KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Kwanza (01)

simulizi ya penzi la mfungwa
Ilikuwa muda wa saa nane usiku zilisikika sauti za wanakijiji wakipiga mayowe.."mwizi mwizii mwizii..", sauti hizo zilitambaa kwa kasi ya ajabu usiku ule kitendo ambacho kiliwafanya wanakijiji waliokuwa wamelala wakaamka ili kumkimbiza mwizi huyo ambaye kimuonekano alionekana kuwa shapu na kasi ya ajabu,alifanikiwa kuruka vigingi mbali mbali akatoka kijijini akakimbilia nje ya kijiji akatokomea kunako mashamba yaliyokuwa kando ya kijiji hicho. 

Hapo mwizi huyo akawa amefanikiwa kuwatoka hao wanakijiji walioonekana kuwa na hasira kali kwani baada kutokemea nje ya kijiji,walibaki kujilaumu huku kila mmoja akiwa na hamu ya kumkata ili wamuadabishe jambo ambalo lilienda kinyume na malengo yao. Mwizi aliwapotea. Baada mwizi kufanikiwa kuwatoka,wanakijiji waliamua kurudi majumbani kwao. 

Kesho yake asubuhi palipo pambazuka mwenyekiti wa kijiji alimtaka mjumbe wake apige mbiyu kuitisha mkutano wa kijiji kwa maana siku hiyo palikuwa na agenda mbali mbali alizotaka kusema na wanakijiji hasa kuhusu suala hilo la wizi kushamili kijijini kwake,lakini wakati mbiyu hiyo inapasa kijiji hapo,upande wa pili alionekana kijana Zabroni akiwa ndani ya nyumba yao ambayo ilikuwa imejengwa na miti ikiparatwa udongo huku juu ikiwa imeezekwa nyasi. 

Kijana Zabroni alikuwa chumbani akihesabu fedha alizopora kwenye duka la muhindi mmoja hapo kijijini kwao,ila kabla hajafikia tamati akasikia mama yake akimuita ikabidi asitishe zoezi hilo haraka sana akazipiga hatua kutii wito wa mama yake ambaye wakati wote alikuwa ni mtu wa kitandani akiugulia ugonjwa wake wa kupolalazi mwili. 

"Naam mama", aliitika Zabroni baada kumfikia mama yake. Mama Zabroni alipomuona mwanaye kafika, alimtazama kisha akasema "Zabro mwanangu,mimi mama yako tayari nimesha jihakikishia umauti. Huna sababu ya kuendelea kuiba mali za watu ili kuokoa maisha yangu. Tafadhali naomba uachane na hiyo shuguli utakufa kingali kijana mwanangu,fanya kazi za kilimo ili upate fedha za matumizi ya kawaida kwani mama yako sio waleo wala wakesho. Sikia mbiyu imelia,na hii ni kutokana na tukio la jana la wizi..

 najua niwewe hakuna mwingine mwizi hapa kijijini. Sasa unajua kwenye huo mkutano watakuwekea agenda gani? Za mwizi ni arobaini mwanangu achana na kazi hiyo wizi haufai baba ", alisema mama Zabroni kwa sauti ya chini kabisa, maneno hayo yalimuumiza sana kijana huyo akajikuta akidondosha chozi kwa uchungu. Ila yote kwa yote Zabroni aliamua kukubaliana na matakwa ya mama yake ili apate kumlizisha kulingana na hali tete aliyonayo, kamwe hapendi kumuona mama yake akikereka. 

"Sawa mama nimekuelewa " alijibu Zabroni kisha akaamka akarudi chumbani kwake kuendelea na zoezi lake la kuhesabu fedha alizoiba usiku wa jana kwanye duka la muhindi kijiji hapo. Alipo zihesabu hizo fedha akakuta ni kiasi cha pesa shilingi laki nane. Hakika alifurahi sana akajikuta akisema"Lakini nane..pesa nyingi sana hizi,mpambanaji haogopi masikini hachoki..nitaendelea kuiba mpaka nitimize pesa ya kumsafirisha mama yangu aende kutibiwa nje ya nchi", kwisha kujisemea hayo akazikusanya fedha hizo akaziweka kwenye mfuko akaingia ufunguni ambapo palikuwa na shimo,huko akawa amezifukia fedha hizo pasipo mtu yoyote kujua zaidi yake yeye. Alipomaliza hilo zoezi alitoka ndani ghafla akakutana uso kwa uso na baba yake mzazi akiwa amelowa umande. 

