

“Nimetoka kidogo mme wangu na si muda mrefu nitakuwa hapo kuna vitu tu nilienda kuvinunua kwa ajili ya safari yangu ya kesho.”

“Sawa huwai kurudi basi maana nimekumisss sana na nimekuletea zawadi nzuri mke wangu..

“Usijali honey nakuja”.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Lucas Manyama alikuwa ametega sikio na kusikiliza kila kitu kilichokua kikzungumzwa. Aliisikia vyema sauti ya boss wake. Roho ilimuuma na hakutarajia kwa picha zile zikimuonesha mke wake na boss wake wamekumbtaina wakicheza musiki Mama Vanesa angeweza toa majbu ya kukera yenye hasira. Na mama Vanesa hasingeongea hivyo kama vile hakuna kitu kibaya kilichotokea. Alitarajia mwanamke huyo atamtukana mwenyewe.

“Samahani boss wako amepiga na usiumie kwa mimi kuongea naye vizuri. Cha msingi tambua namtafutia dawa ya kumkomesha na mimi siku zote maishani mwanangu huwa sipendi kukurupuka na iktokea tatizo huwa natafuta njia ambayo itamuumiza muhusika. Kwa hiyo mkakati upo hivi mimi naenda Dar nitakaa kwa muda wa wiki moja kisha nitardi. Baada ya hapo tutakutana lakini nakuomba kwa wakati huu tuwe makini sana usikurupuke katika maumivu tufanya kama hakuna kibaya cha kuumiza moyo kilichotokea. Mama Vanesaa baada ya kusema hayo alifungua pochi yake na kutoa burungutu la pesa na kumkabidhi. Alitabasamu na kumuaga. Lucas alitamani amwambie hasiondoke lakini tayari ilikuwa ni hatari kama mme wake alishakuwa mjini. Mme wake licha ya kuwa boss katika benk ambayo alikuwa akifanya Lucas pia alikuwa ni mfanyabiashara hapo Musoma na nadiriki kusema alikuwa tajiri. Mama Vanesaa kazi yake kubwa ilikuwa kusimamania biashara hizo. Kwa hiyo ni mwanamke ambaye alikuwa akikutana na pesa karibu kila siku.

Kwa Lucas kupewa fedha ilikuwa zaidi ya ushindi kwa sababu alikuwa hana pesa kabisa. Yaani mfukoni alikuwa amebakiza shilingi elfu 10 na tayari account yake ya benk ilikuwa ikisoma ziro.Baada ya mama Vanesa kuondoka yeye alihesabu zile pesa na kukuta zilikuw laki moja. Alitabasamu na kusema asante Mungu kwa kuendelea kumsaidia kupitia watu.Aliamua kuondoka eno hilo maana anajijua kabisa akikaa baaa hachelewi kuanza kutamani kunywa pombe. Alimwita muhudu akamlipa na huyo akaeleka zake nyumbani kwake alipopangisha mitaa ya Iringo. Alifika akawasha Tv na kuendelea kuangali movie. Lengo lilikuwa ni kupoteza muda na mawazo aliyokuwa nayo. Alimwanza mama Vanesa jinsi alivyoumbika akashindwa kuelewa kwa nini boss wake hatulii wakati ana mke mzuri.

Siku ikawa imeisha hivyo na usiku mama Vanesaa alimtumia sms akimtakia usiku mwema. Usiku pia alimkumbuka Juliaana binti ambaye alimpa mapenzi usiku wa jana na kumfanya hasahu shida kwa muda. Alifikiria mengi na kujikuta akinyanyua simu na kumpigia rafiki yake Kimaro. Alikumbuka fadhila ambazo alimtendea na alimweleza kilichoendelea baada ya yeye kufika Musoma.

“Hapo mbaba ndo muda wa kulipa kisasi boss si kakupokonya mke wako na wewe fanya kweli. Tena kwa jinsi ulivyonielezea ni kwamba huyo mwanamke anataka duduuu.

Kimaro alabaki akiangua tu kicheko na kumwambia yeye anachohofia ni kushindana na watu wenye pesa maana kazi atakosa na gerzani ataingia.

