SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Kumi na Tano (15)
Zabroni na rafiki yake wakuitwa Bukulu walipokuwa njiani wakirudi nyumbani,alimuuliza kipi hasa kilichomfanya yule dada ambaye ni Veronica kumuita ndani ya gari huku akionekana kumwambia jambo fulani. Zabroni alicheka kidogo baada kusikia swali la swahiba wake,na kabla hajamwambia, alisema "Ujue tumesahau kununua mafuta ya kupikia, pia chumvi nayo tumeishiwa ndani".
Bukulu alishusha pumzi kwa kasi huku akiwa ameshika kiuno chake kisha akajibu "Basi ningojee hapa hapa nikimbie dukani mara moja nikanunue,hatuwezi kula CHUKU CHUKU ilihali hela tunayo bwana",alijibu huku akifatisha na tabasamu pana lililomfanya Zabroni naye kuachia lake.
Baada ya hapo alitumua mbio kufuata hayo mahitaji yao,nyuma nako Zabroni akiwa amejiinamia akifimfikiria yule mwadada Veronica.
"Daah hivi ni kweli mimi Zabroni leo hii napendwa na mrembo kama yule? Kwa kipi hasa,maana sina SWAGA sio mtanashati.
Yani nipo nipo tu. Ama kweli nimeamini kupendwa ni nyota tu nasio uvaaji ama muonekano. Hapa ni sawa nimeokota chungwa chini ya mnazi ",kwisha kuwaza hayo alichia tabasamu kwa mara nyingine tena wakati huo huo Bukulu naye tayari alikuwa amerudi ambapo alishangaa sana kumkuta rafiki yake akiachia tabasamu. Kimoyo moyo akajisemea "Sio bure huyu jamaa atakuwa kapewa zawadi na yule binti "
"Zabroni vipi naona utabasamu mwenyewe unatabasamu tu", aliongea Bukulu kwa sauti akimwambia Zabroni, Zabroni aliposikia maneno ya Bukulu alicheka kidogo kisha akajibu "Daah! We acha tu,kiukweli yule msichana nilipo muona mara ya kwanza pale sokoni aliponikanyaga. Moyo wangu ulilia paa,hata maumivu siku yasikia"
"Unamaana gani Zabroni? " Bukulu alihoji.
"Maana yangu ni kwamba,Mungu anajua kuumba kaka. Kusema kweli wakati mungu anamuumba yule msichana alitulia, sio wale ambao aliwaumba akiwa na haraka. Ndio maana utakuta mwanamke anakichogo kama mkono wa bunduki,ukimtazama macho mithili ya nyanya chungu..." , alijibu hivyo Zabroni maneno ambayo yalimfanya Bukulu kuangua kicheko kisha naye akaongezea kusema "Kweli kabisa uyasemayo Zabro,utakuta mwanamke kwanza hajui kutembea. Anatembea upande kama ngadu,sura mbovu mbovu tu halafu maajabu ya watu kama hao mtaani wanalinga. Utasikia mimi nataka mwanaume mwenye gari wakati nyumbani kwao hata baiskeli hawana", alitania Bukulu,hapo sasa ndipo vicheko vilipo sikika huku wakigongeana mikono.
Baaada ya kusema hayo kimya kidogo kilitawala huku wakizipiga hatua kurudi nyumbani kwao,lakini muda mchache baadaye Bukulu alifungua kinywa chake na kisha kusema "Haya sasa niambie yule dada alikuitia nini ndani ya gari"
"Sawa ngoja nikwambie rafiki yangu. Ujue yule dada ni kama anashindwa kuniambia ukweli ila mimi kwa kuwa ni mtalamu wa hayo mambo, nimecheza na hisia zake nimegundua kuwa amenipenda. Na kaniambia kesho niende mjini nikaonane naye", alisema Zabroni, Bukulu alikaa kimya kwa muda wa dakika kadhaa kisha akaongeza kusema.
"Enhee umemjibu nini?.."
"Doh Bukulu,ningemjibu nini sasa zaidi ya nipo tayari? Nimemjibu nipo tayari", alijibu Zabroni huku akionekana kulishangaa swali la Bukulu.
