SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Ishirini Na Mbili (22)
"Mmh naona mpenzi wangu tayari umekua dereva mzuri, lione kwanza ulivyokuwa unaogopa? Eti oooh nitaharibu gari,unadhani kujua kuendesha kwako gari na kuharibu bora nini?
Bora uharibu mpenzi ilimradi tu ujue kuendesha..",aliongeza kusema Lina akizidi kujidhirisha ya kwamba kafa kuoza kwa mtukutu Zabroni. Zabroni alipoyasikia hayo maneno alifurahi sana moyoni akajikuta akijisemea mambo mengi kuhusu Lina.
Wakati huo sasa walisimama baada taa nyekundu kuwaka, zogo mbali mbali ziliendelea wakingojea taa ya kijani nayo iwaruhusu. Punde simu ya Lina ikaita, mama yake alikuwa amempigia. Haraka sana alipokea kisha akasema "Hello mama tupo njiani tunakuja lakini tutachelewa kidogo kwa sababu kuna foreni mama yangu"
"Anhaa sawa basi mwenzio anataka kuondoka",alijibu mama yake Lina.
Lina aling 'aka kisha akamtaka mama yake ampatie simu Veronica ili apate kuongea naye. Veronica alipokea akasema "Lina,mimi naondoka bwana nimekaa sana rafiki yangu. Naomba uniruhusu nitakuja kukuona siku nyingine sawa?.." Lina akajibu " Sijapenda best yangu unajua siku nyingi mimi na wewe hatujaonana,halafu istoshe nakuja na shemeji yako utaki umuone?..",hapo Veronica alicheka kidogo kisha akajibu
"Nataka sana ila nimepigiwa simu kuwa nahitajika mara moja nyumbani,siku nikija kukuona tuatongea mpaka unichoke. Ammh leo naomba nimsalimie japo kidogo",alisema Veronica pasipo kutambua kwamba huyo mtu anayetaka kumsalimia ndio yule aliyemtia hatiani kwa kutumia kivuli cha mapenzi.
Si mwingine ni Zabroni. Zarloni alichukua simu akaanza kwa salamu kisha akamuuliza jina lake"Naitwa Veronica ",alishtuka Zabroni kusikia jina hilo,jambo lingine lililomstua ni baada kusikia sauti inafanana fika na sauti ya Veronica yule aliyemkamatisha. Alipotaka kumdadisi zaidi ili apate japo ahakika kama ndio huyo Veronica anaye mtafuta,taa ya kijani ikawaka kuashiria gari zimeruhusiwa.
Hivyo Zabroni alimrudishia simu Lina kisha akawasha gari safari ikaendelea wakati huo nyuma yake ilisikika gari ikipiga honi kumtaka Zabroni aendeshe gari kwa kasi ili kuokoa muda,lakin Zabroni hakufanya kama alivyotaka dereva huyo wa gari ya nyuma. Kitendo ambacho kilimfanya yule dereva kukasirika,alipopata nafasi alimzunguka akaendana naye sambamba huku akionekana kumtolea maneno machafu Zabroni. Zabroni alipomuona jamaa anafoka, haraka sana alitelemsha kioo chake cha pembeni ili apate kumjibu. Ni Mr Rasi.
Alimkumbuka vema Zabroni wakati huo huo Mr akishindwa kumtambua Zabroni kwa sababu ya giza totoro ila Zabroni alimkumbuka Rasi kutokana na Rasta zake. Ndani ya gari, Lina kuna kitu alikidondosha chini ya miguu yake. Ikabidi awashe taa ili akichukue.
Mwanga huo wa taa ulipomulika tu,upande wa gari ile ya Mr Rasi Tina alipiga chabo kutazama ni nani huyo anayejibizana na mpenzi wake,akamuona Zabroni. Akataharuki akalitaja jina la mtukutu "Zabroni... "
"Zabroni?..",alijiuliza Mr Rasi akishangazwa na jina hilo ambalo sio jipya maskioni mwake,wakati huo huo Zabron aliposikia sauti hiyo alihisi ni sauti ya Tina. Upesi aliingiza gea mbili mfuruluzo,gari ikaongeza kasi huku nyuma Mr Rasi naye alimuuliza Tina kuhusu Zabroni "Huyu ndio yule jamaa uliyekuwa ukimzungumzia?.."
