KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Kumi na Moja (11)

simulizi ya penzi la mfungwa
Kijijini alionekana Madebe akichechea huku mguu ukiwa umevimba,nyoka aliyemgonga alikuwa na sumu kali mno. Na kipindi Madebe akiwa na hali hiyo,ndani Mwenyekiti alimuuliza Bruno "Wapi alipo elekea kaka yako?.." Bruno hakujibu chochote,zaidi aliishia kujisonya kwani hakufahamu ndugu yake alipo elekea..aliondoka bila hata kumuaga. 

Ila wakati Mwenyekiti na Bruno wakiwa na sintofahamu,ghafla nje walimuona Madebe akija huku akkchechema mara ananguka na kuinuka. Bruno alistuka hima akamkimbilia,alipo mfikia alimnyanyua huku akimuuliza kilicho msibu. 

Lakini Madebe hakuweza kujibu chochote,hali yake tayari ilikuwa mbaya sana,sumu imeshapanda kwenye moyo. Bruno alizidi kuchanganyikiwa alirudia kumuuliza kaka yake "Kaka nini kimekusibu?..", lakini Madebe hakujibu,zaidi alijifungua hirizi yake akamkabidhi mdogo wake kisha akasema kwa taabu sana "Zabroni.. Za..broni. mdogo wangu lipa kisasi li..pa ki sa..sasiiii", kwisha kusema hivyo Madebe akaaga dunia. Kiukweli Bruno alilia sana kwa uchungu wa kumpoteza kaka yake. 


Aliamini aliyefanya kitendo hicho ni Zabroni. Wakati huo upande wa pili,Zabroni alikuwa kwenye Makaburi ya wazazi wake huku akijitazama kidonda chake alicho jeruhiwa na sime. Zabroni aliwaza na kuwazua akaona kabisa siku zake za kuishi zina hesabika hivyo hana budi kumaliza mchezo kwa kumuadabisha mlengwa mkuu ambaye ni mzee Fungafunga ili kisasi chake kiweze kutimia.

 Wakati anawaza hayo Zabroni, kwingineko Tina alipoambiwa kuwa anatikiwa kwenda Dar es salam kwa shangazi yake,aliona hawezi kwenda bila kukwichi na mpenzi wake wakuitwa Zabroni ilihari Zabroni naye dawa alizo nazo hatakiwi kufanya mapenzi. Na endapo atafanya basi zitapotea mwili mwake.


Siku tatu sasa zilikatika tangu Madebe afariki dunia,siku iliyofuata ambayo ni siku ya nne ndio siku ambayo Tina alipanga akutane na Zabroni ili wafanye mapenzi. Hivyo siku hiyo asubuhi Tina alidamka akaelekea mahali anapoishi Zabroni, alikuta majivu tu huku nyumba ikiwa imeteketezwa na moto. 

Tina alistuka sana baada kukuta hali ile,alitazama kulia na kushoto wakati huo akijiuliza ni wapi anapoishi Zabroni? Na kabla hajapata jibu mara ghafla alisikia sauti ikimuita,alistuka kisha akatazama kule ilipo tokea sauti akamuona kijana Zabroni akiwa chini ya mti mdogo huku pembeni yakionekana makaburi. Tina alizidi kushangaa kiasi kwamba alionyesha uso wa hofu ila Zabroni akawa amemuondoa hofu yake kwa kumwambia "Njoo mpenzi wangu usiniogope,haya ndiyo maisha yangu kwa sasa"

"Kwanini lakini umeamua kuishi huku?ujue tabia yako mimi sijaipenda" alisema Tina huku akizipiga hatua kumsogelea mpenzi wake. Alipo mfikia alikaa kando kando yake halafu akaongeza kusema "Hivi Zabro unajisikiaje kukaa kwenye mazingira haya? Sehemu nyingine zooote hujaziona mpaka uje kukaa eneo hili?.." Zabroni akajibu 

"Tina,kama nilivyokwisha kusema hapo awali kwamba haya ndio maisha yangu. Nimeamua kuja kukaa huku na wazee wangu ili nipate amani ya moyo wangu kwahiyo naomba usiwaze wala kuumiza kichwa kwa suala hili" alisema Zabroni tena kwa msisitizo.
"Zabro,.."
"Naam "
"Unanipenda kweli?.."
"Ndio tena nakupenda"
"Sawa asante,ila leo kuna jambo naomba nikuulize"
"Jambo gani?.."

