KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Utamu Wa Shemeji Flora Sehemu Ya Ishirini na Mbili (22)

SIMULIZI NZURI YA KUSISIMUA

"Kesho na mimi nitaaga hapa na kumpigia simu Japhet anielekeze huko alipohamia ili tukaishi wote siwezi kuishi mbali naye" alisema Rozi huku akitoka chumbani kwake na kuelekea jikoni kuendelea tena na kazi yake ya kupika chakula na muda huohuo naye Flora akaingia. Rozi alishangaa kwani akujua ni muda gani Flora alikuwa amerudi hapa nyumbani akitokea kule saloon kwake.

"Vipi mbona unanishangaa kama vile ndio kwanza unaniona leo?" Flora alimuuliza Rozi kwa Shari huku akiingia humo jikoni.

"Hapana wala sikushangai, nikushangae kwa lipi ulilokuwa nalo?” Rozi naye alihoji kwa ujeuri. Flora akachukia sana baada ya kumsikia Rozi amesema hivyo. " Yaani wewe Rozi unathubutu kweli kuniambia mimi hivyo?" Flora aliuliza kwa hasira.

"Kwani dada hasira zinatokea wapi tena, au ni kwa vile Japhet hayupo amekukimbia?" Rozi alimuuliza hivyo Flora kwa makusudi aone atajibu nini.

"Naona sasa hivi heshima imepungua Rozi enhe? hayaa utakipata hicho kitu unachokitaka" alisema Flora na kuondoka humo jikoni huku akiwa amekasirika.

Huku nyuma Rozi alibakia anacheka tu çhini kwa chini. "Nikuheshimu mtu kama wewe unayeshindwa kujiheshimu, hadi unafikia hatua ya kufanya mapenzi na Shemeji yako" alijisemea moyoni Rozi na halafu akaendelea na kazi zake za jikoni. Kumbe Lukasi aliweza kuyasikia hayo mazungumzo yao yote akiwa amekaa kule sebuleni akaamua tu kunyamaza.

Muda wa kula chakula ulipofika wakala na baada ya hapo wakatawanyika na kuingia vyumbani mwao kulala. Lukasi na mkewe Flora wakaingia chumbani kwao na Rozi naye akaingia chumbani kwake.

Rozi akiwa amejilaza kitandani mawazo yake yote yalikuwa yapo kwa Japhet akaona ngoja kwanza ajaribu kumpigia simu usiku huohuo. Bahati nzuri simu ya Japhet ilikuwa inapatikana ikaanza kuita.

"Aloo niambie Rozi mpenzi wangu" sauti ya Japhet ilisema baada ya kupokea simu. "Mmh nikuambie nini baby zaidi tu ya kukumiss Mume wangu" Rozi alisema.

"Hee mara hii tayari nimeshakuwa Mume wako? hebu acha kuniletea balaa huko" alisema Japhet kwa utani huku akicheka.

"Kwahiyo leo unanikana Japhet baada ya kuhama huku si ndio enhe?" Rozi naye alijifanya kuuliza kwa sauti ya kudeka.

"Hapana mpenzi wangu siwezi kukukana kabisa, bila ya wewe leo nisingekuwa huku najinafasi kwa raha zangu" alisema Japhet. "Sasa huko kujinafasi ndio nataka na mimi nije ili tujinafasi wote my love" alisema Rozi huku akichekacheka.

"Duuh mbona mapema hivyo mpenzi wangu? subiri angalau kidogo hata zipite siku nne ndio nikuelekeze uje huku" Japhet alisema kwa sauti ndogo iliyopoa.

"Weee nisubiri nini tena hapa? sikiliza Japhet kesho jioni naaga huku, halafu keshokutwa asubuhi nakufuata wewe huko ujiandae kunipokea" alisema Rozi kwa msisitizo. "Lakini Rozi hauoni kama hapo nyumbani kaka pamoja na Shemeji watashtukia kama umekuja kwangu?" Japhet aliuliza. Rozi akacheka kidogo na halafu akasema: "Sioni sababu ya wewe kuogopa kama ikiwa hata uhusiano wetu kaka yako anaujua na ananiita mimi Shemeji, sasa sijui unaogopa nini Japhet?" Rozi aliuliza huku akionyesha kuchukizwa na huo uoga wa Japhet.

"Hapana mimi sio kama naogopa ila nilikuwa nataka huyo Shemeji Flora asijue kama wewe unakuja kuishi huku na mimi" alisema Japhet. "Kama wewe hautaki ajue kama nakuja kuishi kwako, sasa mimi ndio nataka ajue hivyo ili aache kukusumbua au na wewe bado unampenda huyo Shemeji yako? hebu niambie basi nijue" Rozi alisema huku akionekana kukasirika. "Sio hivyo mpenzi wangu naomba usinielewe vibaya, basi kesho wewe waage huko nyumbani, halafu utanijulisha nitakupa maelekezo ya kufika huku" alisema Japhet. Rozi sasa hapo akafurahi baada ya kusikia hivyo.

