KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Utamu Wa Shemeji Flora Sehemu Ya Ishirini na Tatu (23)

SIMULIZI NZURI YA KUSISIMUA
Huo ndio ulikuwa mwisho wa Flora kwani alifariki dunia hapohapo. Lukasi alibakia akiuangalia mwili wa mkewe Flora ambao ulikuwa hauna uhai kabisa kwa wakati huo. "Nisamehe sana mke wangu Flora imenibidi kufanya hivi ili kulinda heshima yangu" alisema Lukasi huku akibubujikwa na machozi ya uchungu.


Kwa upande wa Rozi naye kule chumbani alipofingiwa na Lukasi aliweza kuzisikia zile purukushani zote zilizokuwa zikiendelea kati ya Lukasi na mkewe Flora kule chumbani kwao. "Ooohoo Mungu wangu sijui kama kuna usalama kweli huko" alijisemea Rozi baada ya kuhisi ukimya wa ghafla. Ikabdi ajaribu kuufungua mlango wa humo chumbani kwake lakini kwa Bahati mbaya ndio vile ulikuwa umefungwa kwa nje na ufunguo muda ule na Lukasi alipotoka humu ndani. "Mimi nahisi huko hakutakuwa na usalama mbona siwasikii tena wakigombana?" 

Rozi aliendelea kujiuliza huku akizungukazunguka humo chumbani hapohapo Rozi akapata wazo la kumpigia simu mpenzi wake Japhet amuambie hiki kinachoendelea huku nyumbani. 

Akachukua simu yake iliyokuwa ipo kitandani na kuanza kuitafuta namba ya Japhet na kwa Bahati nzuri akaipata na kuipiga ikawa inaita. Rozi alibakia kusubiri Japhet apokee simu na aweze kumpa taharifa. Mara ghafla akaweza kusikia sauti za RAIA ambao nao walikuwa wamesikia Tafrani hiyo na wakaweza kusogea hadi hapo kwenye eneo la tukio nyumbani kwa Lukasi.

RAIA hao ambao wengi wao walikuwa ni majirani baada ya kusogea mpaka mlangoni ndipo wakagundua milango yote ya kuingilia ndani ya nyumba hii ya Lukasi ilikuwa imefungwa kwa ndani hivyo wakaanza kubisha hodi kwa nguvu na kuomba wafunguliwe ili waingie ndani.

Lukasi akiwa bado yupo kule chumbani kwake akiushangaa mwili wa mkewe Flora ambaye mpaka muda huo alikuwa ameshakufa. Mara ghafla ndipo akasikia sauti ya kugongwa kwa mlango Mkubwa wa kuingilia ndani ya nyumba yake.

"Daah majirani hao wamesikia na wamekuja, sasa sijui nitafanya nini hapa?" Lukasi alijiuliza huku mikono yake yote miwili akiwa amejishika kichwani mwake.

Hapohapo akajikuta anapata na wazo la kujiua ili kukwepa mkono wa sheria kwa kosa la kusababisha kifo cha mkewe Flora. "Nisamehe sana Mungu wangu kwa haya niliyoyafanya najutia sana, Japhet mdogo wangu nimekusamehe yote najua sio makosa yako" alisema Lukasi halafu akaokota kipande kikubwa cha Kioo chenye Ncha Kali na kufumba macho yake. "Mungu baba naomba na mimi unipokee sasa ni muda wangu wa kurejea kwako umewadia" alisema Lukasi na halafu akakikamata kwa mikono yake Kioo hicho na kukishusha kwa nguvu sana Tumboni mwake na kujichoma.

Damu nyingi sana iliweza kumtoka baada ya kujichoma na Kioo hicho ambacho kilimchana na kuzama kabisa ndani ya Tumbo lake na kumpelekea Lukasi kuanguka chini na kuanza kutapatapa na baadae akatulia kimya na kufariki dunia!.



Damu nyingi sana iliweza kumtoka baada ya kujichoma na Kioo hicho ambacho kilimchana na kuzama kabisa ndani ya Tumbo lake na kumpelekea Lukasi kuanguka chini na kuanza kutapatapa na baadae akatulia kimya na kufariki dunia.

Kwa upande wa Japhet naye akiwa kule kwenye chumba chake ajui hili wala lile kuhusu Yale mambo yaliyotokea kule nyumbani kwa kaka yake Lukasi. Majira haya ya usiku Japhet ndio sasa alikuwa anajiandaa kulala Mara baada ya kutoka kupiga story kwa yule rafiki yake Mussa.

Ghafla Japhet akaweza kuisikia simu yake ya mkononi inaita na alipoangalia ni nani huyo anaempigia simu akagundua ni Rozi. "Mmh basi huyu binti ameshaanza tena usumbufu wake wa kutaka kuja huku" alijisemea Japhet huku akiwa anatabasamu na kuipokea simu hiyo.

"Enhe niambie mpenzi wangu, vipi tayari umeshaaga hapo nyumbani?" Japhet aliuliza Mara baada ya kupokea simu.

