KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Utamu Wa Shemeji Flora Sehemu Ya Kumi na Saba (17)

SIMULIZI NZURI YA KUSISIMUA
"Rozi naomba unisikilize kwa umakini kesho asubuhi ilikuwa ndio uondoke humu ndani ya hii nyumba uende kwenu Iringa, lakini nimeghaili utaondoka mwisho wa mwezi huu" alivunja ukimya Flora na kusema hivyo. "Kwanini sasa nisiondoke hiyo kesho, na wakati uliniambia nijiandae na safari ya kurudi kijijini kwetu na mimi nilishajiandaa?" Rozi aliuliza. "Nimeona nikikurudisha kwenu kwa sasa utapata taabu sana" alisema Flora kwa dharau huku akicheka.

"Ni bora nikapate hiyo tabu lakini nipo nyumbani kwetu naishi kwa Amani" alisema Rozi. Flora akacheka sana halafu akauliza: "Kwani hapa auishi kwa Amani au ni mapepe yako tu uliyoyarukia mapenzi kwa Japhet?" Flora aliuliza.

Japhet akacharuka kusikia ametajwa na Shemeji yake. "Shemeji naomba sana tuheshimiane tafadhali, sitaki uniingize kwenye hayo mazungumzo yenu" Japhet alisema huku akijifanya amekasirika.

"Mmh basi nisamehe jamani kama nimekukera" Flora alisema na kumuomba msamaha Japhet. Basi baada ya hapo wakaendelea kula chakula na walipomaliza kula tu Japhet akanyanyuka na kuondoka sebuleni hapo akaelekea chumbani kwake kulala huku akijifanya bado amekasirika. Hata Flora alishindwa kumuuliza Japhet kuhusu huko kwenda kwake kulala mapema. "Mmh ngoja kwanza nimuache nisije nikamkera zaidi" alijisemea Flora moyoni. 

Rozi naye akaondoa vyombo vyote Mezani na kuvipeleka jikoni halafu akaenda bafuni kuoga. "Sasa huyu Japhet naye ndio nimuelewe vipi, hicho chumba amepata au vipi?" Rozi alijiuliza wakati alipokuwa bafuni akioga. Kile kitendo cha kuwakuta Japhet na Shemeji yake Flora pale sebuleni wakinyonyana denda kilimuuma sana Rozi. "Hapa tusipohama na Japhet wangu, huyu mwanamke atamsumbua sana na kulazimisha naye mapenzi" alijiwazia Rozi. Baada ya kumaliza kuoga akarudi chumbani kwake kulala.

Flora naye akaenda chumbani kwake kulala mapema. "Kesho mume wangu anarudi hivyo leo ngoja nizidhibiti Nyege zangu" alijisemea Flora huku akijifunika shuka vizuri kitandani. Japo mwili wake bado ulikuwa unamnyemvua zaidi akikumbuka jinsi alivyokuwa anachezeana na Japhet pale mwanzo.

"Acha tu usiku wa leo upite nitavumilia, ingawa nilimpania sana Japhet" alisema Rozi. Basi ndio ikawa hivyo usiku huo uliweza kupita bila ya mtu kumsumbua mwenzie kwenda kumgongea mlango.



Asubuhi ya siku nyingine mpya ikafika!

Japhet akaamka na kuchukua mswaki wake akatoka chumbani kwake na moja kwa moja akaelekea uwani. "Yaani hata siamini usiku wa Jana umepita bila ya Shemeji au Rozi kuja kunisumbua?" Japhet alijiuliza hivyo. Baada ya kufika uwani akaweza kumkuta Rozi tayari ameshaamka yupo nje anafagia. Wakaweza kusalimiana na halafu Japhet akasema: "Jana nimefanikiwa kupata chumba na tayari nimeshakilipia kodi ya miezi sita" Japhet alisema. Rozi akajikuta anatabasamu baada ya kusikia hivyo.

"Ni maeneo ya huko kwa rafiki yako yule uliyempigia simu?" Rozi aliuliza.

