KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Simulizi : Shida Sehemu Ya Pili (2)

Hadithi nzuri ya kusisimua ya shida
MTUNZI JR. BAITA -0755 957515
"Nani aite gari kwa ajili ya malaya wako huyu, mwanaizaya wewe huna hata aibu? Kazi kuua watoto wa watu, umeniletea UKIMWI hauridhiki unaanza kuwaambukiza watoto wa watu wasio na hatia unawadangaya" aliongea mkewe kwa hasira.

"He!he!he!he! Jaman acheni malumbano, mzee mwenzangu wapeleke hawa ofisi ya mchungaji, acha mimi nishughulike na huyu mgonjwa nitakuja tuyamalize huko" mchungaji alimwambia mzee wa kanisa.

"Jaman tunaomba utulivu kidogo" aliongea mchungaji kwenye kipaza sauti cha kanisa lile na watu wakatulia huku vijana wakimtoa nje Shida na kumweka sehemu yenye upepo ili apate hewa ya kutosha.

"Kila mtu ni shuhuda wa kilichotokea, na uhakika hakuna baya linaloenda kumtokea mwanetu na muumini wetu Shida, nawaomba muwe watulivu wakati tukifanya majadiliano na wazee huko ofisini ndipo tutaleta kwenu kinachopaswa kufanyika, namuomba shemasi wa kiume na kike na wazee wa Baraza la kanisa waingie hapo ofisini mara moja" aliongea mchungaji.



Kule nje wale vijana walitoa mashati yao na kumpepea Shida kwa muda wa dakika tano akawa amerudiwa na fahamu zake.

"Mmmmh! Niko wapi jaman?..............au.....Kolumba...kwa nini mimi? Eee Mungu nimekukosea nini mimi mja wako?" alivuta kumbukumbu baada ya kuamka na kuanza kulia

"Shida usilie wala usijute kwa hili, kwanza tupate ukweli juu ya hili ndipo tujue cha kufanya, nakuomba twende kwenye kikao kama unajisikia nafuu ili tukapate ukweli" alimwambia mzee mmojawapo wa kanisa hili aliyebaki naye pale nje.

Shida aliamka taratibu kutokana na kutokuwa na nguvu za kutosha na akashikiliwa na mzee huyu moja kwa moja mpaka ndani,

Waliingia na kukuta kikao hakiajaanza kwani walikuwa wakimsubilia yeye,akaenda moja kwa moja na kukaa pembeni ya mchungaji na mzee wa kanisa.

"Unajisikiaje mwanangu?" akauliza mchungaji.

"Najisikia vizur baba mchungaji" alijibu na kumwangalia yule dada aliyedai ni mke wa kolumba,yule dada alimpandisha juu chini na kusonya.

"Jaman, hapa ndani hatujaja kwa ajili ya ugomvi hivyo naomba tupunguze hasira ili kikao kiishe kwa amani ya Bwana" aliongea mchungaji na kuendelea


"Nishukuru kwa aliyeleta pingamizi hili kwa sababu amelileta muda muafaka kabisa, kwani angechelewa mpaka ndoa ikafungwa asingepata nafasi ya kusikilizwa....aaaaaa..... Sijui nianze na nani?... Nafikiri mwenye pingamizi ndiye angepata nafasi ya kuongea...mama kwanza jitambulishe kisha uendelee" akaongea mchungaji

Akakohoa kidogo kurekebisha sauti kisha akaanza kueleza


***************

akaenda moja kwa moja na kukaa pembeni ya mchungaji na mzee wa kanisa.

"Unajisikiaje mwanangu?" akauliza mchungaji.

"Najisikia vizur baba mchungaji" alijibu na kumwangalia yule dada aliyedai ni mke wa kolumba,yule dada alimpandisha juu chini na kusonya.


"Mimi naitwa Lydia Kolumba, ni mke halali wa bwana Kolumba, tumefunga ndoa yetu miaka mitano iliyopita, tuna watoto wawili, na hawa hapa nyuma ni wazazi halisi wa Kolumba....Mimi na mme wangu tulizaa mtoto huyu wa kwanza tukiwa wazima wa afya ila baada ya kumzaa huyu mwenzangu akaanza tabia ya uhuni sana, hali iliyosababisha tuanze kuugua mara kwa mara na ikabidi twende kufanya vipimo ndipo tukagundulika kuwa tumeathilika.....tukaanza kutumia vidonge ndipo afya zetu zikawa angalau,vyeti vya ndoa hivi hapa.....na vya UKIMWI pia hivi hapa.........Nilishtuliwa na mtu nisiyemjua kuwa mwenzangu anakuja kufunga ndoa huku,nikaweka mtego na ndipo akaniaga kuwa anasafili kikazi kwa mwezi mzima, nikawafuatilia mpaka hapa kanisani" aliongea huk akikabidhi vyeti vyote kama ushahidi.


