Simulizi : Shida Sehemu Ya Tano (5)
Ilipoishia jana..
Alex akabeba jukumu la kumwelewesha kila kitu kilichotokea mwanzo mpaka mwisho
"Nashukuru sana Alex, wewe ni binadamu wa pekee, sina cha kukulipa ila elewa umeokoa maisha yangu, nakushukulu sana" alitoa shukrani zake.
Songa nayo sasa…
Laiti Mungu angetupa uwezo wa kufahamu mioyo ya watu ikoje Amina asingetoa shukrani ile kwa Alex!!!!
Amina aliendelea na matibabu yake pale kijijini kwao na Alex mpaka akapona kabisa, baada ya matibabu ya kawaida alimueleza mganga yule juu ya tatizo lake la kutokwa na damu na mganga yule aliyekuwa amebobea katika mitishamba akapambana mpaka akafanikiwa kupata dawa iliyoonesha dalili za kuanza kumsaidia Amina
"Nashukulu sana Alex kwa moyo wako huo, angeniua baradhuli yule" Siku moja Amina aliamua kumshukulu Alex
"Usijal Amina,ila muache tabia za kupenda wanaume wenye pesa, hiyo ni tamaa mbaya sana,amini maisha ni mtu mwenyewe,unaweza ukapendana na maskini kama mimi na mkatafuta mpaka mkafanikiwa" akajibu Alex
"Najua Alex,ila ujue wakati naanza naye mahusiano sikujua kuwa yeye anapesa,nilianza naye nikijua ni mwanafunzi,pia sikujua kama kwao ni hapa hapa alinidanganya ni Arusha" akaeleza Amina.
"Sawa, we ishi hapa kama nyumbani" akajibu Alex
Matibabu ya Amina yaliendelea vizuri mpaka akapona kabisa,kipindi chote cha matibabu Alex alikuwa kalibu yake kwa kila hali,alikuwa zaidi ya rafiki ilifikia hatua baadhi ya watu pale kijijini wakajua kuwa wale vijana wana uhusiano
Hakuna sehemu ambayo hawakuambatana,iwe sokoni au kwenye mnada walikuwa wote.
Siku moja Alex aliamua kupasua ukweli wa moyo wake!
"Amina kuna kitu nataka kukuambia" akasema Alex
"Niambie Alex" akajibu
"Nahisi nisiposema nitakuwa sijajitendea haki, moyo wangu una fukuto kali sana, mahaba yananitesa, nahisi upendo huu usipofikia panapohusika nitakufa kwa pressure" akajieleza Alex
"Sijakuelewa, naona kama unanifumba kitu, niambie una maana gani?" akajibu Amina
"Amina nakupenda, nakupenda sana, tena sana, naomba usiukatili moyo wangu na ndoto zangu tafadhali" akaeleza Alex
"Mmmmmh! Alex" akaongea Amina
"Tafadhali sana, najua una maumivu ya mapenzi ila nipe nafasi nikuoneshe upendo wa dhati, tafadhali sana Amina"
"Na hii mimba itakuwaje? " akauliza Amina
"Nimekupenda kama ulivyo na kila ulichonacho, sina zaidi,nikubalie tafadhal" akamaliza Alex
Hakuna kilichozuia haya mahusiano kutokuanza, kila mmoja alikiri kumpenda mwenzake
Familia zikatia baraka na hatimaye wakaanza maisha ya mke na mme
Baada ya miezi miwili Alex akiwa na Amina walisafili na kulekea nyumbani kwao na Amina kwa ajili ya kujitambulisha.
Mapokezo hayakuwa mabaya bali ya furaha sana, Amina aliwaeleza wazazi wake kila kitu kilichomtokea tangu alipofika Dodoma mjini mpaka kukutana na Alex aliyemsaidia
"Tunashuku sana kwa moyo wako baba, tunaamini una upendo wa dhati kwa mwanetu, tunakukabidhi rasmi na muishi kwa amani, swala la mahali nendeni mpaka mtakapopata mtaleta baba, na baraka zetu ziwatangulie" akaongea baba yake.
Penye baraka za wazazi ndipo njia ya mafanikio inapoanzia, baada ya kutoka kwa wazazi wa Amina walirudi kijijini kwao kisha baada ya muda mfupi Alex akaondoka na kwenda Dodoma mjini kutafuta kibarua cha kumuwezesha kutunza familia yake.
Alipokuwa mjini alianzia kazi ya saidia fundi ila akiwa na malengo ya kuwa fundi kamili
Alifanya kazi kwa bidii huku akijitunzia akiba na baada ya muda akaweza kufanya kazi kama fundi na kipato chake kikaongezeka.
Miezi tisa ilipotimia Amina alijifungua mtoto wa kike na akaamua kumpa jina la Shida
Mme wake alipinga sana hilo jina akiamini linamtabilia mabalaa mtoto ila Amina akashikilia aitwe Shida ili iwe kumbukumbu ya yale yote aliyopitia.
