KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Tano (05)

simulizi ya penzi la mfungwa

Zabroni alirudi nyumbani baada kutoka kumsindikiza mzee Maboso,akiwa njiani aliwaza kipi afanye nini sasa baada kumtambua mbaya wake. Je, aendelea kuchoma nyumba ama adili na mbaya wake? Akili ya fasta ikamjia kwamba bora aendelea kuchoma nyumba ikiamini kuwa maumivu aliyonayo moyoni mwake huwenda yakatulia kama sio kupotea kabisa. Yote hayo kijana Zabroni alikuwa akiyawaza huku akirejea nyumbani mikono nyuma kichwa chini,alipo fika nyumbani alikuta karatasi ndogo kwenye meza iliyokuwepo sebuleni. Zabroni alionekana kustuka huku moyo wake ukihitaji kufahamu kilicho andikwa kwenye karatasi hiyo,hatimaye aliichukuwa akakuta maneno yaliyoandikwa "Kijana Zabroni, mjukuu wangu mwanangu pia. 

Nimekupa dawa hii ili uweze kulipa kisasi juu ya kile ulicho fanyiwa,hakuna ubishi mzee Fungafunga ndio muhusika mkuu wa vifo vya wazazi wako. Alifanya kitendo kile baada kuona baba yako anamzungusha kumlipa deni lake alilokuwa akimdai. Zabroni Zabroni lipa kisasi kijana unyama huo kamwe huwezi kuupuzia abdani,mwanaume haogopi. Yote kwa yote nikutakie maisha marefu kijana wangu,mimi narudi nyumbani ila najua ipo siku tutakuja aonana tena", yalieleza maandishi hayo yaliyokuwa kwenye karatasi, Zabroni aliyasoma kwa umakini na uchungu mkubwa, aliyafuta machozi, punde akaendelea kusoma "Kwisha kusema haya napenda kukwambia kuwa dawa hiyo unaweza kujigeuza kiumbe chochote chini ya jua,sharti moja tu ambalo inakubidi utekeleze, usithubutu kufanya mapenzi", ilieleza hiyo barua, 

Zabroni alishusha pumzi ndefu,mwili wake ukasisimka hasira zisizo na mfano zikatawala ndani ya moyo wake akatamani kumfuata mzee Fungafunga muda huo huo lakini akajitahidi kuzizuia hasira zake ambapo aliamua kulala mpaka jioni saa kumi na moja hata hivyo aliamka baada kusikia Tina akigonga hodi. Siku hiyo Tina alikuja na chakula kwa niaba ya mpenzi wake. Zabroni alionyesha kufurahia kitendo kile cha Tina ila moyo wake ulikuwa na kiza kinene,alipiga moyo konde akamkaribisha Tina ndani wakapiga story mbali mbali ilihali muda huo anakula chakula hicho alicholetewa na mpenzi wake.

"Kulikoni mpenzi,mbona babu simuoni?.", aliuliza Tina huku akionekana kumfuta futa vumbi uzushi kijana Zabroni kunako shati yake,Zabroni akameza tonge lililokuwa mdomoni mwake kisha akamjibu "Babu kasafari,karudi kwao"
"Kwao? Kivipi yani"
"Ndio, hakuwa mtanzania kwahiyo jana alikuja ndugu yake kumchukuwa kwa hiyo amerudi nchini kwao" alijibu Zabroni.
"Anha kwahiyo karudi Nigeria ? Jamani babu alikuwa mkarimu yule! "
"Ndio hivyo" alihitimisha Zabroni wakati huo sasa ameshamaliza kula chakula alicholetewa na mpenzi wake,baada kumaliza Tina alihitaji kutulia faragha na Zabroni siku hiyo na ndio maana alimjia saa ya jioni. 

Tina kwa sauti ya upole na yamahaba alimwambia Zabroni asimame ,Kweli Zabroni akasimama bila kupoteza muda Tina alimshika mkono moja kwa moja mpaka chumbani. Walipofika chumbani Tina akamsukuma Zabroni kwenye kitanda cha telemka nikaze,Zabroni alianguka chali, muda huo huo Tina nae alimpanda na kuanza kumpapasa kifuani huku pole pole akitaka kupitisha ndimi yake kwenye kinywa cha Zabro. 

