KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Shemeji Monica Sehemu Ya Tano (05)

 


Aisee Sir Mdharuba natafuta chumba bwana, sijui nitapata wapi?? alianziasha maongezi James wakiwa ofisini akingojea muda wa kipindi chake ufike. ?Vyumba vipo tu humu mjini, unataka cha aina gani kwani?? alisema Sir Mdharuba na kuunganishia na swali. ?cha kawaida tu, cha bei poa? alijibu James. ?hivyo vinapatikana uswahilini, hata pale ninapokaa mimi kuna chumba kiko wazi, kama vipi ukapaone kama panakufaa?. ?sasa si kesho tena hiyo maana naona kama leo muda umeshaenda? alijibu James. ?tunao muda, kwani una dakika ngapi kabla ya kipindi?? alihoji Mdharuba akiangalia saa yake. ?kama 25 hivi? alijibu James mara baada ya yeye kuangalia saa yake pia. Mdharuba akaona zinaatosha sana, wakaondoka pale kituoni kwa kutumia pikipiki ya Mdharuba mpaka maeneo ya uswahilini ambapo alipelekwa kwenye nyumba kubwa yenye vyumba vingivingi kila kimoja kikijitegemea, ilikuwa imejengwa maalumu kwaajili ya kupangisha. James akaoneshwa chumba ambacho kilikuwa tupu, akakiangalia na kuona kilikuwa kinamfaa, akakutanishwa na mma mwenye nyumba ambaye alimpa masharti ya nyumba akaridhikanayo na kulipia pesa ya miezi 6 kama ambavyo mama mwenye nyumba alitaka. Bei ya chumba ilikuwa elfu 20, hivyo kwa miezi 6 ilikuwa ni laki moja na elfu 20, gharama ambayo James aliimudu.

Wakiwa wamerudi kituoni na James akawa anajiandaa kwenda kuanza kipindi chake, simu yake ikaita, namba ilikuwa ni ngeni kwenye simu yake, hivyo hakujua nani alikuwa anapiga, ikambidi kupokea ili kujua mpigaji alikuwa nani. ?hallo James tunaweza kuonana kwenye mgahawa wa hapa nje ya ofisi yenu?? James hakuhitaji kuambiwa kuwa ile ilikuwa ni sauti ya mama yake Julieth. James hakuweza kukataa wito ule, akawaomba wanafunzi wake kumvumilia kwa dakika chache kisha akaenda kumsikiliza mama yake Julieth huku akiwa na wasiwasi mwingi wa juu ya jambo ambalo alitaka kuongelea.



?shikamoo mama? alisalimia James wakati akivuta kiti na kukaa akitazamana na mama yake Julieth. Baada ya kuitikia salam mama Julieth akaanza kuelezea juu ya ujio wake. ?James nataka uniambie ukweli nini kinaendelea kati yako wewe na Julieth? alihoji mama yule, sauti yake ilionesha kuwa alikuwa serious sana na ambacho alikuwa anakifanya. ?sijakuelewa swali lako mama, mblai na kumfundisha Julieth nini kingine kinaweza kuwa kinaendelea?? James alijifanya kama hakuwa na ambalo analijua. ?Julieth ni mwanangu, namjua vizuri sana, hawezi kuficha hisia zake mbele yangu. Jana wakati wa chakula nimegundua kuwa Julieth anakupenda, unaweza kubisha??, mama Julieth akaanza kutumbua jipu na kumuacha James njia panda. ?mama mimi ninachofanya ni kumfundisha Julieth, sina jingine. Siwezi kubisha juu ya kuwa ananipenda maana sijui kilichomo moyoni mwake, illa hajawahi kuniambia na kuna mpaka mkubwa kati yetu, hatuendi zaidi ya kwenye masomo? alijibu James. ?basi wacha nikuulize swali la mwisho na naomba unijibu ukweli? alisema mama Julieth na James akawa tayari kupokea swali hilo. ?tukiachana na swala la kuwa na uhusiano ama kutokuwanao je, unampenda Julieth??. Swali hili lilikuwa gumu sana kwa James kusema kuwa hampendi Julieth mbele ya mama yake ilhali alikuwa akimpenda sana aliona kama ni usaliti, na akajikuta kutmani kusema ukweli.

*****************************


Kusema kweli mama, Julieth ni msichana mrembo sana na mwenye kujitambua, mwanaume yeyote akiamua kuruhusu hisia za kimapenzi juu yake ni lazima atampenda, tena sana! Ila mimi sipendi kuziruhusu hisia za aina hiyo, mimi ni mwalimu wake? aljibu James. ?wewe ni mjanja na una akili nyingi sana, naweza kuliona hilo kutoka kwenye majibu yako. Kwa kumalizia nikwambie kuwa Julieth bado ana safairi ndefu sana, sipendi kuona mtu yeyote akiiharibu safari hiyo, kama unampenda Julieth ufuate taratibu za kistaarabu za kumuoa, ila sio sasa, ni mpaka atakapomaliza masomo. Sijui umenielewa?? alisema mama yake Julieth kwa kumaanisha na James akakubali kuwa ameelewa maelezo yale. ?sasa kama umenielewa sitaki kuona kitu cha ajabu kimetokea, nitakuweka pabaya sana? alichimba mkwara mzito mama yake Julieth.

Maongezi yale yakawa yameisha na James akawahi kwenda kuwafundisha wanafunzi wake ambao walikuwa bado wanamsubiri.

