KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Simulizi : Shida Sehemu Ya Kumi na Sita (16)

Hadithi nzuri ya kusisimua ya shida
Pale pale wakatoka na kuelekea kwenye gari na kupanda, hiyo ikiwa saa kumi na mbili jioni.

Walielekea Orion Hotel pale Tabora kalibu na steshen ya gari moshi pembeni ya chuo cha ualimu cha Tabora

Walipaki gari yao nje na kusubiri kwa muda

"Kuna mtu tunamuhitaji na hatuwezi kumpata bila wewe" akasema Ally

"Una maana gan?" akauliza Shida

"Nafikili unafaham kazi tunayoifanya sisi?" akauliza Ally

"Ndiyo naifaham" akajibu Shida

"Kuanzia leo umeingia kwenye ushilika na hatuhitaj swali katika hilo wala mjadala ila kazi yako itakuwa tofaut kidogo" akasema tena Ally

"Nakusikiliza" akasema Shida

"Tunataka ufanye kadri ya uwezo wako umshike huyu jamaa na baada ya hapo akitaka kuchukua chumba ukatae kwa sababu tumeshafanya uchunguzi na kugundua familia yake imesafiri basi tunahitaji umbembeleze akupeleke kwake na sisi tutamaliza kazi" akasema Ally

Ghafla wakati Shida akitaka kuongea wakamuashiria anyamaze na ikapita Prado nyeupe na kuingia pale hotelin huku akina Ally wakiiangalia kwa makini

"Kazi imeanza, shuka na uende na kukaa kalibu na atakapokaa jamaa aliyepo kwenye hiyo Prado na ujitahidi kumtega mpaka aingie laini na sisi tutakuwa tunawasiliana kupitia hii simu" akasema Ally akimpatia simu aina ya Nokia Asha.

Shida alishuka kwenye gari na kuingia pale hotelini.

Alipokuwa akiingia alimuona jamaa mmoja mwenye asili ya Asia akitoka kwenye lile gari na kisha kuingia pale hotelin

Taratibu na yeye akaanza kuingia pale hotelin,alimuona yule jamaa akikaa kwenye meza moja ya wazi.

Na yeye akachagua meza iliyokuwa jilani na aliyokaa yule jamaa na kukaa

"Naamini hautatuangusha, na pia unafaham ukituangusha nini kitatokea" sms iliingia kwenye simu yake na akaisoma

Aliwafaham vizuri wale vijana akina Ally jinsi walivyokuwa katili sana hasa linapokuja swala la kuua

Akaagiza juice yake na kuanza kunywa,alichokitaka kilitokea ndani ya muda mfupi baada ya yeye kuanza kunywa juice.

Yule jamaa akawa hatulii pale kwenye kiti chake,na Shida alipogundua hilo akawa anabadili mikao pale kwenye kiti chake

Asilimia themanini ya mapaja yake meupe yalikuwa wazi sana na hicho kilizidi kumuumiza yule jamaa



Uzalendo ulipomshinda alinyenyuka na kumfata Shida kwenye siti yake

"Hellow" akasema

"Hi!" akajibu Shida

"Is there somebody else here?" akauliza

"No I am alone" akajibu

"Naomba nikupe kampan tafadhali kaama hutajali ila sio kwa ubaya" akasema

"Hapana,kwa sababu nina mawazo sana i need to be alone,nahitaji kutuliza akili yangu" akasema Shida kimtego

"Ooooh! Veve toto zuri sana,hapana waza bana,ntakupa kampan" akaongea kiswahili chake kilichosababisha Shida agundue kuwa yule ni mhindi

"Ok,u may sit" akasema Shida

Kwanza hakutaka kuonekana wa kiwango cha chini hasa akizingatiwa mtu aliyekuwa pale alionekana kiwango cha juu sana

"Ok, sorry tunaweza fahamiana?" akauliza yule mhindi

"Haina tatizo,naitwa Shi.... No clay" alijikuta akijichanganya

Wakati wakiongea ghafla wakina Ally wakaingia pale na kwenda kukaa kwenye meza ya mbali kias

Yule mhindi alipowaona akina Ally alikosa raha kabisa,akawa hatulii,kila wakati aligeuka kuwaangalia

"Tafadhali,kama hutajali naomba kuondoka na wewe eneo hili twende eneo lililotulia zaidi nina maongezi makubwa na wewe" akasema yule mhindi

Ile hali ilimshangaza sana Shida ila alihitaji kutimiza alichotumwa

"Fanya chochote anachotaka ila mwende kwake nyumbani" sms ikaingia kwake

Shida akabaki kizungumkuti!

Yule jamaa mwenye asili ya uhindi ndani yake alimchukua Shida na kumpakiza kwenye Prado yake kisha akaondoaka eneo lile

Alipita barabara ya kuelekea chuo cha utumishi wa uma pale Tabora,alipofika kwenye geti na kona ya bar ya ziro ziro alipinda kulia na kufata barabara ya kuelekea NMB bank.

