KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Simulizi : Shida Sehemu Ya Nane (8)

Hadithi nzuri ya kusisimua ya shida
"Mbona ulipokuwa unanibaka hukujiuliza jamii itakuchukuliaje?" akauliza Shida

"Huu sio muda wa kulumbana Shida cha msingi wewe kubali tuondoe hii aibu bana, au wee unashaurije nimuache mama yako nikuoe?" akauliza

"Mimi nataka nimwambie mama kila kitu ndipo tujue cha kufanya!" akajibu

Alex alishtuka sana kusikia vile, aliona kama msala huo unaelekea kuwa mkubwa na kufika mbali

"Hapana Shida, nakuomba sana tafadhali, achana na wazo hilo, we fikilia maisha yako, nakuahidi zawadi kubwa sana ukifanikisha hili swala" akabembeleza Alex

Simu ilikatwa pale pale na Shida na akabaki akilia sana kwa lile lililomtokea! Kwa upande wa Alex alibaki akiwa kachanganyikiwa hajui afanye nini ili kujinusuru na lile janga

Utendaji kazi wa Alex ukapungua kiasi kwamba biashara zikaanza kudorora sana, mkewe alipojaribu kudadisi kinachoendelea hakupata majibu ya kuridhisha

Alex akapanga safari za kuelekea Dar na kujaribu kumbembeleza Shida ili wafanikishe lile swala ila bado Shida hakuwa tayari kutoa mimba

"Baba mimi mama aliwahi kuniambia kuwa kwao babu alilaani kutoa mimba, na ndio maana mimba yangu ilishindikana kutoka,sasa wewe unataka tuitoe illi nife ufurahi au?" akaelezea Shida

Alex akaendelea kumshawishi kwa kumdanganya kuwa ile laana ilikuwa ya watoto peke yake na si wajukuu,ila pamoja na ushaur wote bado Shida hakuwa tayali kutoa mimba

Miezi mitatu ilipokatika mimba ya Shida ikaanza kuonekana kwa mbali sana hasa kwa mtu atakayemchungulia kwa makini sana, hapo ndipo alipoanza kuona umuhimu wa kutoa ile mimba kwani alijua atafukuzwa shule na mama yake atataka kujua ni ya nani?

Kaamua kumtafuta baba yake ili washauriane kuhusu lile swala, Alex hakuwa na pingamizi juu ya hilo alichokifanya ni kuelekea moja kwa moja Dar kwa ajili ya zoezi lile

Walienda kwenye dispensary moja maeneo ya Sinza, mahali alipoelekezwa na rafiki yake na zoezi lile likaanza

Baada ya saa moja dokta alitoka kwenye chumba chake akiwa hana amani

"Kaka mimba imegoma kutoka, na kwa bahati mbaya nilipokuwa nikimchokonoa ili itoke nahisi kiumbe kimekufa sasa sijui tufanyeje kwani nahisi tutampoteza huyu binti" alieleza kinagaubaga Daktar yule

"Dokta unasemaje? Mungu wangu mbona balaa! Tunafanyaje sasa?" akauliza Alex

Alex alichanganyikiwa sana kwa taarifa ile, alianza kukumbuka wakati Shida anamueleza kuwa mama yake alishamzuia kutoa kwa sababu babu yao alilaani

"Au ndo laana inafanya kazi Mungu nisaidie" aliwaza mwenyewe

"Hapa hakuna jinsi,inabidi tumfanyie upasuaji ili kuondoa kile kiumbe tumboni,hapo ndipo tunaweza kuwa na asilimia chache za kuweza kuokoa maisha yake" akashaur dokta

"Mimi sina neno,we fanya vyovyote vile ilimradi apone na asife" akasema

"Sasa itabidi uje utie sahihi kuruhusu upasuaji huo"

Waliongozana mpaka ndani na dokta akampa karatasi ya kusaini ili upasuaji ufanyike

Baada ya masaa matatu upasuaji ulikuwa umekamilika vizuri na dokta akatoka

"Mheshimiwa inabidi umshukulu Mungu kwani upasuaji umefanikiwa kwa asilimia zote,ila tatizo limejitokeza moja, huyu binti amepungukiwa damu kwa kiwango kikubwa sana hivyo tunahitaji damu ya kumuongezea,hivyo kama wewe ni mzazi wake twende utoe" akaeleza dokta

"Aaaah! Hapo sasa mtihani dokta,huyu mtoto sio mwanangu," alilalamika

"Itabidi umtafute mzazi wake japo mmoja ili tufanikishe hili" akashaur

"Mama yangu, sasa inabidi mama yake aje? Nitafanyaje mimi Mungu wangu,ninaumbuka sasa" aliwaza Alex

Alex alijikuta katika wakati mgumu sana,alijilaumu kwa kila kitu alichokifanya ila kwa sababu maji yalishamwagika hakuwa na cha kufanya

"Dokta labda nikwambie kitu,ila naomba uahidi kunituzia siri hii, huyu ni mtoto wa mke wangu,nilimuoa akiwa naye,nimejikuta shetani akinipitia na kufanya naye mapenzi na matokeo yake ndiyo haya unayoyaona! Hata sijui nifanyeje dokta" aliamua kuweka wazi ukweli

"Mmmmmh! Mbona pagumu sana ndugu, dah! Ntakusaidiaje?" akaongea dokta

"Dokta hapa sina cha kufanya zaidi ya kutegemea rehema zako,jitahidi utakavyoweza kupata damu au mtu wa kutoa niko tayali kutoa chochote kile" akaendelea kujitetea Alex

