KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Kumi na Nne (14)

simulizi ya penzi la mfungwa
Bruno alipigwa na butwaa baada kuona watu wakimnyooshea vidole,alijiuliza kitu gani ambacho kinapelekea mpaka yeye anyooshewe vidole? Je, wameshajua kama kaka yangu kafa? Ama kuna jambo gani linalo endelea. Hatamaye alikaribia kufika nyumbani kwao,alistuka kuona umati wa watu ukiwa umejikusanya nyumbani kwao huku sauti za vilio zikisikika masikioni mwake. Bruno alishitu mara dufu, hapo sasa kijasho kikaanza kumtoka,mwili wake nao ukihisi kukosa nguvu. Upesi aliachia mazaga zaga aliyokuwa ameyabeba,mazaga ambayo yalifanana fika na yale aliyokuwa nayo Zabroni kipindi anaingia hapo kijijini kwa taswira ya Bruno. 

Macho ya watu walio jikusanya hapo walipomuona Bruno walikunja nyuso zao huku baadhi yao wakizungumza maneno ya kumkashifu,maneno ambayo yalisikika vema ni pale mzee mmoja wa makamo aliposikika akisema "Ama hakika damu ya mtu nzito kuliko maji,ona sasa muuwaji kajileta mwenyewe. Hebu akamatwe haraka sana iwezekavyo"
"Mmh huyu sio mtu wa kawaida jamani,tukimfuata kizembe tutajikuta tunapoteza maisha ",alidakia mtu wa pili akisema hivyo,huyo alikuwa ni kijana wapata umri miaka ishirini na mitano. Hoja yake hiyo iliungwa mkono na baadhi ya watu wengine waliokuwepo hapo wakati huo tayari Bruno alikuwa ameshafika nyumbani kwao ambapo alistaajabu kuona watu wanamkwepa,hali hiyo iliendelea kumjengea hofu moyoni mwake,na ndipo alipopasa sauti akisema "Jamani kulikoni mbona siwaelewi?.." Alihoji huku akijitazama akigeuza shingo huku na kule kutazama sehemu mbali mbali za mwili wake. 

Lakini hakujibiwa,hivyo aliamua kuingia ndani ambapo huko walionekana wanawake wakilia kwa uchungu ila walipo muona Bruno haraka sana walikaa kimya kisha mmoja mmoja akatoka ndani. Hakika watu walimuogopa Bruno,walijuwa ndio kafanya mauwaji kwani wakati anatoka ndani baada kuuwa alionekana na mmoja ya jirani yao huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu. 

Achilia hapo,kitendo kingine ambacho kilipelekea Bruno kuogopwa, ni pale alipomuua hadharani mmoja wa kijana kijijini hapo huku akijigamba kuwa amefanya mauaji kwa kukusudia napia hakuna mtu wa kuweza kumtia hatiani. 

Lakini yote hayo yaliyofanyika hakuyafanya Bruno kama watu walivyodhani,bali mtendaji alikuwa ni Zabroni ambaye alichukuwa taswira ya Bruno na kisha kuuwa ikiwa kama njia ya kumsababishia msala Buruno. Hayo yote Zabloni aliyafanya baada kuingilia ugomvi usio muhusu huku akijaribu kufanya jaribio la kumuuwa.

Bruno alikabaliana na hiyo hali watu kumuogopa,hakujali bali alijongea mpaka mahala pale ilipo lazwa miili miwili ikiwa imefunikwa vitenge. Alipo ifikia akaifunua, alistuka kuona miili ya wazazi wake ikiwa imeuwawa kikatili. 

Alilia sana huku akiwataja wazazi wake walio uliwa, na mwishowe alinyanyuka akatoka ndani. Nje alimuita mzee mmoja aliyemuona anabusara,mzee huyo alipoona anaitwa na Buruno aliogopa kwenda lakini wazee wenzake walipo mtaka aende alitii wito. "Habari yako mzee" alisema Bruno huku moyo wake ukiwa umefura hasira kama nyoka aliyemkosa binadam.

