KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Simulizi : Shida Sehemu Ya Kumi na moja (11)

Hadithi nzuri ya kusisimua ya shida
Kijijini Itogocha mkoa Singida familia ya Bibi Lea ilikuwa na mjadala mzito jii ya sehemu watakayopata kuni za kupikia

"Mama kuni zimekuwa adimu sana tutafanyaje?" aliuliza mwanaye Amina

"Kazi ipo mwaka huu,tufanyeje sasa? Tuingie ndani ya msitu?" akatoa oni mama yule

"Mimi msituni siend mama,nasikia kuna wanyama wanaua watu" akajibu Lea

"Mwanangu mimi naamini ni vitisho vya watu tu,mbona hatujawahi kupata taarifa ya mtu yeyote yule aliyewahi kuliwa na hao wanyama?" akajibu mama yule

"Hata kama mama lisemwalo lipo na kama halipo laja" akajibu Lea

"Hapa cha msingi tuandae mbwa wetu wote tuondoke nao kwenda huko,tofaut na hivyo mnipe mikono yenu nipikie" akajibu mama yule

"Mama mimi siendi" akajibu Amina

"Na mimi siendi" akajibu Na Lea

"Hamuendi? Sasa ingien tulale njaa ikiwashika mtaenda wenyewe" akajibu na kuingia ndani

Kweli mama yule alikuwa hatanii,siku hiyo usiku mji ule kwa sababu ya kukosa kuni walishindwa kupika na mama yule pia aligoma wasipike

Asubuhi kila mmoja aliamka akiwa na njaa kubwa sana

"Mama mimi niko tayali twende kutafuta kuni" alikuwa wa kwanza kuongea Amina

"Hata mimi mama niko tayali" na Lea akasema

"Hee! Kweli njaa noma,mbona hata salam sijapata mmekimbilia kufata kuni?" akaongea yule mama

Wakakaa kimya kwa aibu na baadae wakamsalimia mama yao.

Basi jiandaeni saa nne tuelekee huko

Kweli ilipotimia saa nne waliondoka na mbwa wao kuelekea porini kufata kuni.

"Naombeni tuingie ndani sana wanangu,acheni kukata kuni huku nje,mnaokota vidogo vidogo" mama alitoa tahadhali

Basi wakaondoka na kuzidi kuingia ndani kabisa ya msitu ule

Wakati wakiendelea kukata kuni huku wakizidi kuingia ndani

Ghafla mbwa wakaanza kubweka kwa nguvu wakielekea kwenye kichaka kikubwa kilichokuwa eneo lile.

Mbwa walibweka kwa nguvu sana huku wakikizunguka kile kichaka

"Mama kuna nini huko? Mbona mbwa amekazana kubweka?" Amina akauliza

"Hata mimi sijui mwanangu" akajibu

"Mmmh! Labda ndo kuna wanyama wakali huko mama tuondoke" akashauri Amina.

"Hapana mnyama mbwa hawe kwendapo angekimbia" akashaur yule mama

"Nipeni panga" akaomba

Mama yule hakuwa muoga kabisa.

Akasogea kalibu kabisa na eneo lile,akachungulia ndani hakuona kitu



Akazidi kuchungulia ila hakuona kitu ndani

Wale mbwa walipoona yule mama kasogea pale wakapata ujasiri na kuingia ndani ya kichaka.

Baada ya kuona mbwa wameingia ndani na yule mama akaingia ndani

"Lahaula!!!! Huyu si ni binadam jaman" alijikuta akiongea kwa sauti

Wanaye baada ya kuona mama yao ameingia na kupiga kelele ikabidi na wao wawahi kuingia kule kwenye kile kichaka

"Kweli ni mtu jaman" Amina akasema

Mama Lea aliinama na kumukagua yule aliyelala pale chini

"Atakuwa kauawa huku wamekuja kumtupa huku" alisema

Alipojalibu kumkagua

"Mbona bado ana joto? Atakuwa mzima huyu......mbona anapumua?" akasema

Baada ya kumkagua alijihakikishia kuwa yule binti ni mzima

"We Amina hebu mshike miguu tusaidiane kumbeba tumtoe humu ndan" alitoa maagizo

Walimbeba na kumtoa ndani ya vichaka vile.

Walipofika nje wakamtoa matambala aliyofungwa mdomoni na kisha wakaanza kumfungua kamba kwenye mikono na miguu.

Mikono na miguu kuanzia eneo alilofungwa lilikuwa jeusi sana kutokana na kamba kuzuia damu kupita kuelekea maeneo yale

"Jaman watu wana roho mbaya sana, kweli binadam mwenzako unamfanyia hivi?" aliongea yule mama

"Mmmmh! Hata mimi siamin mama" akasema na Amina

Walisaidiana kumbeba kutoka kule porini mpaka kijijini kwao.

Walipofika moja kwa moja wakampeleka kwa mwenykekiti wa kijiji kile

Walipofika walimweleza kila kitu na mwenyekiti akatafuta vijana wenye nguvu na kusaidia kumbeba kuelekea Dispensary ya pale tarafani.