Daktari aliondoka na kujalibu kwa njia zake zote kutafuta namna ya kufanya ila hakufanikiwa

"Mheshimiwa hapa cha msingi mlete mama yake atoe damu,cha muhimu ni kutunza siri,mimi nitajua cha kumweleza" akashaur daktar

Alex hakuwa na jinsi zaidi ya kumpigia simu mke wake ili aje haraka,hakutaa kumwambia kinachoendelea

"Cha msingi wewe nenda upande ndege uondoke haraka na kuja huku,kuna dharura kuhusu mwanao,mengine utayajua huku huku" alifoka Alex

Amina mama yake na Shida hakuwa na cha kufanya bali kufata maagizo na moja kwa moja alielekea uwanja wa ndege na kupanda ndege mpaka Dar es salaam

Upande wa Daktari na Alex hali ilikuwa tete sana, Shida alizidiwa na kuanza kutapika mabonge ya damu mfululizo

"Alex hapa sina cha kufanya, hali ilipofikia inabidi huyu mtoto tukubali afe ili kutunza siri hii, tofauti na hivyo inabidi umpeleke Muhimbili akatibiwe na ikitokea ukafanya hivyo itajulikana kuwa katolewa mimba, hilo litaniweka hatiani mimi na wewe" aliongea Daktari

"Mmmmh! Mbona mtihani huo dokra......." hakumalizia kuongea na pale akawa kaingia Amina na kuwakuta wakijadiliana na Shida akiendelea kutapika damu

"Mme wangu kuna nini?....na mbona hali ya mtoto ni mbaya na hujampeleka kwenye hospital kubwa?" aliingilia maongezi

Waliona aibu na kujitetea kitoto sana, na kwa sababu yule mama alikuwa keshapaniki wakatafuta gari na Amina akambeba mwanae na safari ya kuelekea Muhimbili ikaanza

Walipokelewa na Shida akaingizwa chumba cha wagonjwa mahututi,huku Alex akienda kuandikisha

"Mpaka mgonjwa anazidiwa hivi mlikuwa wapi jaman? Na mbona anatokwa sana damu,amekuwaje?" waliuliza madaftar

"Tunaomba mmuhudumie jaman, mengine tutaongea" akajibu Alex

Muda wote huo Amina hakupata nafasi ya kupata maelezo ya nini kilichotokea

"Samahan, naomba mzazi wa binti aingie chimba cha vipimo ili apimwe kwa ajili ya kumtolea binti damu kwani amepoteza damu nyingi sana kwenye jaribio lake hili" aliongea Dokta

"Kwani anatatizo gani dokta?" akauliza Amina

"Ina maana hamjui? Mwanenu ametoa mimba kubwa sana na amepoteza damu nyingi sana" akajibu

Amina alishtuka sana kwa kile alichokisikia, aligeuka na kumwangalia mmewe ambaye aliinama chini

"Jaman hakuna muda wa kushangaa hapa,anayeingia aingie" alifoka daktar

Amina aliingia na kuchukuliwa vipimo na kwa bahati nzur damu yake ikakutwa iko sawa na inaweza kuongezewa mwanaye,alitolewa damu na ikaongezwa kwa Shida

Alipotoka pale hakumkuta Alex mmewe kwenye eneo la mapumziko hivyo alikaa mwenyewe akiwaza imekuwaje mwanaye kapata ujauzito,alipojalibu kupiga namba ya simu ya mmewe ikawa haipatikan

Baada ya masaa matatu yakusubiri hatimaye Shida alipata fahamu zake na mama yake akapewaa ruhusa ya kwenda kumwona

Alipoingia ndani

"Mama jitahidi usiongee vitu vitakavyomkwaza huyu binti kwa sababu hali yake sio nzuri kabisa" Dokta alitahadhalisha

Amina aliingia na walipogongana macho na mwanaye Shida alishtuka na machozi yakaanza kumtoka mfululizo

"Nisamehe mama yangu, sikupanga hili litokee" aliongea kwa hisia

"Usijali mwanangu, tumshukuru Mungu umepona na unaendelea vizur, vipi lakin uko sawa kiasi cha kunieleza yaliyokukuta mama?" akaongea kwa upole

Shida aliangua kilio kwa muda mrefu sana huku mama yake akimbembeleza anyamaze

"Baba.....baba...ba...ba ni baba mama" alijibu huku akili.

"Mwanangu ujue sijakuelewa vizur,em rudia tena na uache kulia,nani kakupa hii mimba?" akauliza

"Nisamehe mama, sio maksud alinibaka" aliendelea kusema huku akilia

"Sawa mwanangu,ila sijajua nan huyo?" mama akauliza

"Mama nisameehe mimi, nilibakwa mama" akaendelea kuongea huku akilia

"Haya nyamaza mwanangu na uniambie vizuir, nimekusamehe, nani alikubaka ? Na lin? Na ilikuwaje?" akauliza

"Mama baba alinibaka" akajibu Shida

Mama yake alipatwa na mshtuko mkubwa sana, hakujua afanye nini? Au aamue nini? Akabaki ameganda kama sanamu kwa muda na dakika hazikupita nyingi akaanguka chini kama mzigo

"Nesi.... Dokta...nisaidieni jaman,mama yangu" Shida alipiga kelele kuwaita Madaktari na Manesi

************


:: Unavyodhani nini kitaendelea?



:: Hii ni mojawapo ya riwaya kali sana kutoka kwa mwandishi chipukizi hapa uwanja wa simulizi.



ITAENDELEA

Powered by Blogger.