“Kuhusu kazi usiogope mbaba nitakutafutia hata sehemu ya kujishikiza ila wewe kula huyo sijui mama Vanessa. Na ukifanikiwa nipigie picha mkiwa naye chumbani mimi nitajua cha kufanya. Nitalipa ghali ….aaaaaaaaaaaaaah. Hapa ni mjini hatuwezi sumbuliwa na mtu sijui kisa ana vichenji.”

Wakati wakiendelea kuongea na kupeana mbinu mbaya za kupambana na matatizo yaliyotokea simu ya Lucas ilikuwa ikiita. Alivyokata tu ikaita tena na kuangalia alikuwa Mishel mke wake wa ndoa.



Yaani alijikuta akianza kutetemeka bila yeye kupenda. Hukujua kwa nini mkewe alikuwa akimpigia wakati huo. Alishindwa kabisa kuamini kama mkewe ambaye alikuwa hapatikani takribani wiki mbili sasa ndo huyo alikuwa akimtafuta. Alisita kuipokea na aliiacha maana tayari hasira zilikuwa zimempanda kupita kiasi.Baada ya yeye kukataa kupokea simu kwa hiyari yake kuna sms iliingia.

“Kwa mjinga huenda kicheko kwa mwelevu huenda kilio.Nashukuru kwa kutopokea simu yangu. Ila tambua mimi ni mke wako wa ndoa na hakuna cha kututenganisha.”

Lucas alirudia kuisoma ile SMS na kujikuta akizidi kuchanganyikiwa maana maisha yalikuwa yakimchanganya kwa kiasi kikumbwa.Alitamani hata kulia lakini alilia machozi yaliyoishia ndani ya moyo wake. Kijasho chembamba kilimtoka na kujikuta akiwasha feni ili hewa iiingie. Bado hakupata hafueni na akaamua kutoka nje kabisa. Alikuwa kifua wazi huku akitamani hata kunywa pombe. Alikaa hapo kwenye kibaraza cha nyumba. Mawazo ya uchngu yalizidi kuunyanyasa ubongo wake. Moyo wake ulizidi kunyong’onyea kwa hasira ya mambo ambayo yalikuwa yakiendelea. Alitamani ardhi ifunguke na yeye aingie ndani. Maisha kwake yalikuwa ni mtihani mkumbwa sana ambao kwa kweli uliitaji nguvu za ziada kukabialiana nao. Nyumba aliyokuwa akiishi ni nyumba ambayo ilikuwa ikiongozana na Lodge. Kwa hiyo wakati akiwaza na kuwazua macho yake aliyaelekeza moja kwa moja kwenye lodge hiyo. Aliona gari likiingia eneo hilo na ni kama vile alikuwa akilitambua gari hilo ni la boss wake. Alishangaa kwa sababu walivyoachana na mama Vannesa boss huyo alieleza kuwa amefika nyumbani kutoka Mwanza kwenye semina.

Ilimlazimu kusimama maana alihisi kama amefananisha hilo gari. Kwa kuwa yeye alikuwa gizani hakuwa na hofu sana maana mtu alaiye kwenye mwanaga ilikuwa ni ngumu sana kumwona. Alishangaa kuona boss wake huyo akishuka na mwanamke mwingine ambaye na yeye hakuhitaji mwanga wa mchana kujua kama alikuwa ni mrembo. Alitamani hata kuwapiga picha lakini wahusika hao waliingia kwa haraka sana. Wazo lilomjia ni kumpigia simu mama Vanesa na kumuuliza kama mumewe alikuwepo nyumbani au la. Aliingia ndani na kuchukua simu yake ambayo alikuwa ameiweka chaji. Alipiga namba za mama Vannesa lakini kwa bahati mbaya simu hiyo haikupokelewa. Haikuwa usiku sana lakini alishindwa kupiga tena kwa imani kuwa huenda ni usiku na yupo na mumewe. Aliamua kuamini kuwa alichokiona haikikuwa sahihi na zaidi ilikuwa ni hisia zake tu. Alitamani kwenda mpaka kwenye ile lodge lakini alikuwa na hofu huenda akaanza kuulizwa maswali mengi na mlinzi

