KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Nne (04)

simulizi ya penzi la mfungwa
Usiku ulipo fika,mzee Maboso alimkumbusha Zabroni kuhusu mzizi ambao utamfanya Zabroni kupotea popote pindi atakapo nuia na kisha kugusa kitu chochote.


"Hapa kila kitu kitakuwa sawa kijana wangu", aliongea mzee Maboso huku akiutoa mzizi huo kwenye kitambaa alichotumia kuhifadhia. Akaketi kwenye kigoda, akamtazama Zabroni kwenye mwanga hafifu wa kibatali, akaendelea kumueleza uwezo wa mzizi huo na maneno anayotakiwa kuyaongea pindi atakapo hitaji kupotea kwenye mazingira husika. "Kwahiyo unataka kuniambia kwamba nikishaongea maneno hayo halafu nikagusa kitu chochote iwe nyasi au ukuta napotea?..", aliuliza Zabroni kwa umakini zaidi.


"Naam! Hii dawa sio ya mchezo", alijibu mzee Maboso halafu akamkabidhi. Zabroni aliupokea mzizi huo, akautafuna. Alionekana kukunja uso wake, kwa namna gani mzizi huo ulivyokuwa mchungu. Baada kukamilika suala hilo, sasa akahitaji kufanya jaribio usiku huo huo. Alichomo moto nyumba nyumba tano, katika nyumba hizo hakubahatika kupona mtu hata mmoja. Kesho yake asubuhi, kijiji kikakubwa na janga kubwa la ajari ya moto, wanakijiji walimnyooshea kidole mwenyekiti wakati huo mwenyekiti akimtilia shaka mzee Fungafunga..

Mwenyekiti wa kijiji alimuhisi muhusika wa tukio hilo huwenda akawa ni mzee Fungafunga kwa maana jana alimwambia kuwa yeye ndio aliyehusika kuchoma nyumba ya mzee Ndalo,sasa hatimaye tukio hilo hilo limejitokeza tena. Istoshe limesababisha maafa mkubwa sababu ndani ya hizo nyumba tano zilizochomwa moto hakufanikiwa kutoka mtu hata mmoja,kitu ambacho kiliwasikitisha walio wengi ni familia ile iliyokuwa na watoto Saba pamoja na wazazi wao wawili. Familia yote ikawa imekufa kwa pamoja,huzuni kila pande ya kijiji wakati huo huo mzee Fungafunga akijiuliza "Nitaificha wapi sura yangu mimi mbele ya mwenyekiti? Sijui kwanini nilimwambia jambo lile",alijiuliza mzee Fungafunga huku akionekana kujilaumu jambo lile kumuelezea mwenyekiti ilimradi tu apate ujiko. Katika umati wa watu uliokusanyika katika nyumba ile ya familia saba,mwenyekiti akamtazama mzee Fungafunga kisha akamuita faragha. Mzee Fungafunga akionekana kuwa na hofu alitii wito wa Mwnyekiti.


"Mzee mwenzangu, nini sasa umefanya?" Mwnyekiti akamuuliza Fungafunga huku akionekana uso wake kana kwamba anataka kudondosha machozi,wakati huo huo mzee Fungafunga akashusha pumzi na kisha akajibu "Walaa sio mimi ndugu mwenyekiti, unafikiri kwa utu wangu huu naweza kufanya maafa kama haya? Hapana siwezi mwenyekiti labda tufanye uchunguzi atajulikana tu muhusika" alijibu mzee Fungafunga macho akiwa ameyatoa mfano wa chura aliyebanwa na mlango. Baada ya maelezo hayo mwenyekiti akajikuta akishindwa cha kuongeza kusema zaidi aliyafuta machozi yake yatokanayo na uchungu wa kupoteza baadhi ya wanakijiji wake, maana hali kijiji hapo ilionekana kutisha sana.

Wakati hayo yanaendelea, upande wa pili mzee Maboso na Zabroni walikuwa wakielekea shambani. Walipo kuwa njiani mzee Maboso akamwambia Zabroni "Nadhani umeona hiyo dawa ilivyokuwa noma"


"Dah! wewe acha tu,kwanza nilipofika kwenye nyumba ya kwanza nilichoma kumbe kwa mbali kuna mtu alikuwa anakuja maeneo hayo,bila shaka yule alikuwa mlevi maana usiku wote ule sio wa kutembea tembea hovyo. Basi bwana baada kumuona nikasema hapa haonwi mtu haraka sana nilinuia yale maneno halafu nikagusa ukuta wa nyumba hiyo hiyo nikawa nimepotea " Zabroni akacheka kwanza kisha akaendelea kusema "Nikasema kweli hii dawa ni moto wa kuetea mbali,na kwakuwa ni moto wa kuotea mbali? Hakuna budi kukamilisha methali ile isemayo dawa ya moto ni moto"

"Naam upo sahihi Zabroni", aliunga mkono mzee Maboso na kisha wakagongena mikono wakacheka sana na zogo nyinginezo zikaendelea. Walifika shambani wakafanya shughuli zao mpaka mida ya saa nane mchana waliweza kurejea nyumbani kwao ambapo wakati walipofika tu nyumbani akaja mzee Adenel, mzee huyo alionekana anajambo moyoni mwake lakini pia mzee huyo hana uenyeji na kijiji hicho bila shaka alikuwa mgeni ingawa mzee Maboso alimfahamu fika na ndio maana alipomuona alionyesha kutabasamu.

