KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Mama vannessa sehemu ya Ishirini (20)

Hadithi nzuri ya kusimumua ya mapenzi ya mama vannessa

Mvua ilikuwa inaonyesha na yeye aliamua kujikinga na mvua hiyo kwa kuingia kwenye moja ya kibaraza cha duka. Ingawa alikuwa na mvua lakini hali ya hewa ilikuwa tete. Mvua iliyoambatana na radi ilikuwa ikipiga hivyo pamoja na mwamvuli aliokuwa nao bado alioofia usalama wake maana anageweza kujitafutia matataizo hasa ukizingatia kuwa mwamvuli aliokuwa amumbeeba ulikuwa na rangi yenkundu na wakati huo alikuwa amejijengea imani kuwa radi inafuata rangi nyekundu. Katika kibaraza hicho alichojibanza ili kusubiri makali ya mvua kulikuwa na watu wengi sana na jicho lake lilikwama kwa binti ambaye kwa wakati huo alishindwa kuelewa alikuwa ni mtoto au la. Binti alikuwa amekaa kwenye benchi na uzuri wa sura na umbo lake ndo ulimfanya jicho la lake kukataa kubanduka kabisa. Aliangalia miguu kama haitoshi akaangalia sehemu za kifuani na mara kadhaa macho yao yalikutana.

Ilikuwa ni kijijni kwao hivyo hakujua hata binti huyo alikuwa aitoka boma la nani. Kwanza yeye hakuwahi kuishi kijijini kwa muda mrefu zaidi alikuwa akija kusalimia babu na bibi kipindi cha sikukuu.

Mvua ilipungua na binti wa watu ambaye hakuwa hata na mwamvuli aliamua kujitosa hivyo hivyo ili aweze kuwahi nyumbani.

“Wewe Mishel mvua bado haijaisha vizuri angali isije ikakuletea shida” alisikika dada alaiyekuwa akiuza duka.

“Wacha niwahi mama atanigombeza huwa hapendi giza linikute nikiwa nje ya boma”Alijibu binti huyo kwa sauti laini sauti ambayo ilikuwa ikisisimua masikio ya Lucas. Kipindi hicho Lucas alikuwa ndo kwanza alikuwa yupo form six. Miguu yake ilishindwa kuumlia kuona msichana huyo aliyetokea kumvutia ghafla akiwa anatoweka ghafla kwenye upeo wa macho yake. Bila kutegemea alijikuta akinyanyua miguu na kujaribu kumfuatilia. “Mishel” aliita Lucas na kufanya binti huyo kugeuka kwa mshangaoa. Lucas hakuongea neno linguine zaidi ya kufunika na mwamvuli na kumfanya hasinyeshewe na mvua ambayo ilikuwa imechanganya ghafla.

“Umejuaje jina langu” Mishel alihoji huku kimoyo myo akishukuru kwa kupata msaada huo.

“Usijali mimi ni Lucas ni mjukuu wa mzee Manyama.

INAENDELEAAA.
Powered by Blogger.