"Ndio huyo,sijui anaendeshaje maisha yake. Haeleweki huyu mtu..",alijibu Veronica. Kijasho chembamba kikaanza kumpanda Mr Rasi huku moyoni akijisemea "Leo huyo mtu ama zake ama zangu,atanitambua",kwisha kusema hayo aliendesha gari yake kwa kasi ya ajabu huku akionekana kuwa makini kuzikwepa baadhi ya magari makubwa kwa madogo hasa hasa daladala ambazo kwa upande wake zilonekana kumkera kwani zilikuwa zikisimama hovyo hovyo.
Lakini wakati Mr Rasi anamkimbiza Zabroni,mara ghafla simu yake ikaita. Bosi wake alikuwa amempigia alipokea haraka sana. Sauti ikasikika ikisema "Rasi ukowapi mbona unachelewa wakati saa nne mpambano unaanza? Muda pesa bwana", ililikuwa ni sauti ya Karani bosi wake Mr Rasi. Siku hiyo usiku palikuwa na pambano la V.I.P. Kwahiyo Mr Rasi lazima afike bila kuchelewa.
"Sawa nakuja bosi nipo njiani muda huu",alijibu Mr Rasi kisha akakata simu huku akikanyaga breki. Alishusha pumzi kwa nguvu kisha akageuza gari kuelekea ukumbini tayari kwa niaba ya mpambano ulingoni. Kiukweli moyoni mwake Mr Rasi alijilaumu sana,aliwaza ni lini atakutana uso kwa uso na Zabroni ili alipe kisasi cha wazazi wake lakini pia cha kaka yake ambaye ni Madebe. "Ipo siku yako tu nitakuadabisha", baada ya kuwaza kwa muda mfupi alijisemea maneno hayo Mr Rasi huku akiwa amefura hasira moyoni mwake.
Hatimaye alifika ukumbini,umati wa watu ulikuwa wengi sana. Usiku huo Derick alikuwa ameandaa pambano baada kupita siku nyingi bila kuandaa ligi la tajiri mwenzake ,kwa sababu aliamini kwamba Karani hana mpiganaji anayeweza kufua dafu kwa wapiganaji wake. Ila baada kusikia tetesi kuwa Karani kapata mpambanaji mwingine?
Akaona ni heri aje amsabahi kumdhihirishia kwamba kwake bado sana,inabidi azunguke Nchi mbali mbali kumtafuta bingwa anayeweza kuwatetelesha wapiganaji wake.Hakika Derick alijiamini sana. Na hata muda na wasaa wa mpambano ulipo wadia, kabla hawajaanza kutajiana dau. Derick alisikika akimkejeri Karani. Alisema "Oi Karani naona pesa zimkuwasha sana haya funguka kiasi ulicho nacho. Lakini pia ukumbuke kuwa hapa ni daraja la juu na sio uswahilini"
"Sawa Derick,nadhani niliwahi kukwambia kwamba. Sio kila umuonapo kobe ameinama basi ukajua anatunga sheria. La hasha kobe mwingine anajiuliza atumie siraha gani kukuangamiza. Mimi ni kama Kobe, amini usiamini leo kwisha habari yako", alijibu Karani kwa kujiamini kabisa huku akiachia na kicheko cha madaha. Derrick naye alicheka sana kisha akasema "Sawa mimi naweka Milioni 500.."
"Naweka Bilon moja nukta tano",alijibu Karani. Hapo ikawa ukaanza ushindani wa kuzidiana dau. Mwishowe wakaafikiana baada Derick kusema atatoa Bilion nane nukta nane. Shangwe zilipuka wakimsifu Derick.
Vijana wakaingia ulingoni, mpambanaji na Derick hakuchukua dakika sita ulingoni alipindishwa pua na Mr Rasi akawa amepoteza faham ulingoni. Rasi akaibuka kidedea. Derick alistuka akajiuliza "Mtu huyu wa aina gani?..", wakati huo Karani alisikika akisema "Derick tukutane Sophie hotel, istoshe kajipange upya sasa"
Kipindi hayo yanajili,upande wapili nako Zabroni na Lina tayari wamefika nyumbani.