"Sawa lakini sio wewe uliyeniambia unatafuta nauli ya kwenda Dar es salaam kumfuata mpenzi wako Tina?..", alirudia kuhoji Bukulu swali ambalo lilimfanya Zabroni kushusha pumzi kwa kasi na kisha kujibu "Ni kweli lakini Bukulu tambua Dar ni kubwa sana halafu istoshe inawatu wengi. Sawa Tina yupo Dar lakini sijui yupo Dar maeneo gani"
"Kwa maana hiyo Zabroni unataka kumsaliti Tina?.."
"Hapana ila kaa ukijua siku zote mwanaume lijali hakai na mwanamke mmoja",alijibu Zabroni kwa kujiamini kabisa. Bukulu alistaajabu kusikia jibu la rafiki yake. Akataharuki "Nini Zabloni? .."
"Mimi naona tufanye mikakati ya kuandaa chakula tu hayo mengine hata baadaye tutazungumza",alijibu kwa mkato Zabroni.
"Sawa pika mboga mimi nitapika ugali"
Zabroni huku akicheka akajibu "Aaawapi huwezi kunilisha ugali mbichi tena leo"
"Alaah! Umeshau wewe ulipo pika wali bila kuuosha mchele? .."
"Afadhali mimi. Je, wewe uliyetia chimvi nyingi kwenye mboga istoshe mboga yenyewe maharage. Osha ujuavyo lakini chumvi ipo pale pale. Kukosea kupo ila kwa leo sitaki turudie makosa"
Vijana hao wawili walitaniana , hayo yalikuwa ndio maisha yao utani ukichukuwa nafasi kubwa huku Zabroni akiwa ameshatundika daluga la kisasi cha damu alichokuwa akikifanya.
Usiku ulipo ingia,usingizi kwa kijana Zabroni ulionekana kikwazo sana kuja siku hiyo hisia zake zote alizipeleka kwa Veronica. Alijipindua huku na kule kitandani huku akitamani pawahi kukucha ili akaonane naye,lakini mwishowe usingizi ulimpitia. Hiyo tayari ilikuwa saa sita usiku. Kesho yake asubuhi alikuwa wa kwanza kuamka akajianda kwa niaba ya kwenda kuonana na Veronica kama walivyo kubaliana.
Alimuaga swahiba wake,lakini kabla hajaondoka Bukulu akamwambia "Mbona mapema hivi Zabloni? Subiri basi hata saa nne ama tano ndio uende",Zabloni akatoka nje akaenda kutazama jua kisha akarudi ndani kumjibu Bukulu "Bukulu saa hizi mpaka kufika mjini muda utakuwa umesonga,Kwahiyo acha niwahi"
"Sawa lakini kuwa makini usione vyaelea!"
"Usijali swahiba"
Zabroni akaondoka zake huku nyuma akimuacha Bukulu akitamani ile bahati ingeangukia mikononi mwake.
********
Hatimae Zabroni anaingia mjini,hiyo tayari ilikuwa yapata saa nne kasoro robo asubuhi. Kijijini na mahali ulipokuwa huo mji mdogo palikuwa na umbali kadhaa hivyo licha ya Zabroni kutoka nyumbani mapema lakini alijikuta akifika muda huo,alitumia masaa takribani matatu kwa mwendo wa kawaida.http:
Mahala pale pale walipokubaliana kukutana ndipo Zabroni alipokwenda kutulia, ambapo muda sio mrefu Veronica naye alifika. Veronica alifurahi sana kumuona Zabroni, huku Zabroni naye pia akifurahi kumuona Veronica.
Baada ya maongezi mawili matatu walikwemda moja kumbi maarufu hapo mjini,wakala chakula cha bei. Na mwisho wa yote Veronica akamwambia Zabroni kwamba ametokea kumpenda tangu mara ya kwanza alipomuona,hivyo angefurahi zaidi endapo kama Zabroni atamkubalia ombi lake. Zabroni aliposikia habari hiyo kutoka kwa Veronica alijifanya kuringa ingawa mwishowe alikubali,kitendo ambacho kiliwafanya wote kutabasamu.
Mahusiano kati ya Veronica na Zabroni yakawa yameanzia hapo,huku kila hatua anayo fikia Veronica aliwataarifu makanda wanzake kwani ikumbukwe Veronica alipewa kazi ya kumkata Zabroni mtukutu aliyefanya mauwaji ya kutisha kipindi cha nyuma.
