KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Sita (06)

simulizi ya penzi la mfungwa
"Naam! mzee mwenzangu,pole sana nasikia ngedere wanamsumbua sana huko", aliongea mzee Ngurumo. Wakati mzee Fungafunga akajitayarisha kumjibu Ngurumo. Upande wa pili kijana Zabroni alionekana kasimama kando kando ya nyumba,alitazama kulia na kushoto hakuona mtu. 

Giza tayari lilikuwa limeanza kutanda kwa maana hiyo kijiji kilianza kupoa zaidi zilisikika kelele za vijana wa kijiji kijiweni wakibishana mambo mbali mbali,gumzo ilikuwa ni ujio wa mzee Baluguza kijijini hapo. Wapo waliombenza kwamba mzee huyo si chochote si lolote,lakini pia wapo walimnadi ya kwamba huyo mzee ni moto wa kuotea mbali. 

Hivyo hali hiyo ndiyo iliyoweza kuleta ubishi katika kijiji hicho eneo la kijiweni. Kelele zilipasa kila kona hakuna aliyegusia masuala ya siasa abadani bali wote waliongelea ujio wa Baluguza. 

Lakini pindi mada hiyo ikiwa imepamba moto, mara ghafla ulionekana mwanga mkali angani ulio ambatana na moshi. Kwa maana hiyo tayari nyumba ya mtu ilikuwa inateketea kwa moto mapema tu saa moja usiku. 

Taharuki ilizuka, soga la kumnadi mzee Baluguza upesi zilikatishwa ,hima wakakimbia kuelekea kule kunako fuka moshi na moto. Pindi vijana hao walipokuwa wakielekea huko,upande wa pili nyumbani kwa mwenyekiti walionekana mzee Ngurumo,mzee Fungafunga pamoja na mwenyekiti wa kijiji bila kusahau mzee Baluguza. 

Nao walikuwa wakijadili namna gani ya malipo yatakavyo fanyika pindi mzee Baluguza atakapo kamilisha kazi iliyo mleta, ila makubaliano hayo yaliingia dosari baada mama Tina kupasa sauti ya mayowe alipoona moshi mkali ulioambatana na kipupwe cha moto. "Unaona sasa?..mapema tu leo" alisema mzee Ngurumo huku akinyoosha kidole kule ilipokuwa nyumba inateketea.

"Nadhani hapo mzee mwenzangu utakuwa umeamini kuwa hata zile nyumba za awali sio mimi niliyezichoma moto", alidakia mzee Fungafunga akijitetea mbele ya mwenyekiti ambaye hapo awali baada kuchomwa nyumba tano,Mwenyekiti alimuhisi yeye kwamba ndiyo muhusika kwani aliwahi kung'atwa sikio na mzee huyo kuwa yeye ndiyo aliyechoma nyumba ya mzee Ndalo baba yake Zabroni kwahiyo Mwenyekiti akawa hana imani na mzee Fungafunga lakini siku hiyo alimuamini baada kuona nyumba ikiteketea kwa moto. 

Wazee hao waliazipiga hatua kuelekea kwenye ajali hiyo,walipo fika waliwakuta vijana wakishughulika kuuzima moto lakini hawakuweza kufanikiwa. Nyumba iliungua yote huku ndani akiwemo mzee Kadili mchongaji nguli wa mipini kijijini hapo,mzee ambaye aliishi yeye peke yake, hakuwa na familia.


Kwa mara nyingine tena yanatokea majonzi kijiji hapo,kila mwanakijiji roho juu ilihali huzuni nayo ikitawala mioyoni mwao. Walihofia usalama katika kijiji chao, lakini wakati wanakijiji hao wakiwa katika hali hiyo,mara ghafla mzee Baluguza akamuita kando mwenyekiti kisha akasema "Hivi yule kijana tuliyepishana mude ule yupo hapa? ", Mwenyekiti hakujibu upesi, alikaa kimya huku akijaribu kumkumbuka. Akamkumbuka na ndipo alipo tazama upande ule waliosimama vijana wengi akamuita mmoja wao, naye alitii wito wa mwenyekiti "Zabroni yupo hapa? ..", kijana huyo aliyetii wito wa mwenyekiti aliulizwa.

