KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Pili (02)

simulizi ya penzi la mfungwa
mwandishi alex wamilazo king
Moshi mzito ulioambatana na kipupwe cha aina yake ulipaa angani kwa kasi huku Zabroni naye akizidi kupiga hatua kurudi nyumbani ilihali ndani ya hiyo nyumba inayoteketea kwa moto ilisikika sauti ya mama Zabroni akipiga mayowe kuomba msaada,lakini kulingana na kuugua kwa kipindi kirefu,ilimfanya sauti yake isikike kwa mbali sana kiasi kwamba mtu aliyepo hatua kumi na tano mbele asingeweze kusikia mayowe hayo. 

Nyumba ilizidi kupamba moto,mama Zabroni akakosa msaada akafa namna hiyo hali ya kuwa mwili wa mzee Ndalo ambaye naye alikuwa ameshajinyonga nao uliungua,kamba ikakatika mwili wake ukazidi kuteketea ukiwa chini. 

Zabroni alistuka kuona moshi mkali ukitanda angani,moshi huo ukitokea nyumbani kwao. Hali hiyo ilimfanya kohofia usalama wa nyumbani kwao haraka sana alitimua mbio ili ajue kipi kinachoendelea. "Lahaula" alipigwa na butwaa baada kukuta moto ukiishia huku fito zilizoungua nazo zikidondoka chini. 

Alipagawa,alipasa sauti kumuita mama yake na baba yake lakini harufu ya miili ya wazazi yake iliyoungua ilimfanya Zabroni kuamini kuwa mama yake kaungulia ndani kwani alijua fika kwa hali aliyokuwa nayo mama yake kamwe asingeweza kujinasua kwenye moto huo. 

Alilia kwa uchungu Zabroni,akajiuliza wapi alipo baba yake? Wakati anajiuliza swali hilo miguu yake ilionyesha kukosa nguvu,usongo wa mawazo wa kifo hicho cha mama yake ulimfanya apoteze fahamu bila kutambua kuwa si mama yake tu aliyefariki bali na baba yake pia.

Wakati tukio hilo linatokea, ghafla anaonekana mzee Maboso akiwa ametokea shamba. Mzee huyo ni jirani wa marehemu mzee Ndelo. Alistushwa na kile alichokiona,Maboso akastaajabu sana kuona nyumba ya mzee mwenzake ikiwa imeteketea kwa moto,haraka sana akatupa jembe na panga chini akasogea jirani zaidi ili aangalie kama kapona mtu hasa hasa mama yake Zabroni ambaye alifahamu fika mama huyo hajiwezi. Lakini kabla hajasogea alimuona Zabroni chini akiwa amepoteza fahamu. 

Hapo alisitisha kwanza safari yake ya kwenda kujua kama kuna mtu kapona kwenye moto huo akasogea kumuangalia Zabroni, napo alisimama baada kukuta Zabroni kuzimia. Pumzi alishusha Maboso,akiwa na hofu akaendelea kuzipiga hatua za pole pole mpaka mahali ilipo teketea nyumba. 

"Mungu wangu", mzee Maboso alipagawa baada kuona mwili wa mama Zabroni ukiwa umeungua,alipo tazama upande wa pili akauona mwili wa mzee Ndalo nao ukiwa hivyo hivyo umeungua. Mzee Maboso alisafa,akatazama kulia na kushoto alitimua mbio za kizee kuelekea kwa mwenyekiti wa kijiji kutoa taarifa juu ya maafa yaliyotokea. 

Alipofika hakumkuta mwenyekiti alimkuta mkewe naye alikuwa akijiandaa kwenda kisimani. Mke wa mwenyekiti alipomuona mzee Maboso kaja hima hima alisimama, kwa mshangao akauliza "Vipi kwema huko?.."

"Hapana sio kwema Siwema", alijibu mzee Maboso huku akihema haraka haraka.

"Mmh inamaana jina la mwanangu hulijui mpaka unitaje jina langu? Hebu tengua kauli yako halafu ueleze kinacho kusibu"

"Sawa, samahani sana. Yote kwa yote Mwenyekiti nimemkuta?.."

"Walaa hapana kaenda kukagulia mashamba yake ila muda sio mrefu atarudi,siunajua leo kuna mkutano wa kijiji? Kunani mzee Maboso? "

"La! Hili ni balaa asikwambie mtu mzee Ndalo na mkewe wamefariki kwa ajari ya moto"

"Mungu wangu weee! Imekuwaje sasa jamani!?.." mke wa mwenyekiti aliuliza huku akisikitika. Mzee Maboso akaishusha pumzi yake kisha akajibu.

"Doh we acha tu,ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni. Zabroni naye kazimia,yani hata sijui ni kitu gani kimepita kwenye familia ile"

"Sawa acha mimi nikamwambie mjumbe apige mbiyu ya msiba ", aliongeza kusema mzee Maboso na mara moja akaelekea kwa mjumbe kumpa taarifa.

Alimkuta mjumbe akitengeneza baiskeli yake,baada ya salamu akamueleza kila kitu kilichojili. Mjumbe alimtazama mzee Maboso kwa jicho la husda kisha akasema." Kwahiyo nikishatoa taarifa wewe utafaidika nini?..", Maboso alistushwa na maneno hayo aliyoongea Mjumbe.

"Unamaana gani sasa? Mbona sikuelewi!..", akiendelea kumshangaa mzee Maboso alihoji. Mjumbe hakujibu zaidi aliacha zoezi lake la kutengeneza baiskeli akaingia ndani. Punde akatoka na mbuyu mkononi mwake, akaitupa mbele ya mzee Maboso kisha akasema

"Mbiyu hiyo hapo tangaza mwenyewe, toka zamani mimi na mzee Ndalo ni maadai kwahiyo siwezi kupoteza muda wangu mimi" kwisha kusema hivyo akaendelea na kazi yake ya kutengeneza baiskeli. Mzee Maboso alimtazama,akaona hakuna haja ya kumbembeleza akaondoka zake. Ila kabla hajafika mbali,mara ghafla nyumbani kwa mjumbe akaja mzee Fungafunga. Mzee huyo akacheka sana kisha akasema "Mzee mwenzangu wewe ni mwanaume na unamsimamo wa kiume"

"Kwanini bwana" alihoji mjumbe.

"Kukataa kupiga mbiyu hapo upo sawa,Ndalo hafai abadani ", alijibu Fungafunga akimwambia mjumbe,Mjumbe akafurahi sana kupata ujiko kwa mzee Fungafunga asijue Fungafunga ndio muhusika mkuu wa tukio la mauaji ya mzee Ndalo pamoja na mkewe.

INAENDELEA
Powered by Blogger.