KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Simulizi : Shida Sehemu Ya Kumi na Tano (15)

Hadithi nzuri ya kusisimua ya shida
"Hivi inawezekana Ally asipokee simu yangu? Hapana, au keshanisaliti kwa vipesa kidogo vya huyu bwana mdogo?" aliwaza sana

"Dokta haina haja ya kusumbuka, Iguguno sio mbali, naomba tupande gari tuwafatilie huwezi jua nini kimetokea huko?" akashauri mmoja wa wale vijana

Wazo lile likaonekana jema na pale pale safari ikafungwa kuelekea Iguguno kuwafatilia vijana wale walioenda kuwakamata akina Shida



* * * *



Baada ya kutembea zaidi ya kilometa kumi na tano wakaona basi limepaki njian

Walipolifikia wakasimamisha gari, cha ajabu wakakuta damu nyingi sana zimezagaa pale chini

Nyuma ya lile basi wakashangaa kukuta gari yao waliyokuwa wametumia wale vijana aliowatuma kuwateka akina David

Walipolikimbilia wakashangaa zaidi kukuta miili ya wenzao ikiwa imelala chini ikiwa haina uhai na risasi kadhaa zikiwa zimeihalibu miili ile

Kila mtu alistaajabu ikabidi warudi kwenye lile basi na kukuta watu wote wakiwa wamelala chini huku wengine wakiwa wameuawa na wale walioko hai wakiwa uchi wa mnyama

"Nyie vipi? Nini kinaendelea hapa?" akasema Dokta

Wale waliokuwa kwenye basi wakajua bado wale majambazi hawajaondoka na wapo pale ili kuwamalizia hivyo wakazidi kujichimbia chini ya viti

"Acheni ujinga, amkeni haraka mkae kwenye viti" akafoka Dokta

Wale watu wakaanza kunyanyuka mmoja baada ya mwingine ila kwa tahadhali kubwa sana.

Cha kwanza walichokifanya ni kila mmoja kukimbilia nje kuchukua nguo yake ili avae

Mtafaruku uliotokea pale si wa kitoto hasa pale watu walipokuwa wakivaa nguo za wengine

Baada ya muda kila mtu akawa amekwisha kuvaa na kuwa sawa ndipo mijadala ikazuka na Dokta akapata taarifa ya kilichotokea.

"Sisi tulifika hapa na kukuta magogo kadhaa yamelazwa hapo na wakati tunashangaa wakatokea vichakan vijana kama kumi na kutuweka chini ya ulinzi, wakati wakianza kutushughulikia ndipo likatokea hilo gari hapo nyuma,hawa watekaji wakagawana na wengine wakalifata hilo gari, hapo ndipo tuliposikia risasi zikirindima na hawa waliokuwa humu ndani wakatoka na kwenda kuwasaidia wenzao,walipigana kwa muda mrefu mimi nilikuwa nachungulia dirishani nikaona wenzao na wale wa lile gari la nyuma wawili wakikimbilia vichakan, hao vijana walipoona wenzao wanakimbilia vichakani wakawashambulia na muda huo huo ndipo hawa waliotuteka wakawamalizia" alihitimisha maelezo

"Kwa hiyo walielekea vichaka gani?" akauliza Dokta

"Walikimbilia kichaka kile" akaelekeza

Dokta na wenzake wakaanza kuelekea kwenye kile kichaka walichoelekezwa

Walikutana na damu nyingi sana eneo lile na walipoingia ndani ndipo wakakutana na mwili wa mtu umepigwa risasi nyingi sana

Walipougeuza ulikuwa mwili wa David, Dokta nguvu zikamwishia

"Mwanangu David!" aliumia sana kumuona mwanae kauawa kinyama vile



* * * *

Baada ya wale watekaji kuwaua vijana wa Dokta wote, walielekea kule kichakani kuwamalizia wale walioonekana wakiingia kule

Walipofika walimkuta Shida kajikunyata kama kinda la ndege na David akiwa chini tayali akiwa ameshaaga Dunia.

Mmoja wao alikoki bunduki yake kwa lengo la kutaka kummaliza Shida ila aliyeonekana mkuu wao akamzuia

"Subiri anaonekana kama si mmoja wao? Mbona hakuonesha upinzani na kajificha muda wote wa mapambano?" akauliza yule aliyeonekana mkuu wao

Wakambeba Shida na kuelekea barabarani

"Itabidi tuondoke kwa sababu tumeshatumia muda mrefu hapa na polisi wanaweza kuwasili muda wowote" akatoa maagizo tena yule

Hawakuwa na sauti mbele ya yule mkuu wao, walimbeba Shida na safari yao ikaishia kwenye kijiji cha jilani na pale Iguguno na huko walikuwa wamepaki gari yao.

Wakapanda gari na safari ikaanza kuelekea Nzega.

