KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Kumi na Saba (17)

simulizi ya penzi la mfungwa
Huko alikokwenda,aliwataarifu police wenzake ili wajisogeze karibu na tukio. Kamanda mkuu Molisy alionekana kutoyaamini maneno ya Veronica,lakini alipowahakikishia mara mbili mbili hatimaye walikubali.

Jioni aliporejea nyumbani alimchukua Zabroni akampeleka moja ya kumbi ya starehe,ambako huko walikula na kunywa. Waliporejea nyumbani kila mmoja alionekana kuwa tayari kwa niaba ya kucheza mechi,mechi ambayo ilikuwa ya malengo kwa Veronica. Walifanya mapenzi,baada ya tendo Zabroni alilala moja kwa moja mpaka asubuhi ambapo alipo amka hakumkuta Veronica. 

Alistuka sana kwani haikuwa kawaida ya Veronica kuondoka pasipo kumuaga,wakati akiwa ameshikwa na bumbuwazi..mara ghafla kichwa kikaanza kumgonga kwa kasi mfano wa nyundo inayotua kwenye chuma. 

Hali hiyo ilimtia wasi wasi Zabroni, akatoka ndani huku akiwa ameshika kichwa chake. Nje alikutana na muhudumu wa mle ndani ya hoteli waliyokuwa wakiishi na Zabroni na Veronica. "Umenionea mdada kapita hapa asubuhi hii?..", akiwa na hofu dhufo lihali Zabroni akamuuliza muhudumu wa mapokezi kuhusu Veronica.


"Ndio ila..",kabla muhudumu huyo hajaendelea kusema,mara ghafla alidakia braza mmoja aliyekuwa amesimama kando. Braza huyo alisema " Si yule dada mzuri? Anaishi humu ndani? Mweupe kidogo!.."
"Ndio huyo huyo",alijibu Zabloni huku akiwa amekunja uso kwa sababu ya maumivu ya kichwa.

"Doh nimemuona kule maeneo ya gulioni ameambatana na jeshi la polisi lakini baadaye wakawa wameachana sasa sijui kaenda wapi?.." alieleza Braza huyo. Ghafla Zabroni akastuka kusikia habari hiyo, woga ulimjaa kwa mshangao akahoji "Polisi?.."
"Mmh sawa nisubirini nakuja hivi punde ",Kwisha kusema hivyo alitimua mbio kurudi kijijini kwa swahiba wake huku akiamini kwamba tayari maji yamezidi unga, Veronica amemuingiza mkenge. 

Hivyo aliamua kurudi kijijini kwa niaba ya kuchukua hirizi yake aliyopewa na yule mzee Maboso, hirizi ambayo Bruno aliwahi kuitwaa mikononi mwake baada kumchezeshea kichapo Zabroni cha mbwa mwizi lakini mwishowe akaidondosha pasipo kujua ikawa imerudi mikononi mwa Zabroni kwa mara nyingine tena. 

Kwahiyo dhumuni kuu ni kuchukuwa hirizi hiyo ambayo alikuwa hatembei nayo,ajifunge ili ajitetee kwa jambo lolote litakalo mkabili ingawa uwezo wa kupotea kama awali hakuwa nao tena. Alipofanya mapenzi,nayo ikawa imepotea. Hivyo hirizi hiyo ni kwa niaba ya kuwa na nguvu za ziada za kuweza kupambana hata na watu mia kasoro lisasi aidha panga.


Alipofika nyumbani alizama moja kwa moja chumbani, alikuta mlango upo wazi,huko alimkuta Bukulu akitupa miguu huku na kule wakati huo damu zikivuja tumboni. Akastuka Zabroni, upesii akamvagaa kumuuliza swahiba wake kipi kimemsibu "BUKULU Bukulu nini kimekupata?.." alihoji Zabroni huku akiwa amechuchumaa kumtazama.

"Bru bru...nooo ", alijibu Bukulu kisha akakata roho. Zabroni alizidi kuchanganyikiwa kusikia jina hilo,akajiuliza "Bruno? Inaamana Karudi?..", kabla hajapata jibu alisikia amri ikitoka nje. "Zabroni toka humo ndani kabla hatujafyatua risasi ", akastuka zaidi Zabroni huku kijasho kikimtoka, alitoka ndani. Nje alikuta jeshi la polisi likiwa na siraha zao mbali mbali huku pembeni akionekana Veronica akiwa amevaa kwanda la kipolisi. "Vero? Ni wewe?", kwa TAHARUKI alihoji Zabroni.


