KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Kumi na mbili (12)


simulizi ya penzi la mfungwa

Zabroni alitikisa mkono wake ambao ulikuwa unabembea,wakati huo chini ya ule mti aliotundikwa alikatiza kijana mmoja hivi wa makamo. Kijana huyo alikuwa katika harakati za kuwinda alfajiri hiyo mapema, hivyo akiwa chini ya mti aliotundikwa Zabroni ghafla tonya la damu lilimdondokea kichwani. Lakini alipuuzia akidhania kuwa huwenda tonya la umande ndilo lililomdondokea,ila mwishowe alistuka baada mchirizi wa damu kumdondokea kama maji. 

Hapo ndipo kijana huyo muwendaji alipoinua uso wake kutazama juu akamuona Zabroni akining'ia,alitaharuki. Haraka sana alitimua mbio huku akianguka mielekea mara mbili mbili wakati huo akipiga kelele akimuogopa Zabroni. 

Ila alipo fika mbele kidogo alisimama kisha akageuka kutazama nyuma alipotokea, mapigo ya moyo yalimuenda mbio akijiangalia yupo mikono mitupu. Sime mkuki pamoja na upanga vyote akiwa amevitupa pasipo yeye mwenywe kujielewa, yote hiyo ikiwa ni hofu ya kumuogopa Zabroni.

Kwa kutumia mkono wake wa kushoto,kijana huyo muwindaji alijigusa kichwani kisha akajitazama vidole vyake akaona damu. Akajisemea moyoni "Hii si damu? Mmh huyu jamaa atakuwa amekumbwa na nini sasa,na mbona asubuhi yote hii kanasa juu ya mti wakati sio kawaida yake?..

Loh! Sio bure hapa kutakuwa kuna kitu kimetokea, Zabroni huyu ni naye mjua mimi hawezi kufa kizembe kizembe wala sio wa kujeruhiwa tu hovyo hovyo ", alijisemea muwendaji huyo huku akionekana kutaka kurudi kuchukuwa zana zake za mawindo. Lakini dhumuni hilo lilitoweka baada kukumbuka kasheshe kadhaa alizofanya Zabroni, aliamuwa kitimua mbio kuelekea kijijini kwa niaba ya kueleza kile alicho kiona. 

Na wakati huyo muwendaji alipokuwa akitimua mbio kwenda kutoa taarifa, upande wa pili kijijini. Alionekana Bruno akikuwa na Mwenyekiti wa kijiji pia na wazee wengineo wa kijijini hicho,walikuwa wamekaa wakiomboleza msiba mzito wa mzee Fungafunga na mkewe waliofia ndani pia na vifo vya wahanga wengine. 

Kiukweli yalikuwa ni majonzi ya aina yake,kila mmoja alisikitika kwa staili yake ilihari mioyoni mwao wakitamani Zabroni auwawe kwa njia yoyote kwani unyama aliokuwa akiufanya ulipitiliza kipimo hata Mungu hapendi. 

"Bruno,Huu ni wakati wa wewe kurudi nyumbani kwenu. Umempoteza kaka yako,chunga na wewe usije kupotea. Wazazi wenu mkawacha na viulizo,chukua mizigo yako uanze safari,haya mambo tuachie sisi",ilikuwa ni sauti ya Mwenyekiti akimwambia Bruno kwa masikitiko kabisa. Bruno naye aliposikia maneno hayo,alishusha pumzi kwanza kwa nguvu kisha akajibu. 

"Najua pia natambua ni namna gani mnavyopata shida,lakini mzee wangu labda nikwambie kitu. Siku zote Mungu akitaka kukupa mafanikio haji yeye kama yeye ila atapitia kwa binadamu mwenzako, lakini pia ukae ukijua hapa duniani hakuna mwamba. 

Bali mwamba ni Mungu pekee aliyejuu na sio sisi binadamu tulio umbwa kwa udongo na mwisho wa siku tunarudi kwenye udongo", alijibu Bruno,Mwenyekiti na wazee wengineo waliokuwepo mahala pale kila mmoja alitaharuki kusikia maneno ya kijana mdogo. 

Mzee mmoja alimgeukia kisha akamuuliza "Unamaana gani?.." Lakini kabla Bruno hajamjibu huyo mzee,mara ghafla yule kijana muwindaji alifika mahali hapo kwa kasi huku akihema juu juu. 

"We nawe vipi unawazimu?.." alihoji mzee wa pili huku akiwa amemkodolea macho. Mwenyekiti akaongezea kusema "Huyu kijana huwa namuangalia sana,kiukweli yani akili zake hazina tofauti na akili ya ndezi ama kobe. 

