KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Utamu Wa Shemeji Flora Sehemu Ya Ishirini na moja (21)

SIMULIZI NZURI YA KUSISIMUA
"Naomba uamini mpenzi wangu, kama vile tulivyopanga na ndio hivyo inaenda kutokea ni lazima tuondoke humu ndani ili tukafurahie mapenzi yetu kwa Amani" alisema Japhet na baada ya hapo sasa wakaanza kupanga mipango ya jinsi na Rozi naye atakavyoaga na kuondoka hapa nyumbani kwa Lukasi. 

Ambapo walikubaliana ni siku mbili za mbele baada ya leo Japhet kuwa ndio anahama hapa nyumbani kwa kaka yake. Rozi hakuwa na kipingamizi alikubaliana na hilo jambo. Baada ya mfupi Lukasi na mkewe Flora nao waliweza kuamka na baada ya kusalimiana Lukasi akamuuliza mdogo wake Japhet. "Kwahiyo unataka kuhama asubuhi hii?" Lukasi aliuliza.

"Ndio kaka ni asubuhi hii nataka kuondoka" Japhet alimjibu kaka yake.

"Basi sawa ngoja kwanza niingie bafuni kuoga halafu tunywe Chai halafu tupitie mjini kununua kitanda na godoro pamoja na vitu vingine vidogovidogo na ndio twende huko kwenye chumba chako" alisema Lukasi huku akiingia bafuni kuoga.

Huku nyuma Japhet ndio akapata nafasi nzuri ya kurudi chumbani kwake kwa haraka na kuchukua ule mfuko wa nguo pamoja na viatu bila ya kusahau na Simu halafu akaelekea jikoni ambapo ndio alikuwa yupo Shemeji yake Flora akiandaa Chai. Flora alitabasamu baada ya kumuona Japhet na halafu akasema:

"Naona ndio unaamua kunikimbia kabisa ili nisikusumbue?" Flora alimuuliza Japhet. "Shemeji mimi kwa sasa sina tena muda wa kuongea na wewe, kwanza nashukuru sana kwa hizi zawadi zako ulizoninunulia leo nakurudishia rasmi" Japhet alisema huku akimkabidhi Flora vitu hivyo. 

Flora akagoma kuvipokea na kusema: "Japhet hata kama umeamua kuhama humu ndani kunikwepa mimi, hiyo aimaanishi kama tuna ugomvi na unirudishie hivyo vitu nilivyokununulia" alisema Flora huku akiwa anatabasamu.

"Ni sawa Shemeji hilo nalijua, lakini mimi ndio nimeamua kukurudishia sasa" alisema Japhet. "Unanirudishia hivyo vitu mimi nivipeleke wapi Japhet? naomba uondoke navyo ili ukapate kunikumbuka huko unapoenda pindi utakapoviona" alisema Flora huku akichekacheka.

Basi kwa kuwa Flora aligoma kuvipokea Japhet aliamua kuvichukua na kwenda kuvihifadhi kwenye lile begi lake kubwa ili aondoke navyo hakutaka kaka yake Lukasi avione halafu akaanza kumtilia mashaka ya ni wapi alipovitoa vitu hivyo.

Baada ya kumaliza kunywa Chai na kujiandaa vizuri ndipo Japhet na kaka yake Lukasi wakawa wapo tayari kabisa kuondoka hapa nyumbani. 

Flora huku akiwa na uchungu mwingi sana moyoni mwake pamoja na majonzi tele usoni ya kumkosa Japhet akatoa pesa kiasi cha shilingi elfu hamsini kwa Shemeji yake huyo ili zikamsaisie kwa kuanzia maisha.

"Naamini bado tutakuwa pamoja hata kama unahama hapa nyumbani, naomba usitusahau Shemeji na pia ukumbuke kuja kunichukua siku moja na mimi nije kupaona huko unapoishi" alisema Flora kwa hisia Kali. "Kuhusu hilo wala usijali Shemeji kwa kuwa kaka hapa anaenda kupaona na kupajua basi hata na wewe pia utapajua" alisema Japhet huku akizipokea fedha hizo kutoka kwa huyo Shemeji yake hakuweza kuzikataa.

