KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Utamu Wa Shemeji Flora Sehemu Ya Kumi na Tano (15)

SIMULIZI NZURI YA KUSISIMUA
"Aloo kaka habari za huko?" Japhet alianza kwa kumsalimia kaka yake huyo.

"Za huku ni nzuri mdogo wangu, vipi huko mnawndeleaje?" Lukasi alimuuliza hivyo mdogo wake Japhet kwenye simu.

"Za huku pia ni nzuri kaka" Japhet alijibu.

"Sasa ni hivi mdogo wangu, kesho Mungu akipenda nitakuwa huko Dar es salaam" alisema Lukasi na kuongezea tena: "Kwahiyo nilikuwa naomba uje wewe na Shemeji yako kunipokea pale Ubungo nitawasili na basi la mchana" alisema Lukasi. "Sawa kaka hakuna shida nitakuja na Shemeji kukupokea, tumekumiss sana" alisema Japhet huku akitabasamu.

"Nami pia nimewamiss sana, yaani nilijua nitakaa huku Mwanza kwa wiki mbili kama vile nilivyowaaga lakini nashukuru biashara zimeenda vizuri narudi huko mapema" alisema hivyo Lukasi.

"Nafurahi sana kaka kusikia hivyo, vipi lakini Shemeji umemjulisha kama hiyo kesho unarudi nyumbani?" Japhet aliuliza. "Yeah nimetoka kumpigia simu sasa hivi na kumjulisha, halafu ndio nikakupigia wewe mdogo wangu" alijibu Lukasi.

"Basi sawa kaka karibu sana nyumbani" alisema Japhet.

"Ndio hivyo mdogo wangu Japhet wala usijali nikirudi huko hiyo kesho, nitaanza kufuatilia kuhusu wewe kupata kazi kama nilivyokuahidi" alisema Lukasi.

Baada ya Japhet kuongea na simu na kaka yake hatimaye wakamaliza hayo mazungumzo yao wakaweza kuagana na kukata simu zao.

"Daah afadhali kaka anarudi nipumzike na hivi visa vya Shemeji" alijisemea Japhet.



Baada ya mwendo wa nusu saa hatimaye daladala alilopanda kijana Japhet liliweza kufika maeneo ya hapo Buza Kanisani kama alivyoelekezwa na yule rafiki yake Mussa kuwa ndio anapotakiwa kushuka kwenye kituo hicho. Baada ya Japhet kuwa tayari ameshateremka kwenye ile daladala hapohapo akampigia simu Mussa kumjulisha kama tayari ameshafika. "Oyaa mwamba mimi ndio nimeshuka hapa tayari kwenye gari" Japhet alisema. "Poa tayari nimeshakuona rafiki yangu" alisema hivyo Mussa na kukata simu.

Japhet akiwa bado anashangaashangaa maeneo ya hapo Mara ghafla akahisi anashikwa begani ikabidi ageuke nyuma na kuweza kumuona Mussa akiwa yupo amejawa na tabasamu usoni mwake.

"Ooho best yangu huyo niambie" alisema Mussa huku akimkumbatia Japhet.

"Daah hata siamini kama kweli tumeweza kuonana tena" alisema Japhet.

"Ndio hivyo tena best yangu wahenga wanasema milima haikutani lakini sisi binadamu tunakutana, haya sasa twende nyumbani ukapaone ninapoishi" Mussa alisema. Baada ya hapo wakaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa Mussa huko anapoishi huku njiani vijana hao wakipiga story mbili tatu za kukumbushiana mambo ya zamani walipokuwa wanaishi wote huko kijijini kwao mkoani Dodoma.

Baada ya muda mfupi wakafika hapo nyumbani kwa Mussa ambapo ilikuwa ni nyumba tu ya kawaida na Mussa hapo alikuwa amepanga vyumba viwili alivyokuwa anaishi na mkewe pamoja na mtoto wao mdogo. "Karibu sana ndugu yangu, hapa ndio nyumbani na huyo hapo unaemuona ni Shemeji yako" alisema Mussa wakati alipokuwa anamkaribisha ndani Japhet. "Ahsante sana nashukuru pia kumfahamu Shemeji yangu" alisema Japhet huku akitabasamu. Baada ya hapo Mussa akamtambulisha huyo mkewe kwa kijana Japhet na kuweza kufahamiana.