Kwahiyo baada jeshi la polisi kumuwinda bila mafanikio ya kumpata,ndipo wakaamua kutumia nguvu ya mapenzi ambapo walimteua Veronica Afande mrembo aweze kuimaliza hiyo kazi wakiamini kwamba mapenzi yananguvu sana kwenye huu ulimwengu.
Kweli hatimaye Veronica anafanikiwa kumtwaa kimapenzi Zabroni,shughuli ikiwa imebakia kumpeleleza kijana huyo ili kujua ni nini hasa kinamfanya apotee katika mazingira yoyote? Pia ili ujanja wake huo utoweke njia gani itumike? Na je, hatomstukia pindi atakapo muuliza hayo maswali?
Maswali hayo yalimuumiza sana kichwa Veronica ila swali ambalo aliliona ni pasua kichwa ni kuhusu pindi pale Zabroni atakapo mstukia na kumuona kuwa hayupo naye kimapenzi zaidi ya kumpeleleza.
Siku moja asubuhi mapema Veronica alimpigia simu kamanda mkuu ili amsaidie japo ushauri kuhusiana na hilo swali. Kamamda akamjibu "Mpe mapenzi ya dhati,mfamye awe na furaha wakati wote. Naamini atanogewa na kukuona mtu wa muhimu kwake. Wanaume tukipenda tunakuwa kama mazezeta Kwahiyo nafasi hiyo itumie kumuuliza historia ya maisha yake japo kwa ufupi akisita kukwambia basi mtoe muende kupata kinywaji sehemu nzuri ya utulivu,hapo mmbembeleza kumnywesha pombe. Akilewa yote atasema ", aliongea kamanda mkuu. Veronica aliposikia maelezo ya kamanda wake alishusha pumzi ndefu kisha akajibu "Ahsante sana tutaendelea kuwasiliana"
"Sawa kuwa makini"
Baada ya maongezi aliirudisha simu juu meza halafu akajitupa kitandani. Siku hiyo hakwenda kokote, aliamua kupumzika.
Siku zilisonga..Mapenzi ya Vero na Zabroni nayo yakiendelea kushika kasi. Wiki mbili baadaye zilikatika bila ya wapenzi hao kuonana,hakika kila mmoja alimkumbuka mwenzie hasa hasa Zabroni aliyezama kwenye penzi la Veronica,alitamani sana amtie machoni kwani siku nyingi hawajaonana. Hivyo wakati analitamani hilo suala litokee,mara ghafla Veronica alifika kwenye ghetto lao ambalo aliwakuta vijana Zabroni na Bukulu wakicheza drafti.
Walimkaribisha lakini Veronica hakuweza kukaa bali baada ya salamu alimuita faragha Zabroni kisha akamwambia "Mpenzi unajua siku nyingi hatuja onana? Yote ni kwa sababu ya haraka za masomo chuo ndiyo ilinifanya nikawa kimya. Kwahiyo rasmi nimekuja nina hamu na wewe sana sijui hata nisemeje.
Chazaidi naomba ujiandae twende mjini ukakae japo siku sita tu tufurahi pamoja istoshe sijawahi kulala na wewe au hujui kama mimi na wewe ni wapenzi?.." alisema Veronica kwa sauti nyororo huku akimfuta futa Zabroni nyuzi za buibui kichwani,kwani alikuwa ameegemea ukuta. Kuta nyingi za nyumba za vijijini zinakuwa na utandu wa buibui.
"Najua kama unanipenda, basi kaa kidogo nijiandae ili twende lakini siku sita tu sizidishi sawa?.."
"Sawa mpenzi wangu",alijibu Veronica huku moyoni akiamini kuwa hizo ndio siku pekee za maangamizi. Siku ambayo Zabroni atakamatwa baada kusumbua sana. Siku za hatari.
Zabroni alijiandaa haraka haraka,alipokuwa tayari kwa safari alimuaga rafiki yake ambaye ni Bukulu. Bukulu alimtakia kila raheri huku akimtania kwamba ahakikishe anamfyonza mpaka yaliyofichwa. Zabroni alicheka sana akifurahishwa na maneno ya Bukulu, lakini yote kwa yote Zabroni aliondoka zake sambamba na Veronica.