"Naomba uniambie kwanini unauwa hovyo, unawarudisha wanakijiji nyuma kwa kuchoma nyumba na malighafi zao kwanini lakini.. tazama mpaka baba kaniambia niachane na wewe kutokana na tabia zako eti hawezi kuwa na mkwe mwenye roho mbaya. Kwahiyo Zabro mpenzi hatakama hutaweza kuniambia sababu ila basi achana na unyama huu tafadhali.." yote hayo alikuwa akiyasema Tina akijaribu kumshawishi Zabroni aachane na matendo anayo yafanya,lakini mara baada Zabroni kusikia maneno hayo ya Tina. 

Ghafla alipandwa na hasira,alimtazama Tina mara mbili mbili kisha akayatazama makaburi ya wazazi wake. Akasema tena huku akiwa na hasira kiasi kwamba mdomo wake ulionekana kutetemeka "Abadani Tina huwezi kunibadilisha tabia mimi,lengo nililo liweka moyoni mwangu huwezi kulipangua. 

Tena kawaambie washauri wako waniache ,pia vile vile waambie dawa ya moto ni moto" kwisha kusema hayo Zabroni alisimama kisha akaondoka zake,Tina naye alisimama akaanza kumfuata huku akiomba msamaha pia akiomba japo dakika moja ili aseme nae jambo. 

Zabroni alizidi kutembea huku akikazana lakini aliposikia msamaha wa Tina,hatimaye alisimama kisha akamgeuki halafu akahoji kwa hasira "Unasemaje?.." 

Tina alijishusha akawa mnyonge kisha akasema huku akilia "Zabroni, samahani kama nimekukera. Pia nashukuru kwa kunipa nafasi ya kunisikiliza. Mpenzi mimi naenda Dar es salam siku yoyote. Hivyo naumia sana kukuacha mwenyewe mpenzi wangu,lakini pia nilikuwa nina ombi moja" hapo Tina alisita kidogo ambapo ndipo Zabroni naye alipo pata nafasi ya kumuuliza huku akimtazama usoni "Kitu gani?.."


"Unajua siku..siku siku nyingi mimi na wewe hatujafanya mapenzi,kwahiyo naomba tukumbushie basi hata kwa nusu saa. Ikiwa kama njia pia ya kukuaga, hakika nitafurahi sana nikiondoka huku nikiwa nimefanya mapenzi na wewe kwani nitajiona mwepesi sana" Tina aliongea huku akichezea chezea vidole vyake, uso wake nao ukiona haya. 

Zabroni kijana mtutuku anayelipa kisasi huku tegemezi lake kuu ikiwa ni dawa,dawa ambayo sharti yake kuu hutakiwi kufanya mapenzi. Aliwaza sana,ukweli anampenda sana Tina istoshe anauchupa usio wa kawaida ila tatizo ni hapo tu. Je, atafanya mapenzi? Ilihali tayari anaadui nyuma anamnyemelea. Lakini pia kabla Zabroni hajatoa jibu juu ya ombi la mpenzi wake,alikumbuka kuwa mlengwa mkuu bado hajamalizana naye ambaye ni mzee Fungafunga baba yake Tina. 

Mtihani kwa Zabroni ila mwishowe alimpa jibu moja tu Tina "Nenda tutakatana jioni kwa sasa sina hamu yoyote,siunajua mapenzi hisia?.."Tina alitabasamu baada kusikia maneno ya Zabroni kisha akamwambia "Sawa lakini umenisamehe?.." Zabloni akajibu "Ndio "

"Mmh basi cheka kama kweli umenisamehe", Tina alitania Zabroni akacheka kama Tina alivyotaka huku ikiwa moyoni analake jambo,muda huo huo waliagana Tina alienda nyumbani kwao huku akiamini kuwa jioni atakuwa na mchezo dhidi ya Zabroni. 