"Yes ndio maeneo ya hukohuko na yeye ndie aliyenitafutia hicho chumba" Japhet alisema. "Oooho vizuri sana kwahiyo ni lini sasa tunahamia huko?" Rozi aliuliza tena. "Ngoja leo usiku nitakuja chumbani kwako tutapanga vizuri jinsi ya kuhama hapa, hivi unajua kama leo kaka yangu anarudi?" Japhet alimuuliza Rozi.

"Looh afadhali arudi hapa nyumbani, ili huyu Malaya asiyeridhika aache kabisa kukusumbua" alisema Rozi kwa furaha.

Basi baada ya hapo mambo mengine yaliendelea asubuhi hiyo kama kawaida. Flora naye akaweza kuamka na muda wa kunywa Chai ulipofika wote wakajumuika mezani kwa pamoja na kupata Chai hiyo.

Flora leo aliamka akiwa ni mpole kupita siku zingine hakuwa na mapepe kama anavyokuwa siku zingine zilizopita. Japhet alijua labda upole huo alioamka nao Shemeji yake huyo unasababishwa na ujio wa kaka yake kutoka safarini.

Kwenye majira ya Saa 8:46 za mchana gari ndogo ya kukodi aina ya Taxi iliweza kusimama ndani ya kituo kikubwa cha Mabasi yaendayo na yatokayo mikoani (UBUNGO BUS TERMINAL) Japhet na Shemeji yake Flora walikuwa ndio hao wamekuja hapa kumpokea Lukasi ambaye ndie Mume halali wa Flora na ndugu wa damu kabisa kwa kijana Japhet huku Lukasi akiwa ndio Mkubwa kuzaliwa na Japhet akiwa mdogo. Bahati nzuri basi alilopanda Lukasi kutokea Mwanza kuja hapa Dar es salaam lilikuwa limewasili dakika chache zilizopita hivyo walimkuta Lukasi yupo anawasubiria wenyeji wake wanaokuja kumpokea hapa kituoni.

Japhet na Flora waliweza kumuona Lukasi akiwa kwenye kibanda kimoja kilichokuwa kimepakwa rangi nyekundu na chenye maandishi makubwa meupe yaliyoandikwa COCA~COLA walimuona Lukasi yupo hapo akinywa Soda na Jamaa mmoja hivi. 

Wakati Flora na Japhet wakisogea hapo kwenye hicho kibanda cha Soda wakaweza kumuona Jamaa huyo akiagana na Lukasi kwa haraka na halafu akatokomea maeneo hayo halafu Lukasi akanyanyuka kwenye Kiti alichokuwa ameketi kibandani hapo na kubeba begi lake mgongoni pamoja na mizigo michache mikononi mwake akaanza kuja akiwafuata wakina Flora na Japhet. Flora akamkimbilia Mume wake ili kwenda kumpokea mizigo hiyo huku akiwa amejawa na furaha baada ya kumuona tena Mwanaume huyo. Lakini kwa upande wa Lukasi wala hakuwa na furaha hata huo uchangamfu hakuwa nao alikuwa amenuna na kukunja sura yake.

Kijana Japhet alijikuta anaogopa sana baada ya kumuona kaka yake Lukasi yupo kwenye hali hiyo ya kukasirika.

Baada ya Flora kumfikia Mume wake huyo akaweza kumkumbatia kwa furaha na kumpokea baadhi ya mizigo aliyokuja nayo. "Vipi Mume wangu mbona kama unaonekana haupo sawa, shida nini?" Flora alimuuliza Mume wake.

"Hamna kitu Mke wangu mimi nipo sawa, ni uchovu tu wa safari nilionao" alisema Lukasi. Kijana Japhet naye akaweza kumsogelea kaka yake na kusalimiana naye halafu akampokea begi la mgongoni alilolibeba. Baada ya hapo wakaanza kuifuata ile gari ndogo aina ya Taxi sehemu ilipokuwa imepaki na baada ya kuifikia Taxi hiyo dereva wake akafungua ule mlango wa nyuma kabisa (Buti) na mizigo yote ikaingizwa na kufungiwa humo. 

