KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

Chombezo : Utamu Wa Shemeji Flora Sehemu Ya Ishirini na Nne (24)

SIMULIZI NZURI YA KUSISIMUA
Baada ya siku tatu kupita taratibu zote za msiba ziliweza kufanyika na hatimaye siku ya kwenda kuwazika marehemu hao ilifika. Ndugu na jamaa wa pande zote mbili waliweza kukusanyika nyumbani kwa Lukasi yaani ndugu wa Flora pamoja na ndugu wa Lukasi mwenyewe nao pia walikuwepo huku kila mmoja akijiandaa na maswali ya kumuuliza Japhet kwani ndie ndugu waliyekuwa wanamfahamu anaishi na marehemu kabla ya vifo vyao kutokea. Hivyo walikuwa na uhakika kuwa Japhet atakuwa anajua chanzo chote cha tukio hilo baya na la kutisha. Kila mmoja alijiandaa kumuuliza Japhet anachokijua juu ya vifo hivyo mara baada ya kumaliza kabisa mazishi. 

Kwa upande wa Japhet ilikuwa ni siku ngumu sana pale Masanduku (Majeneza) yaliyobeba miili ya marehemu yalipowasili hapo nyumbani kwa ajili ya kuagwa kabla ya kusafirishwa kwenda kuzikwa. Japhet alikumbuka mengi sana aliyoahidiwa na kaka yake Lukasi kuhusu kutafutiwa kazi na pia akakumbuka hata hivi karibuni alivyomnunulia vile vitu vya kwenda kuanza navyo maisha pindi pale alipoaga kuwa anaenda kuanza maisha ya kujitegemea kumkimbia Shemeji yake Flora aliyekuwa anamsumbua kimapenzi.

"Lakini yote haya ameyasababisa Shemeji Flora na mimi pia nina makosa kama ningeweka msimamo wa kukataa kufanya naye mapenzi leo tusingefikia hatua hii" alijisemea moyoni Japhet huku akilia. Pia akaenda mbali ña kujilaumu ni bora tu hata angetoroka wakati ule alipopata wazo la kutoroka nyumbani kwa kaka yake Lukasi. "Lakini ndio hivyo nguvu ya mapenzi yangu kwa Rozi ndio ilinifanya mpaka nibakie, na kuona bora twende tukapange chumba ili kuepuka usumbufu" aliendelea kujisemea Japhet huku akijifuta machozi. 

Rafiki yake Mussa bado alikuwa naye bega kwa bega katika kumliwaza na kumfariji rafiki yake huyu (Japhet) Baada ya kukamilisha zoezi la kutoa heshima za mwisho (Kuaga) kwa miili ya marehemu hao sasa safari ya kuelekea mkoani Dodoma kwa mazishi ikaanza na Bahati nzuri Lukasi pamoja na mkewe Flora wote walikuwa wanatokea mkoa mmoja isipokuwa vijiji tu ndio tofauti hivyo Mabasi mawili madogo aina ya (COSTA) yalitumika kubeba msiba na waombolezaji. Japhet akiwa yupo njiani akielekea mkoani Dodoma kumzika kaka yake Lukasi pamoja na Shemeji yake Flora. JJaphet alikuwa anawaza na alijua kwa vyovyote vile huko ataulizwa na ndugu nini chanzo cha vifo hivyo. 

Na kibaya zaidi kinachomchanganya Japhet ni huku kutakiwa kuripoti kituoni (Polisi) pindi akirudi kutoka mazishini akaungane na mpenzi wake Rozi kwenye mahojiano. Wakati Japhet akiendelea kuwaza juu ya jambo hilo Mara ghafla akapata wazo. Wazo lenyewe ni kutoroka na kukimbilia sehemu isiyojulikana baada ya kumaliza mazishi. "Yes ngoja nikimbie nimuachie Rozi peke yake hii kesi ya kujibu" Japhet alijisemea moyoni na kuona hiyo ni njia bora zaidi kuyaepuka maswali ya Polisi!.




**************

Wakati Japhet akiendelea kuwaza juu ya jambo hilo Mara ghafla akapata wazo.

Wazo lenyewe ni kutoroka na kukimbilia sehemu isiyojulikana baada ya kumaliza mazishi. "Yes ngoja nikimbie nimuachie Rozi peke yake hii kesi ya kujibu" Japhet alijisemea moyoni na kuona hiyo ni njia bora zaidi kuyaepuka maswali ya Polisi.

Lakini wazo hilo la kutaka kukimbia na kutoroka Japhet hakutaka kulipa nafasi kabisa ndani ya Akili yake. Kwani alijua kama endapo atafanya hivyo kukimbia basi anaweza kujitafutia matatizo zaidi.

"Acha tu nimalize kuzika halafu nirudi mjini nikaripoti kituoni wakanihoji na mimi" Japhet alijisemea ndani ya moyo wake. Mpaka kufikia hapo mawazo yake yakaenda mbali sana Kwani pia akuacha kumuwaza Rozi binti ambaye alimuona kama vile anateseka huko Mahabusu ya Polisi anaposhikiliwa kwa mahojiano zaidi. "Yote haya ameyasabisha Shemeji Flora, endapo kama angenipotezea basi sidhani kama kaka Lukasi angeweza kuhisi kitu kati yetu" 

Japhet aliendelea kujisemea kimoyomoyo huku lawama zote akimtupia Shemeji yake huyo (Flora) ambaye kwa muda huu alikuwa tayari ni marehemu. "Kulazimisha kwake mapenzi kwangu hatimaye ndio hivi sasa kumeleta balaa mpaka kupelekea vifo vya ghafla" Japhet alijisemea moyoni huku akijifuta machozi yaliyokuwa yakimtiririka.