Hakika furaha isiyo kifani ilimjaa moyoni ilihari upande wa pili Zabroni alijisemea kwamba hatoweza kufanya mapenzi mpaka pale atakapo kamilisha zaezi lake la kulipa kisasi. Tina alipo fika nyumbani,baba yake alianza kumfokea. Alimuuliza wapi alipokwenda,lakini binti huyo alikosa majibu ya kumpa baba yake ambaye ni mzee Fungafunga. 

Hivyo kitendo hicho kilimfanya mzee huyo kuhisi kuwa huwenda mwanaye katoka kwa Zabroni jambo ambalo halipendi katika maisha yake. Kwa hasira alimuamuru mkewe amuhimze binti yake wajiandae ili waanze safari ya kwenda mjini ili kesho yake iwe safari ya moja kwa moja Dar es salam. 

Upesi maandalizi yalifanyika,maandalizi ambayo waliyafanya huku Tina akilia kwani aliona anondoka bila kurudia kuhonja penzi la mtukutuku Zabroni. Alijiuliza ni lini tena itatokea hiyo nafasi? Kwa maana hakuwa na imani kama Zabroni ataishi miaka mingi kutokana na mambo anayo yafanya. 

Safari ilianza kati ya Tina na mama yake huku mzee Fungafunga akimsisitiza mkewe awahi mapema kwani hali sio shwari kwenye kijiji. Wakati mama Tina na mwanaye wakiwa njiani,Zabroni aliwaona. Alijua dhahiri Tina atakuwa anasafiri kama alivyomwambia hapo awali, Zabroni alifurahi sana kwani alijua tayaru kapata nafasi ya kukamilisha malengo yake. "Bado muhusika" alijisemea Zabroni kisha akatoweka eneo lile alilokuwa amekaa muda wote.


Usiku ulipoingia, aliamka tayari kwa niaba ya kwenda kukamilisha jambo lake. Siku hiyo mzee Fungafunga na mkewe walilala ndani wakiamini kwamba huwenda siku hiyo mtukutuku Zabroni asitembeze moto. Mke na mume walilala tena kwa furaha huku mzee Fungafunga akijisemea moyoni "Hapa moyo wangu umetulia sasa, kumtoa mwanangu kijijini hapa ni jambo la heri. 

Sasa ngoja nione huyu mwana haramu atachukuwa hatua gani,siwezi kuwa na mkwe mwenye roho mbaya kama huyu",kwisha kujisemea hayo Fungafunga alijivutia shuka tayaru kwa kuanza kuutafuta usingizi. 

Na punde si punde usingizi ulimpitia yeye pamoja na mkewe,walilala fo fo fo ilihari muda huo wazee hao wakiwa kwenye dimbwi la ndoto,Zabroni naye alitua nje ya nyumba. Alifyatu njiti akawasha sigara yake aina ya ngaja kisha moto uliosalia kwenye njiti akatupia juu kwenye nyumba. 

Sekunde dakika moto ulisikika huku mzee Fungafunga na mke wakiwa ndani,walistuka kutoka usingizini huku tayari moto ukiwa mkali kiasi kwamba walishindwa kujiokoa. "Ahahahaha hahahahah", Zabloni alicheka sana baada kufanya kitendo kile,katika akili yake aliamini kuwa tayari shughuli imekamilika. Lakini wakati akiwa katika imani hiyo mara ghafla aliguswa bega!

Baada kuguswa bega alistuka upesi akamgeukia mtu huyo aliyemgusa usiku huo wa manane. Ni Bruno. Mdogo wake marehemu Madebe,sura ya huyo kijana ilikuwa mpya kwa kwa Zabroni japo alimtazama kwa mwanga wa moto ulio tokana nyumba inayoteketea hivyo hakuweza kumtambua,zaidi alijiuliza "Huyu ni nani? Na anawezaje kunigusa bega?..", kabla hajapata jibu la hilo swali,Bruno alisema" Hujui sikujui ila kwa kumbukumbu naweza sema utanikumbuka endapo kama nitakukumbusha"


"We ni nani?..", alihoji Zabroni kwa kujiamini kabisa. Bruno alicheka sana kisha akafumbua kiganja chake,ulitokea mwanga mfano wa video. Katika mwanga huo kiganjani hapo lilionekana tukio lile la Zabroni na Madebe walipokuwa wanapigana,na mwisho wa tukio lile ilionekana ile sehemu ambayo Madebe alikuwa akimkabudhi hirizi mdogo wake huku akimtaka alipe kisasi.

