KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Mama vannessa sehemu ya kumi na nne (14)

hadithi nzuri ya kusimumua ya mapenzi
“Lakni nini? Sikia nakuomba usiwaze tena kuhusu ile kazi yako ambayo ulikuwa ukiifanya mwanzo. Ile itakutia matatizoni zaidi. Tena usiangaike na habari za kwenda sijui idara ya kazi ni kupoteza muda wako. Baba Vanesa ni mtu anayeheshimika sana na ni mtu muhimu sana kutokana na michango yake ingawa hayo yake ya ufirauni na uhuni huwa hayapewi uzito. Ana watu wengi sana hivyo hutoweza kumshinda.

“Mama Vanessa nakuelewa sana na nipo tayari lakini tambua roho inaniuma sana. Kwa nini anipokonye mke wangu?.Mwanamke niliyetoka naye mbali. Mwanamke ambaye nimemsomesha na kumgharamia sana.

“Pole sana najua unaumia lakini ngoja nikuulize kitu, kwenye maisha wewe unataka nini hasa?

“Furaha amani upendo na maisha bora”

“Unahisi siwezi kukupa vyote hivyo”

“Sina uhakika”

“Ok mimi nitakupa chochote utakacho na ata ukitaka aniwe mke wake itakuwa sema nini unahitaji ambacho ndicho hofu yako kubwa?”

“Familia, mimi ni kijana ambaye umri umeenda nilivyooa nilitarajia yule mwanaume anizaliwe mtoto na mimi niitwe baba.

“Jambo rahisi sana mimi nipo tayari kuuzalia mtoto ila kwa sharti moja?

“Kunizalia mtoto!!! Sharti gani hilo?

“Kwamba tutafanya siri na tutammbambikizia hiyo mimba baba Vanesa. Alafu baadaye mtoto akishakuwa ndo utamchukua.

“Mmmm sikuwahi kuwaza kama unaweza kuwa tayari kwa kila jambo. Lakini mama Vanesa kwanini unataka kunifanyia yote haya?

“Kwa sababu nakupenda”.

Lucas ilibidi awe mpole alishindwa kuelewa huyo mwanamke kwa nini aliamua kujitoa muhanga kiasi hicho. Hakuelewa na haukamini kama mke wa boss wake anaweza kumkubali kiasi hicho na eti yupo tayari hata kumzalia mtoto.

INAENDELEA
Powered by Blogger.