Baada ya hapo akaagana na Rozi kwa unafiki kama vile hawapo wote kwenye huo mpango wa kuhama humu ndani.

Huku Rozi naye akijifanya kuwa na huzuni baada ya kumuona Japhet anahama. Baada ya kumaliza kuagana Japhet na kaka yake Lukasi wakaondoka zao huku nyumbani wakibakia Flora na Rozi.



Hatimaye Lukasi na mdogo wake Japhet waliweza kufika mpaka maeneo ya mjini kununua kitanda pamoja na godoro kama vile Lukasi alivyomuahidi mdogo wake huyo (Japhet) kuwa atamnunulia vitu hivyo kwa ajili ya kwenda kuanzia maisha. Wakaingia kwenye duka moja kubwa sana maalumu lililokuwa linauza vitu vyote vya majumbani. Lukasi akanunua kitanda kikubwa cha futi sita kwa sita pamoja na godoro lake jipya kabisa na foronya ikiwa na mito ya kulalia kitandani. 

Pia akamnunulia Japhet na TV ya kisasa (Flat Screen) na Radio kubwa (Subwoofer) na Meza ndogo ya vipodozi Dressing Table pamoja na zulia kubwa la kutandikia chini. "Hayaa mdogo wangu hivi vitu nimekununulia ukaanzie navyo maisha, isingependeza ukalale chini na mimi uwezo wa kukusaidia ndugu yangu ninao" alisema Lukasi. Japhet aliweza kumshukuru sana kaka yake huyo kwa msaada Mkubwa aliompatia kwani akutegemea kabisa kama kaka yake angeweza kumnunulia vitu vyote hivyo.

"Yaani kaka nakushukuru sana kwa kuninunulia vitu hivi vyote, Mungu akubariki sana" alisema Japhet huku machozi yakimlengalenga machoni.

"Usijali kabisa mdogo wangu hili ni jukumu langu kukusaidia, hayaa sasa na tujiandae twende huko kwenye chumba chako" alisema Lukasi na baada ya hapo wakaweza kukodi gari ndogo mizigo (PICK UP) na safari ya kuelekea huko maeneo ya Buza Kanisani sehemu kilipokuwa chumba cha Japhet ikaanza.

Baada ya mwendo wa muda mfupi hatimaye Japhet na kaka yake Lukasi waliweza kufika mpaka huko walipokuwa wanaenda na kwanza walianzia nyumbani kwa Mussa yule rafiki yake na Japhet ambaye ndie alimtafutia chumba Japhet. Baada ya kumkuta Mussa wakamchukua na kwenda naye mpaka kwenye chumba cha Japhet ambapo ni jirani tu na anapoishi Mussa.


Baada ya kufika wakateremsha vyombo vyote kwenye gari na kuviingiza ndani ambapo walisaidiana kwa pamoja kuvipanga na ndani ya muda mfupi chumba cha Japhet kikawa ni chenye kupendeza sana. "Sasa Japhet vipi tena kuhusu yule binti Rozi kule ndio basi tena uhusiano wenu imeisha?" Lukasi alimuuliza mdogo wake Japhet.

"Mmh kwa sasa ngoja kwanza nijipange na maisha kaka, ukifanikiwa kunitafutia kazi ndio nitamfikiria Rozi" alisema Japhet huku akimficha ukweli kaka yake hakutaka kumwambia alichokipanga yeye na Rozi kuhusu kuja kuishi wote huku.

"Ni sawa mdogo wangu hicho unachosema, lakini kumbuka yule binti utamuacha na upweke basi ukipata nafasi uje umchukue angalau aje apaone hapa unapoishi" alisema Lukasi.

"Sawa kaka basi nitafanya hivyo" alisema Japhet. Waliendelea kupiga story mbili tatu na baadae Lukasi akaaga na kuweka kuondoka akiwaaga Japhet na Mussa kuwa anaenda kwenye shughuli zake kabla Lukasi ajaondoka akampa mdogo wake Japhet kiasi cha Pesa kama laki moja hivi kwa ajili ya matumizi madogo madogo ya ndani pia ikiwemo na chakula. 

