Simulizi : Shida Sehemu Ya Kumi na Nne (14)
Alipowaona alipigwa na butwaa na kubaki akiwa na wasi wasi sana
Hawakutaka kuongea naye chochote,walipita moja kwa moja na kutoka nje ya geti na kisha moja kwa moja wakaelekea kituo cha dala dala wakachukua pikipiki
"Tupeleke iguguno" akasema David
"Kwa nini tusiende stand David? Iguguno ndo wap? Na kwa nini tutumie pikipiki?" akasema Shida
"Acha maswali twende, utajua mbele ya safari" akajibu David
Wale boda boda hawakuhoji kitu bali waliwasha pikipiki zao na safari ikaanza na baada saa moja na dakika arobaini na tano wakawa wamefika Iguguno
David aliwalipa na kisha wakaondoka na kutafuta gesti ili wapumzike
Baada ya muda wakawa wamepata na walipoingia ndipo maongezi yakaanza.
"Kwa nini tumekuja hapa David?" akasema Shida
"Baba yangu sio mtu mzuri kabisa" akasema
"Kwa nini?" akauliza Shida
"Baba yangu nje ya udaktari anafanya biashara haramu ya madawa ya kulevya, ndiyo maana maisha ya pale nyumbani ni ya juu sana,
Swala la kuua kwake si tatizo, ni kitendo cha kufanya tu
Mama yangu aliuawa na baba nikiwa na miaka kumi na mbili ingawa baba alinificha ila baadae nilikuja kujua
Kilichosababisha nijue ni mke wa pili ambaye baba alimuoa
Yule dada alikaa na baba miezi saba na nilipokuja likizo akanielezea kuwa yuko hatarini kuuawa
Nilipombana sana akanielezea biashara anazozifanya baba na kuwa baada ya yeye kugundua yule mzee amepanga kumuua
Na hapo ndipo aliponiambia kuwa hata mama yangu aliuawa na baba mara baada ya baba kugundua kuwa ana mahusiano na kijana mmoja hivi
Cha ajabu nilipovuta kumbukumbu nilikumbuka kuwa baada ya mama kufaliki siku chache baadae kijana huyo naye alifaliki
Kutokana na hilo niliyaamin maneno ya baba yangu, nikaanza kufatilia nyendo zake bila yeye kujua
Kweli baada ya siku chache nilimfatilia na kumshuhudia akumuua yule mamdogo kwa macho yangu
Nilishtuka sana na ndipo nikaondoka kurudi kazini na sikutaka kurudi huku mpaka nilipopata taarifa kuwa baba anaishi na wewe
Baba alinieleza historia yako nzima, nilipokuja hapa nilivutiwa na wewe na kukupenda nikaona nikuokoe ila kwa bahati mbaya tumewahi kushtukiwa kabla hatujatimiza lengo letu
Ila nilipanga kukutolosha kutoka pale nyumbani
Kilichosababisha nije hapa ni kuwa,baba ana mtandao mkubwa sana wa vijana wahuni wanaofanya nao kazi hii hivyo tungeenda stand tungepatikana haraka
Nataka tujifiche hapa kwa siku chache ili asahau kisha tuendelee na safar yetu" akamaliza kusimulia David
"Dah! Mbona sura yake haifanani na hayo mambo?" akauliza Shida
Kabla hajajibiwa walishangaa mlango ukigongwa kwa nguvu na kubomoka kuingia ndani
Mbele yao wakasimama vijana waliojazia na wenye sura za kutisha sana
"Unadhani ni rahisi kumkimbia mzee wako?" mmoja wao aliuliza
Wale vijana waliingia chumbani pale na kuanza kuwatoa David na Shida
"Kwa akili yako ndogo unafikili unaweza kumkimbia baba yako?" akauliza mmoja wao
David alinyamaza bila kuwajibu ila walipojalibu kuwanyenyua David alijalibu kuleta upinzani
Wakaamua kufanya kama walivyoagizwa na bosi wao
David alipigwa na kitako cha bunduki kalibu na jicho na kuanguka chini damu zikaanza kuvuja kwa speed kubwa sana
Ilibidi Shida awe mpole ili kuepuka mengi
"David tulia tu,watatuua hawa" akasema Shida
Wakamnyenyua David na kuondoka naye pale gest wakiwa wamemwekea silaha kwa siri ili asijalibu kuleta ujanja wowote ule
"Ukileta ubishi kifo kitakuwa haki yako,hayo ndiyo maagizo ya bosi" akasema yule jambazi
Waliondoka pale gest bila kushtukiwa na mtu yeyote yule mpaka kwenye gari na moja kwa moja wakaiwasha na kuanza kurudi na njia ya kuelekea Singida mjini
"Tafadhali ndugu zangu,naomba muwe na utu,niambie kias cha pesa mnachokitaka nitawapa mniachie na baba mkamwambie mmenikosa" akajalibu kujisaidia David
"Hatujawahi kuhalibu kazi ya mzee wako hata siku moja kwa hiyo usitegemee kitu kama hicho" akajibiwa
"Lakin naamin mkimwambia mmenikosa hatajua na mimi nitapotelea sehemu asiyoijua" akasema David