Halafu wote wakaingia ndani ya gari kwa ajili sasa ya safari ya kurudi nyumbani. Wakati gari ikiwa ndio inaanza kuondoka kituoni hapo Lukasi akasema: "Japhet tukifika nyumbani nitakuwa na maongezi kati yako wewe na Shemeji yako Flora" alisema Lukasi huku akiwa yupo bize na kuipekua pekua simu yake kubwa. Kwa mshtuko Mkubwa Japhet na Flora wakajikuta wanaangaliana usoni!.



**************

"Japhet tukifika nyumbani nitakuwa na maongezi kati yako wewe na Shemeji yako Flora" alisema Lukasi huku akiwa yupo bize na kuipekua pekua simu yake kubwa. Kwa mshtuko Mkubwa Japhet na Flora wakajikuta wanaangaliana usoni.

"Ni mazungumzo gani tena hayo Mume wangu?" Flora uvumilivu ulimshinda akajikuta anamuuliza Mumewe.

"Nimesema mpaka tukifika nyumbani sasa haraka ya kutaka kujua inatokea wapi?" Lukasi aliuliza kwa ukali kidogo.

Hapo tena Flora ikabidi awe mpole na kutulia kimya akabakia na mawazo tele kichwani mwake. "Ina maana Yale yote niliyoyafanya na Shemeji Japhet kule nyumbani, Mume wangu ameyajua?" Flora alijiuliza moyoni mwake. Kwa upande wa kijana Japhet ndio kabisa alizidi kuchanganyikiwa au kama sio kupagawa kabisa kwani akujua hayo mazungumzo anayotaka kuyazungumza huyu kaka yake huko nyumbani yatakuwa yanahusu nini "Vipi tena kaka amejua nini Yale tuliyoyafanya na Shemeji?" Japhet naye alibakia anajiuliza maswali. Safari ya kurudi nyumbani iliendelea huku ikiwa imetawaliwa na ukimya usiokuwa wa kawaida humo ndani ya hiyo gari.

Japhet alikuwa ameketi siti ya mbele kabisa na yule dereva Taxi akiwa yupo pembeni yake. Huku Lukasi na mkewe Flora wao wakiwa wameketi siti ya nyuma kabisa. Kama ni kuwachanganya basi Lukasi alijua kuwachanganya Flora na Japhet kwani walibakia kimya huku kila mmoja akionekana kuchanganyikiwa.

Hatimaye waliweza kufika mpaka huko nyumbani wakitokea kituo kikuu cha Mabasi yaendayo na yatokayo mikoani (Ubungo) gari hiyo ndogo ya kukodi (Taxi) ikaweza kusimama mbele ya nyumba ya Lukasi na wote kwa pamoja wakapata kuteremka ndani ya gari. Baada ya kuwa wameteremsha na mizigo yote dereva naye akapewa Pesa yake na kuondoka zake huku akiwashukuru hao abiria wake aliowaleta hapa nyumbani. Sasa wote wakaweza kuingia mpaka ndani ambapo Rozi naye alikuja kuwapokea mizigo.

"Ooho Rozi huyo vipi wewe aujambo?" Lukasi alimsalimia Rozi kwa furaha.

"Mimi sijambo Shemeji shikamoo" Rozi alimuamkia Lukasi. "Marahaba vipi lakini hapa mlikuwa mnaendeleaje?" Lukasi aliuliza. "Hapa nyumbani sisi tulikuwa tunaendelea vizuri, pole na Safari" Rozi alisema huku akitabasamu. "Ahsante sana nashukuru haya ndio nimerudi" alisema Lukasi na baada ya hapo yeye pamoja na mkewe Flora wakaingia zao chumbani. Japhet alibakia sebuleni akiwa bado amepagawa mawazo yake yote yalikuwa ni juu ya hicho anachotaka kuzungumza kaka yake (Lukasi) kama vile alivyowaambia kule kwenye gari.

"Vipi baby mbona kama vile unaonekana una mawazo unawaza nini, au haujapenda kaka yako alivyorudi hapa nyumbani?" Rozi alimuuliza Japhet kwa kumtania baada ya kumuona yupo kimya huku mkono wake ukiwa upo shavuni.

