KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Simulizi : Shida Sehemu Ya Tisa (9)

Hadithi nzuri ya kusisimua ya shida

Ilipoishia jana..

Mama yake alipatwa na mshtuko mkubwa sana, hakujua afanye nini? Au aamue nini? Akabaki ameganda kama sanamu kwa muda na dakika hazikupita nyingi akaanguka chini kama mzigo

"Nesi.... Dokta...nisaidieni jaman,mama yangu" Shida alipiga kelele kuwaita Madaktari na Manesi

Songa nayo sasa…


Walipofika ilibidi waite kitanda cha wagonjwa na kumpakia kisha wakamuwahisha kwenye chumba cha wagonjwa mahututi

Huku nyuma Shida alilia sana kwa uchungu mpaka akajikuta anapoteza fahamu,alijilaumu sana kwa kumwambia mama yake ukweli ule wenye kuuma

"Ningelijua nisingemwambia jamani, Mungu wangu kama unanisikia naomba uokoe roho ya mama yangu tafadhali" alilia huku akilalama

Madaktari walianza kushughulikia mama yake na Shida haraka sana kutokana na kuonekana tatizo lake ni mshtuko wa ghafla, akawekewa gesi ya oksjeni ili imsaidie kupumua na kisha wakaanza kufanya vpimo

Presure yake ilikuwa chini sana 56/80, hali iliyolazimu madaktari kuanza kutumia vifaa vya umeme kuushtua moyo wake ili mapigo yapande na kuwa katika hali ya kawaida

"Mmmmh! Kuna uwezekano wa kupona kweli huyu?" aliuliza Daktari Aloyce mkuu wa kitengo cha magonjwa ya moyo pe Muhimbili

"Mmmmh! Hata mimi sion dalili, ila hata akipona hawezi kuepuka strock kali sana mwilini mwake" akajibu Thomas kijana aliyekuwaa kwenye mafunzo kwa vitendo

"Hapa tutegemee kudra za mwenyezi Mungu" akajibiwa na Dokta mkuu

Upande wa Shida alikuja kuzinduka masaa manne baadae, na alipokumbuka kilichotokea akaanza kulia upya

Ilibidi manesi wapate kazi mpya ya kumbembeleza mgonjwa huyu

"Niambieni ukweli,mama yangu amefariki?" aliuliza

"Hajafariki binti, we tulia na mama yako atakuwa sawa" akabembelezwa

"Jaman,nina mkosi gani mimi? Mungu nisamehe" alilalamika

Wakati wakiwa katika hayo mazungumzo,ghafla mlango ukafunguliwa na daktari akaingia na Alex

"Jaman naombeni mmpishe huyu mzee aongee na mwanaye kwanza" akaambia manes

Alipoondoka Shida aliogopa kumkabili baba take

"Mwanangu umefanya nini? Umefanya nini Shida nakuuliza?" akafoka

"Nisamehe baba, nilijikuta nimesema na mama alinibana sana, sikuwa na namna ya kujitetea bali kumwambia ukweli" akajibu

"Ukweli??? Ukweli upi sasa? Unaona athari zake? Sasa nakuambia ikitokea mama yako kafariki jiandae kuwa mke wangu" akafoka Alex

"Baba nisamehe usinilaumu, sikupanga iwe hivi mimi, Mungu wangu nisaidie" alilalama

"Mimi naondoka, siwezi kumkabili mama yako, kuna mambo mawili hapa, mama yako afe ili uchukue nafasi yake, au awe mzima wewe na yeye nisiwaone mkikanyaga kwangu milele" aliongea na kuubamiza mlango kisha akatoka

Shida alibaki akilia kwa uchungu sana, alijilaumu kwa kila kitu kilichotokea huku lawama zaidi akizitupa kwa baba yake wa kambo Alex kwa kosa la kumbaka na kusababisha hayo yote.



Upande wa chumba cha wagonjwa mahtuti, madaktari walikuwa wakichakalika kuhakikisha maisha ya yule mama hayapotei

"Jaribu kuleta mashine ili tu boost moyo wake, naona unazidi kushuka kwenye mapigo" alisema kiongozi wao

Waliendelea kuushtua moyo wa yule mama ila kila walipokuwa wakiushtua ulipiga kidogo kisha unashuka

Walijitahidi kadri ya uwezo wao wote ila mwishowe hawakuwa na jinsi bali kukubali matokeo

Wakamwacha mama yule apumzike kwa amani!!!

Alex alipatwa na wasi wasi tangu walipokutwa na mkewe wakipanga kumuua Shida ili kupoteza ushaihidi, alikubali kwa shingo upande kumpeleka Shida muhimbili kwa sababu hakuwa na namna yeyote ya kuliwepa hilo

Walipofika Muhimbili na kumkabidhi Shida mikononi mwa daktari na baadae damu kuhitajika na dokta akatoa taarifa ya swala la mimba iliyotolewa alijua mambo yameshakuwa magumu

Aliondoka pale na kuzunguka pale hospitalini akampata nesi na kumuita kando kisha akatoa bunda la pesa zaidi ya laki moja na kumkabidhi

"Kuna mgonjwa wodi ya wagonjwa mahututi amejaribu kutoa mimba, fatilia kila kinachoendelea juu yake na nipe taarifa kupitia namba hii ya simu" alimwambia nesi huku akimkabidhi Bussines card yake

"Haina tatizo mr" Nesi yule mroho wa pesa kwa kuona anacholipwa si sawa alizifundika zile pesa kwenye sidiria yake na kuondoka

