SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Kumi na Sita (16)
Kesho yake asubuhi, siku ya tatu hiyo. Veronica aliamka akaelekea bafuni kuoga huku akimwacha Zabroni kitandani akiwa bado amelala,haikuchukuwa muda mrefu alitoka bafuni akajiandaa haraka haraka kisha akamuaga Zabroni kuwa anaenda chuo. Utaratibu mzima wa chai pia na chakula cha mchana alimuelekeza muhudumu wa hotel hiyo aliyochukuwa chumba Veronica,akimwambia kwamba ampelekee huduma hizo mtu wake ambaye ni Zabtoni.
Zabtoni aliamini moyoni mwake kuwa mpenzi wake Veronica ni mwanafunzi wa chuo,lakini upande wa pili Veronica hakwenda Chuo kama alivyomuaga Zabroni kwani hakuwa mwanafunzi ila plan yake ni kumuacha Zabroni kwa muda ili akirudi ajionyeshe kukasirika,kitu ambacho aliamini lazima Zabroni amuulize nini tatizo pindi atakapo onekana kukasirika. Kupitia nafasi hiyo sasa ndipo aanze kufanya upelelezi.
Wakati Veronica akiamini hayo,upande wa pili Zabroni alikuwa na shauku ya kutaka kuonja penzi la Veronica. Hasa hasa kila alipofikilia umbile la huyo mrembo,mwili wake ulijihisi kusisimka huku moyoni akipania siku hiyo avunje ukimya azungumze kuhusu hisia zake.
"Nitamwambiaje?.." alijiuliza Zabroni,akifikiria namna gani atamueleza Veronica juu ya yeye kutaka penzi lake. Kwani siku zote alikaa kimya akidhania kuwa huwenda Veronica akajiongeza akawa amembalikia siku yoyote,lakini sivyo kama alivyo dhania.
Kila siku walikula na kutembea baadhi ya kumbi ya starehe kuponda raha,kasoro starehe moja tu ambayo ndiyo hiyo Zabroni alikuwa akiitamani siku yoyote itokee. "Nitajikaza lazima nimwambie,haiwezekani kila siku tunalala kama kaka na dada leo lazima niseleleke naye" alisema Zabroni,akisahau kabisa masharti ya dawa aliyopewa.
Muda ulitaladadi,hatimaye jioni iliwadia. Veronica alipofika chumbani hakusema na Zabroni, alijitupa kitandani huku akiwa amelala kifudi fudi. Zabroni alitaharuki kuona kitendo hicho alichokifanya Veronica, alijiuliza "Nani kamkera? Na mbona sio kawaida yake?..", kabla Zabroni hajapata jibu la hilo swali alilo jiuliza, Veronica akamuuliza
"Zabroni unanipenda kweli ama unanizuga?.." Zabroni alistuka kusikia swali hilo la Veronica, akamgeukia kisha akamjibu "Swezi kuchezea hisia zako,nakupenda sana. Kwanini upo hivyo leo,istoshe kitu gani kilicho kufanya unilize hilo swali?..", alijibu Zabroni kwa sauti ya upole huku akimkodolea macho Veronica ambaye muda huo alikuwa amejilaza kitandani akijifanya kukasirika.
"Mimi nahisi hunipendi,laiti kama ungekuwa unanipenda basi ungenipeleka kwa wazazi wako",aliongeza kusema hivyo Veronica,maneno ya mtego kwani alifahamu fika Zabroni hana wazazi. Na chanzo cha mauwaji yaliyokuwa akiyafanya chanzo ni wazazi weke, Kwahiyo alisema hivyo ili kumtega Zabroni. Zabroni kabla hajamjibu Veronica, alishusha pumzi kwa nguvu kisha akasema "Veronica mpenzi, mimi sina wazazi"
"Huna wazazi?..",aling'aka Veronica akijifanya kusituka.
"Ndio walifariki kwa ajari ya moto ",aliongeza kusema Zabroni,hapo Veronica aliamka akamsogelea karibu kisha akasema "Pole sana mpenzi wangu,lakini unaweza kuniambia hiyo ajari ilikuwaje kuwaje? Samahani mimi mkeo naomba uniambie nikae nikijua",alisema Veronica kwa sauti nyororo iliyomfanya Zabroni kushusha pumzi kwa mara nyingine kabla hajaanza kumsimulia.
