KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Utamu Wa Shemeji Flora Sehemu Ya Kumi na Nne (14)

SIMULIZI NZURI YA KUSISIMUA
Flora akajikuta anapandwa na hasira huku wivu ukimsokota moyoni mwake kwa kumsikia Rozi amesema hivyo. Taratibu Flora akamgeukia Japhet na kusema hivi: "Jana nilikuambia Shemeji Japhet kuwa kipo kitu kinaendelea kati yako na Rozi halafu ukakataa, unaona sasa huyu binti amefichua kila kitu?" Flora alisema na kuuliza hivyo. Kijana Japhet alibakia kimya bila kusema chochote.

Flora akamgeukia Rozi na kumuuliza hivi:

"Sasa na wewe Rozi hapa umekuja kufanya kazi au umekuja kufanya mapenzi?" Flora aliuliza. Rozi bila hata ya kutetereka akamjibu: "Sioni kama kuna tatizo mimi kupendana na Japhet, kama ni kazi mbona najitahhidi kufanya vile nimewezavyo kuhusu hilo jambo la mapenzi ni la kwangu binafsi" alijibu Rozi huku akitabasamu. F

lora akakasirika na kusema kwa ukali: "Utasemaje hilo jambo la mapenzi ni la kwako binafsi, je kama ukipata ujauzito au magonjwa ya zinaa mimi nitawaambia nini wazazi wako huko kijijini kwenu nilipokuchukua?" Flora aliuliza kwa hasira. 

"Mbona inaonekana kama umechukizwa mimi kupendana na Japhet dada? naomba uniache na haya maamuzi yangu kuhusu ujauzito au hayo magonjwa ya zinaa nikipata nitajijua mimi na familia yangu, naomba usiniingilie" Rozi naye alisema kwa ujeuri.

"Yaani wewe Rozi leo unathubutu kweli kuniambia hivyo!?" Flora aliuliza kwa hasira. "Ndio nimekujibu sasa, ukome kumsumbua mpenzi wangu Japhet jaribu kutuliza hisia zako muheshimu huyu ni Shemeji yako" Rozi alizidi kumpa Flora makavu yake na kumuweka kwenye wakati mgumu sana mwanamke huyo.

Flora akapandisha mzuka wa hasira Ghafla bila kutarajia akachukua bakuli iliyojaa maji ya kunawa mikono na kummwagia Rozi usoni kwa hasira. "Wewe ni binti mdogo sana kwangu, hauwezi kunijibu hivyo mimi shenzyy," Flora aliwaka kwa hasira. 

"Shemeji hebu punguza jazba kwanza tuyaongee haya mambo yaishe" Japhet alijaribu kumtuliza Shemeji yake huyo. "Tena na wewe hapo inabidi unyamaze, umekaribishwa kwa kaka yako hapa unakula na kulala bure halafu unajifanya eti ni Kidume Ovyoo!" Flora alimchachafya na Japhet pia.

Kitendo hicho kilimchukiza sana Japhet na kuona kama vile amedharaulika kwa Shemeji yake (Flora) kumwambia hivyo akajikuta bila ya kutegemea anampiga bonge la Kofi Shemeji yake usoni PAAAA!

"Mamaaa nakufaaa yaani Japhet kweli unathubutu kunyanyua mkono wako na kunipiga mimi? sasa tutaona" alisema Flora kwa hasira huku akilia na kujishika shavuni alipopigwa Kofi hilo na Japhet.

Flora akamgeukia Rozi na kumuangalia halafu akamsonya na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake huku bado akiwa analia kutokana na kupigwa lile Kofi na Shemeji yake Japhet. Na habari ya kuendelea tena kunywa çhai ndio ikaishia hapo hakukuwa na mtu aliyekuwa na hamu ya kuinywa chai hiyo. Baada ya Flora kuwa amwingia chumbani kwake huku sebuleni napo alibakia Japhet pamoja na Rozi. 

Japhet akamsogelea Rozi na kumkumbatia halafu akasema: "Pole sana mpenzi wangu kwa kumwagiwa maji" alisema Japhet. Rozi akatabasamu na kusema: "Wala usijali baby cha msingi ujumbe umefika kwa muhusika" alisema Rozi. Baada ya hapo Rozi akakusanya vyombo vyote hapo mezani na kuviondoa kuvipeleka jikoni. Japhet naye akaingia chumbani kwake.