Walikuta Veronica ameshaondoka. Baada salamu na zogo la hapa na pale,mama Lina alimsimulia mwanaye jinsi rafiki yake alivyobadilika kwa sasa baada ya kupata kazi. Na yote kwa yote mama Lina alimpa picha mwanaye ya rafiki yake ambayo alimuachia ili akifika amuonyeshe.
Lina alifurahi sana kisha akasema "Jamani Veronica, kabadilika sana daah! " alisema Lina huku akimkabidhi Zabroni ili naye apate kumuona huyo Veronica. Zabroni aliipokea picha hiyo,alipoitazama akamuona ni yule yule anayemtaka siku zote.
"Huyu ndio rafiki yako?..", kwa tabasamu alihoji Zabroni. Lina huku alijibu "Haswaa wa kufa na kuzikana",baada Zabroni kujibiwa na mpenzi wake,alikaaa kimya huku moyoni mwake akijisemea "Naam! hapa sasa mchezo unakaribia kuisha. Nadhiri yangu ipo pale pale lazima.. Lazima.. Lazima nibandue nyeti yake. Mimi ni Zabroni ", akamaliza kwa kicheko ambacho alikichekea moyoni.
Zabroni alipania kumfanya Veronica hicho kitendo sababu tayari aliamini hilo suala linakwenda kutimia sababu anaukaribu na mtu huyo ambaye alimtia kitanzini baada kumteka kimapenzi.
Zogo kadha wa kadha ziliendelea hapo,na mara baada kuhitimisha maongezi yao waliaga na kisha kuondoka zao.
Walipokuwa njia wakirudi nyumbani kwao,Lina alimwambia mpenzi wake waende club mara moja japo kupozesha koo kwa kupata kinywaji baridi lakini pia nyama choma.
Zabroni alikubali. Walielekea kwenye club moja iliyofahamika kwa jina Alminat Club,hapo palikuwa na kila aina ya vinywaji vile vile walimbwende wazuri ambao shughuli zao ilikuwa ni kusambaza vinywaji huku baadhi yao ambao wanafahamika kwa majina changudoa,wao walikuwa nje kidogo ya kumbi hiyo ya starehe,wao shughuli zao ilikuwa ni kuuza miili yao.
Walipofika mahala hapo wakwanza kushuka alikuwa Zabroni ambapo aliposhuka alizipiga hatua kuelekea kwenye mlango wa gari upande ule aliokaa Lina,alimfungulia mlango kisha akaubana na funguo akamshika kiuno wakaelekea ndani ya kumbi hiyo kupata walau chochote.
Walikunywa na kula nyama choma,walipohakikisha wametosheka ipasavyo waliondoka zao. Lakini wakati wanaondoka nyuma yao alionekana tajiri Derick akiwa na wapambe wake.
Derick alionekana kuvurugwa mno baada kushindwa pambano aliloandaa na Mr Karan,hivyo alikunywa pombe sana ila alipomuona Lina alisitisha zoezi hilo la kunywa pombe kwa pupa,akamuita mpambe wake mmoja kisha akamuambia afanye juu chini amleta Lina mbele yake ili akakeshe naye usiku mzima. "Unanisikia vizuri? Nakutuma.
Nenda kamlete yule mrembo aliyeondoka humu ndani hivi punde, nataka nikalale naye usiku kucha, akitaka pesa mwambie atapata kiasi chochote anacho kitaka,akikataa tumia uzoefu wako. Haya haraka sana nenda.
Aam..no no noooo.. nendeni watu watatu mkafanye hiyo kazi ",alisema Derick kwa sauti ya kilevi, na alipokwisha kusema hivyo akamimina pombe kwenye grasi kisha akanywa mfurulizo. Wapambe wake baada kusikiliza matakwa ya bosi wao haraka sana walikwenda kutimiza azimio.
Walipolifikia gari la Zabroni walimkuta Lina akiwa amesimama nje akimngojea mpenzi wake ambaye muda huo alikuwa amekwenda kumnunulia vocha kwenye duka ambalo lilikuwa hatua kadhaa kutoka mahali ilipo kumbi ile ya starehe.
"Habari yako mrembo ",alisema mmoja ya wapambe wa Derrick huku akiachia tabasamu bashasha.
"Nyie akina nani?..", kwa taharuki Lina alihoji huku akiwatilia shaka hao watu..