Zabroni naye baada kufanyiwa hicho kitendo,mwili wake ulianza kupata hisia mawazo yake yote yakazamilia kuvunja sharti. Lakini kabla kitendo hicho hakijatokea akakumbuka maneno ya ile barua,haraka sana akang'atuka akamsukuma Tina kisha akatoka ndani. 

Tina alishangazwa na kitendo hicho alichokifanya Zabroni kafanye akajiuliza "Kwanini lakini", wakati anajiuliza swali hilo akazipiga hatua kumfuata Zabroni nje. Zabroni muda ulionekana akiwaza na kuwaza jambo akilini mwake. Punde tu Tina akamfikia, kwa sauti ya upole Tina akasema "Zabroni una nini mpenzi wangu? " , kabla Zabroni hajamjibu Tina alishusha pumzi ndefu kisha akajibu "Hakuna tatizo Tina, ila siku ya leo siko poa kabisa"

"Unatatizo gani?..", aliongeza kuhoji Tina huku akionekana kuwa na shauku ya kutaka kujua kinacho msibu Zabroni. Lakini bado Zabroni hakuwa tayari kumwambia Tina ukweli alionao moyoni mwake. Tina alikasirika sana, akamua kurudi nyumbani ingawaje moyo wake bado ulikuwa na mashaka juu ya kitendo kile alichokifanya Zabroni kwani haikuwa kawaida yake.

Baada Tina kuondoka, Zabroni alirudi ndani moja kwa moja akazama mpaka chumbani kwake. Alisimama wima huku akitazama ile karatasi iliyosoma muda mchache ulio pita, kwa mara nyingine tena akaishusha pumzi ndefu kisha akajiuliza "Hivi ni kweli naweza kujigeuza kuwa kiumbe chochote?.."


"Hebu ngoja nijaribuy, nijigeuze kuwa mzee nione kama kweli itawezekana", aliongea baada kujiuliza, kwisha kuongea maneno hayo akanunia na punde si punde akaonekana katika hali ya uzee. Alistaajabu sana, akanyoosha mikono yake kuitazama ngozi ya mwili wake, bado hakuyaamini macho yake, upesi akatoka ndani akaelekea nje kwenye mwanga. 

Napo bado alishuhudia kitendo kile kile, "Ahahahaha hahahahah", aliangua kicheko Zabroni ndani ya moyo wake akajisemea "Kweli huu ni moto wa Nigeria. Sasa kwa hali hii nipo salama kila idara. Hawa watu wamekwishaaaaaaa". Alifurahi sana Zabroni, asilimia za kujiamini zikaongezeka zaidi.

Lakini wakati yupo kwenye hali hiyo ya furaha, upande wa pili kijijini anaingia mzee mmoja wa makamo. Mzee huyo alionekana kubeba begi kukuu, pasipo na hofu alijikongoja huku akionekana ni mgeni kijijini hapo. Hakuwa peke yake mzee huyo, kando alikuwa sambamba na mwenyekiti wa kijiji. 

Taharuki baadhi ya wanakijiji inazuka, wale waliomfahamu mzee huyo walionyesha nyuso za furaha, na wale ambao hawakumfahamu waliishia kuzama kwenye taharuki.
"Huyu mzee Baluguza amefuata nini huku?..", moja ya vijana waliopata wasaa wa kumuona mgeni huyo aliuliza.


"Mmmh kiukweli haujui lakini nahisi amekuja kumsaka huyu kirusi wa matukio haya", alijibu kijana wa pili, mtu wa tatu akaongeza kusema "Ya ngoswe tumuachie ngoswe na kwa jinsi ninavyo mfahamu huyu mzee ukweli lazima atajulikana tu huyu mtu aliyeanziasha zahma la kuchoma nyumba hovyo hovyo", yote hayo yalikuwa ni mazungumzo kilingini. Upande wa pili napo zogo baina ya mwenyekiti na mgeni wake liliendelea. 

