KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Utamu Wa Shemeji Flora Sehemu Ya Ishirini na Tatu (23)

SIMULIZI NZURI YA KUSISIMUA
"Nitajitafutia matatizo kivipi tena kwa kaka yangu endapo nikimuacha?" Japhet alihoji. "Namaanisha hivi huyo binti atakutolea siri yako iliyosababisha wewe uhame kule nyumbani kwa kaka yako" alisema Mussa. Japhet akajifikiria kidogo halafu naye akasema: "Sawa rafiki yangu nimekuelewa ngoja nitampigia simu na kumuelekeza aje huku tuishi wote" alisema Japhet kwa upole. "Yes hayo ndio mambo sasa, na usijichanganye kabisa kumuacha huyo binti utakuja kujuta ndugu yangu nakuambia" alisema Mussa akimpa ushauri huo Japhet.

Basi baada ya hapo wakaendelea kupiga story zingine mbalimbali za kiurafiki.



Majira ya usiku kule nyumbani kwa Lukasi napo baada ya kumaliza kula chakula Rozi naye akaona ngoja na yeye leo aliamshe Dude kama vile alivyofanya mpenzi wake Japhet kwa kuaga hapa nyumbani. "Shemeji na dada Flora leo na mimi ningependa kuwaaga rasmi kuwa natarajia kuondoka hapo kesho asubuhi" alisema Rozi kwa sauti ya upole. 

Flora pamoja na mume wake Lukasi kwanza wakashtuka sana baada ya kumsikia Rozi anasema hivyo. "Rozi kwanini uondoke hapa nyumbani ghafla kiasi hicho enhe?" Lukasi alimuuliza Rozi. "Basi tu Shemeji nimeamua hivyo nimewakumbuka sana ndugu yangu kijijini kwetu Iringa" Rozi aliamua kudanganya. "Sawa hata kama umewakumbuka ndugu zako ndio uage ghafla namna hiyo kama vile kuna ugomvi?" Lukasi bado aliendelea kumuuliza Rozi. 

Kwa upande wa Flora tayari alishaanza kuhisi kitu juu ya huku kuaga kwa Rozi. "Mmh huyu binti nahisi atakuwa anamfuata Japhet huko alipohamia, na inawezekana ikawa ni mipango yao waliyoipanga kunikimbia mimi humu ndani" Flora alijisemea.

"Eti mke wangu unachukuliaje huku kutaka kuondoka kwa Rozi naye hapa nyumbani?" Lukasi alimgeukia mkewe Flora na kumuuliza hivyo. "Sasa kama yeye mwenyewe ndio anataka kuondoka sisi tumzuie wa nini? tumuache aondoke" alisema Flora. 

Rozi kimoyomoyo alifurahi sana. "Hapana mke wangu mimi nahisi hapa kuna tatizo kuanzia kule kuhama kwa Japhet na mpaka kutaka kwa huyu binti nahisi wewe mke wangu utakuwa unajua kila kitu, sasa nataka uniambie bila ya kunificha, nini tatizo mpaka Rozi naye anataka kuondoka humu ndani?" Lukasi alichachamaa na kumuuliza hivyo mkewe Flora kwa sauti ya ukali. Flora sasa alibakia anatetemeka kwa hofu.

"Unasema mimi najua kila kitu, sasa mimi najua nini mume wangu kuhusu Rozi kutaka kuondoka?" Flora aliuliza kwa sauti ya kulalamika. Lukasi akatabasamu kiunafiki na halafu akamuambia hivi mkewe Flora: "Nilikuwa naumiza sana kichwa changu kujua ni sababu gani iliyomfanya mdogo wangu Japhet mpaka akahama humu ndani, sasa sababu hiyo karibia nitaijua na pia utaniambia kwanini na Rozi naye anataka kuondoka" alisema Lukasi na kunyanyuka kwenye kochi halafu akamsogelea mke wake Flora na kumpiga Kofi usoni. 

"Wewe mwanamke leo utaniambia ukweli wote unaoujua" alisema Lukasi kwa hasira. Rozi sasa naye akajikuta yupo kwenye wakati mgumu kwani hakutegemea kama haya mambo yangeweza kufikia hatua hii.

"Mmh yaani huku kuaga kwangu tu ndio kumesababisha balaa hili jamani?" Rozi alijiuliza moyoni huku akiwa anatetemeka na kumshuhudia Flora akilia machozi baada ya kupigwa lile Kofi na mumewe!.


"Mmh yaani huku kuaga kwangu tu ndio kumesababisha balaa hili jamani?" Rozi alijiuliza moyoni huku akiwa anatetemeka na kumshuhudia Flora akilia machozi baada ya kupigwa lile Kofi na mumewe.