Mchungaji alivipitia kimoja baada ya kingine na alipohakikisha ni vyeti halali akamgeukia Kolumba

"Bwana Kolumba je anayoongea mwenzako hapo ni kweli??"

"Ndiyo baba Mchungaji"

Shida alihisi dunia yooote inamwangukia yeye!!

"Why me?.......why me..........kwa nini mimi jaman???" alilia kwa uchungu "Why me???.........Why me??.... Kwa nini mimi lakini?" Aliongea kwa majonzi makubwa sana.

"Kolumba kwa nini umemfanyia hivi huyu binti?" Akauliza Mchungaji.

Kolumba hakuwa na jibu lolote la kutoa, aliinama chini na kuanza kuomba msamaha!

"Sina cha kujitetea, najuta kwa nilichokifanya najuta, Shida nisamehe! Nimekosa sana, mke wangu nisamehe! Mchungaji nisamehe na wazazi wangu pia"

Kila mtu alinyamaza pale na hawakuongea chochote!

"Nawaomba ninyi mmchukue kijana wenu mwende mkamalizie mambo yenu huko kwenu, acha sisi tutajua cha kufanya" alongea mchungaji.

"Lakini mchungaji mi......." alijalibu kuongea Baba yake Kolumba ila Mchungaji akamkatisha

"Nafikiri sitawapa nafasi ya kujadili chochote, kwa sababu mmeshaona alichokifanya sasa msimuongezee machungu binti yetu naomba muondoke" Aliongea kwa hasira mchungaji.

Hawakuwa na namna yoyote ile ilibidi waondoke na watoto wao pale kanisani

Baada ya kuondoka Mchungaji alimgeukia Shida na kuanza kumbembeleza

"Shida maisha yana safari ndefu sana, usichanganyikiwe kwa kilichotokea, amini wapo wagonjwa wengi sana ila wana maisha yao na wanaishi vizuri, kuathirika sio kufa bado kuna maisha tena marefu sana inahtaji ukubaliane na hali halisi na pia mrudie Mungu, samehe saba mara sabini na anza upya mwanangu" alijalibu Kumweka sawa.

"Mchungaji nimekuelewa kwa kila ulichoongea, sitalia tena nakuahidi, ila kuna kazi moja ambayo niliamua nisiifanye baada ya kupata faraja kutoka kwa Kolumba sasa inabidi niifanye kwani naamini nina haki ya kuifanya" akaongea kwa ujasiri Shida


"Kazi?..... Kazi gani hiyo mwanangu?" aliuliza Mchungaji.

"Naitwa Shida hiyo inaonesha nimepitia shida sana, maisha yangu yamekuwa ya shida sana na shida hizo zimesababishwa na wanaume, niliwachukia sana wanaume ila Kolumba alitaka kuibadili akili yangu niwapende ila naona kaniongezea chuki dhidi yao, wamenitesa sana, wamenifanyia vitendo vibaya sana ambavyo siwezi kuvisahau, sasa ni wakati wangu wa kulipa kisasi! NITAWAUA WOTE walioyafanya maisha yangu yawe ya shida sana" aliongea Shida

"Unasema !? Unataka kuwaua wanaume? Walikufanya nini?" akauliza tena Mchungaji.

"Maisha ya tabu yalianzia kwa mama yangu mpaka kwangu, elewa ninahitaji kulipa kisasi, roho yangu imebadilika na sasa imekuwa kama ya mnyama, nahitaji kulipa kisasi, haya ni MAPENZI, USALITI, CHUKI na KISASI sasa naanza kisasi kwa kila mmoja aliyeleta Shida katika maisha yangu, siri ya mimi kuanza kufanya mauaji unaijua wewe peke yako, nawachukia wanamme, na wewe ni mwanamme sasa ukijaribu kutoa siri hii na wewe utaingia kwenye msafala!

Nitakuwa naua kisha nakuja nakusimulia kwa nini nimemuua kila mmoja mpaka wataisha, nafikiri umenielewa" alihitimisha Shida

"Mmmmmmh! Nakuomba mwanangu, Mungu anasema samehe saba mara sabini" alijaribu kushawishi mchungaji

"Sina msamaha, mbona wao hawakunisamehe? Wamenitesa, wameninyanyasa, nimeishi kwa shida maisha yangu yote kwa sababu yao, kwa heri" akaaga na kuondoka kanisani.

INAENDELEA
Powered by Blogger.