Flora akiwa kule chumbani kwake akajibwaga kitandani na kunyamaza kulia: "Napigwa ndani ya nyumba yangu na Shemeji Japhet kwa sababu eti ya mapenzi kweli?" Flora alijiuliza huku akijilaza vizuri kitandani. "Japo Shemeji Japhet amenipiga lakini bado nampenda, lakini huyu Kivuruge Rozi lazima tu nimuondoe humu ndani" alijisemea Flora na kunyanyuka halafu akaenda kwenye Kioo na kujiangalia vizuri usoni mwake alipopigwa na Japhet. 

"Mmh Japhet naye kumbe ni Mkali hapendi dharau, ndio Mwanaume ninayempenda huyo" alisema Flora huku akitabasamu. Baada ya kujiangalia kwenye Kioo akagundua usoni mwake amevimba na pia amekuwa mwekundu kutokana na vipodozi vyake anavyotumia kujipaka usoni. "Kwa kuwa amenipiga Japhet hakuna tatizo lolote nimeshamsamehe huyu kijana kwa kuwa nampenda sana kupita maelezo" alisema Flora na baada ya hapo akajiandaa kwa kuvaa vizuri na kujilemba ili aende saloon kwake asubuhi hii ya leo. 

Baada ya kuwa vizuri akatoka chumbani kwake na kuja mpaka sebuleni ambapo hakumkuta mtu yeyote akaamua kwenda jikoni huko akamkuta Rozi anapanga vyombo ndani ya Kabati. "Sasa wewe Kivuruge leo jiandae kesho alfajiri safari ya kuelekea kijijini kwenu Iringa itaanza, jioni nikirudi nitakupa Pesa yako yote ya mshahara unayoidai uondoke sitaki kukuona tena" alisema Flora kwa majivuno.

Rozi akatabasamu halafu akasema: "Hata na mimi pia sikuwa nataka tena kubakia hapa nyumbani kwako, hivyo nashukuru sana kwa kunitimizia hitaji langu" alisema Rozi. Flora hakuweza kusema kitu chochote akaubinua mdomo wake kwa dharau na kusonya halafu akaondoka.

Akataka kuondoka lakini Flora alipofika mlangoni kwa Japhet akajikuta anabisha hodi. Japhet akiwa chumbani kwake akaenda kufungua mlango na kumkuta Shemeji yake huyo akiwa anatabasamu.

"Nisamehe sana baby haikuwa Akili yangu kusema vile na kukudhalilisha, naomba unisamehe jamani Japhet" Flora alisema kwa unyonge. "Nimeshakusamehe tayari lakini naomba usiniite baby wala mpanzi, wewe ni Shemeji yangu mke wa kaka yangu kwahiyo naomba tuheshimiane" alisema Japhet kwa msisitizo.

"Basi sawa nimekuelewa lakini baadae naomba uje kule saloon kwangu tuongee vizuri Shemeji" alisema Flora.

"Nije tuongee kuhusu nini tena? kama una kitu cha kuniambia naomba uniambie hapahapa nakusikiliza" alisema Japhet.

"Mmh basi tutaongea jioni nikirudi hapa nyumbani, uwe na siku njema nakupenda sana my love Mmwaaaaaa" alisema Flora na kummwagia busu la mbali Shemeji yake Japhet. Kijana Japhet aliishia tu kumshangaa huyu Shemeji yake na kumuona kama vile amechanganyikiwa.

Baada ya Flora kuwa ameondoka kabisa kuelekea saloon kwake huku nyuma Japhet akarudi tena chumbani kwake na kujifungia mlango. Punde akausikia mlango unagongwa tena ikabidi aende kuufungua na kumuona Rozi ndie ambaye alikuwa anagonga. "Baby nakwambia hapa tayari ndio kimeshanuka" alisema Rozi huku akiingia humo chumbani.