"Nzuri..nzuri kijana wangu ", alijibu huyo mzee akiwa na wasiwasi mfano wa mtu aliyefumaniwa ugoni.

"Hivi unawez kunitajia ama unaweza kunieleza ni nani aliyefanya hiki kitendo?.." alihoji, swali hilo lilimshangaza huyo mzee akajikuta akishindwa jibu la kumpatia kwani anafahamu fika kuwa Bruno ndio muuwaji sasa inakuwaje atake kutajiwa muuwaji?..Mzee akajiongeza kwa kukataa kwamba hamjui muuwaji. "Sawa nenda ", mzee alirudi kujichanganya na wenzake. Wakati huo huo jeshi la polisi likiambatana na mbwa watano huku likiwa na siraha mbali mbali lilifika eneo hilo la tukio,kwa niaba ya kumkata muuwaji. 

Bruno bado alikuwa katika hali ya kupigwa na bumbuwazi asijue kinacho endelea,lakini punde alifahamu kinacho endelea baada mama mmoja ambaye alionekana kulia kwa uchungu huku akimnyoshea kidole . Mama huyo akilia alisema "Yule pale muuwaji,kaniulia mwanangu. Hafai kabisa sitaki hata kumuona machoni mwangu",kamanda mkuu alitoa amri kuwa Bruno akamatwe. Bruno alishangaa,akajiuliza "Mimi nimekuwa muuwaji?mmmh hapana!.." 

baada kujiuliza hivyo ikabidi ajitetee lakini Bruno hakueleweka,alikamatwa huku wakimtaka akajieleza mbele kwa mbele. Ndani ya gari la polisi Bruno alirushwa kisha gari likatimua mbio ilihali huku nyuma wakisalia baadhi ya polisi kwa niaba ya kuzika hiyo miili iliyo uwawa kikatili. 

Bruno akiwa ndani ya gari hilo la polidi,alijiinamia huku akijiuliza maswali mengi kichwani mwake. Alijiuliza "Hivi ni nani muuwaji wa wazazi wangu? Na nikipi kinacho pelekea nikamatwe mimi ilihali mimi sio muuwaji?na endapo nitafungwa nitawezaje kulipa kisasi? Na iweje nifungwe kwa kosa ambalo sijafanya?..", alijiuliza Bruno huku akiwa amejiinamia . 

Hatimaye walifika kituo cha polisi ambapo hapo Bruno alishushwa mfano wa gunia la mkaa kwa niaba ya kuuingiza selo ili uchunguzi ufanyike kabla hajapelekwa kizimbani, lakini wakati anaingia ndani ghafla alisikia sauti ikimuita. 

Upesi Bruno aligeukia kule ilipo tokea sauti hiyo ajabu sana alimuona mtu aliyefananae kuanzia sura mpaka nguo alizovaa, si mwingine ni Zabroni. Hapo sasa ndipo Bruno alipofahamu fika mtandaji wa lile jambo ni Zabroni ambaye alifanya jambo lile huku akiwa katika hali yake ili kumsababishia msala yeye. 

Hakika Bruno akiwa na pingu mkononi aliumia sana,machungu yaliongezeka mara mbili kwani tayari Zabroni alikuwa amemuulia wazazi wake. Lakini yote yote Bruno aliingizwa ndani huku nje Zabroni naye akijinasibu kwa kusema "Mimi ndio Zabroni",kwisha kujisemea hivyo alirudi katika umbile lake la kawaida.

Kazi ikawa imemalizika sasa,wabaya wake alikuwa aneshamalizana nao. Hivyo akawa mtu wa amani wakati wote,alijichanganya na wenzake kwani mahali hapo alikuwa mgeni kwahiyo hakuna mtu hata mmoja aliyefahamu historia yake.

Lakini wakati kijana Zabroni akiwa mtu wa amani wakati wote huku akiacha utukutu wake, upande wa pili kule kijijini kwao bado jeshi la polisi lilikuwa likiendelea kumuwinda kwa udi na uvumba. Na mara baada kumtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio,hatimaye kamanda wao alipata wazo. 

