KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Kumi na Tatu (13)

simulizi ya penzi la mfungwa
Ghafla jeshi la polisi lilifika eneo la tukio,polisi hao walikuja na gari lao huku mbavuni mwao wakiwa na bunduki. Polisi mmoja aliyeonekana ndio mkuu wa msafara alitelemka kwenye gari kisha akazipiga hatua kuufuata ule umati,akiwa amekunja uso mithiri ya mtu aliyekula shubili. Polisi huyo alisema "Kuna nini mahali hapa?..", lakini wanakijiji hawakujibu,kila mmoja alionekana kukaa kimya ambapo ndipo yule mkuu wa msafara alipo muita kijana mmoja wa makamo falagha kisha kusema naye. "Kijana habari yako"

"Ni nzuri tu Afande sijui ya kwako",alijibu huyo kijana huku akionekana kujiamini kabisa,kwani hakuonyesha hofu yoyote kusimama na kamanda. Polisi alitazama kwanza upande ule waliosimama watu kabla hajaongeza nanl la pili,baadaye kidogo alirudisha uso wake kwa kijana huyo aliyekuwa naye falagha halafu akaendelea kuasema. "Naomba uniambie kuna kitu gani kimetokea hapa"

"Afande hapa bwana,tumekusanyika kuja kutazama mwili wa mtu aliyefariki usiku wa kuamkia leo. Sisi wanakijiji taarifa hiyo tumeipata asubuhi ya leo kutoka kwa mmoja ya vijana wa hapa kijijini,alitueleza kwamba kuna mtu kauliwa hapa Kwahiyo ndio maana mimi pamoja na wanakijiji wenzangu tumejumuika kuja kushuhudia. Lakini cha kustaajabisha ndugu Afande,maiti hatujaiona", alijibu kijana huyo.

"Unaweza kunitajia jina la huyo mtu aliyefariki?..", alihoji kamanda.

"Ndio, anaitwa Zabroni "

"Zabroni? ..", Afande alistuka kusikia jina hilo ni kama halikuwa jina jipya kuwahi kuisikia masikioni mwake,upesi akamuita kamanda mwenzake.

"Kamanda Pilo hebu njoo mara moja hapa",Afande huyo ambaye alifahamika kwa jina moja tu ambalo ni Pilo, alitii wito haraka sana. Alipomkalibia kiongozi wake alitoa heshima kisha akasema"Naam Afande" aliitikia.

"Pilo,chukua maelezo ya huyu kijana kisha report yake utanikabidhi tukifika ofisini", kwisha kusema hivyo kamanda huyo aliondoka zake akimuacha Pilo akimdadisi mwana kijiji kuhusu tukio nzima,lakini wakati Pilo anamdadisi kijana huyo ghafla alistuka kusikia jina la mtukutu Zabroni. Anamfahamu vizuri Zabroni, hasa hasa kipitia matukio mbali mbali aliyowahi kuyafanya huyo kijana.


Wakati Pilo akifikilia matikio hayo,upande wa pili kamanda mkuu akiwa ndani ya gari aliwaza na kuwazua akajikuta kuwa jina hilo sio jipya masikioni mwake,kuthibitisha hilo akaamua kumuita kamanda mwingine aliyekuwa akizungumza na baadhi ya wanakijiji. Nahe alitii wito wa mkuu wake ambapo alipofika,kamanda alimuuliza "Je, unamfaham Zabroni ", kamanda huyo aliyeulizwa alitaharuki sana kisha akasema "Mkuu huyo mtu tema mate chini,nimeshangaa sana kutuamuru kuja kumtafuta huyu kiumbe wakati mwenzetu anatumia uchawi. 

Eh unona umati huu wa watu uliojikusanya hapa,walikuja kwa niaba ya kuchukua maiti yake waliamini kwamba amekufa lakini cha kushangaza hawajamkuta..

", alijibu kwa hofu kamanda,wakati huo Pilo naye alikuwa amefika hapo ambapo naye alimuunga mkono kamanda mwenzake akisema kuwa maelezo aliyoyapata kutoka kwa yule kijana na ambayo amezungumza akamanda mwenzake hayana utofauti kabisa. Hapo mkuu alishusha pumzi ndefu kisha akahoji "Kwahiyo tunacheza na kifo?.."

"Kabisa "

"Ndio kamanda maisha yetu tumeyaweka rehani kabisa",walijibu hivyo hao maafande kitendo ambacho kilimkasilisha mkuu,kwa hasira akasema "Mkumbuke mliweka kiapo,sasa inakuaje mnakuwa waoga? Kwanza serikali yetu haimini masuala ya kishirikina,naomba kila mmoja afanye majukumu yake mpaka huyu mtu atiwe hatiani sawaaa?.."

"Sawa mkuuu ", walijibu wote kwa pamoja afande Pilo na mwenzake. "Haya nendeni mkuwaambie na wenzenu",aliongezea kusema hivyo kamanda kisha akawatawanya wanakijiji warudi majumbani mwao.

