KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Utamu Wa Shemeji Flora Sehemu Ya Kumi na Tisa (19)


SIMULIZI NZURI YA KUSISIMUA
Flora hakuweza kujibu kitu chochote alibakia akijiumauma midomo yake na kujiinamia chini uso wake kwa aibu kwani akutegemea kabisa kama angekuja kufumwa na Mume wake huyo. Lukasi baada ya kusogea hapo mlangoni na yeye pia akaweza kuzisikia sauti hizo za Mahaba zikitokea chumbani humo kwa Japhet hapo sasa Lukasi ndio akazidi kupigwa na butwaa. 

Kwa haraka Lukasi akamshika mkono mkewe (Flora) na kumtoa mlangoni hapo na kuelekea naye chumbani kwao wanapolala pia akazima na Taa ya ukumbini halafu ndio wakaingia chumbani na kujifungia kabisa mlango.

"Hayaa niambie sasa mke wangu ina maana zile sauti ndio ulikuwa unazisikiliza pale mlangoni?" Lukasi aliuliza baada ya kufika chumbani kwao na kumketisha mkewe kitandani.

"Nisamehe Mume wangu, wakati nilipokuwa narudi kutoka chooni kukojoa ndio nikasikia sauti zile chumbani kwa Japhet nikaamua kusimama na kusikiliza" Flora alijitetea akijisikia aibu. Lukasi alishusha pumzi ndefu na kujikuna kichwa chake halafu akauliza: "Bila shaka ile sauti ya msichana inayosikika huko chumbani kwa Japhet ni ya Rozi na sio sauti ya msichana mwingine yeyote?" Lukasi alimuuliza mke wake. "Ndio mume wangu ile ni sauti ya Rozi" Flora alijibu.

"Ok hakuna shida mke wangu, naomba tulale kesho nitaongea na Japhet kuhusu hilo" alisema Lukasi na baada ya hapo wakajilaza kitandani na kulala usingizi.

Lukasi alilala lakini alijiuliza sana ni kwanini mkewe Flora afanye vile ina maana ndio kazidiwa sana Nyege kiasi hicho kweli? Lakini Lukasi hakupata jibu.

Kwa upande wa Flora yeye alilala na donge zito la wivu moyoni mwake kwa kuona Rozi ameufaidi Utamu wa Japhet.



Kule chumbani kwa Japhet napo baada ya kumaliza kupelekana mchakamchaka wawili hao Rozi na Japhet wakajilaza kitandani huku wakiwa wapo hoi kwa ajili ya shughuli pevu waliyoifanya ya kukata Kiu yao ya Mahaba. "Baby ahsante sana nashukuru kwa kuniliwaza" Rozi alisema huku akitabasamu na kujilaza juu ya kifua cha kijana huyo. 

"Nami pia nashukuru sana mpenzi wangu kwa kunizawadia mwili wako niumiliki vile nitakavyo" alisema Japhet huku akimchezea nywele Rozi. "Ndio hivyo baby hapa tufanye haraka sana tuhame, kwani tukiendelea kubakia hapa tutashindwa kufurahia mapenzi yetu vizuri na Shemeji yako naye atazidi kukusumbua" alisema Rozi.

"Yaani kuhusu huyo Shemeji Flora ndio ananiumiza sana kichwa changu, nahisi anataka kunigombanisha na kaka yangu" alisema Japhet kwa unyonge. "Ndio maana nashauri tuhame hapa haraka sana unajua hautaweza kumuepuka kama bado ukiendelea kuwa hapa, na mimi sitaki kushea hili Penzi lako na yeye Flora" alisema Rozi kwa hisia Kali.

"Lakini mpenzi wangu huko tutakapohamia kwenye hicho chumba chetu hatutakuwa na kitanda wala Kochi" alisema Japhet. "Kuhusu hilo baby wangu naomba uondoe hofu hata kama hatuna kitanda wala Kochi nipo tayari kulala chini kwenye boksi au gunia" alisema Rozi akimaanisha hicho anachokisema.