"Sisi ni wasaka tonge ili mwisho wa siku tuwapate warembo wazuri kama wewe, amini kuna bosi wetu amekupenda. Na anataka ukalale naye usiku kucha atakupa kiasi chochote cha fedha utakacho hitaji",alijibu kwa kujiamini mpambe wa Derick. Lina alikunja uso kwa hasira kisha akasema "Acheni upuuzi wenu,machangudoa hamjawaona mpaka mnifuate mimi? "
"Kwahiyo hutaki?.." aliulizwa Lina.
"Ndio sitaki!..",alijibu hivyo Lina wakati huo akitazama huku na kule kwa mbali akimuona Zabloni anakuja.
Baada Lina kuweka pingamizi,kiongozi wa hao wapambe aliamuru wambebe kwa nguvu ilimradi wamfikikishe katika mikono ya bosi wao. Upesi upesi wakanza kufanya kazi hiyo. Kitendo hicho kiliweza kuzua furumai kubwa eneo hilo lakini ghafla lilitulia baada mtukutuku Zabroni kufika.
"Mnataka nini?.." ,aliongea kwa sauti ya juu Zabroni. Wapambe wa Derrick waliposikia sauti hiyo waligeuka kumtazama mtu huyo aliyepasa sauti yake kwa ukali. Wakamuona Zabroni, ajabu wakatazamana kisha wakaangua kicheko.
"Wewe ni kama nani unajiamini na kuongea huo ujinga wako?..", mmoja wao alimuuliza Zabroni.
"Mimi ni Ramso, nasema sihitaji tufike pabaya. Achana na mpenzi wangu?.."
"Ahahahaha! Eti mpenzi wako. Braza muonekano wako kamwe hauendani na chombo unachomiliki..."
"Unaamana gani?..", akahoji Zabroni.
"Utajua nini namanisha! Apeche,hebu kula naye sahani moja huyo", kiongozi mkuu wa msafara mfupi uliokuwa na dhumuni la kumtaka Lina alitoa amri mpambe Apeche apigane na Zabroni,lakini Apache hakuweza kufurukuta zaidi alipotaka kurusha ngumi,Zabroni aliudaka mkono wake kisha naye akamrushia ngumi kupitia ule mkono wenye hirizi. Ilikuwa ngumi nzito, lakini bahati nzuri ngumi hiyo haikumfikia ila upepo uliosababishwa na uzito wa ngumi ile ulimfanya Apeche kukimbia kumuita bosi wake ndani ili walau aongeze wapambe wengine.
"Acha ujinga,unaweza kuniambia huyo jamaa anajua sana ngumi kiasi kwamba awashinde watu watatu?..", kwa hamaki alihoji Derick.
"Ndio bosi,huyu mtu sio wa kawaida kabisa t ",alijibu Apeche huku akitetemeka mwili mzima.
"Haya twende nikashudie", Derick alitoka ndani akazipiga hatua kuelekea nje ambapo pallikuwa na mpambano mkali kati ya wapambe wake na Zabroni. Lakini alipofika nje alikuta gari ya Zabroni inaondoka zake huku chini watu wake wakigagaa wakiwa wameshika mbavu zao wakihisi maumivu makali. Derick akaona Zabroni bila shaka anaweza kumpoza machungu,haraka sana alisogelea gari yake akamuambia dereva aifuate nyuma gari ya Zabroni. Wakati huo ndani ya gari Lina alikuwa akimwangalia Zabroni mara mbili mbili akimshangaa sana kamwe hakujua kama mpenzi wake ni moto wa kuotea mbali kwenye masuala ya ngumi.
"Doh Ramso mpenzi kumbe unajua sana,unapiga kama..",kabla Lina hajamalizia kusema alichotaka kukusema,mara ghafla Zabroni akamuambia "Naomba funga mkanda mamaa,tunafuatiliwa nyuma" , aliongea kwa msisitizo Zabroni huku akiitazama gari iliyopo nyuma kupitia kioo cha pembeni (Side Mirror).
Lina alituka haraka sana alipandisha kioo kisha akakaza mkanda ipasavyo. Zabroni aliendesha gari kwa kasi kuikimbia gari lile la Mr Derrick ila baadae akaona liwalo na liwe hakuona haja ya kukimbia akahofia kusababisha ajari bila sababu ya msingi,aliweka gari kando kisha akashuka. Wakati huo huo Derick naye aliweka gari kando kisha akashuka.