"Karibu sana wanyumbani",alisema mzee Maboso huku akimlaki mgeni wake. "Nimeshakaribia,habari za siku nyingi ", alijibu mzee Adenel, mzee Maboso akaitikia "Salama sana ngoja nikachukue kigoda ili tukae tuongee zaidi ", baada kusema hayo mzee Maboso alizama ndani akachukuwa kigoda kisha akatoka nacho nje. "Enhe nipe habari hivi ni wewe kweli?..", alihoji mzee Maboso akionekana kutoyaamini macho yake lakini mzee Adenel akamjibu "Ndio ni mimi ujue miaka mingi sana nimekuacha hapa naona sasa tayari umekuwa mwenyeji wa Tanzania. 

Mmh sasa habari ni kwamba unatakiwa kurudi nyumbani. Familia inakuhitaji kwa vyovyote vile", aliongea mzee Adenel akimtaka Maboso arudi nyumbani kwao nchini Nigeria,mzee huyo alikuwa kiutafutaji kijijini hapo na hivyo mtafutaji ambaye alikuwa naye miaka ya nyuma kabla hajarudi nchini kwao leo hii kaja kumchukuwa. 

Hakika mzee Maboso alionekana kupoa huku sana mithiri ya maji ya mtungini, akawaza "Miaka mingi nipo nchi ya watu kiutafutaji sasa leo hii nirudi nyumbani sina kitu? 

Hakuna kilicho badirika Je, haibu yangu nitaificha wapi mimi?", aliwaza mzee Maboso kitendo kilicho pelekea ukimya kidogo kutawala lakini mwishowe kimya hicho kilitoweka baada mzee Adenel kumuuliza kwa lugha ya kikwao "Unawaza nini?"
"Hapana ila najiuliza nauli nitatoa wapi?.." alijibu mzee Maboso naye vile vile alijibu kwa lugha yao.
"Usijali kila kitu kipo cha muhimu wewe jiandae kesho turudi nyumbani"
"Sawa"
"Lakini mbona kuna mahala nimepita nimekuta watu wanaomboleza kulikoni kuna msiba?.." aliongeza Adenel. Mzee Maboso akamjibu "Ndio"
"Sasa kwanini hamjahudhulia",kabla mzee Maboso hajajibu,Zabroni alileta chakula maongezi hayo kuhusu misiba yakawa yamekomea hapo.

Usiku ulipoingia kesho yake ikiwa ndio safari ya mzee Maboso kurudi Nigeria, aliamwambia Zabroni kuhusu ujio na dhumuni la mzee Adenel. Zabroni aliumia sana kwani aliamini swahiba wake kuonana naye tena ni majaliwa hivyo alijiuliza amlipe nini? Ndipo akakumbuka kuwa alifukia fedha aridhini,fedha alizoiba zamani kwenye moja ya maduka kijijini hapo! Fedha hizo aliiba kwa kudhumuni ya kwenda kumtibia mama yake nje ya nchi, ndoto ambayo ilitoweka mithiri ya mshumaa uzimikapo unapokubwa na upepo. 

Haraka sana alikwenda kuzifukua kwa kuangalia ramani kilipokuwepo chumba chake, alifanikiwa kupaona. Aliachia tabasamu na kisha mara moja akaanza kuzifukua. Zoezi hilo lilikamlika, fedha zilikuwa kwenye mfuko wa gunia. Kwa mara nyingine tena akaachia tabasamu, akaona fedha hizo ni fadhila tosha kwa mzee Maboso aliyeamua kumuunga mkono juu ya hatua ya kulipa kisasi aliyochukuwa. Ni fedha nyingi mno.

Kesho palipokucha saa kumi na mbili safari ilianza,Zabroni akaambatana na wazee hao kuwasindikiza mpaka stendi ya magari yaendayo mjini,ikiwa kama hatua ya kwanza ya safari ya kuelekea Nageria Dakika tano nyingi gari ikawa imewadia maeneo hayo,mzee Maboso akamuaga Zabroni lakini kabla hajapanda gari, Zabroni alimpatia mfuko mdogo mweusi wenye fedha ambazo mzee Maboso hakuweza kutambua ni kiasi gani. Maboso akapanga gari na neno la mwisho alimwambia Zabroni 

"Mzee Fungafunga ndio muuwaji wa wazazi wako,nakutakia kazi njema kijana wangu ",kwisha kusema hivyo gari iliondoka pole pole mpaka kasi ilipoongezeka. Huku nyuma kijana Zabroni akionekana kupigwa na butwaa akajiuliza "Yani inamaana kwamba baba yangu mkwe mtarajiwa ndio kafanya kitendo hiki Mzee Maboso hajawahi kunidanganya, acha nitembeze moto sasa mpaka kijiji kiwe jangwa. Tina utanisamehe maana hili ni pigo lisilo saharika katika maisha yangu" kwisha kuwaza hayo Zabroni akidondosha machozi ya hasira.



ITAENDELEA

Powered by Blogger.