SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Ishirini na Tatu (23) MWISHOO
Hatimaye walifika ukumbini,ndani ya dakika kadhaa alipanda ulingoni. Bei zalitajwa kati ya Derick na Karani. Wakati huo Zabroni akijua mtu anayetarajia kukutana naye kwenye mpambano huo,huku mr Rasi ama Bruno yeye akiwa hatambui ni nani anayekutana naye. Lakini punde si punde Rasi alipopanda ulingoni alimtambua. Ni Zabroni.
Yule yule aliyekuwa akimtafuta kwa udi na uvumba pasipo kumpata ikiwa muda huo huo matajiri walifikia muafaka,ndondi zilianza huku Mr Rasi akiwa na nguvu mpya na hali mpya baada kumuona mbaya wake. Na kabla hajarusha ngumi,alisema "Naitwa Bruno,nimetoroka mahabusu kwa ajili yako. Unamkumbuka Madebe?..".
"Maneno mengi humaliza vitendo, Ulivamia vita isiyokuhusu. Lakini kwa kuwa tumekutana kwa mara nyingine tena basi acha nikuadanishe. Ili azma yangu itimie. Unakumbuka kama nilikusamehe kipindi kile ? Sasa hatimaye tumekutana upya",alijibu kwa kujiamini kabisa Zabroni kisha ngumi zikaanza huku shangwe nazo za hapa na pale zikisikika, Bruno alionekana kutawala ulingo kwa sababu alikuwa na ile nguvu ya kupotea na kuibukia sehemu nyingine. Ila Zabroni alitumia nguvu ya hirizi aliyokuwa nayo ambapo aliweza kurusha ngumi nzito kiasi kwamba mpambano ule ukaonekana ni wa watu walikuubuhu. Wataalamu wa kupigana.
Wakati ugomvi huo unaendelea,upande wa pili Lina kuna kitu alikisahau,hivyo ilimbidi arudi mara moja nyumbani. Alipofika aliona damu nyingi ikiwa imesambaa kwenye sakafu,alistuka lakini alizidi kusonga mbele na hatimaye akamkuta Veronica akiwa ameuwawa kikatili. "RAMSOOO? ", alijiuliza Lina huku akiwa na taharuki kubwa moyoni mwake.
Wakati Lina yupo kwenye kwenye hofu dhufo lihari akishindwa kuamini kile akionacho, kwingineko napo pambano lilizidi kupamba moto Tina akiwa jukwaani akitamani sana Mr Rasi ammalize Zabroni ili iwe kama njia ya kulipiza kisasi cha kuwauwa aliwaua wazazi wake mzee Fungafunga na mkewe,na ndio maana siku hiyo Tina akawa anatamani Bruno amuadabishe Zabroni akiamini kuwa walau moyo wake utaridhika.
Pindi Tina anatamani kitu hicho kiweze kutokea, upande wa Zabroni naye alikuwa akifanya jitihada za kusaka ujiko mbele ya Tina ili ajue kwamba bado yeye ni mwamba ulioshindikanika. Hakika ulikuwa mpambano mzuri sana,lakini ghafla polisi walifika kwenye tukio,walipiga risasi juu watu wakasambaaa.
Mlio huo wa risasi ulimstua Bruno ukawa umemtoka mchezoni,nafasi hiyo Zabroni aliitumia kurusha ngumi kwa kutumia mkono wake wenye hirizi, ngumi hiyo ilipomfikia Mr Rasi alianguka chini kisha mapovu yakaanza kumtoka huku akirusha miguu huku na kule.
Ilikuwa ngumi nzito yenye uchawi ndani yake. Amri ilisikika kutoka kwa jeshi la polisi lililofika mahali hapo,walimkamata Zabroni pia na Karani ikiwa Derick yeye alifanikiwa kukimbia.