Kwa kuwa ndani kulikuwa na joto alirudi zake nje na kuendelea kutafakari mustakabali wa maisha yake. Roho iliendelea kupwitapwita kwa kuuma na kutamani kama angekuwa na nguvu ya kupambana na huyo boss. Pamoja kuwa wana pesa sitokubali kwa njia yoyote ile nifukuzwe kazi. “Afanye yote lakini sitokubali kwa maana kama anatembea na mke wangu na mimi nitatembea na mke wake. Sio mke wake tu hata mtoto wake. Nipo tayari hata kufa lakini sio kudhalilishwa kwa kiasi hiki kikumbwa. Mke anauma sana na sijui kwa nini nimeweza kuvumilia kwa kipindi chote hicho. Nitaenda hata kwa mganga kumloga. Maisha ndo haya haya kwa kweli sipo tayari kwa namna yoyote ile kudhalilika kisa madaraka au pesa.” Lucas aliyawaza hayo kisha akakunja uso wake kwa nguvu. Alikunja pia ngumi yake kwa nguvu akaizungusha kwenye uso na kuing’ata.

Usiku uliendelea kuwa mgumu sana kwa bwana Lucas Manyama. Kwa sasa alikuwa akisubiri kwa hamu kumbwa hiyo kamati ya nidhamau na maadili ya kazini kwao. Maisha yaliendelea huku akimwomba mwenye nyumba amvumilie kwa mwezi huo kwani mambo hayakai sawa kwa upande wake. Mwenye nyumba alimweleza bayana kuwa hatoweza kumvumilia zaidi ya mwezi hivyo kama hawezi kulipa kodi basi atafute kitu kingine cha kufanya. Zilikuwa ni kauli za kuumiza lakini alijikaza kama mwanamume na kuamini hizo ni changamoo za maisha na huwa zinakuja kwa nayakati na kuondoka na pengine kusaulika. Siku zilizidi kuyoyoma na hatimaye siku ya kusikiliza shitaka lake ilifika akaitwa. Alifika na kusikilizwa na inaonekana boss alijipanga sana maana utetezi wake haukufua dafu mbele ya kamati hiyo. Maamuzi yakatoka kuwa ataendelea kusimamishwa kazi mpaka hapo atakapo lipa deni la million 5 ambalo yeye amesababishia kampuni hiyo. Alitamani kutoa ya moyoni mwake kuwa boss alikuwa na uhusiano na mfanyakazi mpya ambaye na yeye alianza kuwa uhusiano naye lakini roho moja ilimwambia inampasa kukaa kimya maana anaweza kuharibu kabisa.

Lucas alijijengea katika maisha kuwa kamwe hasifanye maamuzi akiwa na hasira au akiwa hana mtu wa kumsapoti. Alitamani sana kuelezaa kamati hiyo ya maadili ya mabaya yote ambayo amefanyiwa na boss. Alitamani kuwaambia kuwa mfanyakazi mpya aliyekuja ndio chanzo cha ugomvi. Alitamani kueleza kuwa boss amemwaribia maisha kwa kumchukua boss wake. Hasira zilimpanda sana na bila kutarajia aliamua kuondoka hili hali kikao kilikuwa bado kinaendelea.

“Ndugu zangu kwa sasa nina hasira sana ambazo zimechanganyika na uchungu wa kile ambacho kilikuwa kikitokea.. Nina mengi sana ya kuwaeleza kwa kuwa mmeshindwa kunisikiliza naomba nitawakilisha ushahidi wangu wa picha na vitu vingine kuonesha ni jinsi gani nimeonewa sana na nimedhulumiwa haki zangu za msingi. Nimekuwa nikipitia kwenye kipidi kigumu sana na naamini kama kamati ya ndani ya maadili ikishindwa kunitetea basi nitaenda idara ya kazi” Lucas aliyasema hayo kisha akapiga ngumi kweye meza na kuanza kuondoka zake. Hakika alionesha kufadhaishwa sana na kilichojadiliwa hapo na kumfanya aonekane ana mengi sana moyoni lakini hana imani na sehemu hiyo. Alishindwa kuyawasilisha kwa kukosa imani na kamati ya maadili. Kamati ambayo ilikuwa imetengenezwa na boss kamati ambayo ipo radhi kupindisha ukweli kamati ambayo ipo tayari kwa gharama yoyote kulinda maslai ya kampuni.