Wakati Japhet akiendelea kutafakari hayo huku safari ya kuelekea Dodoma kumzika kaka yake (Lukasi) ikiendelea baadhi ya waombolezaji ambao wengi wao ni ndugu na jamaa bado walikuwa na Sintofahamu ya kujiuliza maswali yasiyo na majibu. Wengi walikuwa wanajiuliza nini kisa na mkasa kilichotokea mpaka Lukasi kaka yake Japhet akafikia hatua ya kumuua mkewe Flora na halafu pia na yeye kujiua. Hilo ndio swali ambalo liliwaumiza vichwa wengi bila ya majibu.

Hisia za wengi walipata kuhisi labda itakuwa ni wivu wa kimapenzi ndio uliosababisha ugomvi wao kabla ya kifo kutokea mwishoni. Japhet alionekana ndie mwenye majibu ya maswali yote yaliyokuwa yanawasumbua wengi hivyo kwanza walimuacha mpaka wamalize kuzika halafu ndio wamuulize na awape majibu ya hayo maswali yao.



Hatimaye kwenye majira ya usiku sana ndio walikuwa wanawasili Dodoma mpaka kijijini kabisa kwa akina Japhet. Kwa kuwa Dar es salaam walitoka majira ya jioni ndio maana waliweza kufika muda huo wa usiku. Gari hiyo aina ya COSTA ambayo ndio ilikuwa imetumika kusafirisha msiba pamoja na waombolezaji iliposimama mbele ya uwanja wa nyumbani kwa wazazi wa Japhet vilio viliweza kusikika japokuwa ilikuwa ni usiku lakini huzuni na majonzi vilipata kutawala maeneo hayo. Jeneza lenye mwili wa Lukasi lilipoteremshwa kwenye gari na kuingizwa ndani ya nyumba Japhet aliwashuhudia wazazi wake wakilia kwa uchungu mwingi sana wakimlilia kijana wao Lukasi ambaye ndio alikuwa ni tegemeo na mwenye msaada.

Japhet alijisikia vibaya sana na kujiona kama vile ndio yeye msababishaji wa kifo cha kaka yake. "Ni bora hata ningekataa kufanya mapenzi na Shemeji, labda haya yasingetokea" Japhet alijisemea moyoni kwa huzuni halafu akaungana pamoja na wazazi wake kuomboleza msiba huo wa kaka yake huku wakisubiria asubuhi ipate kufika wafanye mipango ya mazishi.

Mwili wa Flora nao ulisafirishwa mpaka kijijini kwao kwa kuwa mkoa ulikuwa ni mmoja huohuo wa Dodoma isipokuwa vijiji tu ndio vilikuwa ni tofauti na kule kwa akina Japhet. Baada ya kufika hapo kijijini nyumbani kwa wazazi wa Flora ndugu na jamaa na wao pia walikuwa wanasubiria asubuhi ifike ndio mpango wa kumzika mpendwa wao Flora upate kufanyika yaani ilikuwa ni huzuni tupu.

Asubuhi ya siku nyingine mpya ikaweza kufika na baada ya taratibu zote kuweza kukamilika ikiwemo wazazi na ndugu wengine waliokuwa wapo huku kijijini nao kumuaga marehemu Lukasi kaka yake Japhet sasa moja kwa moja mwili wake ukapelekwa makaburini kuzikwa. 

Kwa hakika hiyo ilikuwa ni siku mbaya sana kwa kijana Japhet kuona kaka yake aliyekuwa anamtegemea kwa kila kitu na hata kumuahidi kumtafutia kazi na mambo mengine mengi ya kimaisha leo ndio anazikwa eti kwa sababu tu ya upuuzi wa siku moja alioufanya na Shemeji yake Flora mke wa kaka yake huyo wakati alipokuwa yupo safarini.

 "Daah siamini kama Utamu wa Shemeji leo umegeuka kuwa uchungu kwangu, pumzikeni kwa Amani huko muendako" Japhet alisema huku akiweka mashada ya mauwa kwenye kaburi la kaka yake Lukasi Mara baada ya kufukiwa. Wakati Lukasi huku akiwa anazikwa na mkewe Flora naye alikuwa anazikwa huko kijijini kwao alipokuwa anatokea Flora.

Baada ya hapo waombolezaji wote wakaweza kurudi nyumbani kuendelea na taratibu zingine za kumalizia msiba. Japhet mpaka muda huo bado alikuwa na wasiwasi vipi kuhusu Rozi kule mjini kituo cha Polisi anaposhikiliwa kwa ajili ya mahojiano. "Sijui Rozi atakuwa amewaambia ukweli wote wale maaskari kuhusu kifo cha kaka pamoja na Shemeji?" 

Japhet alijiuliza mwenyewe na jibu asilipate asilani. "Na hapa nyumbani napo wakitaka kufahamu ukweli juu ya vifo vile nitawaambia nini" Japhet bado alizidi kupagawa hakujua hata aseme nini kwa wakati huu ukiachana na huko Polisi ambapo pia anatakiwa aende akahojiwe.

INAENDELEA

Powered by Blogger.