"Hayo sasa ndio maneno mtoto wa kiume, kesho nitakujulisha baby wangu" alisema Rozi kwa furaha. Baada ya hapo wakaagana na kutakiana usiku mwema halafu wakakata simu zao na kulala.



Asubuhi ya siku nyingine mpya ikafika.

Japhet akiwa ndio anaamka huko kwenye makazi yake mapya alipopanga chumba mawazo yake yote alikuwa anawaza Yale aliyoyaongea na Rozi Jana usiku kwenye simu. "Huyu binti naye vipi mbona sasa anataka kuniganda?" Japhet alijiuliza hivyo na kusahau Yale yote aliyoyapanga na binti huyo pale mwanzoni. "Mimi kwa sasa wala sijajiandaa kuishi na mwanamke, basi tu nilikubali kufanya hivi kwa sababu ya kuepuka usumbufu wa Shemeji kule nyumbani kwa kaka" Japhet bado aliendelea kujisemea. 

Baada ya hapo akaamka kitandani na kwenda kupiga mswaki pamoja na kunawa uso wake alipomaliza kujifanyia usafi Japhet akaenda zake dukani kununua mkate pamoja na Blue band bila kusahau na mayai halafu akarudi chumbani kwake na kujipikia Chai yake ya kiselasela. Baada ya kumaliza kunywa Chai akabakia humo chumbani kwake akiangalia TV kwa kuwa hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda kutembea kwani kwa muda huo wa asubuhi yule rafiki yake aitwae Mussa alikuwa ameenda kwenye kazi zake na pale nyumbani kwake alibakia mkewe tu pamoja na mtoto wao mdogo. 

Hivyo kwa Japhet aliona ni ngumu yeye kwenda huko aliona ni bora asubiri mpaka rafiki yake atakaporudi ndio aende kupiga story kwenye muda huohuo Japhet akiwa bado yupo chumbani kwake ndipo akaona simu yake inapigwa. 

Na alipoangalia ni nani huyo anaempigia simu Japhet akaweza kumgundua ni Shemeji yake Flora ndio anaepiga simu hiyo. "Khaa! Huyu Shemeji naye vipi, mimi nimeshahama kumkwepa yeye sasa mbona bado ananiandama kwa kunipigia simu kwani anataka nini tena kwangu?" Japhet alijiuliza na mwishowe akaamua kukata na kuizima hiyo simu kabisa hakutaka mawasiliano na huyo Shemeji yake. 

"Na akiendelea kunisumbua sana nitabadilisha na hii namba ya simu, sitaki anisumbue" alisema Japhet na kuisubiri jioni ifike aende nyumbani kwa rafiki yake Mussa. Na kweli Japhet aliweza kusubiri mpaka jioni ilipofika ndio akaenda kumtembelea rafiki yake Mussa na kwa Bahati nzuri akamkuta amesharudi nyumbani.

"Ooho niambie best yangu mwenyewe" alisema Mussa kwa furaha baada ya kumuona Japhet amekuja kumtembelea.

"Daah ndio hivyo ndugu yangu nipo tu nanyoosha miguu" alisema Japhet.

"Enhe makazi mapya yanasemaje huko?" Mussa alimuuliza Japhet. Kwanza Japhet akatabasamu halafu akasema: "Makazi mapya kusema ukweli ni pazuri sana na tayari nimeshaanza kupazoea" alisema Japhet. "Utapazoea vipi na wakati upo peke yako? inabidi sasa ndio umuite huyo mpenzi wako mfurahie maisha pamoja" Mussa alisema huku akitabasamu.

"Halafu hicho ndio kitu kilichonileta hapa kwako naomba unipe ushauri wako ndugu yangu" alisema Japhet. Mussa akajiweka sawa na kuuliza kwa umakini:

"Nikupe ushauri gani tena ndugu yangu?"

"Nimeona bora nimuache yule binti ambaye ni mfanyakazi wa ndani kule nyumbani kwa kaka, na halafu nitafute msichana mwingine huku wa kuwa naye" alisema Japhet. Mussa akashusha pumzi halafu akauliza: "Kwanini sasa umuache huyo binti na wakati uliniambia hapo mwanzo kuwa ndio yeye aliyekupa huo ushauri wa kuhama nyumbani kwa kaka yako ili umkwepe Shemeji yako anayekusumbua kimapenzi?" 

Mussa alimuuliza Japhet. "Ni kweli kabisa yeye ndie alienishauri na pia hata pesa ya kodi amenipa" Japhet alisema. "Sasa kama pesa ya kodi amekupa kwanini unafikiria kumuacha? hebu acha mawazo hayo ndugu yangu, ukijaribu kumuacha ujue umejitafutia matatizo kwa kaka yako" Mussa alisema kwa msisitizo.

INAENDELEA
Powered by Blogger.