Moja kwa moja watu hao wakafikishwa mbaloni ambapo walimkuta Afande Jimmy tayari yupo mikononi mwa mkono wa dora baada kubainika kuwa anaishi na mfungwa aliyetoroka jela kinyemela. Zabroni alipomuona baba yake mkwe yupo chini ya ulinzi makali alitambua fika kuwa yeye ndio chanzo cha hilo tatizo, hivyo aliweka bayana kuwa yupo tayari kwa chochote watakacho mfanyia ilimradi kamanda Jimmy wamuache huru ilihari moyoni akijisemea kuwa azmaa yake nimehitishi hakuna cha kupoteza.
punde Lina akatokea hapo kituoni kwa sauti kali akasema "Ramso kumbe wewe muuwaji,kwanini umemuua Veronica? Kwanini lakini. Amekukosea nini " ,alihoji Lina kwa sauti ya kilio,muda huo huo nyuma yake Lina alitokea Tina.
Naye akasema huku akilia kwa uchungu "Zabroni, mwanaume gani wewe? Mbona mkatili sana. Umeniulia wazazi wangu,leo hii umemuuwa na mpenzi wangu kwanini Zabroni kwanini lakini...".
Zabroni hakujibu, alinyamanza kimya,habari ya kifo cha Bruno kikimuacha mdomo wazi, akajisemea "Inamaana Bruno naye kafa? Laah! sikutegemea ingawa ni moja ya kisasi cha rafiki yangu Bukulu. Mungu anisamehe",alijisemea hivyo Zabroni wakati huo huo Lina akachomoa bastola kutoka kwa polisi mmoja aliyekuwepo karibu yake kisha akajiwekea kichwani na kisha kusema "Ahsante Ramso kwa mshahara wako,siwezi kuvumilia hii fedhaha..
Kwanini umekuwa na roho mbaya namna hii? Siwezi siwezi kabisa kuishi najiua, ", Lina alipokwisha kusema hivyo akajivyatulia risasi. Zabroni hakuamini machoni mwake, akataharuki sana kwa sauti ya juu akasema "Hapanaaaa Lina usifanye hivyo"
"Hapana Linaaaa",hapo ghafla akazinduka baada kupoteza fahamu kwa muda mrefu. Jopo la madaktari liliingia wodin kumtazama mgonjwa wao aliyekuwa amepoteza kumbukumbu kwa muda wa siku tatu.
Walimkuta akiwa ameketi kitandani huku akihema haraka haraka, mapigo ya moyo wake yalienda mbio kama saa mbovu ilihari kijasho chembamba nacho kikiuosha mwili wake. Pumzi ndefu akashusha, macho yake akayainua kutazama huku na kule na mwishowe kujikuta akiwa katika hali ya sintofahamu baada kugundua yupo Hospital.
"Hali yako?", sauti ya Dokta ilisikika akimuuliza Zabroni. Zabroni huku akisafa akajibu "Njema tu, aah unaweza kuniambia nimefikaje fikaje mahali hapa?.."
"Ndio, uliletwa ukiwa hujitambui. Ulizimia", Zabroni akataharuki kusikia habari hiyo, ndani ya kichwa chake akajiuliza "Inamaana kumbe yote yale nilikuwa nimezimia?..", hakika alijikuta amepoa mithiri ya maji ya mtungini wakati huo akikumbuka mara ya mwisho kabla hajapoteza fahamu alikuwa na nani na pia alifanya nini.
Akakumbuka kuwa alikuwa na mzee Maboso raia kutoka Nchini Nigeria, na walikuwa katika ufukwe wa ziwa Victoria saa za jioni wakijiandaa kuingia kuvua samaki, lakini kabla hawajaingia mzee Maboso akawa amemwambia Zabroni kuwa ziwani kuna mambo mengi sana, kwa maana hiyo si rahisi kuingia pasipo kupakwa dawa ambayo itamrinda na mauza uza ya baharini.