Zabroni akamuuliza baba yake "Baba kulikoni mbona umelowa umande asubuhi yote hii?..", mzee huyo hakujimjibu kijana wake zaidi alizama ndani moja kwa moja mpaka chumbani kwake ambapo alipofika akamtazama mkewe kwa jicho la huzuni, akasikitika sana, ndani ya nafsi yake akajiuliza "Hivi nimemkosea nini Mungu?.." swali hilo lake liliambatana na mchirizi wa chozi.baada chozi hilo alijisonya kitendo ambacho kilimfanya mkewe kumgeukia na kisha kusema "Baba Zabroni kulikoni? kuna nini mume wangu?.."



"Loh! mke wangu nahisi kama dunia imenitenga,kila ninalo lifanya haliendi sawa mpaka muda mwingine najikuta namkufuru mungu kwa kunileta duniani"



"Unaamaana gani?..", akiwa na taharuki alihoji mama Zabroni lakini kabla hajamjibu mkewe,mara ghafla nje ya nyumba yake alisikia mtu akabisha hodi. Baba Zabroni alistuka zaidi hofu ilimjaa akamtazama mkewe kisha akasema "Subiri nikamsikilize kwanza huyu mtu, nakuja sasa hivi", alipokwisha kusema hivyo akatii wito. Hofu na woga ulimjaa baada kufika nje akamkuta ni mzee Fungafunga mdeni wake. "Habari yako bwana Ndalo" Fungafunga alimsalimu baba Zabroni. Mzee Ndalo akainamisha uso wake chini,papo hapo swali likamjia kichwani "Nitamueleza nini leo? Muda nilio muahidi kumlipa pesa zake umewadiwa?.." kwisha kujiuliza hilo swali akaitikia salamu ile "Ni salama tu ingawa sio sana"



"Kwanini? Bado mkewe hali tete?.."



"Ndio bwana hata hivyo nafikiria kukopa pesa nyingine kwa mzee Malila ili niweze kumsafirisha kwenda mbali kidogo na hapa. Nimeambiwa kuna mtaalamu mmoja hivi anaweza kunisaidia "



"Sawa lakini yote kwa yote mzee Ndalo nataka pesa yangu.." alisema mzee Fungafunga huku akiwa amekasirika pasipo mfano. Baba Zabloni akastuka kumuona mzee mwenzake akiwa amemkasirikia punde tu. Hapo akajikuta hana la kufanya,pesa ndani hakuwa nazo nawala hakujua kama usiku wa jana mwanae kaiba pesa nyingi ambazo anaweza kulipa hilo deni na nyingine zikabaki. "Doh nitafanya nini mimi?", alijiuliza mzee Ndalo,akamtazama mzee Fungafunga kisha akasema "Mzee mwenzangu kwa leo nimekwama tafadhali njoo kesho basi uhakika upo! 

Nipo chini ya miguu yako tafadhali ", mzee Ndelo hakuwa mzito kumpigia magoti mzee Fungafunga ili kudhihilisha kile anacho kisema lakini mzee Fungafunga katu hakutaka kuelewa propganda za mzee Ndalo na ndipo alipochomoa kibiriti kutoka kwenye mfuko wa koti lake kukuu akawasha sigara kisha akasema "Sikia we masikini,ulikuja kwa mikono miwili kuomba msaada lakini malipo unasumbua kulipa. Sasa nakupa dakika tano uwe umeleta pesa yangu hapa la sivyo nachoma kibanda chako.." alisema mzee huyo huku akipuliza moshi wa sigara. 

Mzee Ndalo alishusha pumzi,pesa hana je atafanya nini ilihali mzee Fungafunga hataki kumuelewa? Akaona hakuna namna akiwa katika hali ya unyonge aliingia ndani akakata kamba aliyokuwa akiwekea nguo Zabroni kisha akajinyonga, aliona hana mbinu nyingine ya kujinusuru mbele ya mzee Fungafunga. Nje mzee Fungafunga alibaki kusubiri akidhania kuwa mzee Ndelo ameingia ndani kumchukulia pesa yake. 

Muda ulisogea mzee Ndalo hatoki ndani, hatimaye mzee Fungafunga ikamjia akili ya ghafla akadhania kwamba huwenda mzee Ndalo kamtoroka kupitia mlango wa uwani na ndipo alipoamua kuchoma nyumba moto ikiwa ndani yumo mzee Ndalo ambae tayari marehemu pia mama Zabroni ambaye ni mgonjwa hajiwezi. 

Moto ulitembaa kwa kasi kisha mzee Fungafunga akaondoka zake. Punde baada mzee huyo kutokomea muda huo huo Zabroni naye alikuwa njiani akirudi nyumbani baada kutoka kijiweni kusikilizia watu wanazungumziaje wizi uliofanyika usiku wa jana huku mwizi akiwa ni yeye mwenyewe.

INAENDELEA

Powered by Blogger.