"Nahisi unajisumbua kijana,kwa sababu sisi tunaijua roho ya baba yako,tukifika pale bila wewe sisi ni maiti" akajibiwa
David akabaki bila ujanja wa kufanya ili kujinusuru na jangalile
Walipotembea kilomita sita kutoka Iguguno wakakutana na basi mbele yao likipunguza kasi
Wakataka kulipita ile mbele wakaona magogo yametegwa njian
Ni kitendo cha ghafla sana vijana kumi wakatoka vichakan wakiwa na silaha kali sana na kupiga risasi juu na magari yote mawili yakawekwa chini ya ulizni
"Vip mkuu tujibu mashambulizi?" akauliza mmoja akimuuliza kiongozi wao pale
"Hapana,tulia kwanza,ila wakija hapa kuleta ujinga tunazaa nao" akajib
Vijana watatu walilifata lile gari alilokuwepo David na wale vijana waliowateka na wengine saba wakaliteka basi lile
Wale vijana walipolikalibia like gari la kina David wakaanza kuwaamuru wote watoke nje ya gari
Majambazi wale walitoka vizuri mpaka nje na akina David pia wakatoka
"Jisachi ulichonacho na utupe hapo mbele, ujanja hatutaki na msipotoa kitu itabidi mvue nguo zote na kurud kwenye gari uchi" agizo lilitolewa
Kama kuna ujinga walifanya wale watekaji ni kujisahau kwani pale pale mmoja wa wale vijana wa Dokta alitoa bastola yake na kuwaua wale watekaji wote.
Milio ya zile risasi zilileta kizazaa kwa wale watekaji waliokuwa wamelidhibiti basi
Wakatoka speed na kuanza kutupiana risasi na vijana wa Dokta
Pale pale kwenye ule mpambano David alimvuta Shida kwa nyuma pole pole bila kuwashtua wale vijana wa Dokta kushtukia
Mapambano yalizidi kuwa makubwa huku risasi zikitawala eneo lile
David alipoona vijana wa Dokta wamekazana kupambana akamshika mkono Shida na wakaanza kujongea kuelekea kwenye vichaka vilivyokuwa kalibu na eneo lile
Wakati wanazama kichakani mmoja wa Vijana wa Dokta aliweza kuwaona
"Oyaaa oyaaa wanatoloka wale kuleee" alisema
Na wenzake wote wakashtuka na kuangalia upande ule walikooneshwa
Walipiga risasi kuelekea upande ule kwa fujo na zikampata David na akaanguka chini na kutulia
Kitendo cha kugeuka kuwaangalia akina David kiliwapa nafasi wale watekaji cha kuongeza speed ya mashambulizi
Na ndani ya muda mfupi wale Vijana wa Dokta wakajikuta mmoja baada ya mwingine wakianguka chini baada ya risaasi kadhaa kupenya kwenye miili yao
Ndani ta dakika chache wote walikuwa tayari wako chini.
Wale watekaji wakawasogelea kuhakikisha kama wamekufa.
Walipofika wakawamalizia kwa risasi nyingi za kwenye miili yao
"Kuna wenzao wamekimbilia vichakani humo inabid na wao tuwamalize hawawezi kuwaua wenzetu kijinga hivi" akasema mmoja wao
Hayo maneno Shida aliyasikia vizur akiwa kule kichakani na mwili wa David ukiwa chini pembeni yake
"Mungu wangu nimekwisha!!!" aliwaza mwenyewe
Dokta akiwa na jazba sana alisubiri wale vijana wake warudi ili apate nafasi ya kuwashughulikia David na Shida
"Wapuuzi sana hawa vijana, na huyu binti pamoja na fadhila zote nilizompatia anafanya upuuzi wa kunichanganya na mwanangu? Hukumu yake ni kifo" aliwaza
Kitu ambacho Dokta hakukumbukua ni kuwa yeye ndiye chanzo cha Shida kumsaliti, kwani kitendo cha kumwibia siri ya Shida kutaka kuuawa na baba yake wa kufikia Alex ndicho alichotumia David kumpata Shida kiurahisi
Alisubiri sana ila wale vijana hawakurejea
Alipochoka kusubiri ilibidi ajadiliane na vijana wachache waliobaki pale ili wajue cha kufanya
"Kwani bosi huna namba ya Ally umpigie tujue kinachoendelea?" aliuliza mmoja wao
"Kweli nimechanganyikiwa! Sijakumbuka hilo, ninayo ngoja nimpigie" akasema Dokta
Alitoa simu yake na kujaribu kupiga namba ya Ally tall kijana wake anayemuamin katika kufanya matukio makubwa ya mauaji
Simu ya Ally tall iliita mpaka ikakata bila kupokelewa, akajalibu tena hali ikawa ile ile
"Hebu mpigie wewe labda anaogopa kupokea simu yangu" akasema Dokta
Kila aliyejaribu kumpigia simu ya Ally tall iliita bila kupokelewa na walipojalibu kupiga za wengine nazo majibu yakawa hayo hayo hazikupokelewa
**********
:: Unavyodhani nini kitaendelea?
ITAENDELEA