Alipokelewa pale dispensary na kupewa huduma ya kwanza

"Jaman huyu hapa hatuna uwezo wa kumhudumia, tunaomba mmpeleke wilayani" alishauri daktari aliyekuwa pale

Ilibidi usafiri wa haraka utafutwe na Shida akasafirishwa kuelekea Hospitali ya Wilaya Singida.



Hospitali ya Wilaya



Alipofikishwa alipokelewa haraka na kupelekwa ICU chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na hali yake kuwa mbaya sana.

Damu ilikuwepo ya akiba na moja kwa moja ikaanza kutililika kuingia kwenye mishipa ya mwili wake.

Vipimo vikachukuliwa haraka sana na baada ya muda majibu yakatoka

"Anaonekana kuwa na maralia kali sana ila vitu vingine yuko sawa kabisa" alisema Daktari

Akatundikiwa drip ya dawa ya maralia huku akiendelea na matibabu mengine.

Taarifa ilitumwa kituo cha polisi na baadhi ya askari wakafika ili kupata maelezo kidogo.

Mama Lea ndiye alityetoa maelezo yote kutokana na jinsi alivyolifahamu tukio lile.

"Mama umesema umemkuta ametupwa porin?" aliuliza Askar

"Sio ametupwa,sisi tulimkuta kicchakan akiwa hana fahamu huku amefungwa kamba miguu na mikono,sasa kama alitupwa mimi sijui" alieleza.

"Sawa,je kuna mtu yeyote yule ambaye ameonesha kumtambua?" akauliza tena Askar yule

"Mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyemtambua" akajibu Mama Lea

"Sawa mama tunashukuru kwa ushilikiano wako,tukihitaji msaada zaidi tafadhali usisite kutusaidia" akasema tena yule Askar

"Sawa,nitafanya hivyo" akajibu mama Lea

Matibabu ya Lea yaliendelea vizuri na baada ya saa nane alipata fahamu.

Ilikuwa furaha kwa wale madaktari

"Sikutegemea kama ataamka,hali yake ilikuwa mbaya sana" alisema dakatar

"Hata mimi dokta,nilikata tamaa,ila amepata fahamu mapema sana" akajibu nesi

Taarifa ile ilikuwa nzuri kwa mama Lea alipotaka kumuona alizuiwa

"Hata hawa askari hatutawaruhusu kumuona kwa sasa,mpaka tuhakikishe hali yake iko sawa" alisema daktari

Kila mmoja alikubaliana na hali ile ingawa kila mmoja pia alikuwa na ham ya kuongea naye ili kujua yaliyomkuta.

Baada ya saa nzima Shida alikuwa na uwezo wa kuongea

"Pole mwanangu,tumshukulu Mungu umepona" alisema Mama Lea baada ya kuruhusiwa kuingia kumuona akiwa na wale askari.

"Ahsante,,kwani wewe ni nani? Na hapa nimefikaje?" aliuliza

"Mwanangu nimekuokota huko porini ukiwa na hali mbaya sana,wakushukuliwa ni Mungu,hatukutegemea kama utapona " akajibu yule mama Lea

"Aaah pole sana binti" akasema askar

Shida alishtuka sana kumuona yule askari pale,

"Hawa wamejuaje? Inamaana kuna matatizo tena?" alijiuliza

"Ahsante sana" alimjibu Askari yule

"Samahan sana binti,sijui unaitwa nan?" akauliza Askar

"Naitwa Shida!" akajibu

"Samahan binti unaweza kutuelezea kilichokukuta?" akauliza Askar

Shida alifikilia sana juu ya kujibu swali lile.

"Nikiwaeleza hawa hili swala,lazima watafatilia kumshika Alex,na yeye anapesa sana anaweza kuhonga na kuachiwa kisha kuniua,inapaswa ninyamaze ili Alex ajue nilishakufa,la sivyo sasa aataniua kiukweli ukweli" aliwaza

Pale pale akapata akili ya kufanya ili kuepuka kujibu swali lile.

Ghafla wote waliokuwa pale walishangaa kuona Shida akitoa machozi na akaanza kulia

Alilia sana huku wakimbembeleza ili anyamaze ila hakunyamaza.

Ghafla akaanza kushtuka kama mtu anayekata roho.



Wakachanganyikiwa!!!!

"Dokta nini kimetokea???" aliuliza yule askari

"Naomba kila mtu atupishe tumshughulikie mgonjwa kwanza" akajibu Dokta

Watu wote wakaondoka pale ndani huku wakiwa hawaelewi nini kimemtokea Shida

Baada ya watu wote kutoka nje

Shida aliamka na kukaa, hali ile ilimshtua sana dokta

"Shhhhhhiiiiiiii!!!!" akamfanyia daktari ishara ili anyamaze


**********



:: Unavyodhani nini kitaendelea?





ITAENDELEA

Powered by Blogger.