"Enhe niambie ndugu yangu, vipi maisha yanasemaje?" Mussa alimuuliza Japhet.

Maisha ndio hivyohivyo yanasogea nipo kwa kaka yangu ndio ninapoishi" Japhet alisema. "Ok ni vizuri sana, vipi lakini kaka ajambo?" Mussa aliuliza tena.

"Kaka ajambo sana, amesafiri kibiashara yupo Mwanza, lakini leo amenipigia simu ya kunijulisha kuwa kesho anarejea" alisema Japhet. Wakati wanaendelea na mazungumzo ya hapa na pale ndipo mke wa Mussa akamkaribisha soda Japhet ya kupooza koo angalau. "Karibu soda Shemeji" alisema mwanamke huyo huku akimmiminia soda hiyo kwenye Glass.

"Ahsante sana Shemeji," alisema Japhet.

Baada ya hapo mke wa Mussa akaelekea jikoni kwa ajili ya kuandaa chakula cha mchana. Huku wakabakia Japhet pamoja na mwenyeji wake Mussa wakiendelea na maongezi yao huku wakionekana kufurahi kwa kuonana kwao. Japhet akaona sasa ndio hapahapa kwa kumueleza Mussa shida yake iliyomleta huku. "Ndugu yangu kwanza naomba unisikilize kwa umakini haya nitakayoambia, lakini nitaomba iwe ni siri yako na nitahitaji msaada wako" alianza kwa kusema hivyo Japhet.

Mussa akajiweka vizuri kwenye Kochi alipokuwa ameketi halafu akasema: "Kuhusu hilo ndugu yangu wala usijali, niambie tu nakusikiliza na nitaitunza hiyo siri pia nitakusaidia" alisema Mussa.

Japhet akashusha pumzi ndefu na kuanza kumsimulia Mussa mambo yote yanayoendelea kule nyumbani kwa kaka yake Lukasi ambapo yeye (Japhet) ndio anaishi bila hata ya kumficha Mussa akamsimulia jinsi Shemeji yake (Flora) anavyomsumbua kimapenzi na kutaka kufanya naye mapenzi lakini akamficha kuhusu alivyofanya naye mapenzi ile siku moja na akamueleza pia uhusiano wake na Rozi ambaye ni dada wa kazi (House Girl) kule nyumbani kwa kaka yake.

"Kwahiyo ndio hivyo ndugu yangu, msaada ninaouomba kwako naomba unisaidie kupata chumba maeneo ya huku ili nihamie huku na huyo binti niepuke vishawishi vya Shemeji" Japhet alisema. 

Mussa baada ya kumsikiliza Japhet kwa umakini naye akasema: "Duuh kwanza nakupa pole ndugu yangu kwa hayo majaribu ya kutakiwa na huyo Shemeji yako kimapenzi, Pili nikupongeze kwa uamuzi wako wa kuhama hapo nyumbani kwa kaka yako na huyo binti kumkwepa huyo Shemeji yako" alisema Mussa. "Ndio hivyo sasa ndugu yangu naomba msaada wako unitafutie chumba" alisema Japhet. 

Mussa akafikiria kidogo na kusema: "Kuhusu hilo jambo la chumba ondoa shaka kabisa kitapatikana kwani yupo Mzee mmoja hapa jirani nafahamiana naye nyumbani kwake kipo chumba anapangisha" alisema Mussa. Japhet alifurahi sana kusikia hivyo haraka sana akasema: "Nipeleke hata sasa hivi kwa huyo Mzee nikakione hicho çhumba, hapa nilipo nimekuja kabisa na Hela ya kodi” alisema Japhet. "Basi kama ni hivyo sawa ndugu yangu, twende ukapaone ni sehemu nzuri sana nina imani utapapenda" alisema Mussa huku akinyanyuka kwenye Kochi.

Baada ya kumuaga mke wa Mussa kuwa wanatoka Mara moja lakini wangerudi baada ya mfupi kuja kula chakula kwani wasingechelewa huko wanapoenda. Mussa na Japhet wakaweza kuondoka.




ITAENDELEA

Powered by Blogger.