KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Sitasahu sehemu ya Kumi na mbili (12) . Mwisho

hadithi nzuri ya kusisimua

"Kila aliye na mahusiano na mtu anayempenda huwa katu hawezi kutamani kumpoteza. Kuwa na mtu unayempenda kwa dhati ni zaidi ya raha ya kawaida unaweza kujikuta muda wote uko na furaha, japo mipango ya maisha yako haijawa ya kuvutia. Faraja na amani utakayoipata kwa kuwa na yule unayempenda kwa dhati huweza kutibu majeraha yaliyopita, hatimaye kuyaona maisha kuwa ni kitu bora cha kufurahisha" nikawaona wapenzi hao wakitazamana huku wametabasamu......falsafa wasiojua nilichomaanisha.....

Mlio wa mlango unaosukumwa ukatufanya sote tuyaelekeze macho yetu mlangoni kushuhudia kiumbe kinachoingia........watoto wawili mapacha wenye jinsia tofauti wenye umri kati ya miaka 2-3 walikuwa wanaingia eneo hilo huku yule wa kiume akimkimbilia mama yake na yule wa kike akienda kutua kifuani mwa baba yake. Tukio lenye kusisimua.....

Bila shaka hawa ni watoto wao kutokana na mfanano wao..sikutaka hata kutambulishwa kwa jinsi walivyo fanana na wazazi wao....Atimaye wakanitambulisha watoto hao yule wa kike aliitwa Nadia nafikiri Richard alitaka kumuenzi Nadia binti wa ajabu aliyemlipia nauli kwenye bus huku yule wakiume akiitwa Johnson kwa heshima ya marehemu mzee Johnson Ndeluma"

Ilinilazimu kuwaaga na kuondoka....wakati namalizia ngazi ya mwisho ili nitoke nje nikakumbuka kuna jambo sijalisema ambalo nilitaka niwaambie nikarejea haraka ndani nikawaita kwa mara nyingine "Mr and Mrs Richard"......Naomba niwaambie siku zote watu hujifunza kwa mifano. Mifano huwakilisha kwa ustadi wa hali ya juu hisia na hali halisi ya jambo fulani kwa tafsiri maridhawa. Kukutana kwenu ilikuwa katika namna ya tafsiri. 

Na kilichotokea kitakuwa mfano kwa vijana wengi nchini. Asante kwa ushirikiano wenu. Nakuahidi Mr Richard nitafanya kila jitihada, kuwatafuta popote sitachoka kutembea mchana hata usiku ikiwa nitawapata Patrick na Nice nitawakutanisha tena ili muifanye familia zao na yenu marafiki.....tafadhali kubalini ombi hili..... "Bila shaka" Wote walitamka kama vile walikuwa na mawazo yanayofanana.... Nikacheka! Nikacheka! kwa kupata bahati ya kuifahamu simulizi hii.

Ni mwaka wa tatu sasa....naendelea kuwatafuta Nice na Patrick ili nitimize agano langu.....sijapata hata fununu za watu hawa walipo....najua simulizi hii itasomwa na watu hao bila shaka mtakapoisoma msisite kuwasiliana nami nahitaji kufahamu ukweli wenu....ukweli husiosahaulika.

Mwisho.

AHSANTENI SANA KWA KUWA NASI TANGU MWANZO MPAKA MWISHO WA KISA HIKI CHA KWELI. TUNATUMAI KUWA MTAKUWA MMEJIFUNZA JAMBO KWENYE KISA HIKI. TOA MAONI YAKO

Powered by Blogger.