Lucas Manyama aliondoka na kurudi nyumbani. Alikuwa ni mtu mwenye hasira sana na alichokifanya ni kununua pombe kali na kunywa. Alikunywa viroba japo huwa hapendi kabisa kunywa. Aliingia ndani na kulala. Alifanikiwa kupata usingizi akalala na alikuja kushtushwa na njaa ambayo ilikuwa ikimkabili. Alijinynyua na kwenda kutafauta kitu cha kula. Alikula na baaada ya hapo alaipata fusa ya kutafakari yote yaliyotokea kwenye kamati ya maadili. Limshukuru Mungu hakuweza kutoa ya moyoni maana anageweza kuchafua hali ya hewa na kufanya hata watu wapigane.Aliwaaambia yaliyojiri na wengi walimshauri kuwa awe mvumilivu kwa kipindi hiki na pia awaambie hiyo kamati yao impe kwa maandishi kila walichokijadili na maamuzi yake ili wasije mgeuka kipindi atakapoeenda idara ya kazi. Alikubali kufuata ushauri huo na akaseam kesho ataenda kazini. Baada ya kuongea na washauri wake kuna namba ngeni iliyokuwa ikimpigia , aliamua kuipokea.

“Helow mpenzi nimekumiss sana na siamini kama kweli umefika Musoma na hujataka kunitafuta.” Lucas alitega sikio kwa umakini sana na kufanikiwa kugundua kuwa alikuwa ni Juliana.

“Samahani sana mwenzio sipo sawa kwa kweli yaani maisha yananichanganya. Sio mimi ni maisha tu ndo yamenifikisha hapa.” Lucas aliongea kwa sauti ya upole.



“Usijali mpenzi najua unaweza kuchanganyikiwa kwa majanga yaliyokukuta mke anauma sana na pengine kuliko kitu kingine chochote. Cha msingi kwa sasa usipende kukaa mwenyewe kuwa na marafiki watakusaidia sana”



“Asante sana Juliana kwa kuendelea kuwa karibu nami.Naamini pia katika ushauri wako, Wewe ni mwanamke mwenye akili ubarikiwe kwa ukarimu na ushauri.

“Mungu yu mwema naomba niwe karibu yako nahitaji kukupa faraja kwa muda wowote. Naamini kuwa naiweza hiyo kazi naomba nikupe faraja kwa kiwango cha kukufanya usahau shida kwa muda.

“Nashukuru sana Juliana kazi hiyo nimeshakupa na endelea kuifanya kwa umakini zaidi.”

Waliongea mengi na Lucas alimwaidi mrembo huyo kuwa wikiendi Mungu ikijalia ataenda tena Mwanza ili waweze kuwa pamoja. Jambo ambalo Lucas hakulijua ni kwamba Juliana alikuwa amepewa kazi hiyo ya kumpa faraja akishirikiana na Julieth kwa shinikizo la mpenzi wake Kimaro. Kulikuwa na ukaribu mkumbwa uliofanywa ili angalau Lucas hasione kuwa dunia ilikuwa imemtenga. Lucas akashindwa kuelewa kwa nini kipindi hicho wanawake walikuwa wakiwa karibu yake sana. Aliona kama ni bahati na anaweza hata kufanya maamuzi magumu ya kuwa na wasichana wengine wengi maradi kupunguza machungu ya kupokonywa mke wake. Pamoja kuwa alikuwa akitaka kufuata taratibu za sheria za kazi bado alikuwa akiamini na akatamani kuivuruga familia ya boss wake. Alianza kuifuatilia familia hiyo kuwa na habari za ukaribu. Kwanza aliambiwa boss huyo alikuwa na mtoto wa kike ambaye alikuwa mkumbwa na alikuwa akisoma chuo kikuu cha Dar es salaam.


ITAENDELEA TENA KESHO
Powered by Blogger.