Julieth aliweza kuigundua hali ya upole kwa James alipokwenda kwao kwaajili ya kumfundisha siku hiyo, hakujua alikuwa amkumbwa na nini lakini aliiweza kuona alikuwa tofauti. Julieth alipomtaka wakasomee chumbani kama ilivyokuwa siku liyopita James alikataa na kusisitiza kuwa alitaka wasomee pale sebuleni, ikambidi Julieth kukubaliana na matakwa ya mwalimu wake huyo. Katika kumfundisha pia siku hiyo James serious kama mwalimu, ule utani utani wake wa siku zote haukuwepo. Julieth akaanza kujiuliza alikuwa amemkosea nini, lakini hakuona popote alipokuwa amekosea toka waachane jana yake wakiwa na furaha. Baada ya kipndi kuisha James akaaga na kuondoka, Julieth akataka kumsindikiza ila James akakataa na kusisitiza amuache tu aende mwenyewe, ?jamani, nakutoa tu mpaka hapo getini? alisema Julieth ambaye aiona sasa walikuwa wamefika pabaya. ?No, wacha niwahi? alijibu James na kuondoka bila kungoja majibu. James aliamua kupunguza mazoea anapokuwa kwenye mazingira ya nyumbani kwa kina Julieth kwani aliona mazoea yale yangemrudisha tena kwenye maongezi na mama yake Julieth,mpengine wkati huu angekuja vibaya zaidi.

CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

James alifika nyumbani na kumkuta shemji yake, Monica akiwa na mtoto wake wakipiga story za hapa na pale, naye akajumuika nao, kaka yake alikuwa bado hajarudi.

Baada ya kupata chakula cha usiku story zikaendelea mpaka Peter, mtoto wa kaka yake James alipochoka na kwenda kulala, haikuchukua hata nusu saa na James naye akaingia chumbani kwaajili ya kulala, mara akasikia mtetemo wa simu yake ukiashiria kuwa ujumbe ulikuwa umeingia,alipotoa simu yake akagundua kuwa zilikuwepo jumbe mbili, moja ya Monica na nyingine ya Julieth. ?nimekumiss, njoo chumbani kwangu nikuoneshe kitu kizuri? ujumbe wa Monica ulisomeka hivyo, James akaupuuza na kufungua ule wa Julieth. ?hivi James nimekukosea nini mimi? Kama hunipendi kwanini usiniambie tu? Haya ni mapenzi ya namna gani, mara unafuraha mara umeninuia, mimi nitashindwa kwakweli?, ujumbe huu wa Julieth ulimuingia vizuri James, mpaka ndani ya moyo, akajaribu kuvaa viatu vya Julieth ambaye hakuwa akijua nini kimetokea baina ya James na mama yake, akaona kweli binti wa watu atakuwa katika wakati mgumu kulielewa hili swala. ?Julieth kwanini unakuwa mgumu kunielewa? Hapo ni kwenu, tukiendekeza mapenzi utaniletea matatizo, kwanini hulioni hilo? Nakupenda sana lakini sitaki uwe sababu ya kuharibika kwa future yangu? alijibu ujumbe ule James kisha akaamua kurudi kwenye ujumbe wa Monica na kuujibu ?hivi ni kazi sana kumtoa mwanamke bikra?? akatuma ujumbe huo ambao haukuwa na uhusiano wowote na ule ujumbe ambao Monica alitangulia kumtumia.

James acha kutafuta visingizio, kila mtu anakupenda hapa nyumbani, unamuogopa nani atakaye kudhuru?? ulikuwa na ujumbe mwingine wa Julieth. ?mama yako alinifuata ofisini mchana na akanitaka kukaa mbali na wewe? James akaamua kutumbua jipu baada ya kuona lawama zote zimehamia upande wake. ?khaaa, kwanini mama anaifanyia hivi?, kwakweli sikubali, lazima nionge naye? alijibu Julieth akionesha kukasirishwa sana na alichokifanya mama yake. ?ukiongea naye kuhusu hili unanigombanisha zaidi na mama yako, naomba usifanye hivyo? James kajibu ujumbe ule na Julieth akaona anachokisema ni kweli. ?sasa itakuwaje, tutakuwa tunakutana wapi? Mimi siridhiki na maisha haya? lijibu Julieth. ?kama tunataka kuwa na futurenzui hatuna haja ya kupapatikia mambo, tunaweza kuharibu kila kitu, siwezi kugombana na wazazi wako kama kweli nataka uje kuwa mke wangu baadae? James akajibu. ?yani wewe unataka nikufundishe namna ya kumidhisha mwanamke mwingine? Kwani mimi sina wivu?? ulikuwa ni ujumbe wa Monica ambao James hakuujibu. ?kama unataka nikufundishe njoo? Monica alituma ujumbe mwingine baada ya kuona ule haukujibiwa. ?hapana, nakiheshimu sana hiko chumba cha kaka yangu, siwezi kuja? alijibu kwa kifupi James. ?mara hii umeshasahau mashatri yangu? Tulikubaliana utakuwa unafanya ninachokwambia lakini umenigeuka? alijibu Monica lakini kwa mara nyingine James akapuuza uumbe wake na kulala, kitendo ambacho alijua fika kinamkera sana Monica na kama sio uwepo wa Peter, mtoto wa wake basi lazima Monica angemfuata pale chumbani.

BONYEZA HAPA KUPATA MSG ZA MAPENZI

INAENDELEA

Powered by Blogger.