"Hapana ", alijibu kijana huyo,jibu hilo alilisikia na Mzee Baluguza.Akalizika nalo akatikisa kichwa halafu akamuuliza tena Mwenyekiti "Unapajua anapoishi?..", lakini kabla Mwenyekiti hajamjibu Baluguza, ghafla ilionekana mwanga mkali angani na moshi mwingi. Kiashiria hicho kilimanisha kuwa tayari kuna nyumba nyingine inateketea,Mwenyekiti aligeuka akatazama kule akaona mwanga ule unatokea mahali ilipo nyumba yake. "Lahaulla nyumba yangu", alitaharuki mwenyekiti huku akiweka mikono kichwani alijua fika nyumba yake inateketea.

Haraka sana vijana wa kijiji wakajigawa magundi mawili, kundi moja liliendelea kuuzima moto kwenye nyumba hiyo inayoteketea, na kundi lingine lilielekea kule inapoungua nyumba nyingine ambayo mwenyekiti aliamini kuwa ni nyumba yake. Mzee Baluguza aliposikia maneno ya mwenyeji wake ambaye ni Mwenyekiti, haraka sana akapotea eneo hilo akaibukia nyumbani kwa Mwenyekiti. Alikuta nyumba ya mwenyekiti ipo salama, ila nyumba nyumba ya jirani yake ndiyo iliyoonekana ikiteketea. 

Mzee Baluguza akastaajabu kumuona mchomaji akiendelea kufyatua njiti. Mtu huyo hakuwa mwingine ni Zabroni ambaye baada kuchoma nyumba hiyo aliamua kujibadilisha umbile lake akachukuwa umbile la mzee Ngurumo. 

Hivyo alipokuwa katika umbile hilo la mzee aliendelea kufyatua njiti kuchochea moto wakati mzee Baluguza akimtazama mara mbili mbili mwishowe akakumbuka mtu huyo kamuacha kule alipotoka, aliingiwa na hofu akaona ni mchezo mchafu anachezewa. Aliguna kisha akajisemea "Nimekupata ila siku zako zinahesabika nitakukomsha"., maneno hayo mzee Baluguza alijisemea ndani ya moyo wake huku Zabroni naye akiwa na umbile la mzee Ngurumo alionekana kuishia zake kwenye giza totoro akiacha nyumba ikiteketea vile vile akimuacha mzee Baluguza akiishia kumsindikiza kwa macho tu wakati huo akifahamu fika kijana huyo anauwezo wa ajabu sana. 

Na pindi Zabroni alipokuwa njiani akitembea kwa kujiamini katika umbile la mzee Ngurumo, mbele yake walionekana wazee wa wawili wakitembea kuelekea kule anakotokea yeye wazee hao ni mwenyekiti wa kijiji sambamba na mzee Ngurumo mwenyewe!


Lakini kabla kijana Zabroni hajawafikia wazee hao,machale yalimcheza. Bila kuchelewa alijibadilisha akawa katika sura yake ya kawaida kisha akapotea maeneo hayo ambapo mzee Ngurumo na mwenyekiti walipo fika eneo lile alilopotelea Zabroni kamwe hawakuweza kumuona,zaidi walijikuta wakihisi joto ambalo nalo hawakuweza kulitilia maanani kwani walikuwa na haraka za kwenda kutazama nyumba ya nani inaungua. 

Mwenyekiti alipo kuta nyumba yake ipo salama alifurahi sana lakini pia hakusita kutoa pole kwa jirani yake aliyechomewa nyumba,wakati huo huo mzee Baluguza naye alionekana kuinamisha uso wake chini akitafakari jambo fulani. 

Lakini punde si punde mzee huyo alitoka kwenye dimbwi la tafakari baada kuguswa bega na mwenyekiti,Baluguza aligeuka akakutana na uso wa Mwenyekiti. "Kulikoni mwenzetu naona umetukimbia kimaajabu" Alisema Mwenyekiti akimwambia mzee Baluguza, kwa sauti ya unyonge huku akiutazama ule moto unaolanda kwenye nyumba alisema "Hii ni kawaida yangu mzee mwenzangu,naona hakuna muda wa kupoteza. Kesho naomba uitishe mkutano wa kijiji ili nimuumbue mbaya wenu " alisema mzee Baluguza.

