KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Utamu Wa Shemeji Flora Sehemu Ya Ishirini (20)


SIMULIZI NZURI YA KUSISIMUA
Lukasi akafikiria kidogo halafu akasema:

"Mdogo wangu Japhet naomba usinifiche niambie ukweli wako, kumbuka mimi ni kaka yako wa damu kabisa na kama utanificha utakuwa unakosea sana" Lukasi alisema kama kumtega Japhet.

"Sasa nikufiche kitu gani tena kaka? huo ndio ukweli wangu niliokuambia" Japhet alisema kwa kujiamini. Hapo tena Lukasi akakosa cha kuongea akabakia kimya.

"Kwani kaka umehisi nini mpaka ukaamua kuniuliza hivyo?" Japhet aliuliza.

"Sikufichi mdogo wangu Jana usiku Shemeji yako nilimkuta kwenye mlango wa chumbani kwako, akiwa anajaribu kuwachungulia baada ya kuzisikia sauti za Mahaba zikitokea humo ndani" Lukasi aliamua kusema ukweli wote kwa mdogo wake huyo. Japhet alishtuka sana baada ya kusikia hivyo. "Kwani mimi Jana usiku niliingiza msichana chumbani kwangu?" Japhet alijifanya kuuliza hivyo.

"Ndio Jana ulikuwa na Rozi usiku humu chumbani hata mimi pia nilisikia sauti hizo, lakini hiyo mimi ainishtui kabisa kilichonishtua ni kwanini Shemeji yako Flora awachungulie chumbani" Lukasi alisema kwa hisia kali. Japhet akaona hili sasa balaa kumbe waliyoyafanya Jana usiku na Rozi yalisikika na kugundulika.

"Hapo kaka hata mimi sijui kwanini Shemeji aje kutuchungulia, lakini pia naomba msamaha sana kama nitakuwa nimekosea kumuingiza Rozi humu ndani chumbani" Japhet alisema kwa unyonge.

"Usiogope kuhusu hilo mdogo wangu, Rozi wewe ni halali yako kabisa unaweza kuwa na mahusiano naye bila tatizo" alisema Lukasi na baada ya hapo akamuaga Japhet na kurudi zake kule sebuleni huku nyuma akimuacha kijana huyo akiwa na lundo la mawazo kichwani. "Hayaa sasa kumekuchaa, kaka ameshtukia mchezo hivi na Shemeji naye kwanini anashindwa kujizuia?" Japhet alijiuliza peke yake na asipate jibu.

"Hapa cha msingi ni kuhama tu, bora ya lawama kuliko fedhea nikiendelea kubakia hapa nijiandae na balaa" alijisemea moyoni mwake Japhet.

Hatimaye muda wa kula chakula cha usiku nao uliweza kuwadia na Familia yote ilikutana Mezani kwa ajili ya kula chakula hicho. Japhet bado kichwani mwake aliendelea kuwaza ni vipi atapata ujasiri wa kuaga mbele ya kaka yake na Shemeji yake Flora. 

"Ni bora tu kuwaaga aijalishi kaka atanichukuliaje" Japhet bado alijiwazia. Waliendelea kula kimya kimya bila kusemeshana kitu chochote jambo ambalo sio la kawaida kwa Familia hii kwa mbali Japhet akapata kuhisi mpasuko unakaribia kuikumba Familia ya kaka yake. Baada ya kumaliza kula chakula Rozi akaondoa vyombo vyote Mezani hapo na kuvipeleka huko Jikoni.

Japhet sasa akaona hapahapa ndio kwa kuliamsha Dude aanzishe mazungumzo.

"Kaka na Shemeji nilikuwa na maongezi kidogo hivyo naombeni mnisikilize" Japhet ndio alianza hivyo. Flora kwanza alishtuka sana kumsikia Japhet anasema ana maongezi anataka kuyaongea hapo mawazo yake yakaenda mbali na kuhisi labda Japhet anataka kutoa siri ya kusumbuliwa kimapenzi na yeye (Flora)

"Maongezi gani tena hayo mdogo wangu? haya unaweza kuongea sisi tupo hapa tunakusikiliza" alisema Lukasi huku akijiweka tayari kumsikiliza Japhet anataka kuongea nini. Kwanza Japhet akakohoa kidogo kuliweka sawa koo lake halafu ndio akasema: "Kaka pamoja na Shemeji napenda kuwajulisha kuwa mimi nina mpango wa kuhama humu ndani na kwenda kupanga chumba changu" Japhet alisema bila hata kupepesa macho yake.

Kiukweli hiki alichokisema Japhet kilimshtua sana Lukasi pamoja na mkewe Flora. "Kwanini sasa Japhet unaenda kupanga chumba, na wakati unajua kama wewe ndio nakutegemea hapa nyumbani pindi nikiwa nipo safarini enhe?" Lukasi alimuuliza Japhet. "Hilo nalijua kaka lakini imenibidi kufanya hivyo ili na mimi nipate kujipanga vizuri kimaisha" Japhet alisema kwa sauti yenye kujiamini.

