KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Simulizi : Shida Sehemu Ya Kwanza (1)

Hadithi nzuri ya kusisimua ya shida
MTUNZI JR. BAITA -0755 957515
Shida alikuwa na furaha isiyo na kipimo,Baada ya shida nyingi kama jina lake alizopitia katika maisha yake ya kawaida na kimapenzi hatimaye sasa alikuwa anakalibia kwenye pumziko kuu na la milele

"Ndoa.....ndoa.... Hatimaye Mungu hamtupi mja wake,kesho na mimi naolewa jaman! Rafiki zangu hatimaye naolewa" aliwaambia rafiki zake usiku huu wakiwa chumbani kwake akiwa anajiandaa na sherehe yake ya kuolewa na kijana Kolumba kesho yake..

Baada ya mapenzi ya muda wa miezi saba kati yao,huku Kolumba akimuonesha mapenzi ya dhati, akimpa chochote alichohitaji ili kuikamilisha furaha ya msichana huyu aliyepitia shida nyingi sana katika maisha yake.

"I was always crying, why me? But now there is somebody to weap my tears"nimekuwa nikilia kila marakwamba kwa nini mimi?? Ila sasa yupo wa kuyafuta machozi yangu" alendelea kuwaambia rafiki zake

"Usijali best, amini Mungu amesikia kilio chako cha muda mrefu na sasa unaenda kupata faraja maishani, tunakutaman mwenzetu, sisi hatujui kama tutaolewa" akasema Amina mpambe wake mkuu katika harusi hii.

"Usijali Amina utaolewa, wewe umetoka familia bora tofauti na sie kapuku na wewe ni mzuri sana,utaolewa tena na mdosi balaa" akasema shida.

"I wish siku moja na mimi itanitokea, by the way matroni alisemaje juu ya ile shela? Itapunguzwa?"akauliza Amina

"Hivi sijakwambia best? Mbona ishapunguzwa na nimejaribu imefiti balaa, nakwambia kesho! Ntaringaje? Ndani ya shela na Mr ndani ya suti, we subiri" akaendelea Shida

Laiti binadamu tungepewa macho ya kujua yatakayojili mbele yetu,nafikiri Shida angelia usiku kucha akiombolezea maisha yake

Kolumba kijana mdogo anayemiliki kampuni ya kusambaza sola vijijini ila makao makuu ya kampuni yakiwa Dar, alimpenda Shida siku aliyomwona akiwa kaenda kuomba kazi ofisini kwake, hakuwa na papara, alimwajiri na katika ufanyaji wa kazi ndipo wakaangukia katika penzi hili tamu ambalo hitimisho lake lilikuwa kesho asubuhi kanisani Njiro huko mkoani Arusha.


Asubuhi ya siku ilofuata

Maandalizi ya ndoa hii yalikuwa moto moto,kila aliyehusika kwa namna moja au nyingine alikuwa busy kuhakikisha kitengo anachosimamia kinakaa sawa kabla harusi haijakamilika

Shida akiwa na mpambe wake walifuatwa na gari maalumu na kupelekwa saloon , huko wakapambwa na kupambika haswaaa.

Shida alipendeza sana, ule uzuri wake wa asili akachanganya na madoido kidogo, hakika alionekana mrembo sana hasa katika siku hii muhimu sana kwake

Walitoka saloon saa mbili ikielekea saa tatu na moja kwa moja wakarudi nyumbani

Shida hakutaka kitu zaidi ya maji ya kunywa kwa kuogopa kuchafua tumbo

"Best, nimetoka ukumbini muda si mrefu, pamependeza balaa, yaani nimetamani harusi ingekuwa yangu" aliongea Rose, rafiki mwingine wa Shida

"Kweli eee?" akauliza Shida.

"Nakwambia! Dah! Kuna watu wanapamba, wee acha tu" akajibu.

"Natamani mama yangu angekuwepo leo hii kushuhudia tukio hili muhimu kabisa katika maisha yangu" aliongea shida huku machozi yakianza kumtoka

Ikabid rafiki zake waanze kumbembeleza.


Kanisani saa 11.00 asubuhi

Baada ya watu wote kuingia kanisani na kuketi, mchungaji Jafari aliingia katika madhabahu na kuanza zoezi hili muhimu la kufungisha ndoa hii.

"Wakati mliokuwa mkiusubiri sasa umefika, nawaomba maharusi na wazazi wao waje hapa mbele" akaongea Mchungaji.

Kanisa zima likalindima vigelegele. Wakasogea mpaka pale mbele na mchungaji akaanza taratibu zote zinazohusika na ufungishaji wa ndoa.

Baada ya kuapa kikafika kipindi ambacho Kolumba alikuwa akikiogopa kuliko vyote

Kipindi cha kuulizia kama kuna pingamizi.

"Kabla sijaifungisha ndoa hii rasmi, kuna yeyote mwenye pingamizi?" akauliza mchingaji.

Kanisa lote kimya,akarudia mara ya pili kimya!

"Mara ya tatu na ya mwisho na mkumbuke mkikaa kimya basi mkae kimya milele, je; Kuna yeyote mwenye pingamizi?" aliuliza mara ya tatu mchungaji.

Mara ghafla nyuma ya kanisa akasimama mdada wa saizi kiasi cha kukadilia umri wa miaka thelathini na ushee,

"Nina pingamizi mchungaji" akasema

Kolumba akatetemeka mpaka nikashangaa!!

Yule dada alipoanza kuondoka kuja mbele nyuma yake wakafata watoto wawili wadogo,

Wakatokea poa mzee na mkewe na wakaanza kuongozana kuja mbele na walipofika

"Nina pingamizi mchungaji, huyu kolumba ni mme wangu halali na cheti cha ndoa ninacho, amenitoroka na kuja kufungia ndoa huku Arusha na kimada wake, hawa unaowaona hapa ni wazazi wake halisi na sio hao, lakini kinachoniumiza ni kuwa mimi na Kolumba ni waathirika, badala ya mwenzangu kukaa tujadiliane jinsi ya kumwandalia maisha mwanetu yeye anafikiria kuambukiza wengine" aliongea kwa uchungu sana

Puuuuuu!!! Kikatokea kishindo kanisani.

Shida akawa kaanguka na kuzimia pale pale!!!

Baada ya Shida kuanguka chini watu walianza kulia na kelele pale kanisani hali iliyoleta tafrani ya aina yake.

Kolumba yeye aliinama na kuanza kumwamsha Shida aliyekuwa amepoteza fahamu

"Shida....Shida......shida....tafadhali amka Shida, jaman iteni gari haraka tumuwahishe hospitali" aliongea kwa woga baada ya kuona kama anazalisha tatizo lingine.

INAENDELEA.
Powered by Blogger.