KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Ni Shiida! Sehemu Ya Sita (6)

 LOVE STORY: ni shiidaI - 4
Wakati Juliana anampa mama yake simu, mkono ukalegea, ikaanguka chini na kuvunjika kioo…
"Mama simu yangu jamani."
"Mbona umelegea mikono wewe, ala!" alifoka mama mtu. Akaendelea…
"Hakijaaribika kitu, toa laini niweke kwenye simu yangu, nataka kumjua huyo Bitte unayemsema wewe ni nani?"

"Kwani mama wewe umefikiria ni nani?"
"Ndiyo nataka kumjua."
Moyoni Juliana akasema…
"Ungejua si Bitte ni Bitungu…"
Naye mama mtu moyoni akasema…

"Ungejua nafananisha jina hilo na la dogodogo wangu Bitungu."
Juliana alitoa laini, akampa mama yake huku simu yake ikiwa imezima baada ya kuanguka. Naye mama mtu aliichukua laini na kuipachika kwenye simu yake, akawasha. Yalikuja majina mengi sana lakini jina la Bitte halikuwepo. Maana yake ni kwamba, jina liliseviwa kwenye simu yenyewe ‘hand set', au wanasema ‘phone book'.
"Hebu lete simu yako."

Juliana alimpa mama yake simu, akatoa laini na kuipachika humo tena, akawaisha, simu haikuwaka kutokana na kule kuanguka.
Akamtupia simu mtoto wake huku akisema…
"Nitataka kumjua huyo Bitte."
"Sawa mama."

***
Bitungu alishangaa kumkosa Juliana kwa siku hiyo, kila alipompigia ilionekana simu yake imezimwa…
"Huyu leo vipi tena?" alijiuliza kijana huyo.

Juliana alifika kwa fundi na kueleza shida ya simu yake, akaambiwa ni lazima ibadilishwe kioo lakini gharama aliyotajiwa ilimshinda, akaamua kwenda kununua simu ya tochi kwanza.
Hata hivyo, alijua hataweza kumpata Bitungu kwa sababu namba zake ziko kwenye simu iliyokufa kioo.
Alinunua simu, akarudi nayo nyumbani ili kuiweka kwenye chaja kwa muda. Lakini nyumbani hakumkuta mama yake na akashindwa kujua aliko.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya nusu saa, Juliana alichomeka laini kwenye simu yake ya tochi, akaiwasha. Ndani ya dakika moja meseji kibao zikaanza kuingia mfululizo, ikiwemo ya mama yake akimwambia anatoka kidogo.
Ikaingia nyingine iliyomwonesha kwamba ni ya Bitungu kwani ilisema…

"Baby mbona sikupati hewani? Ujue unanipa wakati mgumu sana mwenzio?"
Juliana aliipiga simu hiyo. Wakati simu inaita, Bitungu alikuwa amekaa na mama Juliana…
"Hebu pokea simu kwanza mpenzi wangu ndiyo tuendelee na mambo mengine," alisema mama Juliana, lakini naye Bitungu alipoona ni Juliana aliogopa. Hata hivyo, ili kuua soo aliipokea huku akipunguza sauti…

"We vipi mbona hupatikani kwenye simu?"
"Simu mbovu my dear, kweli tena!"
"Pole sana, mi nilikuwa sijui."
"Ndiyo hivyo. Uko wapi?"
"Nipo mitaa ya Sinza Palestina, nitakutafuta baadaye."
"Poa."

Baada ya kukata simu, mama Juliana alishangaa kuona simu yake iikimpa mrejesho kwamba meseji aliyotuma kwa Juliana muda fulani ndiyo inamfikia sasa, akampigia…
"Umetengeneza simu?"
"Bado mama, pesa ni nyingi nimeamua kununua simu ya tochi kwanza."
"Sawa, ilimradi simu."
"Uko wapi mama?"

"Nipo maeneo ya Sinza Palestina japokuwa sipendi kuulizwa nilipo na wewe," alisema mwanamke huyo huku akimshikashika mwilini Bitungu. Walikuwa ndani ya gesti.
Baada ya kukata simu, Juliana alijiuliza maswali mawili ya msingi sana…
"Mama anasema yupo maeneo ya Sinza Palestina, Bitungu naye anasema yupo mitaa ya Sinza Palestina. Inawezekana wapo wote?

"Mmh!" aliguna baada ya kukosa jibu na kuamua kuachana na hayo.
Muda ulivyozidi kwenda alihisi kwamba mama yake akirudi lazima atataka kumjua Bitte kwa maana ya kumuuliza maswali mengi. Lakini pia aliisevu namba ya Bitungu upya, akaandika Stella Goms, yaani Stella wa Gongo la Mboto.

INAENDELEEA
Powered by Blogger.