"Hapana kwanini nisipende kaka yangu kurudi nyumbani? basi tu kuna mambo flani kichwani yananichanganya" Japhet alisema. Rozi akatabasamu na kusema: "Basi mimi ninavyokuona hivyo najua labda umechukia kuona kaka yako amerudi nyumbani, labda atawanyima nafasi ya kujivinjari na Shemeji yako" Rozi bado aliendelea kumchombeza Japhet.

"Hebu achana na mawazo hayo Rozi" Japhet alisema kuonyesha amekereka.

"Mmh haya basi yaishe, ni kitu gani sasa hicho kinachokuchanganya mpenzi?" Rozi aliuliza. Japhet akanyanyuka kwenye Kochi na halafu akaondoka sebuleni hapo na kuelekea chumbani kwake huku akimwambia hivi Rozi: "Usihofu mpenzi wangu nitakuambia baadae chumbani" alisema Japhet na kuondoka. Rozi akabakia sebuleni hapo huku moyoni mwake akiwa amejawa na furaha baada ya Lukasi kaka yake na Japhet kurejea hapa nyumbani kwani alijua sasa hayo Mapenzi ya Japhet na Shemeji yake Flora ndio yatakuwa yamefikia mwisho.



Kwenye majira ya usiku wote wanne yaani Lukasi na mkewe Flora na huku Japhet na Rozi sasa wakakutana Mezani kwenye kupata chakula cha usiku. Mpaka muda huo bado Lukasi alikuwa ajaanzisha hayo mazungumzo aliyodai kuwa nayo anataka kuongea pindi watakapofika nyumbani.

Kitendo cha Lukasi kuendelea kunyamaza kimya kilizidi kuwanyima raha sana Flora na Shemeji yake Japhet.

"Sasa Mume wangu mbona unazidi kutuweka roho juu mwanzo ulituambia kuwa utakua na mazungumzo kati yangu na Shemeji Japhet baada ya kufika hapa nyumbani mbona aungei sasa?" Flora alimuuliza Lukasi. Kwanza Lukasi akatabasamu halafu akasema: "Inaonyesha mke wangu una wasiwasi sana na hicho ninachotaka kukiongea?" Lukasi alimuuliza Flora. Muda huo wote Japhet alikuwa yupo kimya roho yake ikimdunda kwa hofu. 

"Hapana sio kama nina hofu Mume wangu, lakini kumbuka ni wewe ndio ulituambia kuwa una hayo mazungumzo na sisi" alisema Flora huku akimuangalia Japhet. Lukasi akajiweka sawa na kusema: "Ok ni kweli kabisa Mke wangu niliwaambia muda ule kuwa nitakuwa na mazungumzo na wewe hapo pamoja na Shemeji yako Japhet, lakini kwanza nawaomba muwe na Amani kwani mazungumzo yenyewe ni ya kawaida tu" alisema Lukasi. Japhet akashusha pumzi kusikia hivyo. Lukasi akaendelea tena kuongea: "Nilichokuwa nataka kusema ni hivi, kwanza nafurahi kurudi nyumbani salama na kuikuta familia yangu yote ikiwa na furaha kama nilivyoiacha" alisema Lukasi huku akitabasamu. 

Japhet na Flora hapo wakajikuta wanaangaliana tena usoni na kuona kama vile Lukasi anawazunguka kwa kuwaambia hivyo. "Mmh Mume wangu hebu acha kutufanya sisi watoto wadogo, yaani hicho ndio kitu chenyewe kweli ulichotaka kutuambia?" Flora aliuliza kwa waaiwasi. Lukasi akacheka kidogo na halafu akasema: "Mke wangu kama auamini basi lakini hicho ndio kitu chenyewe nilichotaka kuwaambia" Japhet alisema huku akiwaangalia kwa zamu Japhet na Flora. Rozi yeye alikuwa yupo kimya akiendelea kula chakula taratibu.

INAENDELEA

Powered by Blogger.