KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Mama vannessa sehemu ya kumi na tisa (19)

Hadithi nzuri ya kusimumua ya mapenzi ya mama vannessa
Aliiangalia ile simu kwa hasira sana na aliinyanyua ili aweze kuipokea. Kwa bahati mbaya nguvu ziilimwishia na kuhisi kabisa anaweza kupewa habari mbaya ambazo zitamchanganya kabisa siku hiyo. Lucas aliona kabisa hasira na kinyongo alichokuwa nacho juu ya Mishel. Kuna sms iliingia.

“Najua ukiona simu yangu unaumia sana lakini jua maisha ni mau kuna kipindi huwa yananyauka na kuna kipindi huwa yanachanua.Nimekukumbuka mume wangu.”

“Huyu mwanamke sijui ni jinni?” Lucas aliwaza.Alitupa simu pembeni na kushika kichwa. Aliwaza sana ni nini kinachomsibu huyo mwanamke. Alianza kurudisha kumbukumbu kipindi cha nyuma. Taswira ya picha za kumbukumbu za wakati uliopita juu ya mwanamke huyo zilimjia. Alikumbuka siku ya kwanza kabisa kukutana na mwanamke huyo. Ilikuwa ni zaidi ya miaka saba imepita. Kipindi hicho huyo binti alikuwa mdogo sana kwanza ndo alikuwa form three.


ITAENDELEA
Powered by Blogger.