Upande wa pili, ndani ya mji huo huo mdogo. Alionekana Bruno akikatiza moja ya mitaa ya sokoni,lakini punde si punde alipotea kimazingara wakati huo huo jeshi la polisi likiambatana na mbwa wao wakionekana kulisambalatisha soko hilo baada kugundua kwamba Bruno yupo mahali hapo.
Bruno alikuwa ametoroka kabla siku ya kupandishwa mahakamani kusomewa hukumu haijawadia, nia ya kutoroka ni kutaka kulipa kisasi kwa Zabroni. Ikumbukwe Zabroni alimuuwa kaka yake Bruno ambaye ni Madebe,lakini pia aliwauwa wazazi wake huku akiwa na sura ya Bruno ili Bruno agundulike ndio muuwaji mwishowe ahukumiwe jela,nage Zabro aishi maisha bila kusumbuliwa.
Ndivyo alivyo amini Zabroni kwamba Bruno kamwe hatorudia kumsumbua kwani atakuwa jela kwa kesi ya mauwaji aliyomsababishia, na ndio maana hakujali sharti la dawa aliyokuwa nayo, sababu alijuwa kazi kuu alishaikamilisha. Asijue kwamba Bruno karudi uraiani huku anasakwa na jeshi la polisi, naye anamsaka mbaya wake popote pale alipo ili akamilishe lengo lake la kulipa kisasi.
"Nimekukubali wewe ni mwanaume wa shoka, kama kweli ulilipa kisasi hakika ulistahili kufanya hivyo. Lakini uliwezaje kutembeza hiyo dozi katika hicho kijiji? ",alisema Veronica akisindikiza na swali,kwani alisema hivyo baada Zabroni kumsimulia kisa na mkasa kuhusu kifo cha wazazi wake.
Zabroni hakuishia hapo,alienda mbali zaidi kwa kusema kwamba alilipa kisasi. Jambo ambalo lilimfanya Veronica kumsifia kijana huyo,ambapo hakuishia hapo alimuuliza pia ni namna gani aliweza kutembeza dozi katika hicho kijiji.
Zabroni alikaa kimya kidogo huku akionekana kutafakari jambo fulani,Veronica alipoona hiyo hali akamsogolea karibu zaidi kisha akasema "Niambie shujaa wangu,kidume kati ya vidume. Uliwezaje kutembeza kichapo kijijini. Ikumbukwe wewe ni mtu mmoja,sasa iweje upigane na uma? Ama ndio hivyo unanidanganya?..", aliongea Veronica wakati huo sasa mikono yake ikishughulika kuvua nguo ya juu huku akibaki na sindilia.
Kifua chake kikawa wazi, ngozi nyororo isiyo na mikwaruzo ilionekana kwenye mwili wake,kiasi kwamba ilimfanya Zabroni kusisimkwa mwili wake baada kutupia jicho upande aliokaa Veronica.
"Niambie basi" ,aliongeza kusema Veronica. Zabroni alishusha pumzi ndefu kisha akasema "Kiukweli sikuogopa kitu,kile kifo cha wazazi wangu kilinipa shinikizo. Mmoja baada ya mwingine niliuwa. Hasa hasa yule aliyejaribu kunifuatilia kwa niaba ya kunikatisha kile nilicho kipanga. Nilichoma nyumba hovyo pale kijijini wakati huo tayari ninacho cha kujivunia."
"Mmh kitu gani hicho? Alihoji Veronica.
Zabroni akajibu huku akianza kwa kicheko "Hirizi,Nilipewa dawa na mzee yule ambaye nilikwambia kwamba baada wazee wangu kufa nikawa naishi kwake. Huyo mzee ni mtu kutoka Nigeria, alinisaidia kunipa hiyo dawa ili niweze kulipa kisasi kwa uhuru zaidi" .
Kimya kilitawala kidogo,kimya ambacho kilimstua Zabroni ambapo alimuuliza nini hasa kilicho mfanya akaye kimya,aidha maneno aliyomuambia? "Vero mbona upokimya ama umeogopa maneno yangu? Usiogope bwana hiyo ilikuwa zamani. Kwanza kwa sasa nipo kawaida sana,istoshe wabaya wangu nilishawapiteza Kwahiyo wala usiwaze.