"Nafurahi kusikia hivyo mpenzi wangu, sasa kesho nitaenda mjini kununua mashuka na mapanzia pamoja na vyombo vidogovidogo vya ndani halafu nitaenda kuvihifadhi kule kwa rafiki yangu usiku ndio nitaaga kwa kaka pamoja na Shemeji" alisema Japhet. "Sasa mimi nitapajuaje huko kwenye hicho chumba?" Rozi aliuliza. 

"Usijali nitakuelekeza kwa njia ya simu namna ya kufika huko mpenzi wangu, unajua sio vizuri kama tukiondoka wote kwa pamoja" alisema Japhet. "Hayaa bwana mimi nakusikiliza wewe tu baby, lakini kwa upande wangu naona sawa tukiondoka wote" alisema Rozi na baada ya hapo akaondoka humo chumbani kwa Japhet na kurudi tena chumbani kwake kulala. Japhet naye pia akaweza kulala usingizi mzito.



Asubuhi na mapema ya siku nyingine mpya nayo ikaweza kufika Rozi kama kawaida akaamka na kuaza kufanya kazi zake za kila siku hapo nyumbani. Baada ya muda watu wote ndani ya nyumba wakaweza kuamka na kuketi mezani kwa ajili ya kupata kunywa Chai asubuhi hii ya leo isipokuwa Flora tu ndio alibakia amejifungia chumbani na kujidai amelala.

"Vipi kaka mbona Shemeji amechelewa kuamka, au leo ajisikii vizuri?" Japhet alimuulizia Shemeji yake (Flora) kwa yake Lukasi. Japhet akajifikiria kidogo halafu akamjibu mdogo wake: "Yeah ajisikii vizuri Shemeji yako lakini usijali baadae ataamka na utamuona" alisema Lukasi.

Baada ya kumaliza kunywa Chai Rozi akaondoa vyombo mezani hapo na kwenda uwani kuviosha. Lukasi akaaga na kusema anatoka Mara moja lakini asingechelewa kurudi hapa nyumbani.

Lukasi kilichokuwa kinamuumiza kichwa ni kile kitendo cha kumkuta mkewe (Flora) pale mlangoni kwa Japhet usiku wa Jana yake akisikilizia sauti za Mahaba zilizokuwa zikisikika kutokea chumbani kwa Japhet wakati mdogo wake huyo (Japhet) alipokuwa anafanya mapenzi na Rozi ambaye ni dada wa kazi za ndani.

"Sishangai mdogo wangu Japhet kuwa kwenye mahusiano na huyu binti Rozi, ila kinachonishangaza ni kwanini mke wangu Flora awafuatilie kwa kuwasikilizia mlangoni wanayoyafanya chumbani? hapa ni lazima tu kutakuwa na kitu kimejificha" alijisemea Lukasi moyoni na alipanga mchana au jioni atakaporudi kutoka kwenye shughuli zake basi ni lazima atawaweka kikao Rozi na Japhet kutaka kuwahoji juu ya huo uhusiano wao wa kimapenzi ili ikiwezekana uweze kutambulika rasmi na sio wa kujificha.

Baadae na Japhet naye akamuaga Rozi na kuondoka hapo nyumbani ambapo alielekea maeneo ya katikati ya jiji la Dar es salaam kununua baadhi ya vifaa na vyombo vidogovidogo vya nyumbani kama vile alivyokubaliana na mpenzi wake Rozi. "Bora tu kuhama pale nyumbani kwa kaka yake nikiendelea kuishi mambo yataharibika muda sio mrefu sana, nahisi kaka yangu tayari ameshaanza kushtukia mchezo" alijisemea Japhet moyoni akiwa yupo ndani ya daladala. Kwa upande Fulani alimshukuru sana Mungu kwa kumpatia mpenzi muelewa na mwenye kuonyesha mapenzi kama Rozi. "Kiukweli huyu binti nakiri ndani ya moyo wangu ananipenda, nami pia nampenda sana japo Shemeji anataka kuharibu mambo kwa tamaa zake binafsi za kimwili hapa ni lazima nimuepuke ili kulinda Penzi langu kwa Rozi" aliendelea kujisemea Japhet.