 "Ndio mimi hapa natakiwa nifanye kile kitu kaka alicho nituma,hakika damu yake inanidai", alisema Bruno baada kumaliza kumuonyesha Zabroni ile video fupi kwenye kiganja chake. 

Lakini kijana Zabroni licha ya kuambiwa hayo maneno,kamwe hakuonyesha kustuka. Alicheka kisha akajibu "Nirahisi sana kunitamkia hayo maneno lakini ni vigumu kuyafanyia kazi kwa vitendo. Dogo, mimi leo ndio rasmi nimekamilisha kazi niliyofanya miezi kadhaa iliyopita. 

Hivyo sistahiri kuendelea kutenda dhambi zaidi,niliyo yafanya yanatosha", Kwisha kusema hayo Zabroni aliondoka zake. Bruno akamfuata,na ndipo Zabroni alipo amua kupotea kimazingara. Akaibukia kando kando ya mto,ilihali muda huo huo Buruno naye akatokea. Alistuka Zabroni baada kumuona kijana huyo anazidi kumganda wakati yeye hayupo tayari tena kufanya mauaji. "Bwana mdogo unataka nini tena kutoka kwangu?.." 

Zabroni alimuuliza Bruno tena kwa hasira. Bruno akajibu "Nataka kichwa chako Zabroni, sifa zako mbaya zimezagaa kila pande kwa sababu ya mauwaji yako,inakuwaje unauwa watu bila hatia? Hivyo basi kama utaweza niuwe na mimi basi lakini tofauti na hivyo utakufaa wewe ", alijibu Bruno huku akijiandaa kumrushia kombola Zabroni, ila kabla hajarusha. 

Zabroni akamwambia "Sawa, siunataka kuniuwa? Tazama juu kuna nini"
"Hapana huo ni ujanja wako Zabroni, sitegeki kishamba mimi", Bruno alijibu kisha akamtupia Zabroni moto wa kichawi. Moto huo ambao ulikuwa na nguvu ya ajabu ndani yake ulimpata Zablrni ukamtupa katikati ya mto ambapo muda huo huo Bruno alipaa juu huku akiwa amekunja ngumi nzito,ambayo alishuka nayo mpaka kwenye tumbo la Zabroni. 

Kitendo ambacho kilimzamisha chini zaidi kijana huyo mtukutu. Mamba samaki pia na wadudu wengineo waishio majini kwenye mto huo walitulia kupisha mpambano huo uliojumuisha nguvu za giza, Bruno alifanikiwa kumuadabisha Zabroni kwani kila Zabroni alipotaka kujitetea alijikuta akizidiwa ujanja na Bruno kwa kupigwa ngumi za haraka haraka zilizo changanywa na nguvu ya giza. 

Dakika kumi tu Zabroni hoi alisahau hata yale maneno ya kunuia ili abadilike kuwa kiumbe chochote kwa maana ngumi nzito iliyotua kichwani kwake iliweza kuyumbisha ubongo,hali iliyopelekea Zabroni huo muda kupoteza fahamu. Alipigwa sana kila mahala,Bruno alionyesha kujawa na hasira moyoni mwake. Hasira hiyo ndiyo iliyompelekea kumpiga Zabroni bila huruma kwani kila alipomkumbuka kaka yake ndivyo nguvu za kuchezea na mashavu ya Zabroni zilivyozidi kuongezeka. 

Mwishowe Zabroni alionekana kulegea kabisa mithiri ya kambale,hapo Bruno akajua tayari kazi imekwisha lakini ataamini vipi kama kweli kafa? Ndipo alipoamua kumvuta nchi kavu ili amuhakikishe. "Naam! Kazi imekwisha,hakuna mwamba chini ya jua zaidi ya muumba aliyekuumba. 