Zabroni alijikuta akisahau masharti ya yule babu kutoka Nigeria, ikumbukwe kipindi Zabroni anajiwekea nia ya kulipa kisasi cha wazazi wake tayari alikuwa nyumbani kwa huyo babu. Kwani hakuwa na sehemu nyingine ya kuishi,nyumba yao iliteketea kwa moto huku wazazi wake wakifia ndani ingawa baba yake alikuwa ameshajinyonga.
Hivyo mzee yule kutoka Nigeria alimkabidhi dawa Zabroni ya kumfanya apotee mazingira yoyote,kitu kilicho mplekea Zabroni kulipa kisasi kwa uhuru huku akijivunia hiyo dawa. Na kila aliyejaribu kumfuatilia alipotezwa kama mzee Baluguza mganga nguli,lakini pia Madebe bila kumsahau Bruno.
Wote hao walipotezwa kiani yake. Lakini sharti moja ya hiyo dawa aliyopewa Zabroni ni kufanya mapenzi,endapo kama atafanya mapenzi basi dawa hiyo itapotea.
Walifika mjini,hapo sasa ndipo mkakati wa Veronica ulipoanza. Siku ya kwanza Veronica aliitumia kuzurula mjini hapo na Zabroni huku akimpitisha kwenye kumbi mbali mbali za starehe, kumbi za hadhi huku wakila na kunywa kwani bajeti aliyopewa Veronica ilidhihirisha kabisa. Hapo Zabroni akaamini kwamba mke kapata, kiasi kwamba ilimpelekea pole pole kumsahau Tina.
Siku ya pili,siku hiyo Veronica aliitumia kuzungumza na Zabroni kuhusu mahusiano yao ambayo yalionekana kunawili kila kukicha. Kiukweli mtukutu Zabroni alionekana kumpenda sana Veronica ikiwa upande wa Veronica,yeye hakumpenda abadani ingawa usoni alionyesha hisia kwa kwake ila ukweli ukiwa ni kwamba alikuwa kikazi. Ukitaka cha uvunguni sharti uiname ndio msemo aliodumu nao moyoni Veronica, afande aliyekabidhiwa jukumu la kumkamata Zabroni.
Katika ya mgawahawa mmoja ndani ya huo mji mdogo. Mgahawa ulionekana kuwa wa kifahari ,walionekana Veronica na Zabroni wakiwa wameketi huku wakinywa vinywaji. Tabasamu lao lilionyesha kuwa bashasha,vile vile kila muda walikuwa wakigongeana mikono kudhihilisha kwamba zogo walililokuwa wakipiga lilikuwa limenoga.
"Zabroni unajua kwamba wewe ni mwanaume mzuri sana?..na pia namuomba Mungu atujalie tuje tuzae watoto!", alisema Veronica akimwambia Zabfoni. Zabro aliachia tabasamu pana kisha akanywa kinywaji chake kilichokuwa ndani ya grasi halafu akamjibu "Asante sana,vile vile hata mimi naona ni bahati kuwa na mrembo kama wewe. Veronica we mzuri bwana"
"Kweli?.." alihoji Veronica.
"Ndio kwani huamini? "
"Sawa naomba tupendane mpenzi wangu",aliongeza Veronica ambapo waligongeana grasi ishara ya furaha halafu wakanyeshwana. Zabroni akimnywesha Veronica kinywaji chake,ilhali Veronica nae akijibu mapigo. Hakika furaha ilionyesha kutawala eneo hilo,na mwisho wa yote walishikana mikono wakarejea nyumbani kupumzika.
Usiku wa siku hiyo wala wa jana Veronica hakutaka kufanya naue mapenzi Zabtoni ingawa alimuweka katika matamanio,kitendo hicho kilimuumiza sana Zabroni kwani usiku wa jana aliamini kwamba huwenda akapewa kitumbua siku ya kesho ambayo ndio siku hiyo ambayo nayo ilionekana hakuna dalili yoyote ya kupewa ili ajilie vyake.
Sio kwamba Veronica alikuwa hajui jinsi Zabroni anavyoumia,lahasha alifahamu fika ila alifanya hivyo makusudi ili kesho yake amuulize mambo kadhaa wa kadha huku akimuahidi kumpa $$## chake endapo kama atamjibu inavyotakiwa.
INAENDELEA