Nakupenda sana tena sana Veronica wangu",alisema Zabroni akimwambia Veronica, ndani ya moyo wake Vero aliamini tayari Zabroni hana ujanja kwake. Hivyo kupitia nafasi hiyo alimuuliza "Mmh nitakuaminije? Usije ukaniuwa na mimi humu ndani"
"Kukuuwa? Hapana siwezi bwana hebu acha utani",alijibu Zabroni huku akiyastaajabu maneno aliyoyasema Veronica.
"Kwahiyo unataka kusema kwamba dawa imeshaisha mwilini? ", akijifanya mtu mwenye hofu alimuuliza swali hilo Zabroni.
"Kabisa,hata hivyo yule babu alinambia kwamba ili dawa aliyonipa ili ipoteze nguvu ni pale nitakapo fanya mapenzi, na tangu niachane na yale matukio sijawahi kufanya mapenzi ingawa naaamini kwamba dawa imeshapoteza ubora kwani kitambo sana sijaitumia"
"Mmmh",aliguna Veronica wakati huo moyo wake ukiwa umefura furaha isiyo kifani.
"Ndio hivyo"
"Kwahiyo unataka kusema hujalala na mwanamke?.."
"Niamini Veronica kama mimi nilivyokuamini mpaka nikaweza kukwambia hii siri nzito. Sijawahi kumwambia mtu yoyote ila wewe,ingawa nakusihi usimwambie mtu yoyote. Ingawa wanasema hakuna siri ya watu wawili lakini naomba hii iwe siri ya watu wawili tu. ", Zabroni alisisitiza.
"Zabroni mpenzi ", kwa sauti ya upole Veronica akamuita Zabroni.
"Naam! Mpenzi Veronica "
"Unanipenda kweli?.."
"Ndio nakupenda sana"
"Sawa nikuulize swali?.."
"Uliza tu upo huru"
"Hivi ikitokea labda nimevujisha hii siri utanifanya nini?..", akastuka Zabroni baada kuulizwa swali hilo,alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Sitikufanya chochote ila nitafurahi kama utaniomba msamaha". Veronica alicheka kidogo halafu akasema "Hapana siwezi kufanya hivyo kwani hata mimi nakupenda sana"
Siku ya tatu ikawa imeishia hivyo,hapo Veronica alibaki kumaliza kazi aliyopewa kwani tayari kile alichokuwa alikitaka amekipata. Ndani ya nafsi yake akajikuta akijisemea "Ama kweli dunia ina mambo. Kwa mwendo huu kamwe wasingemuweza huyu mtu". Upesi akatoa taarifa kwa uongozi "Safi sana Veronica, wewe ni jembe unafaa sana.
Sasa nafikiri ng'ombe mzima umeshamaliza bado mkia tu", alijibu kamanda wake mkuu akifurahishwa na hatua nzuri aliyofikia kamanda Veronica ambaye ametwishwa jukumu nzito la kumpeleleza mtukutu Zabroni ili mwisho wa siku atiwe katika mkono wa sheria baada kusumbua kwa kipindi kirefu sana.
Siku ya pili yake ilipo fika,siku ya nne sasa. Asubuhi mapema Zabroni alimuamsha Veronica ili ampe madini ajilie,lakini Veronica muda huo akajifanya kuamka kwa haraka haraka akidai kwamba kachelewa shule. "Baby unajua mimi nikadhani lao mapumziko.
Afadhali ulivyoniamsha acha niwahi ingawa leo nitatoka mapema ili nije nicheze na wewe mpaka pale hamu yako utakapo kata. Alisikika akisema hivyo Veronica akimwambia Zabroni ambaye yeye muda huo alimuamsha kwa niaba ya kutaka $$## lakini Vero akawa ameingizia mambo mengine tofauti na aliyo yatarajia Zabroni.
"Subiri atakuja kunielewa atakavyo nipa nafasi lazima aombe mchuzi wa supu",alijisemea Zabroni ndani ya nafsi yake akionekana kumkamia Veronica pindi atakapo mpa penzi lake. Na wakati Zabroni anajisemea hayo,Veronica alikuwa bafuni kuoga. Punde si punde alirejea akajiandaa haraka haraka kisha akamuaga mpenzi wake akawa ameondoka zake akiwa katika hali ya kujifanya mwanafunzi.
INAENDELEA