Hakujua kuwa jina pia linaweza tabili yajayo kwa mtoto yeye kwake alichukulia hizo kama imani potofu
Maisha yakasonga na Alex akapata chumba kizur akamhamishia mke wake pale,na kumfungulia biashara ya genge dogo
"Mke wangu ndoto zangu ni kutajirika, naomba tujinyime na kupanua hii biashara ili tuweze kufungua zingine na hatimaye kuwa na maisha bora"
Maisha yakazidi kusonga na baada ya miaka miwili wakapata mtoto wa pili huku biashara ikizidi kukua!
Maisha yalizidi kuwanyookea sana, wakafanikiwa kufungua duka la pili kubwa la kuuza bidhaa za ndani!
Alex alizidi kupambana na maisha akiwa na malengo makubwa katika maisha yake
"Mke wangu nafikiri sasa unaamin kuwa hakuna mtu maskini dunian, umaskini mtu anautaka mwenyewe, naamin huu ni mwanzo tu, nitakuwa tajiri mkubwa sana" Alex alimwambia Amina siku moja
"Naamin hivyo mme wangu, niko nawe bega kwa bega, na nitazidi kupambana kwa ajili ya maisha haya" Akamjibu
Maisha yakaendelea kunyooka na kuwa mazuri, baada ya muda mfupi wakawa wanamiliki maduka matatu, moja la spea za pikipiki na mengine ya bidhaa za majumbani, baadae akanunua costa ndogo ikawa inafanya safari zake kwenda wilaya ya Kondoa
Walipoona mambo yanazidi kuwanyookea wakaamua kuanza kujenga nyumba, wakatafuta kiwanja Area C na kuanza ujenzi wao haraka ili wahamie katika nyumba ile.
Miaka kumi baadae
Amina na mumewe Alex walikuwa na maisha mazuri sana, pesa kwao haikuwa tatizo, walibadilisha magari jinsi walivyotaka na kuishi kwa namna waliyotaka
Mtoto Shida sasa hakuwa mtoto tena bali mtu mkubwa akiwa na miaka kumi na mitano
Alikuwa akisoma shule ya binafsi ya LOYOLA huko Dar es salaam, akiwa kidato cha pili, kwa sababu maisha yalikuwa mazuri sana uzuri wa Shida alimchanganya baba yake na mama yake, ukawa umeanza kuonekana dhahiri
Alikuwa na hipsi zilizojazia kiasi, na tumbo dogo, mguu ukiwa na mvuto wa uhakika, kiukweli alionekana mzuri sana kiasi cha kuanza kupata usumbufu kutoka kwa walimu na wanafunzi tangu akiwa kidato cha kwanza.
"Mwanangu heshima ya mwanamke ni kutulia, hawa jinsia ya kiume hata afanye uhuni kiasi gani ataonekana wa kawaida tu na ataoa anapotaka, ila sisi jinsia ya kike ukijichanganya tu watu watakupa majina ya ajabu, utaonekana hufai ndani ya jamii, tulia sana, jichunge, mtunzie mme wako bikra yako na utaheshimika" alikumbuka maneno ya mama yake
Akajitunza na hakutaka mwanamme yeyote yule awe karibu yake hata kidogo, hata ushiriki wake darasani haukuwa karibu na wanaume, alitaka ashirikiane na wasichana peke yao.
Likizo moja Shida alirudi nyumbani kusalimia na kupumzika
Baba yake wa kambo Alex ndiye aliyeenda kumpokea uwanja wa ndege
Shida alifanya kama alivyozoea, alimkimbilia baba yake na kumkumbatia kwa nguvu kuonesha upendo wake na pia jinsi alivyommis
Alivyomkumbatia tu baba yake, chuchu zake zilizosimama zikamchoma baba yake mpaka akasisimkwa
"Mmmmh! Hii balaa, huyu mtoto mbona amependeza hivi? Mmmh haya majaribu, shetani na ushindwe" aliwa Alex
Shida hakujua anayowaza baba yake huyu wa kambo,
Waliondoka kuelekea nyumbani na baba yake akamwacha pale na wadogo zake ambao tayari walisharudi likizo na yeye akarudi kwenye biashara zake
Shetani akiamua kufanya kazi kwenye akili ya mtu huwa hashindwi na ndicho kilichotokea kwa Alex, njia nzima alikuwa akiziwaza hipsi za Shida, mara akakumbuka zile chuchu zilivyomchoma kifuani, ila akapambana na zile hisia mpaka zikapotea
Likizo iliendelea vizur pale nyumbani ila kwa Alex ilikuwa shida tupu
Maisha aliyowazoesha wale watoto wake ndiyo yaliyompa shida
Shida alishazoe tangu utoto wake kuvaa vinguo vifupi sana na hata wakati mwingine vikaptula vifupi pale nyumbani, aliendelea na tabia ile bila kujishtukia kuwa keshakuwa mtu mzima,aliiona familia yake ya kizungu,hakujua baba yake wa kambo anapata wakati mgumu
Siku moja Alex alirudi nyumbani mchana kupata chakula cha mchana, akamkuta Shida kavaa kanga peke yake kiunoni na kutokana na kuwa na mzigo wa haja kule nyuma kila alipotembea alileta mtafaruku mkubwa kwa Alex
INAENDELEA