Wazo ambalo aliwaeleza wenzake kwamba ili wamkamte Zabroni basi itawalazimu wamtumie mwanamke,kwani kufanya hivyo inaweza kupelekea kijana huyo kukamatwa bila kutoa jasho. 

Kwa sababu siku zote mwanaume kwa mwanamke huwa ni mzaifu sana,hivyo Mwanamke huyo atakaye teuliwa ni lazima aweke ukaribu na Zabroni wakati huo akimuuliza mambo mbali mbali kuhusu uwezo wake wa kupotea katika mazingira yoyote. Na pia asisahau kumuwekea utani kwa kumdadisi kwamba ili ujanja wake ufike tamati njia gani itatakiwa ifanyike. 

Kufanya hivyo inaweza kuwa rahisi sana kumkataa Zabroni pasipo kutoa jasho lakini pia mwanamke mwenyewe lazima awe mrembo,sio mwanamke awe na uso mkavu kama fenesi, pua kama nyundo. Kichogo kama kinu . 

Mwanamke awe mzuri kiasi kwamba akijiweka kwa Zabroni,basi mtukutu asisite kujenga naye uhusiano. Walikubaliana hilo suala wakaona linafaa, lakini ugumu kujua mahali alipokimbilia mtukutu huyo vile vile wapi watampata mrembo wa kuvutia. "Kamanda kuhusu hilo halina shaka,yupo huyu binti aliyeanza kazi wiki iliyopita Afande Veronica,huyu anafaa sana siunaona alivyokuwa mrembo? .."

"Ni kweli anafaa itabidi aje ofisini leo ili niweze kuzungumza naye hili suala ili siku yoyote aanze kazi"

"Sawa kamanda"

Siku hiyo hiyo Afande Veronica alitii wito aliambiwa jinsi hali inavyotakiwa kuwa huku akiahidiwa ZAWADI nono pia kupandishwa cheo pindi atakapo funga ukurasa wa mishe hiyo. Wakati wanafikia muafaka Veronica na mkuu wake, mara ghafla kituoni hapo alikuja raia kutoa taarifa kwamba Zabroni yupo mahali fulani anaendelea na maisha yake. Jambo la heri kiukweli kwa upande wa hao Makanda hao kwani waliona tayari mchezo unakwenda kumalizika.

"Vero,"

"Yes kamanda"

"Wewe mrembo bwana,siku mbili hizi anza kazi,hautokuwa peke yako bali na sisi tupo nyuma yako kukupa ushirikiano. Vaa nguo za kiraia anza kazi"

"Usijali kamanda,wanaume nyie wa kwetu kamwe hamruki katika suala zima la mapenzi hasa kwa mwanamke mzuri kama mimi. Nakuhakikishia hapa kanasa ",alijibu kwa masihara na kujiamini pia Afande Veronica,Afande ambaye alionekana kuvutia kila kona ya mwili. Ngozi nyororo uso mzuri mpaka mwili wake ulivutia umbo namba nane.


Wahenga waliwahi sema kwamba,ukitaka kuruka?sharti uagane na nyonga. Abadani hawakukosea kusema msemo huo,bila shaka waliona mbali sana na ndio maana wakaamua kusema huo msemo ambao unatumika sana kwa mtu aliyeamua kujitosa kutenda jambo fulani. Ndivyo ilivyokuwa kwa kamanda wa kike Veronica, kamanda ambaye aliamua kujitolea kumtia Zabroni kwenye mkono wa sheria kwa kutumia mbinu ya aina yake. 

Ikimbukwe Zabroni kipindi cha nyuma aliwahi kufanya mauaji mbali mbali,alitia watu hasara mali zao lakini alifanya kila jambo mbaya ambalo hata mwenyezi mungu hapendi. Vitendo hivyo vilipo shamili,jeshi la polisi ndipo lilipo amua kuingilia kati ingawa bado walichemka kwa sababu Zabroni hakamatiki kwa siraha. 

Baada kumshindwa kwa siraha ndipo walipoona kwamba watumie njia ya mapenzi,kwani mapenzi siku zote yananguvu kuliko kitu chochote hapa duniani kwani mapenzi hayana komando. Sasa basi njia hiyo itweza kumtia mtukutu Zabroni kwenye mkono wa dola? Je, Veronica ataweza?