"Ukiishiwa na Pesa ya matumizi naomba haraka sana unijulishe, huku mimi bado naendelea na mchakato wa kukutafutia mdogo wangu" alisema Lukasi. "Sawa kaka nashukuru sana" alisema Japhet. Baada ya hapo Lukasi akaweza kuondoka huku akiahidi kuja tena siku nyingine kumtembelea akiwa na Shemeji yake Flora. Japhet baada ya kumsikia kaka yake akisema atakuja kumtembelea tena Flora alitamani hata kumwambia asije naye kwani hakutaka kabisa mwanamke huyo apajue hapa sehemu alipoahamia lakini alishindwa kumwambia hivyo kaka yake Lukasi.

Baada ya Japhet na Mussa kumsindikiza Lukasi walirudi mpaka nyumbani kwa Mussa na kuchukua vile vyombo vingine ambavyo Japhet alivinunua Jana yake alivyomkabidhi rafiki huyo amuhifadhie na kwenda navyo sasa kule kwenye chumba chake alipohamia ili akaanze kuvitumia. "Sasa hapa mambo ni motoo najua nitaishi kwa Amani bila ya kupata tena usumbufu kutoka kwa Shemeji, halafu na Rozi naye sijui nimtose nitafute demu mwingine mpya wa kuanzia maisha" alijiwazia moyoni Japhet huku akifikiria namna ya kumuacha Rozi.



Kwenye majira ya jioni Lukasi aliweza kuwahi kurudi nyumbani kwake na kwa Bahati nzuri aliweza kumkuta Rozi akiwa yupo peke yake kwani mkewe Flora alikuwa bado ajarudi hapa nyumbani kutoka kule saloon kwake anapoenda.

"Hii ndio nafasi nzuri niliyokuwa naitaka ngoja sasa niongee na huyu binti" alijisemea moyoni Lukasi huku akiketi kwenye Kochi sebuleni na baada ya hapo akaanza kumuita Rozi ambaye alikuwa jikoni akipika chakula cha usiku. "Abee Shemeji nimekujaa" alisema Rozi kwa adabu zote baada ya kufika sebuleni.

"Ok naomba uketi hapo kwenye Kochi nina mazungumzo kidogo na wewe" alisema Lukasi. Rozi baada ya kusikia huyu bossi wake ana mazungumzo na yeye akaanza kuingiwa na hofu.

"Kuwa tu Amani Rozi ni mazungumzo ya kawaida hivyo usiogope" alisema Lukasi akimtoa hofu binti huyo. Rozi akaweza kuketi kwenye Kochi na sasa alikuwa yupo tayari kabisa kusikiliza hicho kitu alichoitiwa. "Kwanza kabisa naomba nikuombe radhi kwa kukukatishia kazi zako" alianza kwa kusema Lukasi.

"Wala hakuna shida Shemeji" alisema Rozi huku akitabasamu. Hili neno Shemeji analomwita Lukasi kwa sasa lilikuwa na maana mbili kwa Rozi hapo mwanzoni alikuwa anamwita Shemeji kwa sababu ya Flora kumchukulia kama vile ni dada yake hivyo Lukasi akaanza kumchukulia naye pia kama Shemeji yake kwa kuwa ndio Mume wa Flora. Lakini maana nyingine ya Pili kwa Rozi ni kutokana na kujiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi na Japhet ambaye ni mdogo wa Lukasi hivyo kwa sasa Rozi kumwita Lukasi Shemeji anaona ni haki yake kabisa. "Nilichokuitia hapa Rozi nataka uniambie jambo moja tu bila kunificha, kama kweli unaipenda kazi yako na pia kama unampenda sana mdogo wangu Japhet" Lukasi alisema hivyo na kuanza kumtisha Rozi.

"Jambo gani tena hilo Shemeji?" Rozi aliuliza kwa ndogo ya sauti wasiwasi.

