KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Mwajuma Utamu Sehemu Ya Pili (02)

Katika kipindi hicho ambapo nilikuwa katika mapenzi na Mzee Gidion, Daniel mtoto wa Mzee huyo na yeye alianza kunitamani, sijui nilimvutia na nini ila nilishangaa akinitongoza, alionekana kunihitaji kupita maelezo.
"Daniel embu acha kunitania bhana," nilimwambia huku nikionekana kutomuamini kabisa.
"Sikutanii Mwajuma kweli nakupenda, nahitaji kuwa na wewe," aliniambia Daniel.

"Umenipendea nini sasa?" nilimuuliza.
"Vingi tu vingine siwezi kukuambia," alinijibu.
Unajua kwanini sikuweza kumuamini Daniel? Kwanza alikuwa ni mtoto aliyetokea katika familia ya kitajiri, alikuwa ni msomi ukiachana na mimi ambaye nilifeli kidato cha nne, pili alikuwa ni handsome, alivutia mno, kwa kumtazama ilikuwa ni vigumu kuamini mvulana kama yeye kukosa msichana.

Alinisumbua sana, kila siku ombi lake lilikuwa ni moja, kuna kipindi nilimuonea huruma alipoingia chumbani kwangu kisha akawa ananibembeleza nimkubalie. Haikuwa rahisi kumkubalia kwani tayari nilikuwa katika mapenzi mazito na Baba yake na tulikuwa kwenye mipango mingi, nilikuwa nikisubiria itimie.
"Hapana Daniel siwezi kukubali hilo litokee wewe ni kama kaka yangu," nilimwambia Daniel.

"Mwajuma nakupenda, macho yangu yamekutazama wewe, una kila sababu za kuwa na mimi, umeuteka moyo wangu wa mapenzi tafadhali naomba usiuumize nitakufa," aliniambia Daniel huku machozi yakimlengalenga.
Nilishindwa kuvumilia kumuona Daniel akiendelea kuteseka kwa ajili yangu, nilimuonea huruma sana, mwisho wa siku nikajikuta nikishawishika na kumkubalia tukawa wapenzi.

Daniel alifurahi sana, hakuamini kama alifanikiwa kunipata huku nyuma ya pazia hakujua nini kilichokuwa kikiendelea kati yangu na Baba yake.
Kitendo cha kumchanganya Baba na mtoto kimapenzi hakika kilikuwa ni hatarishi sana, sikutaka kumwambia lolote Daniel, nilihofia mambo mengi mabaya ambayo yangeweza kunitokea.

Nilizidi kufaidi utamu wa penzi la Baba na mtoto huku kila mmoja kwa nafasi yake akikiri kunipenda kupita kawaida.
Siku ziliendelea kukatika, Mzee Gidion alianza kuingiwa na wasiwasi juu yangu, alihisi kuna mchezo mchafu ambao nilikuwa nikimchezea, hakutaka kuamini jambo hilo hata mara moja, alianza kufanya uchunguzi wake na mwisho wa siku akafanikiwa kugundua kuwa nilikuwa nikitembea na mtoto wake. Hilo lilimuumiza sana, alinilaumu mno. Naweza kusema siku hiyo ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza kumuona mwanaume mtu mzima kama Mzee Gidion akilia mbele yangu huku sababu ikiwa ni mapenzi, hakutaka kuamini kama yeye pamoja na mtoto wake walishiriki mapenzi na mimi.


Mzee Gidion alipagawa, hakuamini kile kilichokuwa kikiendelea, moyo wake ulimuuma mno, aliponitazama alionekana kuwa mwenye hasira, machozi yalikuwa yakimdondoka kwa wakati huo.
Nilishindwa kuamua la kufanya kwani mpaka kufikia muda huo nilikuwa tayari nimeshafanya makosa. Kwanza nilikuwa nikitembea na mume wa mtu kwa kujua, pili niliwachanganya kimapenzi baba na mtoto. Haya yalikuwa ni makosa ambayo kiukweli sikuwahi kukaa na kuwaza kwamba kuna siku yangeweza kunigharimu maisha yangu.

Nilishindwa kuvumilia kumuona Mzee Gidion akiendelea kulia mbele yangu kama mtoto mdogo, ilibidi nimsimulie kila kitu kilichotokea kwa Daniel mpaka nikajikuta nikimkubalia na kuwa wapenzi, sikuacha kumuomba msamaha kwa kosa nililokuwa nimelifanya, nilikiri kukosea na kumuahidi kutorudia tena makosa.

Baada ya kumueleza hayo pamoja na kumuomba samahani Mzee Gidion hakutaka kunielewa kabisa, alinichukia, alinifananisha na kahaba ambaye nilikuja kwenye familia yake kwa lengo la kutembea na ukoo mzima.
Hilo lilizidi kuniumiza mno, kitendo cha kuniita kahaba ambaye nilikuja kwenye familia yake kwa lengo la kutembea na ukoo mzima hakika kiliniumiza sana, moyo wangu ulikuwa kwenye maumivu makali mno.

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuishi maisha ya visasi kila siku, Mzee Gidion alikuwa ni mtu wa kunitishia maisha, alinikosesha amani ya moyo niliyoishi nayo kwa muda mrefu, sikuwa huru tena, muda wote nilikuwa nikimfikiria pamoja na vitisho alivyokuwa akinipa.

Kuna kipindi nilitamani kumueleza mke wake ukweli wote wa kile kilichokuwa kikiendelea kati yangu na mume wake lakini unafikiri ningeanzia wapi? Ningeupatia wapi ujasiri huo wa kumueleza kila kitu na wakati hapohapo tayari nilishamkosea kwa kitendo cha kutembea na mume wake.

Hiyo iliendelea kubaki siri ya moyo wangu, siri iliyokuwa ikinitesa mno. Mzee Gidion hakuacha kushiriki kufanya mapenzi na mimi, aliendelea kunitumia kimwili lakini safari hii haikuwa kama hapo awali, alibadilika na alikuwa akifanya mapenzi na mimi kama sehemu moja wapo ya starehe, yaani alinifanya kuwa kama kahaba ambaye alinitumia wakati alipohitaji kufanya mapenzi tu. Hilo liliniumiza sana, siwezi kusema ni maumivu kiasi gani niliyokuwa nayo katika moyo wangu lakini naweza kusema tamaa zangu za pesa ndizo zilizonipelekea nipitie katika wakati huu mgumu.

Daniel alikuwa ndiye mtu wa kwanza kuigundua tofauti yangu japo Mama yake alianza kuniuliza kuhusu mabadiliko yangu lakini nilimficha, sikutaka kumueleza ukweli.
"Niambie nini kinachokusumbua mpenzi, malaika, mke, malkia wa maisha yangu," aliniuliza Daniel.
"Hakuna kitu," nilimjibu.

ITAENDELEAAAA....
Powered by Blogger.