Lukasi sasa alikuwa amecharuka ile vibaya sana alipandisha hasira sana kupita kiasi. "Nasema hivi sitaki mnifanye mimi mpumbavu, hapa nataka mniambie ukweli wote bila hata ya kunificha" Lukasi aliunguruma. Flora akazidi kulia machozi huku akiuliza: "Sasa Mume wangu jamani unataka tukuambie ukweli gani tena?" Flora aliuliza huku akilia kwa kwikwi.

"Tena wewe hapo ndio nakutaka sana uniambie, inaonyesha unajua kila kitu kinachoendelea" Lukasi alisema huku akimkaba mkewe shingoni. Kwa hakika Flora sasa alikuwa anatia huruma sana.

"Rozi njoo unisaidie jamanii ,,, mdogo wanguuu ,,,ananiuaaa hukuuu" Flora alijikuta akimuomba Rozi msaada kwa sauti ya shida. Rozi huruma ikaweza kumuingia na kumuambia Lukasi hivi: "Jamani Shemeji naomba umsamehe dada basi amekosa atorudia tena" Rozi alijaribu kumtetea Flora na kumuombea msamaha kwa Lukasi. "Rozi naomba uniache kabisa kumbuka na wewe pia nilikuuliza tena kistaarabu tu, lakini ukanificha sasa ngoja nitumie nguvu" alisema Lukasi kwa hasira na kumpiga tena Flora bonge la Kofi usoni. PAAAAA!

"Jamanii Lukasi utaniuwa mume wangu naomba unisamehe sirudii tena ,," Flora alilia na kuomboleza kwa uchungu sana.

"Kufaaa kabisa Malaya mkubwa wewee ," Lukasi aliendelea kufoka kwa hasira.

Baada ya hapo akaanza kumvuta na kum'buruza chini mkewe Flora kumpeleka ndani chumbani kwao wanapolala huku akimuacha Rozi sebuleni akiendelea bado kutetemeka. Lukasi alitisha sana!

Lukasi aliweza kum'buruza mkewe Flora mpaka chumbani na halafu akachukua mkanda wa suruali yake na kumuambia hivi: "Nitakurudia tena muda sio mrefu sana mpumbavuu mkubwa wewe" Lukasi alisema kwa hasira na kutoka kwa kasi humo chumbani huku mkanda wa suruali akiwa ameushika mkononi na kuweza kumfungia mlango kwa nje na ufunguo

Halafu Lukasi akarudi tena mpaka sebuleni na kumkuta Rozi amejikunyata kwenye kochi huku akitetemeka kwa hofu kubwa sana. "Na wewe nimekuja kwako nataka uniambie ukweli, kwanini Japhet amehama humu ndani na halafu na wewe pia kwanini unataka kuondoka hiyo kesho kama ulivyoaga?" Lukasi alimuhoji Rozi kwa hasira. "Shemeji mimi kweli vile sijui kwanini Japhet alihama hapa nyumbani" alisema Rozi kwa sauti ya kutia huruma huku akilia machozi. WAAAAAA! huo ni mlio wa mkanda wa suruali ukitua mwilini kwa Rozi baada ya kupigwa na Lukasi.

"Mamaaa weeee nakufaaaa, Shemeji mimi unanionea sijui kitu chochote ,," Rozi alipiga mayowe na kusema hivyo.

"Uwe unajua ukweli au haujui mimi hapa ninachotaka mniambie nini kinaendelea" Lukasi alisema na halafu akaanza kumvuta na Rozi pia akampeleka mpaka kwenye chumba anacholala binti huyo na kujifungia mlango kwa ndani akiwa na Rozi humo chumbani. "Sikiliza Rozi naomba uniambie ukweli bila hata ya kunificha ni kitu gani kilikuwa kinaendelea humu ndani wakati mimi nipo safarini?" Lukasi aliuliza kwa sauti ya taratibu.

"Shemeji naomba uniamini kweli vile mimi sijui kitu chochote" Rozi bado aliendelea kukataa na kuficha ukweli.

"Rozi ujue mimi sitanii hapa, sema ukweli wote unaoujua vinginevyo na wewe pia utaumia nimewasikieni pale mwanzo mlipokuwa jikoni mkilumbana na dada yako Flora inaonyesha kuna kitu kati yenu kinaendelea juu ya Japhet" alisema Lukasi kwa hasira huku akionekana hana mzaha hata kidogo. Rozi akaona hapa asiposema ukweli anaweza kufa hivihivi lakini akajifikiria ataanzaje kusema kile anachokifahamu yeye. 