"Naujua uhusiano wako wa kimapenzi na mdogo wangu Japhet, sasa naomba uniambie wewe unajua nini kuhusu uhusiano wa Japhet na Shemeji yake Flora?" Lukasi aliuliza huku akimkazia macho yake Rozi na kuzidi kumtisha.

"Mbona sielewi Shemeji, uhusiano gani aliokuwa nao Japhet na dada Flora zaidi ya kuwa ni mtu na Shemeji yake tu?" Rozi alijibu swali la Lukasi kwa mtindo wa kuhoji mwishoni. "Sikiliza Rozi najua kama unajua kila kitu kuhusu Japhet na Shemeji yake Flora nini kinaendelea baina yao, sasa naomba uniambie ukweli" alisema Lukasi kwa sauti kavu.

"Jamani sasa mimi nitakuambia nini Shemeji? kweli vile mimi sijui chochote" alisema Rozi huku akitia huruma.

"Rozi unajua kila kitu ila tu unaamua kunificha, OK naomba kujua kitu kimoja je uhusiano wako wa kimapenzi na Japhet mke wangu Flora anaujua, na kama anaujua naomba unijibu anaufurahia?" Lukasi aliuliza. Hapo sasa ulikuwa ni mtihani kwa Rozi kwani ni kweli Flora alikuwa anaujua uhusiano wake na Japhet na ndio chanzo kinachopelekea mpaka Flora kumnunia Rozi na kumuonea wivu juu ya kijana huyo (Japhet) ambaye hata na Flora pia anampenda licha ya kuwa ni mdogo wa Mume wake wa ndoa (Lukasi) hivyo hata kama anachukiana na Flora inabidi hapa Rozi akatae kusema ukweli kwa Lukasi ili kumlinda mpenzi wake Japhet japo ni kweli kabisa anajua yote juu ya Flora na Japhet mpaka alipowashuhudia siku ile usiku wakifanya mapenzi chumbani kwa Flora baada ya kuwachungulia kwenye Tundu la kuingizia funguo mlangoni.

"Hapana sina uhakika kama dada Flora anaujua uhusiano wangu na Japhet" Rozi alisema na kukanusha kabisa.

"Ok kama umeamua kunificha basi, naomba uchukue hii shilingi laki moja utaenda kununua chochote unachotaka siku ukiwa tayari najua tu utaniambia" alisema Lukasi huku akimkabidhi Rozi fedha hizo. Rozi aligoma kuzipokea.

"Naomba uzipokee hizi fedha wala usiogope Rozi, nakupa kwa kuwa wewe ni Shemeji yangu kwa mdogo wangu Japhet" alisema Lukasi huku akijaribu kutabasamu. Rozi akakubali na kuzipokea fedha hizo kutoka kwa Lukasi.

"Ahsante sana Shemeji nashukuru" alisema Rozi huku akipiga goti la heshima. "Wala usijali Shemeji yangu nenda tu kaendelee na kazi zako" alisema Lukasi akimruhusu Rozi. Baada ya Rozi kuwa ameondoka pale sebuleni Lukasi akajisemea kwa sauti ndogo: "Huyu binti anajua kila kitu ila tu anaamua kunificha, sasa kesho nitampa tena fedha zingine na nitamuuliza upya nitahakikisha mpaka ananiambia ukweli wote" alisema Lukasi.

Rozi baada ya kuachana na Lukasi moja kwa moja akaenda chumbani kwake kuzihifadhi zile fedha alizopewa na Lukasi. "Mmh sitaki kuvunja ndoa ya watu na kumponza mpenzi wangu Japhet, pale kama ningesema ukweli ingekuwa ni hatari kwa Japhet" alijisemea moyoni Rozi. 

Hapohapo akaanza kumkumbuka Japhet na mambo yake matamu ya kimahaba ambayo anamfanyia. "Kesho na mimi nitaaga hapa na kumpigia simu Japhet anielekeze huko alipohamia ili tukaishi wote siwezi kuishi mbali naye" alisema Rozi huku akitoka chumbani kwake na kuelekea jikoni kuendelea tena na kazi yake ya kupika chakula na muda huohuo nao Flora naye akaingia!.


ITAENDELEA

Powered by Blogger.