"Sawa mzee wangu mimi nakusikiliza wewe tu, kwa sababu siku zote ukitaka kuruka sharti uagane na nyonga", alijibu Zabroni. Mzee Maboso, mzee ambaye kwenye safari ile ya kulipa kisasi cha kifo cha wazazi wake alimpatia dawa ya kupotea kimazingara, aliangua kicheko kisha akasema "Ni kweli kabisa, lakini yakupasa kujiamini ili ikuwee vyepesi kuzoea hii shughuli"
"Sawa", Zabroni akawa tayari kupakwa dawa ile ambayo mahususi kuzuia janga litakalo tokea ziwani. Mzee Maboso akampaka Zabroni dawa katika paji la uso wake na mikononi pia, na baada zoezi hilo kukamilika ghafla Zabroni akahisi kizungu zungu, baadaye hakujua kilicho mpaka pale alipojikuta yupo wodini huku akiwa ameota mambo ya ajabu sana.
BAADA SIKU TATU
Aliruhusiwa kurudi nyumbani, siku hiyo alilala usingizi mzito. Na pindi alipokuwa amesinzia mambo yale yale yakajirudia kwa mara nyingine tena katika ndoto kwa matukio tofauti tofauti. Ndoto ya ajabu kabisa kuwahi tokea kwa kijana huyo. Ndoto ambayo alianza kuiota usiku wa jana yake yake saa tatu alipopitiwa na lepe la usingizi,usingizi ambao alilala fo fo fo kutokana uchovu mwingi aliokuwa nao baada kutoka Hospital,alihema kwa nguvu baada kutoka usingizini,siku hiyo alichelewa pia kuamka.
Akiwa kitandani anaitafakari ndoto hiyo,alisikia sauti ya mtu akibisha hodi. Zabroni aliamka akaenda kumsikiliza. Ni Tina mpenzi wake,alikuja kumjulia hali baada kusikia kwamba amerejea kutoka Hospital.
"Khe Zabroni wangu, pole kwa maswahibu?..", alisema Tina ambaye alimuota akiwa amehamisha mapenzi yake kwa Bruno ama Mr Rasi.
"Daah we acha tu Tina,kwanza baba na mama yako wazima?..",alijibu Zabroni huku akiacha na swali ambalo liliambatana na miayo.
"Ndio kwani vipi kuna tatizo?.."
"Hapana, hakuna tatizo",alijibu Zabroni.
"Mmmh! Unanificha wewe hebu niambie ukweli wako basi "
"Tina usihofu hakuna tatizo"
"Sawa, nimepita tu kukujulia hali. Naelekea kisimani kuchota maji.."
"Sawa baadae basi",alikatisha maongezi Zabroni kisha akarudi ndani kuitafakali ndoto hiyo na ukweli wa kuhusu mzee Maboso.
"Ndoto hii? Inamana gani?. Na huyu mzee Maboso alifanyia kitu gani hasa Loh! Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni.
Naam! Leo nimepata kujionea maajabu makubwa katika ulimwengu usio wa kawaida" Yote hayo Zabroni alikuwa akijisemea ndani ya kichwa chake. Na baadahe jioni alitembea kijiji kizima, alipita hasa zile nyumba ambazo kwenye ndoto aliota kuwa amechoma moto. Alikuta zipo salama salimini.
Vile vile alipita nyumbani kwa mama yule mjamzito ambaye kwenye ndoto aliota kwamba kamtumbua mimba yake. Hapo alikuta umati wa wamama wakiwa nje, kwa mbali Zabroni alisikia kuwa huyo mama amejifungua mtoto wa kike.
Zabroni alishusha pumzi kisha akaendelea na safari moja kwa moja alielekea mpaka kijiweni, huko sasa alikutana na kundi la vijana wakipiga zogo huku birika lenye chai ya tangawizi likiwa mbele yao. Katika vijana hao alikuwemo na Bluyner,kijana ambaye Zabroni alimuota kwamba Bluyner ni nyampara gerezani. Nyampala ambaye alimpa taabu sana kwa kumkosesha amani gerezani.