Mwenyekiti alikuwa akimpa habari namna kijiji kinavyo karibia kuwa jangwa na hata mfanyaji wa matukio hayo asijulikane. Mzee Baluguza alihuzunika sana hasa familia ile ya watu saba iliyokufa kwa pamoja, kwa kinywa chake akamthibitishia Mwenyekiti kuwa mtu huyo atajulikana, na atathubutu kumpoteza sehemu isiyojulikana. Mwenyekiti alifurahi sana kusikia maneno hayo, na punde mbele yao alionekana Zabroni. 

Mzee Baluguza alisita kidogo baada kumuona, alistuka wakati huo mwili wake ukimsisimka. Mwishowe alitikisa kichwa ishara ya kukubali jambo fulani, akaishusha pumzi ndefu kisha ndani ya moyo wake akajisemea "Naam! Kazi imekwisha"


Kwisha kujisemea maneno hayo aliachia tabasamu bashasha huku akimsindikiza kwa macho Zabroni kitendo ambacho kilipelekea mwenyekiti kuingiwa na hofu akajiuliza maswali mengi ambayo aliyakosa majibu yake,ilihali upande wa pili Zabroni o naye aligeuka kumtazama mzee Baluguza ambaye kwa macho yake ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona. Alistuka baada macho yake kugongana na macho ya mzee Baluguza ila hakujali zaidi aliendelea na safari yake kama alivyofanya mzee Baluguza.

"Huyu ni nani?..", ndani ya kichwa chake Zabroni alijiuliza. Upande wa pili mwenyekiti alimkalibisha nyumbani mzee Baluguza kwa furaha huku akimpa tumaini kwamba ajisikie yupo nyumbanin,Baluguza akakaribia kwa bashasha ya hali ya juu. Baada ya maongezi mawili matatu,mwenyekiti akazipiga hatua kuelekea nyumbani kwa mzee Ngurumo ambaye ndio balozi wa nyumba kumi.

 Alimkuta. Akamwambia nia na dhumuni ya ujio huo,mzee Ngurumo alimuelewa vema tena akampongeza kwa hatua aliyochukuwa ya kumleta mzee Baluguza mganga mashuhuli aliyefamika kwa huduma yake maridadi isiyokuwa na utapeli.
"Ama kweli wananchi waliokuchagua hakika hawakukosea,kiukwe hili ni tatizo tena sugu. Tusipo chukuwa hatua mapema tutajikuta tukipoteza mpaka familia zetu", aliongea mzee Ngurumo huku akifunga mlango wa nyumba yake. Mwenyekiti alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Ni kweli ,si unajua tusipo ziba ufa tutajenga ukuta? .."
"Kabisa ndugu mwenyekiti"
"Basi hima twende tukazungumze naye tujue hili tatizo atalikomesha vipi" aliongeza kusema mwenyekiti wakati huo tayari wameshatoka nyumbani hapo kwa mzee Ngurumo na sasa walionekana kuanza safari kurudi nyumbani kwa mwenyekiti. 

Ila kabla hawajafika,Ngurumo akatoa wazo akasema "Unaonaje tukamuone na mzee Fungafunga? Maana hili suala kama linamuhusu na yeye?.."
"Sawa hakuna shida twende ingawa sidhani kama atakuwa karudi kutoka shamba,nasikia ngedere wanasumbua sana shambani. Wami unamsumbua sana"alijibu mwenyekiti.

"Loh. Nikweli lakini tukajaribu"
"Sawa twende"
Mwenyekiti na mzee Ngurumo walielekea kwa mzee Fungafunga, bahati nzuri walimkuta akiwa tayari ametoka shamba alionekana kuchoka sana.
"Hodi! Hodi! Bwana Fungafunga " Ngurumo alisema.

"Anhaa KARIBU bwana,karibu sana. Mama Tina leta vigoda haraka", alijibu mzee Fungafunga kwa tabasamu bashasha ,na punde si punde Mama Tina alileta vigoda. Mzee Ngurumo na mwenyekiti wakapata kuketi kisha soga zikaendelea.

Powered by Blogger.