"Kimenuka kivipi tena mpenzi wangu?" Japhet aliuliza. "Huyu Shemeji yako mcharuko kesho asubuhi anataka kunisafirisha kunirudisha kijijini kwetu Iringa" Rozi alisema huku akicheka na kwenda kuketi kitandani kwa Japhet.

"Duuh kwahiyo na wewe upo tayari kurudi kijijini kwenu?" Japhet alimuuliza Rozi.

"Nipo tayari kuondoka, lakini sipo tayari kuondoka na kukuacha wewe hapo mpenzi wangu ni lazima tuondoke wote Japhet" Rozi alisema huku akitabasamu.

"Hapana Rozi siwezi kwenda na wewe huko kijijini kwenu" Japhet alisema.

Rozi akacheka kidogo halafu akasema:

"Sio kama tutaenda kijijini kwetu Japhet, tunaondoka hapa tunaenda kupanga chumba chetu au wewe unahitaji kubakia na huyu Shemeji yako na hivi visa vyake?" Rozi aliuliza. Japhet akajifikiria kidogo na halafu akasema: "Sio kama mimi nataka kubakia hapa Rozi, lakini pesa niliyokuwa nayo ni ndogo sana haiwezi hata kupangisha chumba" alisema Japhet.

"Usiwaze kuhusu pesa baby wangu, hizi hapa ni shilingi tatu na nyingine atakuja kunipa Shemeji yako jioni leo akirudi" alisema Rozi. Japhet akuamini macho yake baada ya kuziona pesa hizo kwa Rozi. "Hivi umewezaje kuwa na pesa zote kama hizo mpenzi?" Japhet aliuliza.

"Nilikuwa naweka kidogokidogo ili nimtumie Mama huko kijijini ajengee anagalau nyumba nzuri maana nyumba yetu ni mbovu sana na inavuja wakati wa mvua zinaponyesha" alisema Rozi.

Japhet akashusha pumzi ndefu na halafu akasema: "Sasa mpenzi wangu kwa nini usimpelekee mama yako hizo pesa, kwa maisha ya hapa mjini shilingi laki tatu ni hela ndogo sana kwenda kupangia chumba na huku tukiwa hatuna hata kitanda na godoro pamoja na vyombo vidogovidogo hebu fikiria upya mpenzi" Japhet alisema na kutoa ushauri wake.

"Sikiliza Japhet ngoja nikuambie kitu maisha ni popote na Riziki anayetoa ni Mungu hivyo hatupaswi kuwa na uwoga hata kwenye boksi chini tutalala cha msingi ni tuwe kwetu na maisha yetu" alisema Rozi kwa kujiamini.

Japhet akamsogelea Rozi na kumkumbatia halafu akasema: "Yaani wewe binti ndio maana nakupenda sana unajiamini mno" alisema Japhet.

"Sasa chumba tutakipata wapi?" Rozi alimuuliza Japhet. "Mmh yaani hata sijui kwani mimi sina uzoefu kabisa hapa mjini" alisema Japhet kwa sauti ndogo.

"Mimi nafikiri tungepata chumba maeñeo ya mbali na hapa ingependeza zaidi" alishauri Rozi. Japhet akajifikiria kidogo halafu akasema: "Nimekumbuka yupo rafiki yangu mmoja tulikuwa tunaishi wote Dodoma, lakini kwa sasa na yeye yupo hapahapa mjini anaishi maeneo ya Yombo Buza sijui nimjaribu yeye labda anaweza kutusaidia kupata chumba" alisema Japhet. 

Rozi akatabasamu na halafu akasema: "Hebu jaribu kumpigia simu kama namba yake unayo atusaidie" Rozi alisema. Japhet hapohapo ikabidi achukue simu yake ndogo aina ya Tecno ile ya batani sio Smartphone aliyoletewa na Shemeji yake Flora. Japhet akapekua namba kadhaa zilizokuwa kwenye simu hiyo na kufanikiwa kuipata namba ya huyo rafiki yake na akaweza kumpigia.

Baada ya muda simu ikaweza kuita upande wa Pili na kupokelewa. "Aloo nani mwenzangu anaongea?" Sauti ya upande wa Pili ilisikika ikimuuliza hivyo Japhet.

