KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Mwajuma Utamu Sehemu Ya tatu (03)

"Usiniambie hakuna kitu wakati nikikuangalia nakuona kabisa kuna kitu unanificha," aliniambia.
"Kweli hakuna kitu."
"Usinifiche tafadhali."
"Naogopa kukuambia Daniel."
"Unaogopa nini wewe niambie au mimba imengia?"
"Hapana bora ingekuwa mimba ningejua baba yake yupo."
"Ni nini sasa?"
"Ni kuhusu baba yako."

"Amefanyaje?" aliniuliza Daniel kisha nikaanza kumsimulia kila kitu. Nilipomaliza kumsimulia nikamuona akivuta pumzi ndefu na kuziachia kwa pupa, kama ilivyokuwa kwa Baba yake na yeye pia hakutaka kuamini, kitendo cha kuwachanganya kimapenzi na Baba yake kilimuumiza mno.

Nilishangazwa na maamuzi aliyoyachukua Daniel, hakutaka kuendelea kuushuhudia uchafu kama huo ukiendelea mbele yake, alichoamua kukifanya ni kuniambia kuwa siku hiyo ndiyo ulikuwa mwanzo na mwisho wa mapenzi yetu, hakutaka kusikia nikimuita mpenzi tena.

Niliumia sana baada ya Daniel kuchukua maamuzi hayo, mtu ambaye niliamini ndiye angeweza kuwa msaada wangu kwa wakati huo hakutaka kunisikia hata mara moja.

Maisha yalibadilika ndani ya nyumba, kila siku nilikuwa ni mtu wa kumuomba Mungu aninusuru na mabaya ambayo yangeweza kunitokea. Nilifahamu hapakuwa na amani tena, kuanzia Baba na Mtoto wote walikuwa na visasi juu yangu, hawakunitazama kwa macho ya wema tena, nilionekana kuwa mbaya tena adui mkubwa ambaye walitakiwa kuniepuka.
Vitisho havikuishia hapo, Mzee Gidion aliendelea kunitishia kuniua kila kukicha, wakati mwingine alikuwa akiniambia ni lazima niondoke katika nyumba yake nikiwa maiti ndani ya jeneza.

Wakati yote haya yakiendelea mke wake alikuwa hafahamu lolote, iliendelea kubaki siri katika moyo wangu mpaka pale nilipoanza kukosa uvumilivu, nilitishiwa sana, sikuwa na amani tena katika moyo wangu, uhuru wangu wote ulipotea, nilikuwa nikiishi maisha kama ya mfungwa aliyetoroka gerezani.

Wazo la kutoroka likanijia kichwani, nilichokuwa nikikiwaza kwa wakati huo ni kutoroka na kwenda mbali. Sikuwa mwenyeji wa jiji la Daresalaam, tangu nilipoweza kufika kwa mara ya kwanza maisha yangu yote yalikuwa ni ya kukaa ndani, labda siku moja moja za wikiendi niliweza kupata bahati ya kupelekwa katika fukwe za Coco ambapo hata njia ya kufikia huko nilikuwa siifahamu.

Nadhani unaweza ukaona ni kwa jinsi gani nilivyokuwa mgeni katika jiji hili. Wakati ambapo nilikuwa sifahamu mtaa hata mmoja tayari nilikuwa nimejiwa na wazo la kutoroka. Unafikiri nilifanikiwa katika mpango huu? Jibu ni hapana, niliendelea kujiuliza maswali ambayo yalizidi kuniumiza kichwa.

Inaendeleaaah
Powered by Blogger.