"Habari yako kaka mkubwa!.. Aaamh hakuna haja ya uhasama. Mimi ni mtu mwema sana na nimependa mapigo yako kwahiyo kama hutojali Naomba tupige pesa",alisema Derick huku akitabasamu. Zabroni alikumbuka siku za nyuma kidogo jinsi Mr Rasi alivyo mchukulia mpenzi wake,akawaza "Ama Tina alipenda upigaji wa Rasi? Na dhani hawa ndio wale wale acha nikubali ili nimuonyeshe Tina kuwa alichokipenda kwa Rasi hata mimi ninacho pia", kwisha kuwaza hayo akaachia tabasamu akionekana kufurahi dili tata lililopo mbele yake pasipo kujua kuwa Mr Rasi ndio Bruno kijana ambaye anamsaka kwa udi na uvumba ili alipe kisasi cha kifo cha kaka yake Madebe lakini vile vile cha wazazi wake.
"Nashukuru kukufahamu",alijibu Zabroni.
"OK kama hutojali shika kadi hii,ina namba zangu kesho nipigie ili tufanye kazi" , aliongeza kusema Derick. Upesi Zabroni alipokea kadi hiyo kisha akarudi ndani ya gari wakaondoka zao huku nyuma wakimuacha Derick akijinasibu kwa kusema "Karan umekwishaaaaa" .
*****
Kesho yake Zabroni aliwasiliana na Derick pasipo Lina kujua mkakati wake,makubaliano yalifanyika na mikataba ikasainiwa. Hivyo kilichokuwa kimebaki ni Zabroni kuanza kazi,na kizuri zaidi aliambiwa kamwe hatofatiliwa na serikali kwani wao pia ni serikali tosha.
Jambo hilo lilimpa matumaini kibao Zabroni istoshe aliambiwa pindi atakaposhinda mpambano atapata pesa za kutosha ambayo itamfanya aendeshe vema maisha yake. Kumbe kipindi Zabroni anaaminishwa jambo hilo,upande wa pili tayari siri ilibuma baada kubainika kazi inayofanyika haipo kisheria yani kihalali.
Ipo kiharamu zaidi,hivyo serikali iliamuwa kuwafukuza wale wahusika ambao wapo serikalini waliokuwa wakipokea rushwa kutoka kwa matajiri hao waliokuwa wakifanya kazi hiyo pasipo kibari maalumu na sasa shunghuli nzima ikabaki kuwakamata wahusika wakuu Karani na mwenzake wa kuitwa Derick pia na wengineo wachache.
Siku zilisogea,Zabroni sasa akawa ananogojea siku ya pambano iweze kufika ili apate ujiko mbele ya mpenzi wake wa zamani ambaye ni Tina. Hatimaye siku moja saa ya jioni simu yake ya mkononi iliita alipotazama jina akaona Derick bosi wake amempigia kwa wakati huo .
Zabroni alipokea. Derick akasema "Rasmo jiandae sasa wiki ijayo utakuwa na pambano kali,kama unamjua ama umeshawahi kumsikia jamaa mmoja hivi anaye itwa Mr Rasi. Huyo ndio utapigana naye kwahiyo inabidi ujifue vya kutosha sitaki uniangushe sababu pambano hilo ndio litatufanya kuuaga umaskini", akamaliza kwa kicheko Derick.
"Sawa bosi kwa hilo ondoa shaka.",alijibu Zabroni kisha akainua mikono juu ishara ya kumshukuru Mungu sababu alihisi Mungu kayjibu maombi yake ya muda mrefu.
"Hahahaha, pasipo na shaka. Mungu amejibu maombi yangu", alijisemea kwa furaha wakati huo akitamani siku hiyo usike iwahi kufika.
Siku tatu nyuma kabla siku yenyewe ya mpambano haijawadia,ndio siku ambayo Zabroni alianza kupanga mkakati wa kumaliza azima yake iliyomtorosha jela kwa sababu alisikia Lina akiongea na Veronica akimwambia kuwa siku si nyingi atakuja kumtembelea.