Walifika Nzega jioni na kuunganisha kuelekea Tabora mjini

Walifika Tabora mjini usiku wa saa tano kutokana na gari yao kwenda kwa mwendo wa taratibu sana

"Tuonane kesho, windo ni langu" aliongea yule kiongozi wao

Kila alichokuwa akikiongea kwao ilionekana kama agizo ambalo halihitaji mjadala

Aliwashusha nje kidogo ya mji wa Tabora maeneo ya Isevya na kisha yeye akaendesha gari yake kuelekea mjini Tabora

Aliingia eneo la Kanyenye kwenye nyumba yake mlinzi akamfungulia geti na akaingiza gari yake

"Jisikie huru sana hapa binti," akasema jamaa

Sura ya huyu jamaa ilikuwa ya kutisha sana,umbo lake lilijengeka kimazoezi sana

"Naitwa Ally" alijitambulisha

Muda huo wote Shida alikuwa hajui hatima yake ni nini ila alitulia bila kuleta fujo ili ajue hatima yake

"Chumba chako cha kulala kitakuwa hiki,utafanya chochote unachotaka ila kwa sharti moja pekee,hautaruhusiwa kututoloka kwa namna yeyote ile na utafanya chochote kile tutakachokuamrisha" Ally aliMweleza Shida.

Usiku wa siku hiyo ulikuwa mgumu sana kwa Shida,alijalibu kutfuta sehemu inayoweza kumsaidia kutoloka ila ikakosekana.

Alijalibu kuwafikilia majambazi hawa ila hakupata jibu la wanachowaza juu yake, ila akili yake yote ilimtuma kuwa wanataka kumgeuza mke wao



Kila alipokumbuka maisha yake yalipopitia hasa kuanzia kubakwa na baba yake aliumia sana

Kesho yake asubuh alipewa kifungua kinywa na kisha jamaa akamchukua na kumtembeza kwenye sehemu mbalimbali za mji wa Tabora

Baada ya kupitishwa kila mahali alirudishwa nyumbani

"Naomba uwe na aman, hakuna atakayekufanyia kitu kibaya hapa,ilimradi usituchokoze na pale tutakapokupa kazi ya kufanya uifanye kwa uaminifu" alipewa tena maagizo

Hakuna kilichomuumiza kichwa kama kutokufaham hawa jamaa wanania gani naye?

Siku zilizidi kukatika huku Shida akipelekwa sehemu mbalimbali za mji huu ili auzoee.

Alilishwa vizur na kununuliwa kila aina ya nguo aliyoitaka.

Shida akapendeza, akavutia na ule uzuri wa mama yake Amina ukajitokeza kwake.

Kila baada ya siku chache wale jamaa waliondoka usiku na kurudi asubuh au siku inayofata wakiwa na vitu vingi sana walivyopora

Kitendo cha kuishi na majambazi kilimtisha Shida ila alifurahia ule wema waliomuonesha.

"Tunaomba ujiandae kesho na wewe ndo utaingia kazini, ninachokuomba ujitahidi kuondoa uoga, ukikamilisha hiyo kazi ya kesho tutakulipa milioni mbili" aliambiwa

"Lakini Ally nimeshakubali kuwa nitafanya kazi, kwa nini usiniambie aina yenyewe ya kazi?" akaomba Shida

"Utaijua wakati ukifika,cha msingi jitahidi kuondoa uoga na utafanikiwa,tena ukishazoea utatajilika sana na kazi yenyewe sio ngumu" akasema Ally

"Sawa ila naomba japo unidokezee aina yenyewe ya kai" akaomba Shida

"Wakati ukifika utajua" akajibiwa na Ally akaondoka

Siku hiyo nzima Shida alishinda akiwa hana raha kwa sababu alikuwa akifikilia kazi anayopaswa kufanya siku hiyo

Kesho yake jioni wale vijana walimchukua Shida na kumpeleka saloon akatengenezwa kwa style wanayotaka wao

Shida alipendeza sana kiasi kwamba kila mwanamme aliyemuona alimtaman

Baada ya hapo wakaelekea nyumbani na kumpatia nguo alizopaswa kuvaa

Shida alipoingia chumbani na kuzivaa alishangaa

Ilikuwa gauni fupi sana inayoishia juu kabisa ya mapaja yake,alishangaa kazi anayopaswa kufanya na nguo ya aina ile!Baada ya kumaliza kuvaa ile nguo alijiangalia kwenye kioo kilichokuwa pale chumbani na kujishangaa ila kwa sababu aliwafaham wale jamaa walivyokatili akaamua kunyamaza na kufanya kama wanavyotaka.

Alitoka pale chumbani na kuelekea sebuleni ili kuungana nao.

"Umependeza sana Shida, naomba kuanzia sasa ubadilishiwe jina" akasema Ally

"Kwa nini nibadili jina?" akauliza

"Kwa sababu hilo jina lako halina mvuto katika kazi yetu" akajibiwa

"Kwa hiyo unahitaji niitweje?" akauliza

"Utwaitwa Clay na kabila lako ni Mmakonde" akasema Ally

"Poa haina shida" akajibu

"Tafadhali usije ukasahau hilo jina, narudia tena Clay" akasema tena Ally

"Usijal kamanda" akajibu



**********

INAENDELEA
Powered by Blogger.