Zabroni Zabroni sasa ni wakati wako wa kwenda kulipwa yale uliyo yafanya hapa duniani", alisema Bruno baada kumkagua Zabroni kila sehemu ya mwili wake na kukuta tayari mtukutu kaaga dunia. Mara baada kusema hayo alimalizia kusema tena " Mimi ni Bruno shujaa... kwani siku zote shujaa hafi vitani bali shujaa ni yule anaye pambana na kurudi nyumbani na ushindi", 

Hapo alikata hirizi iliyokuwa kwenye mkono wa Zabroni kisha akawaza aondoke zake amuache Zabroni pale nchi kavu aidhaa amtupie mtoni apelekwe na maji sehemu isiyo julikana ikiwezekana awe chakula cha mamba? Kwani kwa hali ile kamwe mamba wasingemuacha salama,hirizi ambayo ingemlinda tayari ilikuwa mikononi mwake. Hivyo Zabroni atakuwa chakula cha mamba na samaki. 

Lakini kabla Bruno hajafanya huo uamuzi akajiuliza kwa mara nyingine tena "Tayari huyu mtu alikuwa ni tishio hapa kijijini je, hata nikipeleka habari ya kifo chake kwa wanakijiji wataniamini kweli?", alijiuliza Bruno mwishowe akaona ambebe begani moja kwa moja akaenda kumtunduki juu ya mti mkubwa kando ya barabara nyembamba ipitikayo kwa wingi na watu waendao na kurudi gulioni. Hapo ndipo Zabroni alipo tundikwa juu juu kwenye huo mti ule ambao kipindi cha nyuma aliwatundika vijusi alivyo vitoa tumboni kwa mama mjamzito. 

Kwisha kufanya hayo Bruno aliondoka zake na hirizi ya Zabroni. Akiwa amelowa jasho na damu aliitia hirizi ile kwenye mfuko wa koti alilokuwa amelivaa,kabla hajapotea kimazingara alizipiga hatua kadhaa kutoka pale alipo Zabroni hatua zipatazo kumi na tano kisha akasimama, akageuka kuutazama mti ule aliomtundika Zabroni akatikisa kichwa na akasema "Kufa tu hukuna namna mwanaharamu mkubwa wewe", kwisha kusema maneno hayo akachukuwa kitambaa akajifuta damu kwenye mikono yake halafu akapotea. 

Alipo fika kijijini alikuta nyumba tatu zimeteketea kwa moto usiku huo huo. Ndipo hapo Buruno alipokumbuka maneno ya Zabloni alipo mwambia
"Sawa, siunataka kuniuwa? Tazama juu kuna nini" Buruno alipokumbuka hayo maneno akajiongeza kwa kusema "Alaah! kumbe huyu mshenzi alimanisha nitazame juu kuangalia mwanga wa nyumba zinazo ungua? Ooh Mungu wangu" Bruno aliumia moyoni kisha akajipa moyo akisema "Sawa natumaini pindi wahanga hawa watakapo kuona ukiwa maiti basi mioyo yao itajaa tabasamu bashasha",alisema Bruno huku akiingiza mkono mfukoni aitoe hirizi ile aliyoichukua kwa Zabroni ili aitupie kwenye moto,lakini ajabu hakuikuta.

 Alistuka sana huku asijuwe kwamba muda ule alipotoa kitambaa kujifuta damu kiganjani aliidondosha chini. Pumzi ndefu alishusha na pindi alipotaka kurudu kuichukuwa, Mwemyekiti aliifka eneo la tukio kisha akamwambia "Hii ndio taabu ya hapa kijijini kijana wangu,hakika sitoamini siku nikimuona huyu mwanaharamu kauwawa". 

Hapo sasa Bruno alishindwa kumtoka Mwenyekiti ili aifuate hirizi ile kwani angeonekana hajaguswa na kitendo hicho cha nyumba kuungua. Muda huo sasa alfajiri tayari ilikuwa imeingia,umande na baridi ulimfanya Zabroni kutikisa kiuongo kimoja cha mwili wake,kumbe mtukutu alikuwa bado hajafa! U hai.

Powered by Blogger.