Flora kwenye majira ya mchana ndio alikuwa anaamka kitandani na kutoka chumbani kwake ambapo alishangaa kuona hapo nyumbani amebakia yeye na Rozi tu bila ya kumuona Shemeji yake Japhet. 

"Au Shemeji Japhet atakuwa ameondoka pamoja na kaka yake nini?" Flora alijiuliza mwenyewe bila ya kupata jibu. Hakutaka kabisa kumuuliza Rozi juu ya hilo kwani alishaamua kumchunia kwa sababu ya Wivu wake kwa binti huyo kumuona anaufaidi Utamu wa Shemeji yake (Japhet) "Yaani usiku mimi nipo nahangaika na Nyege zangu halafu yeye anakamuliwa na Japhet, mume wangu naye goigoi anashindwa kuniridhisha" alisema Flora akiwa yupo sebuleni amejilaza kwenye kochi anaangalia TV. Ndani ya moyo wake alijikuta anaanza kumchukia kabisa mume wake Lukasi na kujikuta mapenzi yake yote anataka kuyapeleka kwa Shemeji yake Japhet.

"Nitafanya kila njia huyu binti humu ndani aondoke na kumuacha Japhet ili mimi nimfaidi peke yangu pindi kaka yake atakaposafiri tena" alijisemea Flora huku akitabasamu bila ya kujua kama na wenzake nao (Rozi na Japhet) walikuwa ndio wanapanga mipango ya kuhama humu ndani ya nyumba kumkimbia yeye wamuache na pepo lake la Ngono.



Japhet baada ya kufanikiwa kuvipata vitu vyote alivyohitaji kuvinunua akaweza kupanda tena daladala kutoka maeneo ya katikati ya jiji hadi kule maeneo ya Buza Kanisani kwa rafiki yake Mussa ambapo ndio alipokuwa amepata chumba cha kupanga. "Hivi vyombo bora tu nivipeleke kwa Mussa akavihifadhi, mimi kazi yangu ibakie ya kuaga nyumbani kwa kaka" alijisemea Japhet. 

Baada ya kufika nyumbani kwa Mussa alipopanga ambapo alikuwa anaishi na mke wake. Japhet aliweza kumkabidhi vyombo hivyo rafiki yake huyo na kumuomba avihifadhi halafu yeye atakuja kuhamia rasmi kesho yake kule kwenye kile chumba alichomtafutia. "Usijali kabisa ndugu yangu kuhusu hilo ondoa shaka" alisema Mussa akimuambia hivyo Japhet.

"Halafu pia nilikuwa naomba unisaidie kitu kimoja unitafutie mtu wa kukifanyia usafi kile chumba ili hiyo kesho nikija nikute mazingira yapo vizuri" alisema Japhet huku akimkabidhi rafiki yake Mussa noti ya shilingi Elfu Kumi kwa ajili ya kumpatia mtu wa kufanya usafi. Baada ya kumaliza kula chakula cha mchana hapohapo nyumbani kwa rafiki yake huyo Japhet akaaga na kuondoka akirudi kule nyumbani kwa kaka yake Lukasi.



Kwenye majira ya Saa 12:30 za jioni Japhet aliwasili nyumbani kwa kaka yake na kumkuta tayari amesharudi kutoka kwenye shughuli zake. Baada ya kusalimiana pale Japhet akaingia zake chumbani huku akimuacha kaka yake huyo na mkewe (Flora) sebuleni wakiangalia TV muda wote tangu Japhet alipoingia humo ndani ya nyumba Shemeji yake alikuwa akimuangalia kijana huyo kwa jicho la matamanio huku Rozi naye akiwa yupo jikoni anapika zake chakula cha usiku. Japhet baada ya kuingia chumbani kwake akaketi kwanza kitandani na kuanza kuvua viatu vyake miguuni. 