Siku hiyo ilipofika,Lina alimpasha habari hiyo njema mtukutu Zabroni. Habari hiyo ilipomfikia Zabroni hakika alifurahi sana. Kwa tabasamu bashasha akasema "Jambo jema sana mpenzi lakini pia itabidi tumpe taarifa kwamba mwezi ujao tunatarajia kufunga ndoa"
"Ahahahah, sawa", Lina alikubaliana na wazo la Zabroni na hata asijue ya kwamba Zabroni hana wazo la kufunga naye ndoa ila yupo katika jiji la Dar es salaam kimpango tu wa kutimiza nadhiri yake aliyopania.
Majira ya saa saba mchana,ndio safari ya Veronica ilipoanza kuelekea mahali anapoishi rafiki yake na mpenzi wake. Alipewa maelekezo mpaka akafanikiwa kufika ingawa aliishia nje kwa sababu nyumba ilikuwa kubwa halafu istoshe ilikuwa kimya sana.
Lakini wakati yupo nje,Zabroni alifunua pazia kutazama nje, macho yake mawili yakapata kuiona gari Rava4 ya Veronica ikiwa imesimama nje. Akaachia tabasamu pana kisha akafunika dirisha kwa pazia ikiwa muda huo huo Lina alitoka ndani upesi akamfuata Veronica nje.
Alipomfikisha sebuleni ghafla simu yeke ikaita, ni mama yake ndio aliyempigia. Lina alipokea ikasikika sauti ya mama yake ikisema "Lina fanya haraka uje baba yako kakamatwa na jeshi la polisi,tafadhali njoo mwenyewe usije na Ramso.
Njoo moja kwa moja hapa kituo Stakishari ", kwisha kusema hayo simu ilikatika. Lina akastushwa na taarifa hiyo, haraka sana akajiandaa akamuaga Zabroni kiaina pia akamuaga na Veronica akimwambia kuwa aendelee kumsubiri anakuja muda si mrefu huku akimtaka amngoje huku wakipiga zogo na shemeji yake pasipo kujua kwamba kakabidhi fisi bucha.
Veronica alitulia sebuleni akimngojea shemeji yake aje ili waongee mambo mawili matatu,punde si punde naye akatokea. Ni Zabloni. Veronica alistuka kumuona mtukutu huyo,akiwa na hofu dhufo lihari akasema "Ni Wewe ama macho yangu?..", mtukutu Zabroni akiwa amekunja sura yake kwa hasira na ghadhabu akajibu
"Ndio ni mimi Zabroni ukajua nani?..."
Ulijiona mjanja sana! Ukasau kutambua kwanini mungu alianza kumuumba mwanaume na sio mwanamke?.. Veronica mshahara wa dhambi siku zote huwa ni mauti", alisema Zabroni kisha akachomoa kisu kikali, alizamilia kumuuwa Veronica. Veronica akastaajabu sana kumuona mtukutu huyo kwa mara nyingine tena, alijua tayari yupo matatani na hivyo haraka sana akaomba msamaha lakini Zabroni kwa muda huo hakuwa tayari kutoa msamaha, moyoni aliamini kuwa malipo huwa ni hapa hapa Duniani na mbiguni ni hukumu tu.
Basi upesi akamchoma kisu upande wa titi la kulia,Veronica alipasa sauti ya kilo huku akizidi akiomba msamaha. Lakini Zabroni hakutaka kuelewa alirudia mara ya pili kisha mara ya tatu akakiingiza kisu hicho hicho sehemu nyeti ya Veronica, hapo Veronica alirusha miguu huku na kule akakata roho.
Hakika ulikuwa unyama uliokidhiri alio ufanya Zabroni ambapo hakuona haja ya kuendelea kukaa katika nyumba hiyo, alitimua mbio. Alipofika nje hakuikuta gari, Tina aliondoka nayo. Hapo sasa Zabroni alijihisi kuchanganyikiwa haraka sana alimpigi simu Derick ili amtume mpambe wake aje kumchukuwa,kweli punde si punde gari ilifika.
Zabroni alipanda safari ikaanza, safari ya kwenda kwenye mpambano huku nyuma tayari akiwa ameshamaliza azma yake. Istoshe hiyo siku ndio ilikuwa siku ya mpambano.
INAENDELEA