"Zabroni,pole sana kwa matatizo bwana", alisema Bluyner. Zabroni alibaki kushangaa tu huku akilini bado akiitafakari ile ndoto. Alikaa kijiweni dakika kadhaa kisha akarudi nyumbani kwao kutuliza akili, alipokuwa njiani kabla hajafika nyumbani kwao alikutana na mzee Maboso,mzee ambaye alilowea Tanzania ila mzawa wa Nchini Nigeria. K
wenye ndoto Zabroni alimuota mzee huyo kuwa alimpatia dawa ambayo ilimfanya awe mtu wa kupotea katika mazingira yoyote,lakini pia awe mtu mwenye nguvu za ajabu. Zabroni alimsalimia mzee Maboso, Maboso akaitikia salamu hiyo kisha akasema "Pole sana kijana wangu ila kuna jambo nitakueleza".
"Jambo gani hilo?", Zabroni akauuliza kwa mashaka.
"Ahahah usijali ondoa papara ila leo soka limechezwa kwa uzuri kabisa. Timu yetu ya kijiji imeshinda lakini tuwashukuru wale vijana wageni walee..Bruno na kaka yake Madebe. Loh! Vijana wale wanajua sana soka sio mchezo. Nafikiri Miembeni wamewatambua vizuri",aliongeza kusema hivyo Mzee Maboso huku akicheka. "Bruno?..Madebe?.." Zabroni alijiuliza majina hayo, kwenye ndoto aliota namna gani walivyompa shida vijana hao ambao walikuja kijijini kwao kutafuta maisha kwa kulima vibarua, ambapo mwishowe wakajiingiza kwenye vita isiyowahusu.
"Unataka kuniambia hawa wageni ndio wametusaidia?..",aliuliza Zabroni kwa wasi wasi. Mzee Maboso alijibu "Haswaa, na huyu Bruno kapiga mpira mwingi sana. Mpaka kuna mwanadada mmoja hivi amempatia pesa"
"Nani huyo?..", alihoji Zabroni.
"Kwa jina nimesikia anaitwa Veronica, ni binti fulani hivi mgeni alikuja kushuhudia mchezo wa leo"
"Veronica?"
"Ndio! Kwani unamfahamu?..
"Hapana", alikataa Zabroni ila alijua fika ni Veronica mwadada ambaye kwenye ndoto aliota namna alivyomtia hatiani baada kumuamini katika mapenzi..
"Na sio huyo tu, Zabroni umekosa vingi. Ukweli mchezo wa lao ulijaza mabinti wengi. Nafikiri ungelikuwepo ungepata ujiko. Yupo binti mmoja hivi zamani kidogo aliondoka baada wazazi wake kuhamia mjini. Lina.
Sijui unakumbuka? Naye alikuwepo pia ..", aliongeza kusema mzee Maboso huku akimaliza kwa kicheko. Ni jambo ambalo lilizidi kumshangaa mno Zabro na baada ya hapo waliagana,Zabroni aliendelea na safari yake ilihali mzee Maboso naye aliendelea na safari yake. Hapo walau furaha ikawa imetawala kwa kijana Zabroni ama wakuitwa mtukutuku, baada kufika nyumbani na kuwakuta wazazi wake wakiwa tayari wamerudi kutoka shamba,huku pembeni akimuona baba yake akiwa na mzee Fungafunga wakisikiliza taarifa ya habari kwenye radio mbao.
Wakati kwenye ndoto aliota kwamba mzee huyo Fungafunga alikuwa na uhasama na baba yake.Hivyo Yote hayo ikabaki kuwa ndoto tu kwa kijana Zabroni,lakini aliyakumbuka maneno ya mzee Maboso "Pole sana kijana wangu ila kuna jambo nitakueleza",kwisha kuyakumbuka maneno hayo akaishia kutabasamu tu ikiwa upande wa pili Mzee Maboso akacheka sana Kishan akajisemea "Lengo langu litatimia tu"
***MWISHO**"