"Japhet naomba uache chochote unachokifanya sasa hivi njoo huku nyumbani haraka sana" Rozi alisema kwa pupa baada ya kuisikia sauti ya Japhet.

"Wee Rozi kuna nini tena kimetokea huko nyumbani? hebu niambie kwanza" Japhet naye alijikuta anauliza kwa wasiwasi.

"Nimekuambia njoo haraka sana, haya mambo ya huku utakuja kuyajua pindi utakapofika naomba uzingatie hiki ninachokuambia Japhet" alisema Rozi na kukata simu yake ghafla. Japhet alibakia njia panda hakujua ni kitu gani tena hicho kilichokea huko nyumbani kwa kaka yake Lukasi. "Mmh kuna nini huko? mbona sasa naanza kupata wasiwasi" Japhet alijisemea kwa sauti ndogo. Hapohapo akapata wazo la kumpigia simu yake Lukasi ili ajue kinachoendelea lakini kwa Bahati mbaya simu ya kaka yake huyo ilikuwa inaita tu bila hata ya kupokelewa.

"Sasa naanza kupata mashaka kuwa huko hali itakuwa sio shwari, hebu ngoja niende" alisema Japhet na hapohapo bila ya kupoteza muda akanyanyuka kwenye kitanda alipokuwa amejilaza na kuanza kujiandaa harakaharaka kwa kuvaa nguo za kutokea na halafu akaufunga vizuri mlango wa chumba chake na kuondoka.

"Hebu ngoja kwanza nipitie kwa rafiki yangu Mussa" alisema Japhet huku akikatiza mitaani usiku huo kwenda kwa rafiki yake Mussa kumuomba ushauri na ikiwezekana hata amsindikize huko nyumbani kwa kaka yake Lukasi. Japhet alipoangalia saa kwa kupitia simu yake ya mkononi ikamjulisha kuwa ni majira ya saa 4:56 za usiku Japhet akaondoka.



Rozi naye akiwa bado yupo chumbani alipofungiwa na Lukasi. Baada ya kukata simu yake ghafla pale alipokuwa anaongea na mpenzi wake Japhet sasa Rozi aliweza kusikia sauti ya zogo la majirani huko nje ya nyumba ambao nao walikuwa wamekuja hapo baada ya kusikia ile Tafrani iliyosababishwa na Lukasi. Ikabidi Rozi ajiongeze kwa kusogea hadi dirishani na kuanza kupiga makelele ya kuomba msaada kwa watu hao ambao wapo nje. "Jamaniii msaada hukuu nipo hapa dirishaniiii" Rozi alipaza sauti yake kwa nguvu. 

Bahati nzuri sauti hiyo ya Rozi iliweza kuwafikia vyema Raia hao na kwa haraka wakasogea mpaka dirishani iliposikika sauti ya binti huyo na wakaweza kumuona akiwa amesimama kwa ndani. "Vipi binti mbona hivyo tumesikia makelele na milango yote ya kuingilia ndani imefungwa, kwani nini kimetokea?" Mzee mmoja wa makamo ambaye ndie mjumbe wa nyumba kumi (10) kwenye mtaa huo alimuuliza Rozi.

"Babu yaani hata mimi sijui kilichotokea, kwani nimefungiwa humu chumbani na Shemeji kwa nje" alisema Rozi. Kwa hayo maelezo kidogo ya Rozi yalitosha kabisa kuwajulisha Raia hao kuwa humu ndani ya hii nyumba kuna hatari imetokea. Hivyo baada ya kushauriana wote kwa pamoja hatimaye mjumbe huyo wa nyumba kumi akaamuru mlango Mkubwa wa kuingilia ndani hapa nyumbani kwa Lukasi uvunjwe ili waweze kuingia ndani wakaone kuna nini kimetokea. 

Vijana wenye nguvu wakafanya kazi hiyo ya kuvunja mlango na baada ya muda mfupi waliweza kufanikisha zoezi hilo na wakaweza kuingia mpaka ndani ya mjengo huo na kujionea hali halisi. Kwa hakika ulikuwa ni mshtuko Mkubwa sana pamoja na majonzi yaliweza kuwakumba Raia baada ya kuikuta miili ya wanandoa hao (Lukasi na mkewe Flora) ikiwa ipo imelala chini chumbani kwao huku ikivuja damu bila ya kuwa na dalili ya uhai. 

Ikabidi kwanza wamfungulie na Rozi naye kule chumbani kwake alipofungiwa na baada ya hapo ikapigwa simu mpaka kituo cha Polisi na kutoa taharifa ya hili tukio. Rozi hakuweza kuyaamini macho yake baada ya kufunguliwa chumbani na kuonyeshwa miili ya mabossi wake wote wawili wakiwa wamefariki dunia. 