Bruno alionekana kuchoka maradufu,asiamini kama kweli Zabroni ni mzima. Alijiuliza ni dawa gani anayotumia kijana huyo kiasi kwamba awe moto wa kuotea mbali?. Kibaya zaidi zaidi kilicho mtia hofu kijana Bruno ni baada kufikiria kisasi gani atakacho kuja nacho huyo Zabroni ikiwa hapo awali alimueleza kuwa hayupo tayari tena kufanya unyama baada kukamilisha azma yake. "Inahitaji moyo pia na nguvu za ziada ",alijisemea Bruno huku akiwa na mwenyeketi wakitembea kurudi kijijini baada kutawanywa na jeshi la polisi. .

Usiku ulipo ingia hali ilikuwa shwari kijijini hapo,siku takribani tatu sasa zilikatika bila balaa lolote kutokea. Siku ya nne usiku,Bruno alimwambia Mwemyekiti wa kijiji ambaye pia ndio alikuwa mwenyeji wake hapo kijijini,alimwambia kuwa muda wa kurudi nyumbani kwao sasa umefika. "Mzee nimekaa sana hapa kijijini mimi pamoja na marehemu kaka yangu enzi ya uhai wake, nimeona changamoto mnazo kutana nazo kiukweli zinatisha. 

Kaka yangu amejaribu kupambana na huyu mtu lakini hajaweza kufua dafu,mwisho wa siku ameambulia umauti. Mimi pia nimejaribu kupambana na huyu mtu mpaka tonya la mwisho mpaka nikajua nimemmaliza,ila wapi kumbe jamaa bado yupo hai.

Kiukweli huyu mtu hafai hata chembe,anatisha sana inatakiwa nguvu ya ziada kumdhibiti. Je, nguvu hii nitaipata wapi? Kwani bado inanibidi nilipe kisasi cha kifo cha kaka yangu. Nisipo fanya hivyo sitokuwa na amani ndani ya moyo wangu mpaka naingia kaburini. 

Sasa basi ili nilipe kisasi ni lazima nikaongeze nguvu kwenye mizimu ya ukoo wetu ili niweze kumkabili huyu mtu. Kesho narudi nyumbani mzee wangu,lazima nipambane na huyu mtu mpaka mwisho ",alisema Bruno huku akiongea kwa uchungu kutoka moyoni. Mwemyekiti alimtia moyo akimwambia kuwa hakuna mwamba chini ya jua ipo siku yake naye atakwama.

Kesho yake asubuhi mapema Bruno alianza safari ya kurudi nyumbani kwa niaba ya kuongeza makali ya kuweza kumkabili mtukutu Zabroni, lakini wakati yupo njiani,alionekana kijana Zabroni akizurula katika kijiji chakina Bruno. 

Na punde si punde Zabroni alijibadilisha akawa katika umbo la Bruno kisha akajongea mpaka nyumbani huku mkononi akiwa na mifuko iliyojaa vitu mbali mbali,huku mgongoni akiwa amebeba begi. 

Hakika watu walimshangaa sana Bruno mlowezi aliyerejea,wakati huo wengineo wakitamani kumuona na kaka yake malehemu Madebe kwani waliondoka wote katika shughuli za utafutaji maisha. 

Ni kiini macho na ujanja aliotumia mtukutu Zabroni ili amalize hasira zake, watu waliamini kuwa ni Bruno karejea wasijue kwamba huyo sio Bruno wanao mjua wao,bali huyo ni mtukutu Zabloni aliyechukuwa taswira ya Bruno ili afanye balaa kwa kutumia kivuli cha Bruno,mwisho wa siku msala uangukie kwa kijana huyo ambaye naye yupo njiani anarudi kuongeza dawa za kufanikisha kumkabili Zabroni. Wazazi wa Bruno walifurahi kumuona mtoto wao,Bruno alijieleza kuhusu kutokuwepo sambamba na kaka yake. Akiwa na furaha alisema "Kaka nimemuacha huko anafuatilia madeni yake,ila nafikiri kesho naye atafika "

"Aaah hakuna tatizo baba yetu, yani kama umerejea salama basi Mungu atamsaidia na yeye kurejea salama pia", akiwa na wingi wa furaha mama Bruno alimwambia kijana wake.

Kesho yake asubuhi Zabroni aliwauwa wazazi wa Bruno kisha akaondoka zake,hiyo ikiwa kama moja ya malipo ya kufatiliwa na mtoto wao aliyejikita kwenye vita isiyo muhusu. Ila atafanya nini sasa ili amuachie msala Bruno?. Hapo sasa ndipo alipomuuwa mmoja ya vijana hapo kijijini hadhalani huku baadhi ya watu wakishuhudi balaa hilo la kinyama kwani tayari ilikuwa ni asubuhi. 

Hivyo alivyokwisha kufanya hicho kitendo alijigamba "Mimi ndio Bruno,hakuna atakae niweza. Nimeua kwa mikono yangu ",alisema Zabroni akiwa na taswira ya Bruno kisha akatokomea zake huku akiacha maswali mengi kwa wenyeji. 

Habari zilizagaa upesi kila pande kuhusu hayo mauwaji, walijua dhahiri shahili Bruno ndiye aliyefanya mauwaji ilihali wakati huo huo stendi ya gari alionekana kijana Bruno mwenyewe akishuka kwenye gari baada kufika kijijini kwao alipo zaliwa,macho na hisia akitamani kuonana na wazazi wake ili wamsaidie katika kitu alicho pania kula nacho sahani moja na mtukutuku Zabroni.

INAENDELEA.



Powered by Blogger.