"Ndio mimi nilikuwa kikazi Zabroni,hakuna mwamba chini ya jua. Hatimaye umekamatika mshenzi mkubwa wewe",alijibu kwa dharau na kebehi Veronica. Mkuu wa msafara huo uliofika kumkata Zabroni akatoa amri Zabroni akamatwe. Hukumu ikatolewa kuhukumiwa kifungo cha maisha huku akizushishwa kumuua Buruno kwa mikono yake.
*****
Ndio hivyo ilivyokuwa washkaji, ila siwezi kuendelea kuishi jela. Adui yangu kajitokeza mwingine, lazima nikale nae sahani moja vile vile nikammalize na yule dogo aliyemuuwa Swahiba wangu. Alisema Zabroni huku akiwa amezungukwa na kundi la wafungwa,katika gereza la Ukonga jijijini Dar es salaam. Wafungwa hao walikuwa wakisikiliza mkasa wake huo ambao uliwaacha vinywa wazi.

"Kwahiyo utafanye sasa mwamba?.?", alihoji mmoja wa mfungwa aliyekuwepo hapo. Zabroni alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Nitatoroka siku yoyote"

Gumzo gerezani,kila sehemu wafungwa walikuwa wakimtazama Zabroni kwa jicho la tatu,yote ikitokana na simulizi fupi aliyowasimulia wafungwa wenzake kisa na mkasa kilicho muingiza jela. Na kitu pekee kilicho mpelelea Zabroni kuogopwa zaidi na wafungwa baadhi,ni kauli aliyoitoa kwamba atatoroka gerezani hapo muda wowote.

Mkasa huo wa kutisha aliosimulia Zabroni, hatimaye ulimfikia kijana mmoja aliyefamika kwa jina Bluyner. Kijana aliyetunikiwa cheo cha nyampala gerezani. Ni kijana ambaye alionekana kujazia mbavu na misuli ya mikono yake,uso wake nao ukiwa mkavu zaidi ya kiatu cha mtemebeza nyegere. 

Sio kwamba Bluyne hakumfahamu Zabroni,la hasha alimfahamu fika ila Hadithi ya maisha yake hakuifahamu. Hivyo siku hiyo akawa ameambiwa, alistuka sana lakini hakutaka kuamini kama kweli Zabroni anaweza kufanya hayo yote sababu matendo hayo hayaendani na muonekano wake. 

Kupitia hilo Bluyner akihisi huwenda ufalme wake ndani ya gereza hilo ukifikia tamati kwani kupitia simulizi ile ya Zabroni itawafanya wafungwa kumuogopa na kisha kumzarau yeye,kitu hicho Bluyner hakuta kitokee hata mara moja. "Ipo siku nitamfumua mbele yao ili heshima izidi kubaki kwangu",alijisemea Bluyner baada ya kumtafakari Zabroni kwa muda mrefu.


Siku iliyofuata asubuhi ya mapema,kengere iligongwa. Wafungwa wote walikurupuka kutoka vyumbani mwao haraka sana wakawahi mstarini kuhesabu namba ilihari huku upande wa pili kijana Bluyner alionekana akitembea chumba baada ya chumba akimsaka Zabroni. Hatimaye alimuona,muda huo Zabroni alikuwa akielekea mstarini. Lakini kabla hajafika,mara ghafla aliguswa bega.

 Zabro alistuka akasimama akageuka kumtazama mtu aliyemgusa bega akamuona Bluyner kiongozi wao. Kwa sauti ya ngumu iliyojaa utashi wa kibabe Bluyner akamwambia Zabroni "Kijana wewe mzuri sana",aliongea hivyo Bluyner huku akimgusa kidevu Zabroni. 

Zabri alibaki kumshangaa Bluyner, lakini mwishowe alimshika mkono kisha akamng'atua Kwenye mwili wake halafu akasema "Kwahiyo kama mimi mzuri,inakuhusu nini wewe?..",Bluyner akacheka kwa madaha kisha akajibu "Leo kikombe chako cha uji nakunywa mimi",Hapo Zabroni hakujibu chochote,zaidi aliishia kumsonya kisha akazipiga hatua kuelekea mstarini kuhesabu namba kabla hawajanywa uji na kisha kwenda kulitumikia taifa kwa nguvu. 

Wakati Zabroni anaondoka zake,huku Bluyner aliishia kucheka ingawa naye alijisogeza mahali hapo japo hakujipanga mstari kama ilivyokuwa kwa wafungwa wenzake.

Sauti za kuhesabu namba zilisikika zikipasa,punde si punde zoezi hilo likawa limemalizika ambapo amri ya kupanga mstari kwa niaba ya kupokea uji ilitoka kwa mkuu wa magereza. Wafungwa wote walipanga mstari kisha mmoja baada ya mwingine alipokea kikombe cha uji pamoja na viazi viwili. 

Hatimaye zamu ya Zabroni ilifika ambapo naye alipewa kikombe cha uji na viazi viwili kama ilivyokuwa kwa wafungwa wenzake. Alienda kujiweka kando kabisa na eneo lile la kupokelea uji ili apate kujinafasi ingawa walitangaziwa muda maalumu wa kuhitimisha hilo zoezi la kunywa uji,hivyo Zabroni aliketi chini akaanza na kiazi kabla hajabugia funda la uji. Na baada ya hapo alihitaji kisukumizio ambacho ni uji,kabla hajachukua hicho kikombe ili anywe,mara ghafla akatokea Bluyner akachukuwa uji huo na kisha akaunywa. 