Hivyo akaamua kumrudishia Flora msala wake mwenyewe. "Sikiliza Shemeji nenda kwa dada Flora yeye anajua kila kitu, kuhusu mambo yote yanayoendelea atakuambia" alisema Rozi. Lukasi alishusha pumzi ndefu baada ya kumsikia Rozi amesema hivyo. "Una uhakika ataniambia bila ya kunificha, na asiponiambia Je?" Lukasi aliuliza kwa mashaka. "Nina uhakika atakuambia tu vizuri, na asipokuambia njoo tena kwangu mimi nitakuambia" Rozi sasa aliamua kujitoa muhanga.

"Ok hebu ngoja niende nikamjaribu" alisema Lukasi huku akitoka kwa kasi humo chumbani kwa Rozi na halafu akamfungia mlango kwa nje na ufunguo.

Lukasi akarudi tena kule chumbani kwao ambapo alimfungia Flora pale mwanzo na kuingia mpaka ndani akamkuta Flora amenyamaza kulia na amejilaza juu ya kitanda. "Sikiliza mke wangu nataka uniambie ukweli wote kuhusu uhusiano wako wewe na mdogo wangu Japhet, kama utanificha damu itamwagika humu ndani" Lukasi alisema kwa hasira.

"Wala haina sababu ya kunitisha mume wangu nitakuambia kila kitu, kiukweli mimi nampenda sana Shemeji Japhet" Flora aliamua kufunguka ukweli wake.

Lukasi alishtuka sana hakuamini hiki kitu alichokisikia kutoka kwa mkewe Flora.

"Unasemajee mke wangu, hivi una kichaa wewe!?" Lukasi aliuliza kwa mshangao.

"Ndio nina kichaa tena cha Mapenzi mdogo wako amejua kunikoleza na kunifikisha Kimahaba pale ambapo wewe pamekushinda kunifikisha, hivyo nina haki zote za kumpenda yeye nampenda sana Shemeji Japhet" Flora alisema kama vile mtu aliyechanganyikiwa. Lukasi alibakia ameduwaa anamuangalia mkewe Flora Mara mbili mbili hammalizi kabisa.

"Flora mke wangu hicho unachosema ni cha kweli?" Lukasi aliuliza huku machozi yakimlengalenga machoni mwake.

"Kwanini nikufiche mume wangu, au wewe unajiona unaniridhisha kimapenzi?" Flora alimuuliza Lukasi huku akiwa anatabasamu. Lukasi akaona hii sasa ni dharau kubwa sana kwake. "Noooo mke wangu siwezi kuvumilia dharau hiyoo" alisema Lukasi na moja kwa moja akaenda kumvamia Flora pale kitandani na kunyanyuka naye wakasimama wima.

"Mke Flora umejua kunidhalilisha sana, hivi wewe ni wa kufanya mapenzi na mdogo wangu Japhet kweli?" Lukasi aliuliza huku akitetemeka kwa hasira.

"Ndio nimeshafanya naye sasa, na hapa natamani nifanye naye zaidi na zaidi kila siku nampenda sana Japhet" alisema Flora kwa kujiamini na kujitoa ufahamu.

"Hapanaaaa inatoshaaa Floraaaa" alijikuta anabwata hivyo Lukasi na kumkamata kwa nguvu mkewe Flora akaenda kumpigiza kichwa chake kwa nguvu kwenye kabati kubwa la nguo.

"Mamaaa nakufaaaa unaniuaa Lukasi ,," alipiga yowe la uchungu Flora baada ya kupigizwa kichwani kwenye kabati. Kwa Bahati mbaya sana Flora alifikia usoni kabatini hapo na kujipigiza sehemu ya kwenye Kioo na kupasuka kabisa halafu vipande vya Kioo vikamchana vibaya sana usoni na kupelekea damu nyingi sana kumvuja. "Hayo ndio malipo yako ya Usaliti Malaya mkubwa wewe" alisema Lukasi kwa hasira. Flora alilia sana kwa maumivu huku akijishika usoni mwake.

"Sawa ndio nakubali kama haya ndio malipo yangu, lakini naomba utambue jambo moja mume wangu kuwa Utamu wa Shemeji ni zaidi kukushinda wewe" alisema Flora. Lukasi alikasirika sana akachukua kipande kikubwa cha Kioo na kwenda kumpiga nacho kichwani mkewe Flora. "Jamaniiii Lukasi unaniuaa mume wanguu ,," alisema Flora na baada ya hapo akaanguka chini na kutulia kimya.

INAENDELEA

Powered by Blogger.