Alipofika lilipo jengo la Posta alipinda na kuiacha bara bara ya NMB na kuelekea Kanyenye,akazamisha gari kwenye mitaa ya Kanyenye kwenye Hostel zilizojazana hapo

Alipohakikisha hafatiliwi na mtu aligeuza gari na kisha anakurudi na Njia ya kuelekea Chuo cha ualimu Tabora na mwisho akafika makutano ya barabara nyingi pembeni ya chuo cha ualimu akanyoosha kwenda Nzega.

Mpaka hapo alijua ameshawapoteza mbali akina Ally.

Kumbe wakati anaondoa gari eneo lile akina Ally waljua ataelekea Nzega iwe isiwe na pia walishamwekea Shida kifaa chenye GPS ambacho kiliwafanya waonekila mwelekeo wake.

Yule Mhindi aliwapita wakiwa wamepaki kwenye kituo cha mafuta jirani na Makutano yale waliyopita kuelekea Nzega

"Muache aende japo kilometa kadhaa ndipo tumfatilie" Ally aliwaambia wenzake

Baada ya kushika barabara ya Nzega yule mhindi aliongeza kasi ya mwendo wa gari ili awahi kufika Nzega

"Mbona sikuelewi? Na huku unanipeleka wapi?" Akalalama Shida

"Utajua tu we twende" akajibu yule Mhindi

Safari ya masaa mawili kutokana na speed ya yule mwarabu walikuwa wameshaingia Nzega akashika barabara ya kuelekea Da es salaam na baada ya mwendo mfupi akashika njia ndogo ya vumbi na kuendelea na safari baada ya muda mfupi wakaingia kwenye kasri kubwa sana

Geti lilifunguliwa na gari ikaingizwa ndani

Shida alishushwa na kisha akaingizwa kwenye chumba kilichosheheni vitu vya gharama kubwa sana

"Utakitumia hiki chumba kwa muda,utakaa na mimi kwa siku tatu kisha nitakulipa million tatu na kukuachia kwa sababu mke wangu atakuwa anarejea" akasema yule Mhindi

"Sijakwelewa mpaka sasa,na vip umewakimbia wale jamaa pale hotelin?"akauliza Shida

"Wale jamaa ni adui zangu" akasema

"Nieleze ili nijue tafadhali" akasema Shida

"Ukweli ni huu,wale vijana walikuwa vijana wangu wa kazi,unajua sisi matajiri mara nyingi tunakuwaga na biashara haramu kwa siri" akasema

"Nakusikiliza" akajibu Shida

"Sasa wale vijana walikuwa wakinifanyia kazi haram,kuna kipindi niliwatuma kwenda kuchukua dhahabu Kahama,kuna rafiki yangu ana mgodi kule,ukawa umetema sana wakati anajiandaa kusafilisha nikawatuma wale vijana waende kuichukua ile kitu,baada ya kuiba na kumuua jamaangu wakaja na kutaka tugawane wakati sio makubaliano yetu" akaendelea

"Sikukubali kwa sababu tangu mwanzo walikuwa wananifanyia kazi nawalipa,sasa wakataka tugawane,nikawadhurumu na kisha kuajili vijana wapya,tangu hapo wamejenga uadui mkubwa sana na mimi na wananitafuta waniue" akamaliza kusimulia

"Wale jamaa,niko pamoja nao ila sipendi kuifanya hii kazi,nahitaji kuiacha ukinisaidia nitakusaidia" akasema Shida

"Sema unavyotaka tutaelewana tu" akajib Mhindi

"Naomba milion tano peke yake,sasa hivi kisha kesho niachie niende kwao kwa sababu naamin utakuwa umewapoteza tayali,nikifika huko nitawaua,ila unisaidie sumu ya njoa ya hewa ili inisaidie kuwapulizia" akajibu Shida

Mhindi hakutafakari mara mbili zaidi ya kuondoka pale chumbani na kurudi akiwa na burungutu la pesa akamkabidhi Shida

"Million tatu hizo, ukimaliza kazi nakupa Million saba juu" akasema Mhindi

"Haina tatizo " akajibu Shida

Walikula kunywa na kisha wakastareheshana kwa ngono

Usiku saa sita risasi zikarindima kwenye makao ya Mhindi huyu

Kitu ambacho Shida hakujua ni kuwa akina Ally walikuwa majambazi wazoefu na hivyo walijua anaweza wageuka na wakampandikizia kifaa cha mawasiliano chenye GPS ambacho kilinasa mazungumzo yake yote na mhindi

Yule mhindi alitoka mkuku bila kuvaa nguo kisha Shida akabaki peke yake akiwa haelewi mwisho wake ni nini?

Hakujua ni jinsi gani Ally na wenzake walivyopafaham mahali walipokuwepo

"Lazima watakuwa akina Ally hao,nifanyeje sasa?" aliwaza

Muda si mrefu akasikia risasi zikilia ndani ya Nyumba na sauti aliyoifaham kabisa kuwa ni ya Ally ikiunguruma



" Kabla hatujakuua tunaomba utuambie huyu malaya alipo hawezi kutusaliti sisi" sauti ya Ally ilifoka

Shida akatetemeka mpaka mkojo ukapita!!!





**********
INAENDELEAH
Powered by Blogger.