Chizi sio chizi,mwehu sio mwehu. Sijui ana akili gani huyu konono", alisema Mwenyekiti kwa hasira kali kwani huyo kijana aliwastua sana kwa kasi aliyokuja nayo,baadhi ya walitaka kukimbia wakidhania kuwa tayari mtukutu katia maguu. 

"Haya zungumza kilicho kufanya utoke huko mbio mbio mpaka hapa", muwendaji huyo ambae ni shuhuda,alituliza nafsi yake kwanza kabla hajaanza kuongea kile alicho kiona kule mstuni. Watu wote waliokuwepo pale kwenye maombolezo walimtazama yeye,naye alipo jihakikishia kuwa tayari yupo sawa alisema "Zabroni....",watu wote kasoro Bruno walistuka kulisikia hilo jina,Ghafla mmoja mmoja aliinuka na kisha kuondoka zake wakiogopa kwamba huwenda Zabroni yupo nyuma,ndio aliyekuwa anamkimbiza kijana huyo muwendaji aliyekuja mbio mbio. 

Upande wa Bruno yeye hakuwa na hofu kwa sababu aliamini kuwa tayari huyo kijana atakuwa ameona maiti ya Zabroni na hivyo atakuwa amekuja kutoa taarifa rasmi hapo kijijini kuhusu kifo cha huyo mtukutu,kitu ambacho ndicho alikuwa akikitamani na ndio maana alimtundika eneo lile la wazi ili mpita njia ama muwindaji yoyote atakae katiza eneo lile aweze kuishuhudia. 

Hivyo hofu ilitanda hapo,mama mmoja alisikika akiitikia kwa kusema "Heeh Zabroni? Aawapi jamani nilikuwepo nitarudi baadae", aliongea huku akiambaa na njia kutafuta mahali pa kujibanza ili kama Zabroni atafika pale yeye asiwepo. Lakini kabla hajafika mbali alisikia sauti zikisema "Mmmh jamani kweli ? "

"Aah sidhani,mzee Baluguza mtalamu. Mganga kati ya waganga kamshindwa eti leo hii ndio afe. Tena kirahisi rahisi tu? Teh teh teh..hiyo ndoto ya mchana "

"Sio bure huyu jamaa anakuwa kajambiwa na ndezi wake huko polini,anakuja kutueleza ujinga wake"

"Teh teh teh teh..Ni rahisi sana panya kubeba mimba ya paka kuliko mtu wa kawaida kumuua Zabroni, acheni kudanganyana bwana", zote hizo zilikuwa ni sauti moja ya maongezi yaliyosikika kwa fujo maeneo hayo,yote kutoka na kijana yule muwindaji kusimulia kile alicho kiona huku akisisitiza kuwa Zabroni kafa. Fujo ilisikika huku baadhi ya watu wakidiriki kumtukana,lakini baada Bruno kuona utata unazidi ndipo alipotaka kukata mzizi wa futina ili kuwaweka wanakijiji katika hali ya amani. 

Alifikinya kiganja chake kwa kutumia mkono wa kulia alifikanya kiganja cha mkono wa kushoto,kisha akafumbua kiganja hicho ambapo ulionekana ule mpambano aliopigana naye mpaka tamati. 

Hakika wanakijiji walishusha pumzi kila mmoja akimtazama Bruno kwa jicho la tatu na kumuona ni shujaa wa kukumbukwa katika hicho kijiji,yule mzee aliyemuuliza swali hapo awali alipata jibu la swali lake . Ambapo Bruno alipo mtazama,naye akamuonyeshea dole gumba kuonyesha kuwa tayari jibu analo. Furaha ilitawala sasa,hata wale walio kimbia mwanzo walirudi kuungana na wenzao kufurahia kifo cha Zabroni.

Baada ya hapo msafara wa wanakijiji ukiambatana na shujaa wao Bruno huku kiongozi akiwa Mwenyekiti,ulijikusanya ukaenda kuufuata mwili wa Zabroni ili wauchome moto. Lakini walipo fika eneo hilo hawakuuta mwili huo,walitaharuki wakamtazama Bruno ilihali Bruno naye akionekana kushindwa kujua kilicho tokea. Hofu kwa mara nyingine tena ilitanda mioyoni mwao,kila mmoja akionekana kuwa na sintofahamu kuhusu mtukutu. 

Na wakati wote wakiwa katika hali hiyo mara ghafla ilisikika sauti ikisema huku ikijirudia mara mbili mbili. Sauti hiyo ilisema "Mimi ndio Zabroni. Nimerudi ",sauti hiyo ikamaliza kwa kicheko kikali. Punde baada kusema hivyo ghafla....!



ITAENDELEA

Powered by Blogger.