"Hapa leo baada ya kumaliza kula chakula cha usiku tu, nalianzisha kwa kuaga sijui Shemeji Flora atajisikiaje wakati nitakapokuwa nawaaga" Japhet alijisemea huku akitabasamu na kufurahi sana moyoni mwake baada ya kuona anakaribia kuviepuka visa vya Shemeji yake huyo. Mara ghafla mlango wa chumbani kwake ukafunguliwa na Lukasi akaingia ndani humo chumbani na kuufunga mlango kwa ndani na funguo.

Japhet kwanza alishtuka na kushangaa kumuona kaka yake akiingia bila hodi.

"Vipi kaka kuna usalama kweli?" Japhet alimuuliza kaka yake huyo.

"Usalama upo mdogo wangu, nimekuja kwako ghafla nataka uniambie mambo mawili tu na unipe maelezo ya kutosha" alisema Lukasi kwa sauti kavu yenye msisitizo. Japhet alishtuka sana!

"Mambo gani tena hayo kaka unataka nikupe maelezo ya kutosha?" Japhet alijikuta anauliza kwa hofu kubwa sana.

"Jambo la kwanza nataka uniambie kuhusu uhusiano wako wewe na huyu binti Rozi upoje, na jambo lingine la Pili nataka uniambie nini kinaendelea kati yenu na Shemeji yako Flora" alisema Lukasi huku akimkazia macho yake makali mdogo wake huyo halafu akaenda kuketi hapohapo kitandani kwa Japhet.

Kijana Japhet alijihisi kuchanganyikiwa!.





"Jambo la kwanza nataka uniambie kuhusu uhusiano wako wewe na huyu binti Rozi upoje, na jambo lingine la Pili nataka uniambie nini kinaendelea kati yenu na Shemeji yako Flora" alisema Lukasi huku akimkazia macho yake makali mdogo wake huyo halafu akaenda kuketi hapohapo kitandani kwa Japhet.

Kijana Japhet alijihisi kuchanganyikiwa.

Alibakia kimya hakujua hata amjibu nini huyu kaka yake aloyeonyesha kuhitaji majibu ya haraka kutokana na maswali aliyomuuliza. "Nahitaji maelezo yako mdogo wangu Japhet, mbona unakaa kimya sasa?" Lukasi aliuliza na kuweza kumzindua Japhet kwenye mawazo.

"Yaani kaka sio siri nashindwa hata nikujibu nini kwa jinsi ulivyoniuliza" Japhet alisema kwa sauti ndogo sana.

"Nijibu pale unapoona panafaa kwa kuanzia cha msingi maelezo yako yawe yenye kujitosheleza na kuniridhisha" alisema Lukasi huku akikaa tayari kabisa kumsikiliza mdogo wake atakachosema.

Japhet akaona sasa hapa akiendelea kubakia kimya au kubabaika ndio itakuwa sababu ya kumfanya kaka yake aanze kumfikiria vibaya na kumuona kama vile kuna jambo zito lipo ndani ya moyo wake hivyo Japhet akaamua kuvunja ukimya.

"Kaka ngoja nikuambie ukweli kuhusu uhusiano wangu na Rozi jinsi ulivyo, sio siri kabisa Rozi ni mpenzi wangu na pia nampenda sana" Japhet aliamua sasa kufunguka na kusema ukweli wake.

"Ok hakuna shida kuhusu hilo, na vipi kuhusu huyu Shemeji yako Flora?" Lukasi aliuliza kwa sauti ndogo ya utulivu.

Hapo Japhet akashusha pumzi ndefu na kusema: "Kuhusu Shemeji Flora, ngoja tu nikuambie kaka hakuna chochote kibaya kinachoendelea baina yetu namuheshimu sana na yeye pia ananiheshimu kama Shemeji yake" Japhet alisema.

INAENDELEA
Powered by Blogger.