Rozi alijikuta anaangusha kilio cha uchungu na kuwalilia mabossi wake hao. Japo jibu lilikuwa ni rahisi kuwa Lukasi ndie chanzo cha mauaji haya kwa kumuua mkew Flora na baadae kujiua yeye mwenyewe. Lakini majirani nao hawakuwa nyuma katika kuusaka 'Ubuyu' (Umbeya) kwa kumdadisi Rozi awaeleze nini kilitokea mpaka hawa wanandoa wamekumbwa na mauti. Kwa jinsi Rozi alivyokuwa amechanganyikiwa hakuweza kutoa jibu lolote la maana kwa Raia hao zaidi tu ya kulia machozi. Basi wakaamua kutulizana na kuwasubiri Askari Polisi waje hapa eneo la tukio na huku kundi kubwa la Raia wakipiga picha za tukio hilo kwa kutumia simu zao na kurusha kwenye mitandao ya kijamii.



Wakati gari mbili aina ya DEFENDER za jeshi la Polisi zikifunga break Kali hapa nyumbani kwa Lukasi ndipo na muda huohuo nao Bajaj iliyompakia kijana Japhet na rafiki yake Mussa nayo pia ilikuwa ndio inawasili maeneo haya. Japhet na Mussa walishangazwa na huu wingi wa watu waliowakuta hapa na kilichowashtua zaidi ni kuona hizo gari mbili za Polisi pamoja na Askari wake.

"Mmh Mussa ndugu yangu hapa hakuna usalama kabisa" alisema Japhet huku mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio.

"Usipagawe ndugu yangu hebu twende huko ndani tukaone kuna nini ambacho kimetokea" alisema Mussa huku akilipia Pesa ya Bajaj iliyowaleta hapa. Baada ya hapo Mussa akamshika mkono Japhet aliyeonekana kuchanganyikiwa au kama sio kupagawa kabisa na halafu akaanza kumuongoza kwa kuingia ndani.

Baada ya kuingia ndani ya nyumba sasa kila kila kitu kilikuwa Hadharani kwani Japhet akaweza kuishuhudia kwa macho yake miili ya marehemu hao ambao ni kaka yake Lukasi pamoja na Shemeji yake Flora. Hapo Japhet sasa alijikuta anakaribia kuwa mwendawazimu kwa haya aliyoyaona hapa. Mussa akapata kazi ya ziada kumtuliza rafki yake huyo.

Japhet alilia machozi kama vile mtoto mdogo watu wengi sana walimuhurumia na hata Polisi nao baada ya kumgundua kuwa huyu ni mdogo wa marehemu Lukasi wakamsogelea na kujaribu kumuuliza maswali mawili matatu lakini kutokana na kupagawa Japhet akashindwa kujibu vyema maswali ya Askari hao na kuishia tu kulia machozi.

Basi baada ya Askari kufanya uchunguzi wao wakaichukua miili ya marehemu hao na kuipakia kwenye gari ya Polisi tayari kwa kwenda kuhifadhiwa hospitalini. Rozi naye akajikuta anaingia matatani kwenye mikono ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi. "Inabidi tumchukue huyu binti kwanza tunaenda kufanya naye mahojiano juu ya tukio hili, halafu pia na wewe tutakuhitaji baada ya kumaliza taratibu zote za mazishi ya ndugu yako pamoja na Shemeji yako" alisema mmoja wa Askari aliyeonekana kuwa na cheo kikubwa. "Lakini afande huyo binti anahusikaje na hili tukio?" Japhet alijikuta anauliza hivyo. 

"Sikiliza kijana sisi atujasema kama huyu binti anahusika na hili tukio, tunachohitaji ni kujua nini chanzo cha ugomvi wao mpaka vifo vyao vikatokea" alisema Askari huyo. Basi ikabidi Japhet akubali kuwa mpole. Gari za Polisi zikaondoka eneo hilo huku gari moja ikielekea hospitli ya Taifa kwenda kuhifadhi miili ya marehemu na ile gari nyingine ikielekea kituo cha Polisi kumpeleka Rozi ambaye alikuwa anashikiliwa kwa mahojiano zaidi. 

Japhet na Mussa walibakia nyumbani hapo kwa marehemu na kuanza kutoa taharifa za msiba huo Mkubwa kwa ndugu na jamaa wote usiku huohuo kwa njia ya simu.

Japhet licha ya kupagawa na msiba huo wa kaka yake pamoja na Shemeji yake lakini hakuacha kujiuliza maswali ndani ya kichwa ni kitu gani kilitokea mpaka haya mambo yakafikia hatua hii mbaya kiasi hiki cha kusababisha mpaka vifo.

Bahati mbaya sana akuwahi kuongea na Rozi baada ya kufika hapa na kumuuliza kilichotokea kwani ndio vile tena Rozi yupo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.

"Mmh nahisi Rozi atakuwa ametoa siri kwa kaka Lukasi mpaka amefikia hatua ya kumuua Shemeji Flora na halafu na yeye pia akajiua, na kama ataenda kusema hivyo hadi huko Polisi basi tumeisha" alisema Japhet kwa sauti ndogo ya chini huku machozi yakimtiririka machoni.

inaendelea

Powered by Blogger.