"Oyaa Mussa ni mimi hapa Japhet wa Dodoma" alijibu Japhet. "Oohoo Japhet niambie mchizi wangu, vipi upo pande zipi?" Mussa alimuuliza Japhet.

"Mimi kwa sasa nipo huku maeneo ya Ukonga Banana kwa kaka Lukasi, sema nini mzee baba nilikuwa na shida ya kuonana na wewe siku hii ya leo" alisema Japhet. "Poa hamna noma rafiki yangu mimi nipo tu hapa nyumbani, wewe panda tu gari za Tandika zinazopitia Buza halafu teremkia kituo kinachoitwa Kanisani na baada ya hapo utanipigia simu nitakuja kukufuata" alisema Mussa.

"Daah poa sana best yangu ngoja hapa nijiandae fasta tu nitakuwa huko" alisema Japhet na kukata simu yake halafu tena akamgeukia Rozi na kumuambia: "Sasa mpenzi wangu mambo yote yako vizuri jamaa anasema niende nikamuone" alisema Japhet. "Yaani baby mwenzio hata bado sijaamini, hebu fanya haraka kamuone huyo rafiki yako" alisema Rozi huku akimkabidhi Japhet zile Pesa zote.

"Hapana mpenzi wangu usinipe Pesa zote laki tatu, nipe kwanza laki mbili " alisema Japhet na kumrudishia Rozi shilingi laki moja iliyobakia. Baada yà hapo Japhet akaenda kufungua begi lake na kutoa Pesa nyingine ni ile shilingi laki moja Pesa aliyopewa na Shemeji yake Flora siku aliyofanya naye mapenzi kwa Mara ya kwanza na sasa Pesa hiyo anampa Rozi aihifadhi. "Naomba uitunze hii Pesa mpenzi wangu itatusaidia kwa kuanzia maisha yetu tukifanikiwa kupata chumba" alisema Japhet na Rozi akaweza kuipokea. 

Baada ya hapo Japhet akajiandaa kwa kuvaa vizuri na halafu akamuaga mpenzi Wake Rozi. "Mimi ndio naondoka sasa lakini sitachelewa kurudi, kama Shemeji atarudi na kuniulizia mwambie aujui nilipoenda" alisema Japhet na baada ya hapo akaagana na Rozi kwa mabusu motomoto yaliyo na Mahaba mazito ndani yake. Japhet akaondoka zake kwenda kuonana na huyo rafiki yake aitwae Mussa. 

Hapo nyumbani akabakia Rozi akiendelea na kazi ndogondogo. "Yaani namuomba Mungu huko aendapo Japhet afanikiwe kupata hicho chumba tuondoke humu ndani tukajinafasi kwa raha zetu, tumuache huyu mwanamke na hilo pepo lake la Ngono” alijisemea Rozi huku akionekana kumchukia sana Flora.

Kijana Japhet naye akaweza kufika hadi kilipokuwa kituo cha kupandia daladala na kupanda gari ya kuelekea Tandika kwa kupitia Yombo huko anapoishi Mussa.

"Haina Jinsi itabidi nihame tu nyumbani kwa kaka yangu, haijalishi nitaishi maisha gani na Rozi huko tutakapohamia kuliko kuendelea kumsaliti kaka kwa kufanya mapenzi na Shemeji" Japhet alijisemea moyoni mwake huku akiwa ameketi kwenye siti ndani ya daladala hiyo. 

Mara ghafla simu yake ikaanza kuita ikabidi aangalie ni nani huyo anaempigia simu. Japhet alipatwa na mshtuko mkubwa sana baada ya kuona huyo anaempigia simu hiyo ni kaka yake Lukasi ambaye yupo safarini Mwanza. Japhet akajikuta anaingiwa na mchecheto kwa hofu ya kile alichokifanya na Shemeji yake (Flora) ambaye ndie mke wa kaka yake huyo. Mwishowe akajikaza na kupokea simu!.


Japhet akajikuta anaingiwa na mchecheto kwa hofu ya kile alichokifanya na Shemeji yake (Flora) ambaye ndie mke wa kaka yake huyo. Mwishowe ikabidi ajikaze na kupokea simu hiyo.

INAENDELEA

Powered by Blogger.