KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Mama Vannessa sehemu ya kumi (10)

hadithi nzuri ya kusimumua ya mapenzi
Muhudumu aliwasikiliza na kwenda kuchukua vinywaji. Mara Mama Vanesa naye alikuwa akija kutoka kwenye hotel. Alichukua muda mrefu lakini haikuwa tatizo kwa Lucas maana anajua kabisa wasichana linapokuja swala la kubadili nguo lazima waanze kujiremba upya. Ni kweli maana mama Vanesa alikuwa amebadilika kabisa na kuzidi kuonekana kuwa alikuwa ni msichana mdogo. Alivaa kimini kilichofanya kuacha mapaja yake nje. Alionekana ni binti mdogo pengine waweza kusema ni msichana amabye hajaolewa. Lucas hakujua kwa nini amevaa hivyo lakini huenda labda aliamua kujiachia mara baada ya kuhisi kuwa watakuwa wawili tu. Hakujua kama kuna wageni wanaweza kuja. Hata hivyo hakuonesha kushtushwa sana alivuta kiti na kukaa. Kimaro aliyatumbua macho na hakuamini kama huyo ndo mke wa boss ambaye alikuwa akizungumziwa..


“Habari zenu” Mama Vanessa alitoa salamu ya jumla.



“Nzuri” Kimaro na kimwana aliyekuja naye walijibu kwa pamoja.Kimya kikatawala kidogo kabla ya Lucas kuvunja ukimya.



“Mama Vanessa huyu anaitwa Kimaro ni rafiki wangu wa kufa na kuzikana. Mr Kimaro huyu ndio mama Vanessa mwanamke aliyeamua kuniokota mara baada ya Mishel kunitupa.



“Nashukuru sana bwana Lucas nashukuru pia kumfahamu mama Vannesa..Kimaro aliongea huku akimpa mkono mama Vanessa. Alifanya utani wake kidogo kwa kuubinya mkono kwa nguvu jambo lilofanya mama Vanesa ahisi maumivu.



“Aiseee kweli unastahili hili kuitwa mrembo mikono laini kama maini” Kimaro aliongea huku akionesha kushangaa.



Wote kwa pamoja walicheka na kufanya kuchangamka. Muhudumu alikuja tena na kumleta kinywaji mama Vanesa. Safari hii alibadilisha na kuanza kunywa wine. Stori mbili tatu za kuchekesha ziliendelea na kufanya muda kuzidi kuyoyoma. Kimaro alitumia muda huo vizuri kuwafurahisha na kuwachekesha kwa sababu moja ya vitu alivyojaliwa ni kuwafurahisha watu na kuwafanya wamsikilize kwa muda mrefu.

CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Wakati stori zikiendelea mama Vanessa yeye alikuwa ulimwengu mwingine kabisa. Alikuwa akiwaza ni jinsi gani atarudi Musoma hili hali muda ulikuwa umeenda sana. Aliendelea kunywa kinywaji huku akili yake ikifanya kazi ya ziada juu ya uwongo gani afanye ili mme wake amuelewe. Yaani mama Vanesa alikuwa ni mwanamke wa ajabu sana huku duniani kwa sababu ingawa mme wake alikuwa akimtenda vibaya kila mara lakini hakuwahi kuwa mkaidi. Siku zote amekuwa mtiifu na amekuwa akijishusha. Haya yote aliyafanya kwa sababu alitokea kwenye familia masikini. Alijifanya kipofu kwa kwa mabaya yote ambayo alikuwa akitendewa na mumewe. Lakini alikuwa na lake moyoni kwa kuwa muda huo yeye kujifanya boya ulikuwa umekwisha. Tayari alikuwa ameshachuma mali za kutosha. Alishajenga kwao na alishakuwa na nyumba mjini. Mumewe alimwamini sana na hakujua kuwa ipo siku atabadilika.


“Mbona mama Vanesa anaonekana kama mwenye mawazo?”Kimaro aliuliza mara baada ya kuona huyo ametulia tu.


“Hamna mimi sina mawazo yoyote tupo pamoja” Mama Vanesa alisema huku akitaka kusema kuwa anataka kuondoka. Ila aliamua kujiuliza maswali na kujijibu mwenyewe.Sasa nitaondokaje na kilichokileta huku sijakipata. Hata hatujaweka mikakati ya kumkomesha baba Vanesa. Ilibidi amuandikie sms Lucas kumueleza nia yake ya kutaka kuondoka. Lucas na yeye alimuuliza swali lile kuwa sasa ataondokaje wakati bado hatujapanga mikakati. “Mimi naona utafute njia ulale kwa sababu tayari chumba kipo.Lucas alishauri na wakati huo huo Lucas pia alianza kuchati ana Kimaro kumwambia kuwa mama Vanesa anataka kuondoka. Kimaro akasisitiza kuwa hilo haiwezi kutokea kama yeye yupo.


“Inaoenkana watu mmekaa kiunyonge nyonge sasa napendekeza tuhame kwa muda kuna mahali nasikia kuna nyama choma twendeni tukale.” Kimaro aliongea huku akiinuka na kumpa mkono msichana aliyekuja naye kisha kuanza kupiga hatua na kuondoka. Lucas alitamani kucheka lakini alijikausha na yeye akafanya kumpa mkono Mama Vanesaa.

Inaendelea

Powered by Blogger.