****

Baada ya makubaliano kufanyika, siku tatu zilikatika. Siku ya nne kamanda Veronique alianza kazi ambapo aliambiwa mahali ambapo Zabroni hupendelea kukaa katika hicho kijiji,hiyo ikawa rahisi kwake kwani alipotembelea maeneo hayo siku ya kwanza hakumkuta lakini siku ya pili alimkuta akishirikiana na wenzake katika shughuli za jamii. 

Baada kumuona alichomoa picha ndogo aliyokabidhiwa,aliitazama kisha akamtazama Zabroni kule alipokuwa akichakarika. Alipo jihakikishia kuwa ndiyo huyo,aliirudisha kwenye mkoba wake picha ya Zabroni kisha akarejea mjini nyumba ya wageni alipokuwa amepanga chumba. Akiwa amechoka alijilaza kitandani huku akiwa na nguo ya kulalia,kifua chake kikiwa wazi. Kiukweli kilivutia sana,chuchu zilikuwa zimesimama. 

Ngozi yake ikiwa nyororo pia kitovu chake kilikuwa kina shimo kidogo,tumbo lake likiwa laini kama nyama ya ulimi. Kamanda Veronique alivutia sana kizuri kisifie. Basi hapo baada kujilaza kitandani,akili yake yote aliifikiria namna ya kumkamata Zabroni. 

Mawazo ambayo yalimpelekea kupitiwa na usingizi ila aliamshwa na sauti ya simu ikiwa inaita,alikurupa kutoka usingizi alipo tazama jina la mtu aliyempigia akaona jina limeandikwa "Kamanda Molisy" alibonyesha kitufe cha kijani kisha akaweka sikioni alisema kwa sauti ya upole "Afande"

"Mmmh Veronique habari yako?..",ilisikika sauti ikijibu hivyo kwa mbali.

"Salama tu sijui kwenu huko"

"Kwetu salama,mbona wasikika kwa upole?..", alihoji kamanda Molisy ambaye ndio mkuu wa kikosi hicho cha kina Veronica.

"Aahmm.. nilikuwa nimelala siunajua kazi ilivyo? Lakini ondoa shaka leo nimebahatika kumuona,nina uhakika kazi itakuwa nyepesi sana", aliongea Veronica huku ikijonyoosha akizipiga hatua kwenye begi lake ili achukue taulo aingie bafuni kuoga.

"SAWA kazi njema,tutakuwa tunawasiliana. Ikitokea tatizo usisite kutupa taarifa mapema ili tuweze kulitatua", alisema Molisy.

"Sawa Afande" Veronica akakata simu kisha akaitupia kitandani,akajongea mpaka kwenye mlango wa bafuni akafungua akaenda kuoga.

Kesho yake asubuhi kabla Veronica hajaanza safari ya kwenda kijijini kuendelea na majukumu yake,alikatiza mitaa ya mji huo mdogo alikuwa amepanga chumba akatokea sokoni kufanya manunuzi mbali mbali matunda na vitu vinginevyo. Lakini wakati yupo ndani ya hilo soko, mara ghafla alimuona Zabroni akiwa na jamaa mmoja ambaye bila shaka alikuwa ni rafiki yake. 

Veronica alistuka, haraka sana akazipiga hatua mpaka pale alipo simama Zabroni. Alipo mkalibia alimkanyaga makusudi huku akijifanya kumpisha mtu aliyekuwa akipishana naye,kwani eneo hilo palikuwa na msongamano wa watu. 

Veronica alipo mkanyaga Zabroni alinyanyua mguu haraka sana kisha akasema "Jamaani pole mkaka", Zabroni aliposikia hiyo sauti nyororo alitabasamu kisha akajibu "Usijali najua ni bahati mbaya", alijibu kwa upole huku macho yake akitupia kwenye uso wa Veronica kitendo ambacho kilimfanya Veronica kuachia tabasamu pana huku aking'ata mdomo. 