Baada ya masaaa sita Alex akapokea taarifa kutoka kwa Nessi juu ya mama yake Shida kuambiwa kila kitu na mwanaye na kupoteza fahamu

"Mtafute daktari anayehusika na matibabu ya huyo mama nikija nimuone" alihitimish

Baada ya dakika chache alifika hospitalini na kweli Nesi akawa ameshaandaa utaratibu wa daktar

"Najua wewe ndiye unayehusika na yule mama, nahitaji kumuona nikiwa mwenyewe, unataka shilingi ngapi?" akauliza

"Kumuona kivip?" dokta akauliza

"Nimekwambia mwenyewe, sema unataka shilingi ngap?" aakaongea tena

"Laki mbili inatosha" dokta akajibu

Alex aliingiza mkono mfukoni na kutoa laki mbili akamkabidhi dokta

"Na bakshishi juu,nataka kufanya kazi " akasema

Dokta aliiikia kwa kutikisa kichwa na Alex akaelekezwa na nesi chumba alichokuwepo mama Amina,akaingia

Alipofika akamuangalia kwa majonzi sana kisha

"Nakupenda sana Amina ,wewe umekuwa mwanamke wa maisha yangu ila najua kwa nilichokifanya hautanisamehe, utaniacha tu na itakuwa aibu kwangu milele, hivyo sina cha kufanya zaidi ya kukunyamazisha! Kwa heri tutakutana ahera" alimaliza kuongea

Pale pale Alex alichomoa sindano na kuvuta dawa kutoka kwenye chupa ndogo kisha akamchoma nayo Amina

"Dawa hii ikichomwa kwenye mshipa vizur mgonjwa mapigo yake yatapungua taratibu mpaka atanyamaza, na madaktari watajua kuwa amekufa kwa sababu ya presure ya kushuka" alikumbuka maelekezo aliyopewa na yule daktari rafiki yake ambaye walijaribu kumtoa Shida mimba yake pamoja

Baada ya kumaliza zoezi hilo alimfata Shida kwenye chumba chake na kumkuta ameshazinduka tayali

"Mdomo wako umemponza mama yako na pia usipoangalia utakuponza na wewe pia, kwa hiyo chunga sana, tena uchunge sana" aliongea akimsukuma na kidole Shida kichwani

Alipotoka hospitalini alielekea kwa yule daktari ili kusubiri majibu ya kile alichokifanya

Haukupita muda mrefu sana simu yake ikaita na alipoangalia mpigaji alikuwa ni yule nesi, akapokea

"Kaka huku mambo si mazuri!" aliongea kwa uoga

"Kwa nini? " akauliza

"Mgonjwa wako hatunaye tena duniani, amekufa kwa sababu presure ya kushuka na iliposhuka sana tukashindwa kumzindua" akajibu Nesi

Alex alikata simu pale pale na kufurahi sana huku wakipongezana yeye na Dokta waliyesaidiana kuifanya kazi ile pamoja

"Aisee kaka nakushukulu sana,nahisi bila wewe nilikuwa niumbuke kabisa,na sijui sura yangu ningeificha wapi?" aliongea Alex

"Usijali kaka, hapa ni mwendo wa kushirikiana tu, na ukiwa na shida tena usisite kuniambia tafadhali" akajibu

Alex akazamisha mkono mfukoni na kutoa bulungutu la pesa na kumkabidhi daktari yule na kuaga!!!

Baada ya kutoka kuonana na Shida na kumpa vitisho vingi ili kuficha siri Alex alianza kupiga simu kwa ndugu, Jamaa na marafiki ili kuwataarifu juu ya msiba wa ghafra uliowakumba

Wengi walishangaa hasa wale waliomuona marehemu siku moja kabla ya kifo chake

"Mbona alikuwa mzima? Nini kimemtokea jaman?" wengi waliuliza mwaswali na jibu lilikuwa moja pekee,alipatwa na mshtuko baada ya kumkuta mwanaye akiwa mgonjwa sana na hivyo presure ikasababisha kifo chake

Maandalizi yaliendelea kufanywa kwa ajili ya mazishi ya tajiri anayetikisa mji wa Dodoma, Bwana Alex

Matajiri wakajikusanya na kuchanga pesa nyingi sana kama rambi rambi kwa Alex na familia yake!

Familia ya Amina ilipotaarifiwa waliumia sana, hasa mama yake alilia sana kumpoteza Amina, shujaa aliyebadilisha maisha yao kutoka kwenye dhiki kuu mpaka kuwa na maisha mazuri

"Mkombozi wangu ameondoka jaman!!!!!! Nani atanitunza? Nani atanibeba kama mama, nani atanitendea yote aliyonitendea mwanangu" alilalama Mama Amina kwenye msiba ule

Shida aliletwa siku ya mazishi kutoka hospitalin kwa ndege mpaka Dodoma chini ya uangalizi wa walinzi maalumu ambao waliajiliwa na Alex ili kuwa sambamba na Shida asije akatoa siri ya yote yaliyotokea kwa mtu yeyote yule

"Kwa nini mnanilinda?" aliuliza Shida

"Ni agizo kutoka kwa baba yako, hakuamin, anaogopa unaweza kuvujisha siri" akajibu mmoja wa walinzi

Hata alipofika nyumbani kwao hakupewa nafasi kubwa ya kuongea na ndugu na jamaa, alipelekwa kuwasalimia na kupeana pole peke yake kisha walinzi walimtoa pale





************
INAENDELEA
Powered by Blogger.