KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Shemeji Monica Sehemu Ya Sita (06)



Asubuhi James alidamkia mjini ambapo alienda kununua godoro na vyombo vichache ambavyo alivipeleka kwenye kile chumba chake, alikuwa amepanga kuhamia kesho yake maana hali ya shemeji yake,Monica alikuwa anaelekea kubaya, akaona bora ahame kulinda undugu wao na kaka yake, Paul.

Leo hatusomei nyumbani, nimeaga kuwa umeniambia kuna sehemu tutaenda kusomea, so tafuta sehemu. Na mama akikupigia kuhakikisha ukubali? ulikuwa ni ujumbe wa Julieth kwenye simu ya James. Huyu binti ana akili gani? Alijiuliza James, naye akaandika ujumbe kumjibu ?hapana, tutasomea nyumbani, tumeshaliongea hili swala?. ?nyumbani nimeshaaga na nimeondoka, sahivi nakaribia hapo kazini kwako, nakuja kukungojea umalize kazi tuondoke, na mama atakupigia wakati wowote, andaa maelezo mazuri ya kumpa? alijibu Julieth na kuichangaya akili ya James ambaye alikuwa amekaa na Sir Mdharuba mule ofisini akingojea muda wa kipindi chake. ?please rudi nyumbani kama kweli unanipenda? alijibu James. ?no, safari hii na wewe fanya kitu kwaajili yangu. Nakuja, kama kunifukuza unifukuzie hukohuko? Alijibu Julieth.

****************************************

BONYEZA MAANDISHI HAYA KUPATA VICHEKESHO

ITAENDELEA

Powered by Blogger.