Alikunywa funda la kwanza akanywa la pili akanywa la tatu,uji wote wa Zabroni akawa ameumaliza hakujali ni wamoto kiasi gani. Zabroni alibaki kumshangaa Bluyner, akajiuliza "Ananitafutia nini mimi? Au anataka ugomvi?", wakati Zabro anajiuliza maswali hayo kichwani mwake,Bluyner akacheka nakisha kusema "Usikasirike kijana mzuri. 

Ukikasirike utaonekana mbaya na mwishowe utazikosa sifa zako",akamaliza na kicheko Bluyner,papo hapo akachukuwa na kiazi cha pili cha Zabroni halafu akaondoka zake akimuacha Zabroni na kipande kidogo cha kiazi mkononi. Kwahiyo asubuhi hiyo Zabroni akawa ameambulia kiazi kimoja tu. Aliumia sana.


Punde si punde amri ilitoka kuwa umefika muda wa kwenda shambani kulima, gari mbili za wazi zilikuja. Kwa puta ya hali ya juu,wafungwa walipandishwa ndani ya hizo gari. Baada wote kupanda,dereva alilisongesha mpaka kwenye shamba la magereza ambapo napo wakati wa kushuka walikurupushwa huku wakipigwa mateke,kitendo kilicho pelekea kutokea purukushani za hapa na pale.

***********

Kipindi hayo yanatokea gerezani,upande wa pili Bruno baada kumtafuta Zabroni kwa udi na uvumba bila mafanikio ya kumpata hatimaye aliamuwa kutimkia ndani ya jiji la Dar es salaam. Huko alienda kwa niaba ya kujificha kwa sababu kipindi chote hicho alichokuwa akimtafuta Zabroni, naye vile vile alikuwa akitafutwa na serikali kwa kosa la kutoroka rumande kabla hajapandishwa kizimbani. 

Kwahiyo Bruno alipofika Dar es salaam alibadilisha jina na muonekano wake,ambapo alijiita Mr Rasi. Hakuwa na rasta lakini alijitahidi kuzifuga nywere,zilipokuwa ndefu ndipo akasokota rasta. 

Na hapo ndipo rasmi kijana Bruno akawa Rasta man,jina ambalo liliendana na muonekano wake. Nitaishije ndani hili jiji? Ndilo swali alilojiuliza kijana Bruno ama Mr Rasi. 

Kwani baada kujificha kwa kipindi kirefu nje ya kidogo ya Dar akingojea nywere zake zikue zimuweke katika muonekano mwingine ambao utamfanya mtu asimtambue,hatimaye akawa ameingia mjini sasa ambapo hilo ndilo swali alilojiuliza huku akiwa amesimama moja ya eneo ya kinondoni saa za usiku.

 Muda ambao jiji la Dar es salaam linaonekana kuwa na mishe mishe nyingi utaweza sema mchana ndio usiku na usiku ndio mchana,watu hawalali wanatafuta salali.

Mr Rasi akiwa haelewi jinsi atakavyoishi ndani ya hilo jiji,mara ghafla kando yake alipo simama alionekana binti mmoja wa makamo akingojea daladala. Lakini punde si punde yule binti akasikika akipiga mayowe "Mwizi mwizi mwizii jamani kanikwapulia mkoba wangu",Mr Rasi aliposikia sauti hiyo akatoka kwenye dimbwi la mawazo,akatazama upande ule alio simama huyo binti kisha akautazama ule uma wa watu uliokuwa bize kugombania daladala huku wengine wakiendelea na mambo yao bila kumsaidia dada huyo aliyekuwa akilalama kuibiwa. "Kwanini hawajishughilishi na hili lililotokea?..",alijiuliza Mr Rasi. 

Papo hapo akapotea kama upepo kumfukuzia yule mwizi, punde si punde akasimama mbele yake. Kibaka alistuka wakati huo huo Bruno ambaye ndio Mr Rasi akamwambia 

"Dondosha mkoba chini kisha utimue mbio",kauli hiyo ukilinganisha na namna alivyomtokea,ilimuogopesha yule kibaka ambapo alifanya kama alivyo amrishwa kisha akatimua mbio. Mr Rasi akuchukuwa mkoba huo upesi akamkabidhi yule binti huku akimsihi awe makini. 

Binti alishukuru sana lakini pia alihitaji kumjua jina sababu amemsaudia kwa kiasi kikubwa mno. Ni mgoba ambao ulikuwa na vitu kadhaa vya thamani "Naitwa Mr Rasi",alisema Bruno huku uso wake akiwa ameinamisha chini, kofia aina ya kepu aliyovaa ukiuficha vema uso wake.

"Naitwa Tina, ahsante sana Rasi kwa msaada", alijibu binti huyo. Ni yule Tina mpenzi wa Zabroni,siku hiyo anakutana na mbaya wa mpenzi wake pasipo kujua.

INAENDELEA

Powered by Blogger.