KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Shemeji Monica Sehemu Ya Nne (04)



Pale ndani James alishaanza kuchanganyikiwa, maneno ya mama Julieth yake yalionesha kuwa alikuwa na mashaka ya nini kinafanyika nyani, hasa baada ya kuona mlango umefungwa, ?tuko busy? alijibu Julieth kwa sauti ya juu. ?njooni basi angalau mpate chakula kwanza, muda umeenda? alisema mama Julieth na kusababisha James kuangalia saa yake na kugundua kuwa ilikuwa saa mbili na nusu usiku. ?tunamalizia? alijibu Julieth na mama yake akaondoka. ?inabidi niondoke, tutawaudhi wazazi sasa? alisema James huku akisimama, Julieth naye akasimama na kumpiga busu zito mdomoni, kisha akatangulia kufungua mlango James akifuata nyuma yake. ?karibu tujumuike mezani mwalimu? alisema baba yake Julieth ambaye alikuwa kwenye safari ya kutoka eneo la kupumzikia pale sebuleni, kuelekea eneo la chakula. ?asante mzee muda umeenda sana, nitakula siku nyingine? alijibu James kwa kifupi akiendelea na safari yake ya kwenda nje. ?kwa heshima yangu naomba tupate mlo wa pamoja leo? alisema baba yake Julieth, maneno ambayo James hakuwa na nguvu ya kuyapinga. Wakajumuika mezani na kupata chakula, chakula kilikuwa kitamu


kikitawaliwa na mazungumzo ya hapa na pale, baba yake Julieth alikuwa mcheshi sana na alikuwa hakauki simulizi z kuchekesha, hivyo muda wote wa chakula walikuwa wakicheka kwa furaha. James aligundua Julieth ambaye walikuwa wamekaa kwenye meza wakitazamana alikuwa akitumia mudamwingi kuuangalia zaidi ya kula na macho yao yalipogongana alitabasamu, ikambidi James kujitahidi kumkwepa kwani alidhani wazazi wa Julieth wangeweza kusoma jambo pale. Baada ya chakula hakuna ambaye alikuwa na sababu nzuri ya kumzuia James asiondoke, japo mama yake Julieth alimtaka kumpa namba zake za simu ili iweze kurahisisha mawasilano kama angemuhitaji, jambo ambalo James alilitekeleza bila wasiwasi wowote.

Alipofika nyumbani James alishangaa kumkuta kaka yake, ilikuwa ni mapema mno kwa kaka yake kuwepo nyumbani, maana toka alipofika kwenye mji ule kaka yake alikuwa akichelewa sana kurudi nyumbani na hurudi akiwa amelewa, lakini siku hii hakuonekana kama aliyelewa. ?naona umekuwa mwenyeji sana sasa? alisema kaka yake James huku akitabasamu. ?yeah, sasa mtu haweza kunipoteza mji huu? alijibu James, wakacheka. ?sasa wameanza hata kuniibia mume, dalili mbaya hizi za kurudi mida hii? alitania Monica. ?pengine mume anakuwa nje anakutafutia, acha wivu? alijibu kaka yake James ambaye dongo lile la mkewe japo lilikuwa utani lakini linnamlenga yeye zaidi. ?shemeji karibu chakula? alisema Monica akimuelekeza James kuelekea mezani kupata chakula, hali ya meza ilionesha kuwa wengine wote walikuwa wamekula tayari. ?asante shem, ila nimeshakula tayari huko nitokako? alijibu James. ?jamani jamani dalili mbaya hizi? alitania tena Monica, wote wakacheka. ?shikamoo bamdogo? alisalimia Peter, mtoto wa Paul ambaye alikuwa akitokea chumbani, Peter alikuwa amekuja siku hiyo kutokea shule ambako alikuwa akisma


‘boarding’. James akafurahi sana kumuona mtoto huyu wa kaka yake ambaye hakuwa ameonana naye kwa kipindi kirefu, wakasalimiana na kuulizana maendeleo ya shule. ?hii ni suprise kwelikweli, sikujua kama kinaja anakuja leo? alisema James. ?we huoni leo baba yake mapemaaa yuko nyumbani, kama sio ujio wa mwanae angekuwa hapa saa hizi?? alilenga dongo lingine Monica ingawa alilitoa kama anatania. James hakupenda hali ile ya Monica kuwa anamrushia mume wake vimaneno, alijiona kama alikuwa na mchango mkubwa kwenye kusababisha Monica afanye vile kutokana na mambo ambayo wamekuwa wakiyafanya, pengine yamepelekea kumuona mume wake hana maana yoyote,pamoja na kuwa asilimia kubwa ya matatizo yale aliyasababisha yeye mwenyewe (kaka yake James). James akajikuta amepata wazo la ghafla, akaona kuendelea kuwepo mule ndani kunaweza kusababisha mpsuko siku moja, hasa kutokana na mambo ambayo amekuwa akiyafanya na shemeji yake, akaona utatuzi ni kuhama mule ndani. ?jamani mimi nilikuwa nawaza kupanga chumba nianze kujifunza maisha? alijaribu kuliingiza wazo lake kwenye vichwa vya wenyeji wake


hawa ili kuona litapokelewaje. ?kwanini umefikia uamuzi huo, kuna jambo lolote limekukera?? alihoji kaka yake ambaye habari hizi zilikuwa za ghafla sana kwake, hakutegemea kuona mdogo wake huyu akiondoka kwake hivi karibuni. ?hapana, nimeishi kwa amani sana ndani ya nyumba hii, na ninashukuru sana ila nadhani ni wakati wa mimi kujaribu kuwa mkomavu na kujitegemea? alielezea vuzuri James na kaka yake akamuelewa haraka. ?au kwasababu Peter karudi umeona chumba hakiwatoshi?? alichangia Monica. ?kwani Peter ni tembo? Chumba chote kile kinaachaje kututosha?? alijibu James kiutani na wote wakacheka. ?lakini huna muda mrefu utaenda chuo, sasa huoni kama hiko chumba hata hutokikaa?? alihoji tena Monica ambaye James alitarajia upinzani mkali kutoka kwake. ?maamuzi yangu ni kutokwenda tena kijijini, maisha yangu yatakuwa hapa, hata kama nitakuwa nakwenda chuo likizo zote nitakuwa hapa kwahiyo chumba changu kitatumika tu? alijibu James. ?mi nadhani sio jambo baya, maadam umeamua mwenyewe na unaamini kuwa utamudu changamoto za maisha, bora tukutakie kila lakheri? alisema kaka yake James na Monica akaonesha kukubaliana, jambo ambalo James hakulitegemea. Wakaendelea na story za hapa na pale mpaka walipochoka na kwenda kulala.

SOMA HAPA MAKALA ZA MAFANIKIO

INAENDELEA

Powered by Blogger.