KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo: Mama vannessa sehemu ya ishirini na moja (21)

Hadithi nzuri ya kusimumua ya mapenzi ya mama vannessa
“Eee mbona mimi sijawahi kukuona kwani unaishii wapi”.

“Naishi mjini Mwanza na nasoma huko huko huku nakujaga tu likizo kumsaliamia bibi.”

“Ooooh sawa, asante kwa kunikinga na mvuaa”

Safari iliendelea mpaka wakawa wamefika kwa kina Mishel. Lucas kipibdi hicho ndo kwanza alikuwa ameenza kumiliki simu.

“Samahani Mishel utakuwa na simu?”

“Jamani mimi simu niipate wapi?

“Sasa huwa unawasialiana vipi na ndugu zako”

“Huwa natumia ya mama.

“Basi chukua namba zangu …….”Lucas alijikuta akitaja namba kwa mtu ambaye hana simu.

Mishel akamwamba asijlai akifika nyumbani atachukua simu ya mama yake na kumtafuta.

“Ebu nitajie kama kweli umezishika hizo namba.” Mishel alirudia kuzitaja namba hizo bila kukosea.

Lucas lalifurahi sana na kuona msichana huyo alikuwa na uwezo mkumbwa wa kukariri. Aliondoka zake na kurudi nyumbani. Alikaa kwa muda wa siku tatu bila kupokea simu kutoka kwa Mishel. Kila siku alikuwa akipita kwenye ile nyumba ili aweze kuangalia nini kilikuwa kikiendelea na kama anaweza kumuona binti huyo. Haikuwa hivyo hakuweza kabisa kumuona binti huyo. Ilikuwa ngumu sana kwake na roho ilimuuma maaana muda wa kufungua shule ulikuwa umefika. Hatimaye aalifungua shule na kuondoa zake. Roho yake ilimuuma sana kwa maana simu shuleni walikuwa wakikatazawa na hata wakituia kwa ujanja uajnja sana sana ni wikiend

Mwezi mzima ulipita kabla ya siku moja kupokea simu ngen kutoka kwa msichana. Sauti hiyo nyororo iliyosisimua masikioni mwake haikuw aya mtu mwingine bali ya Mishel. Mishel alaimweleza kuwa namba zake alikuwa bado anazikumbuka na hakumtafuta kwa sababu siku ile walivyoachana alaianza kuugua na alailaza. Huo ukawa mwanzo wa mawasiliano yao. Mpaka Mishel anamalaiza form four na Lucas anamalaiza form sx watu hawa walikuwa wapenzi wa kwenye simu. Baada ya Mmishel kumalaiza form four alaienda Dar kwa dada zake wengine ambao kipindi hicho walikuwa wameolewa. Na kama bahati vile na Lucas alienda huko huko. Wawili hawa sasa waliweza kukutana.

Lucas mawazo yakaamia siku ya kwanza kabisa kushiriki tendo la ndo na binti huyo. Anakumbuka aaimkuta binti huyo akiwa na bikira kabisa. Anakumbuka jinsi alivyopata tabu kukivunja kikombe cha udongo cha binti huyo. Anakumbuka jinsi alivyoangaika nae kufanikisha hilo. Tangu siku hiyo ukurasa wa mapenzi baina yao ulikuwa umefunguliwa. Mishel alikuwa akimpenda sana nay eye alikua akimpenda sana. Kuna vipindi vigumu walivyopitia na vyote walikuwa wakivikumbuka. Moja ya kipindi kigumu ni pale Mishel mataokeo yake yalivyotoka hayakuwa mazuri hivyo ilimlazimu kubaki Dar kwa dada yake wakati Lucas akaiendelea na chuo. Huko Dar Mishel alijifunza hizo kozi fupi ndani ya mwaka. Baaada ya hapo sasa aliajiriwa. Uzuri wake ukawa chachu ya kuwavutia wanaume wengi ikiwemo boss. Mishel alibadilika sana na hakumthamini tena Lucas. Mishel jiji lilimkubali sana alikuwa mrembo mara dufu. Hakuwa wa hadhi ya Lucas tena bali alikuwa akitoka na watu wenye fedha zao. Kipindi hicho Lucas alikuwa ameijiunga na masomo kwenye chuo kikuu cha Dar es salaam. Hapo safari ngumu na histori ya uhusiano wa watu hawa ndipo ilipokuwa ndefu. Lucas alikuwa akaimpenda sana bint huyo na hakuweza kabisa kukubaliana na matokeo kuwa aliachwa kwa kigezo kuwa hakuwa na fedha. Roho ilimuuma sana na hakuamini kuwa kama kweli binti huyo amebadilishwa na starehe za jiji. Tukio hili lilimfanya Lucas kumwaga machozi na aliona tabia ni kama ngozi ya mwili huwezi kuibadili.

Maisha ni safari mbwembwe za Mishel ziliishia njiani mara baada ya waliokuwa wakimpa kiburi kuanza kumyanyasa. Walimchoka baada ya kupata walichopata. Mishel alichoka akachakaa hiyo ni mara baada ya kuugua kwa muda mrefu na haikujulikana alikuwa akiumwa nini lakini afya yake ilikuwa imedhoofu mno. Uzuri wake ulifubaa na alififia machoni kwa wanaumme wakwere. Fimbo ya shida za maisha ilimpiga maana hata dada yake aliyekuwa akimpa hifadhi alifariki dunia. Mishel ilimlazimu kurudi kijijini ambapo alikuwa hana mbele wala nyuma. Huko ndipo Lucas alipopata kumuona tena.Alimuonea sana huruma maana binti huyo alianza kuzeeka ingali alikuwa bado mdogo. Mishel alimuomba msamaha Lucas na kumtaka amsamehe tu kwa yote aliyomtendea hata kama hawatakuwa tena wapenzi.

Lucas kama ilivyo imani ya dini yake aliamua kumsamehe binti huyo lakini alisema kuwa kwa sasa watakuwa kama kaka na dada. Lucas akamshauri binti huyo arudie mtihani wa kidato cha nne na akafanikiwa kwenda form five basi yeye atamsomesha. Mishel kwa kuwa hakuwa na mbele wala nyuma alikubaliana na mawazo hayo. Lucas kwa kutumia pesa ya mkopo aliyokuwa akipewa chuoni aliweza kumlipia pesa ya usajili. Lucas alikuwa na moyo wa ajabu sana maana alirudisha moyo wa pendo kwa binti huyo. Akaanza kumuhudumia kwa vitu vingi na hatimaye urembo wa binti huyo ukaanza kuonekana tena. Kadri siku zilivyozidi kwenda walikuta wakitamaniana nakutamani kuvunja ahadi kuwa kwa sasa wataishi kama kaka na dada. Lucas pia alivutiwa na mwenendo wa Mishel maana aliokoka na kuwa mcha Mungu. Mishel alikuwa wa kusali na kuomba yeye na biblia biblia na yeye. Shetani aligeuka kuwa malaika.

INAENDELEAA...
Powered by Blogger.