Ghafla Zabroni alipagawa ilihali muda huo huo Veronica aliondoka zake,nyuma mkungu wake wa ndizi ukitikisika kiaina yake. Vijana walio mtazama Veronica hawakusubitu kupepesa macho,mirunzi ilisikika kutoka kwa madereva piki piki na wasukuma mikokoteni. Yote hiyo ikiwa ni shamra shamra ya kumuona Veronica akitembea huku makilio yake yakicheza,kiukweli alijaliwa ingawa sio sana.

"Daah ama kweli mjini kuna mambo Zabroni" ,alisema huyo jamaa aliyekuwa na Zabroni.

"We acha tu,tuachane na hayo. Vipi mzigo huu tutauza ama? Kwa sababu bei tuliyoikuta tofauti na tuliyo tegemea"

"Ni kweli,lakini ujue hata tusipouza ni sawa na bure tu. Hizi ni nyanya Zabroni hazichelewi kuoza, Kwahiyo kuliko tupate hasara ni bora tuuze tukagange yajayo", alisema jamaa huyo. Zabroni alijikita katika mambo ya kilimo baada kuona kumaliza kisasi chake. Hivyo siku hiyo yeye na rafiki walikuwa mji mdogo kwa niaba ya kuuza mazao yao.

Walikubalina wakawa wameuza mazao ya kwa hiyo hiyo bei waliyoikuta gulioni,na mara baada kupokea ujira wao walianza safari ya kurejea kijijini ambapo huko hukukuwa na mtu hata mmoja aliyemfahamu Zabroni. Aliishi kwa amani pasipo kuwa na shaka. 

Lakini kipindi wanatoka gulioni mara ghafla Zabroni akakutana tena Veronica, wote kwa pamoja waliachia tabasamu hasa Zabroni baada kukumbuka kwamba kuna muda aliyekanyagwa na huyo binti akawa amemuomba radhi. 

Safari hiyo Veronica alikuwa anafungua mlango wa gari teksi,kabla hajaingia ndani alimuuliza Zabroni wapi wanapo elekea,Zabroni akataja na hapo ndipo Veronica alipowataka wapande kwa madai kwamba naye anaelekea huko. Zabroni na rafiki yake walifurahi sana kupata lifti,Veronica akamwambia dereva wake afungue buti nyuma ili waweke tenga ambalo walibebea nyanya. Safari ikaanza kuelekea kijijini,wakiwa ndani ya gari walipiga zogo mpaka mwisho wa safari ya safari ya Zabroni na rafiki yake ambapo walishuka kisha wakatoa shukrani zao. 

Kabla hawajaondoka Veronica alimuita Zabroni ndani ya gari huku nje akibakia rafiki yake akiwa amesimama...Ndani ya gari Veronica alimwambia Zabroni "Smahani kama hutojali nilikuwa naomba kesho uje mjini tukale pamoja chakula cha mchana,usistuke nimevutiwa sana na ukarimu wako unaonekana kijana mpole,kiukweli kaa ukijua tu kwamba umenivutia sana na pia nitafurahi endapo kama utanikubalia", alisema Veronica kwa sauti nyororo huku uso wake ukionyesha haibu. Zabroni aliposikia maneno ya huyo dada,moyo wake ulistuka. 

Ndani ya nafsi yake akajiuliza "Bahati gani hii inanitokea? Hili ni zali la mintali siwezi kulipuuzia " kwisha kuwaza hayo alijibu "sawa nipo tayari usijali. Je, tukutane wapi?",Veronica alimuelekeza mahali pakukutana,Zabroni akawa amemuelewa ambapo alisisitiza kutokukosa.

Baada ya hapo waliagana,Veronica akaondoka zake lakini pia Zabroni naye akajua hamsini zake huku kila mmoja akijanasibu kiana yake. Mtukutu Zabroni akijigamba kwamba huwenda akawa amepata zali la mentali kwa Veronica, ilihali Veronica naye akiamini kuwa yule ndege mtutundu anakaribia kunasa kwenye tundu bovu!

Powered by Blogger.