"Sasa utaenda vipi kujipanga kimaisha na ikiwa hauna hata kitanda wala godoro na isitoshe pia hata hiyo kazi nayo hauna?" Lukasi aliuliza huku akimuangalia usoni Japhet. 

"Ndio kaka najua kama sina kitanda wala godoro na hata kazi pia sina, lakini vyote hivyo nitaenda kuvipata hukohuko" alisema Japhet. Flora muda wote alikuwa yupo kimya akiwaza ndani ya Akili yake na kuona hii ni mbinu ya Japhet kumkimbia au kumkwepa yeye.

"Sawa mdogo wangu sisi hatuna uwezo wa kuyapinga maamuzi yako, lakini ujue umetusononesha na hii taharifa vipi sasa kuhusu kazi niliyokuahidi nitakutafutia?" Lukasi aliuliza kwa sauti ndogo ya huzuni. 

"Kuhusu kazi wala usijali kaka bado nitakuwa nakusubiria na kukutegemea wewe unitafutie" alisema Japhet. Flora naye akavunja ukimya na kuuliza: "Sasa Shemeji unataka kuhama lini hapa nyumbani na ni wapi huko unapohamia?" Flora aliuliza kwa sauti ndogo iliyopoa.

"Nafikiria nitahama hapa kesho, na huko ninapohamia ni maeneo ya Yombo Buza Kanisani" Japhet alimjibu hivyo Flora.

"Mbona unataka kuhama kwa haraka kiasi hicho, kwani hicho chumba tayari umeshakipata?" Lukasi aliuliza.

"Ndio kaka chumba tayari nimeshapata na kodi ya miezi sita pia nimelipia" alisema Japhet kwa sauti ya msisitizo.

Mpaka hapo Lukasi na mkewe Flora walikuwa wamebaki hoi kwani walijua Japhet alikuwa amejiandaa vya kutosha kwa upande wa Lukasi hakuwa anaijua ni sababu gani haswaa inayomfanya huyu mdogo wake (Japhet)) mpaka anataka kuhama kwa ghafla kiasi hicho. Lukasi alibakia anaumiza kichwa chake na hatimaye akasema: 

"Sawa hakuna shida Japhet ila ningeomba hiyo kesho unipeleke huko unapohamia ili niweze kupaona na ikiwezekana nikununulie hata kitanda pamoja na godoro la kuanzia maisha huku nikiendelea na mchakato wa kukutafutia kazi" alisema Lukasi.

Japhet hakuweza kukataa kuhusu kaka yake kwenda kupajua anapohamia hivyo aliweza kukubali kwenda naye. Basi na maongezi hayo yaliishia hapo na kila mmoja akaenda chumbani kwake kulala hata hamu ya kuangalia Tamthilia kwenye TV usiku huo kama wanavyofanya siku zote leo hakukuwa na mtu mwenye hamu hiyo waliingia vyumbani mapema kulala.



Japhet akiwa amejilaza kitandani chumbani kwake kidogo alijisikia kuwa na Amani moyoni mwake baada ya kuona amepata Baraka za kaka yake na kumruhusu kuhama hapa nyumbani.

"Sasa ndio utakuwa ni wakati wetu mzuri wa mimi na Rozi kuyafurahia mapenzi yetu kwa Uhuru bila ya kuingiliwa na Shemeji huko tuendapo" Japhet alijisemea moyoni huku akitabasamu.

"Najua kama Shemeji ananipenda sana lakini itakuwa ngumu kuwa naye, siku ile ni Bahati mbaya tu imetokea mpaka nikafanya naye mapenzi naapa sitaki ijirudie tena najuta kumvunjia heshima kaka yangu" alisema Japhet kwa huzuni huku akiukumbuka usiku ule aliofanya mapenzi na Shemeji yake Flora baada ya kuja kumgongea mlango usiku wa manane na kumtega kwa mitego ya kimahaba na mwisho wake wakajikuta wanafanya mapenzi kabisa. Japhet alijisikia vibaya sana baada ya kukumbuka jambo hilo. 

"Kama angekuwa ni mwanamke mwingine na sio Shemeji yangu, ningekubali kuchepuka naye ili nimchune fedha na zawadi zake lakini sasa Bahati mbaya ndio Shemeji yangu tena ni mke wa kaka yangu ngoja tu nimpotezee yasije kunikuta makubwa" alijisemea Japhet huku akiivuta shuka mwilini na kujifunika akaanza kuutafuta usingizi akiisubiria hiyo kesho yake kwa hamu kubwa sana ili apate kuhama. Kwa usiku huu wa leo hakuwa na ahadi ya kukutana na Rozi humo ndani chumbani hivyo kijana Japhet alilala usingizi.