Kesho yake palipo pambazuka mbiyu ya kijiji ililia, taarifa zikagonga masikioni mwa wanakijiji kwamba kutakuwa na mkutano wa wakijiji siku hiyo. Hivyo haitakiwa mwanakijiji yeyote akose kuhudhulia. Mbiyu hiyo aliisikia na kijana Zabroni ,akiwa kitandani kwake. Akajiuliza "Wanamikakati gani mbweha hawa?..ni lazima na mimi nihudhulie ili nijue wanamikakati gani ",alisema Zabroni huku akisimama kutoka kwenye kitanda chake,alichukuwa bukta yake iliyokuwa imekatwa miguu kwa kuzidiana kisha akaelekea mahili yalipo makaburi ya wazazi wake. 

Hapo Zabroni alienda kwa niaba ya kuyasafisha kabla muda wa mkutano haujawadia, na pindi kijana huyo akifanya hicho kitendo upande wa pili kijiji kilionekana kuzizima majonzi. 

Wanakijiji walikuwa wakisikitika kuwapoteza wanakijiji wenzao waliokufa usiku wa jana kwa ajari ya moto,hali hiyo ikawafanya kuwa na shauku kila mmoja kufika mkutano ni. Hali hiyo ilimpelekea mazishi kufanyika mapema sana ili watu wawahi,haikuwepo haja tena ya kukaa msibani mpaka jioni kwani hali iliyokuwepo sasa ilitisha kila familia haikuwa na amani nyumbani kwake,wazee kwa vijana wote walianza kuogopa. Hivyo siku hiyo waliposikia mbiyu wakaamini kuwa huwenda mbiyu hiyo ikawa na jambo la heri katika kijiji chao.

Na hatimae Muda uliwadia sasa,watu walianza kukusanyika mkutanoni. Kwa muda wa nusu saa wanakijiji wote walikuwa wamefika ingawa si wote kwani kuna baadhi walikuwa bado wanajiandaa kuanza safari,ilihari wengine tayari walikuwa wameanza. Vile vile Upande mwingine Zabron naye alianza safari ya kujongea kwenye mkutano huo,nia na madhumuni kutaka kusikiliza mikakati gani inayo endelea kijiji hapo. 

Na wakati Zabroni alipokuwa akitembea njiani,Ghafla mbele yake akaona kamba. Alipoiona kamba hiyo akajipapasa kwenye mfuko wa bukta yake akakuta kibiriti. Aliachia tabasamu baada kujihakikishia kwamba kibiriti anacho upesi akaichukuwa kamba hiyo akaenda nayo mpaka kwenye nyumba moja ambayo ya mzee Ngurumo. Alipo fika hapo alitazana kulia na kushoto kuangalia usalama wake akagundua hakuna mtu yoyote mahali hapo. 


Pasipo kupoteza muda aliifunga kamba kwenye fito ya nyumba kisha akailaza hatua mbili za mtu mzima kutoka mahali ilipo nyumba. Kwa mara nyingine tena akarudia kutazama kila pande, alitazama kulia na kushoto pia nyuma yake hakuona mtu,haraka sana akachukuwa nyasi kavu akizisambaza kidogo juu ya kamba ile kisha akafyatua njiti, nayo ikaripua moto akaishusha kwenye zile nyasi nazo zikanasa moto ambao pole pole ulitembea kwenye ile kamba ya kitambaa. Kamba ambayo pia ilikuwa pana na ndefu kwa kiasi chake. 

"Mchezo umekwisha", alijisemea ndani ya nafsi kisha akaondoka kuelekea kwenye mkutano wakati huo huo huo mzee Baluguza alionekana kutoka ndani ya nyumba ya Mwenyekiti huku mkononi akiwa na jungu ambalo lilikuwa na makorokoro mengi ndani yake, wanakijiji walitulia kimya mpaka mzee huyo anafika kwenye umati wa wanakijiji. 

Alipo fika alisimama akitaka kusema jambo,lakini kabla hajasema akamuona Zabroni naye akijisogeza kwenye mkutano. Mzee Baluguza alimkazia macho ila mwishowe akajifanya kupotezea ili mtukutu Zabroni asijishuku. Zabroni alifika mkutanoni akaungana na wenzake alitulia chini akisubiri kujua kipi kinacho taraji kutokea. Muda huo huo Baluguza akamnong'oneza Mwenyekiti, akamwambia "Nenda kanichukulie nyayo za yule kijana"

"Kijana yupi? .."alihoji Mwenyekiti huku akiwa makini kumsikiliza mtalamu Baluguza.

INAENDELEA
Powered by Blogger.