Chumbani kwa Lukasi na mkewe Flora nao walikuwa wamejilaza juu ya kitanda na Lukasi aliweza kuigundua huzuni ya mke wake huyo Mara baada ya Japhet kusema anataka kuhama hapa nyumbani hiyo kesho. "Mbona mke wangu namuona yupo na huzuni sana juu ya huku kuhama kwa Japhet humu ndani? hapa ni lazima kutakuwa na jambo linaendelea kati yao" alijisemea moyoni Lukasi huku akimuangalia mkewe aliyekuwa amejifunika shuka gubigubi mwili mzima kitandani hapo. Sio siri taharifa aliyoitoa Japhet kuwa anataka kuhama humu ndani ya nyumba ilimchanganya sana Flora kwani kiukweli ndani ya moyo wake alijikuta amempenda sana kijana huyo. Sasa aliona endapo kama Japhet atahama ina maana ndio itakuwa mwisho wa ndoto zake anazoota muda wote kuwa ataufaidi Utamu wa Shemeji yake huyo siku zote. Flora aliumia sana moyoni mwake kumkosa kijana Japhet.

Wakati Flora akiendelea kuhuzunika huku mumewe (Lukasi) alikuwa bado yupo anaumiza kichwa chake na mawazo.

"Kwanini Japhet anataka kuhama humu ndani ghafla na Pesa ya kodi ameipata wapi na ikiwa hana kazi yeyote? nahisi kuna jambo atakuwa amelitenda yeye na Shemeji yake sasa anaona bora ahame ili kukwepa tatizo" alijiwazia hivyo Lukasi na hapohapo akamgeukia mkewe na kumuuliza hivi: "Eti mke wangu hivi unachukuliaje huku kuhama kwa Shemeji yako Japhet?" Lukasi alimuuliza mkewe huyo kwa mtindo flani hivi wa kumtega ili kuona atajibu nini. "Mume wangu naomba uniache kwanza sijui hata nikujibu vipi, kwani Shemeji Japhet nimemzoea sana hivyo kutaka kwake kuhama ni maumivu makubwa sana kwangu" alisema Flora na hapohapo akaanza kulia machozi ya kilio cha kwikwi kuonyesha ana huzuni sana.

Lukasi akajaribu kum'bembeleza Flora huku pia akishangaa hata usiku huu ajasumbuliwa kabisa kuhusu kufanya mapenzi na mkewe huyo kama vile ilivyokuwa usiku wa Jana yake uliopita.

"Ngoja kesho nikishaenda kupaona huko anapohamia Japhet halafu nikirudi hapa nyumbani nitam'bana vizuri Rozi na ikibidi hata kiasi cha Pesa nitampa ili aweze kuniambia ukweli, inawezekana yule binti atakuwa anajua kila kitu kuhusu Japhet na Shemeji yake wakati nilipokuwa nipo safarini" Lukasi alijisemea moyoni huku akichukua shuka na kujifunika!.



"Ngoja kesho nikishaenda kupaona huko anapohamia Japhet halafu nikirudi hapa nyumbani nitam'bana vizuri Rozi na ikibidi hata kiasi cha Pesa nitampa ili aweze kuniambia ukweli, inawezekana yule binti atakuwa anajua kila kitu kuhusu Japhet na Shemeji yake wakati nilipokuwa nipo safarini" Lukasi alijisemea moyoni huku akichukua shuka na kujifunika na kulala.

Asubuhi ya siku nyingine mpya nayo ikaweza kufika. Japhet aliamka mapema sana siku hii ya leo tofauti na siku zingine ambazo mara nyingi anakuwa anachelewa kuamka. Hivyo kijana Japhet baada ya kuamka asubuhi hii ya leo alianza moja kwa moja mchakato wa kupanga vizuri nguo zake na kuzihifadhi kwenye Begi lake kubwa. "Hizi nguo alizoninunulia Shemeji sijui niende nazo au nimrudishie?" Japhet alijisemea huku akiziangalia nguo hizo alizopewa na Flora kama zawadi. Hata hivyo Japhet aliamua kuziacha nguo hizo pamoja na viatu vyake na hata pia ile simu ya Smartphone nayo aliamua kutaka kumrudishia Flora.

"Sihitaji kuwa naye kimapenzi sasa ni kwanini nivichukue vitu vyake? siwezi kuondoka navyo nitamuachia hapahapa" alisema Japhet na baada ya hapo akachukua mswaki wake akauweka dawa ya meno na halafu akatoka zake humo chumbani na kuelekea uwani kwenda kunawa uso wake na kupiga mswaki.

Japhet baada ya kufika huko uwani akamkuta na Rozi naye tayari ameamka yupo anafagia uwani hapo. Rozi baada ya kumuona Japhet akaacha kufagia na kwenda moja kwa moja kumkumbatia kijana huyo. "Yaani baby hata bado sijaamini kama leo ndio unahama humu ndani" alisema Rozi huku akiegemea kifuani kwa mpenzi wake Japhet.

INAENDELEA

Powered by Blogger.