KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Kumi na Nane (18)

simulizi ya penzi la mfungwa
Naam! Siku zilisonga,jina Mr Rasi likiendelea kujizatiti kwa kijana Bruno. Ilihari upande wa pili napo gerezani baada Zabroni kuchoshwa na mnyanyaso kila uchwao kutoka kwa Bluyner,hatimaye siku moja akaamuwa kutangaza pambano. Taarifa hiyo ilipomfikia muhusika mwenyewe kiongozi Bluyner alifurahi sana,kwa maana ndicho alichokuwa akikitafuta kwa muda mrefu. 

Na wakati Bluyner akifurahia taarifa hiyo, upande wa Zabroni yeye alipania siku hiyo ya pambano ndiyo siku ambayo atakayotumia kutoroka gerezani huku akijanasibu kuwa endapo kama atafanikiwa kurudi uraiani atabadilisha jina hali ya kuwa kimya kimya akiwasaka wabaya wake.


"Haya manyanyaso siwezi kuyavumilia,mimi ni mwanaume na yeye pia ni mwanaume. Sasa kwanini niogope? Iweje niitwe mzuri na mwanaume mwenzangu,ama kwanini ajione yeye ni mwamba humu ndani eti kisa amepewa cheo cha kutuongoza? Hapana. 

Mimi ni Zabroni, hivyo kile nilicho kisimulia itabidi nikiweke hadharani ili heshima itawale",alisema Zabroni ndani ya nafsi yake,muda huo akiwa amelala na wafungwa wenzake. 

Baada kusema hayo alijishika kwenye msuri wa mkono akakumbuka hana hirizi ambayo ingempa walau nguvu. Hapo sasa ndipo kumbukumbu ilipomjia zaidi,akakumbuka namna gani Veronica alivyomteka kimapenzi mpaka kupelekea kupoteza dawa yake ambayo ingemfanya asikamatike kirahisi. Zabroni hakuishia hapo,alikumbuka pia kifo cha Bukulu ambaye alikuwa ni rafiki yake kipenzi. 

Neno la mwisho ambalo Bukulu alimwambia Zabroni kabla hajakata roho ni kwamba Bruno ndio aliyemfanyia hicho kitendo,kwa maana hiyo Zabroni alijua fika kuwa Bruno karudi uraiani kwani alidhani kwamba baada kumsababishia msala basi atakuwa anehukumiwa jela kitu ambacho kilienda kinyume na jinsi alivyodhania. Bruno yupo,na ndio huyo aliyeamua kujibadisha jina na kujiita Mr Rasi.


Pumzi alishusha Zabroni mara baada kutoka kwenye dimbwi la mawazo,kisha akaanza safari ya kulitafuta lebe la usingizi ambalo kiukweli lilimuwea ngumu kumjia ingawa mwishowe alifanikiwa japo alichelewa sana.

Kesho yake aljajiri kama ilivyo ada,kengere ya kuwamsha wafungwa iligongwa. Wafungwa wote walikurupuka haraka sana kukimbilia mstarini kasoro Zabroni ambaye yeye alikuwa bado amelala kwa sababu usiku wa jana alichelewa kulala kwahiyo alikuwa akimalizia usingizi aliokuwa nao,asijue tayari kumekucha. Wafungwa walihebu namba,na hapo ndipo namba ya Zabroni ilipo kosekana.

 Amri ikatoka kwa mkuu wa gereza,amri ambayo ilimtaka nyampala Bluyner akakague kila chumba wanacholala wafungwa. Bluyner kwa madaha huku akitunisha mbavu zake,alizipiga hatua kwenda kukagua chumba kimoja baada ya kingine ili kujihakikishia kama kuna mfungwa kasilia ama katoroka. Hatimaye akiwa nje alimuona mfungwa mmoja akiwa amelala,aliingia ndani akamkuta ni Zabroni.

Alichuchumaa kisha akamtingisha kitendo ambacho kilimkurupusha Zabro kutoka usingizi akakutana na uso wa adui yake ambaye ni Bluyner. Bluyner akacheka kidogo kisha akasema "Naona unalala tu kama upo kwa mama yako" alisema Bluyner, maneno ambayo yalimfanya Zabroni kumkumbuka marehemu mama yake. 

Alijitahidi kufanya juu chini ili akamtibie mama yake ugonjwa aliokuwa akiumwa ugonjwa wa kupooza,lakini bahati mbaya juhudi hizo zikawa zimeota mbawa baada mama yake kufia ndani kwa kuteketezwa nyumba yao. 

Hivyo nikama Bluyner aliweza kumkumbusha Zabroni machungu aliyokuwa ameanza kuyasahau kichwani mwake,hasira za ghafla zilimjia ambapo alikunja ngumi nzito kisha akamtupia Bluyner. Bluyner aliiona,akaikwepa kisha akasimama ili amuadabishe vizuri. 

Zabroni naye akawa si haba, alisimama kidete ili akabiliane naye.
Wakati hayo yanaendelea kati ya Zabroni na Bluyner,upande wa pili alionekana Tina akiwa sebuleni na shangazi yake wakipiga zogo. Tina alisema "Yani Ant nikwambie kitu?.."
"Niambie wala usijali "
"Kweli nimeamini siku zote usimdhanie mtu kutoka na matendo yake"
"Ni kweli ulicho kisema Tina,haya nieleze unamaana gani kusema hivyo?.."
"Maana yangu ni kwamba. Kuna siku fulani nilikuwa kwenye kituo cha daladala nasubiri gari ili nirudi nyumbani,sasa bwana akatokea kibaka akanipokonya mkoba wangu akakimbia nao. 

Nilipiga kelele kuomba msaada lakini hakuna mtu hata mmoja aliyenisaidia ila mkaka mmoja hivi ambaye yani kimuonekano alionekana yupo yupo tu..alimkimbiza yule kibaka akamkamta akanirudishia mkoba wangu. 

Kiukweli nlishukuru sana sijui hata nisemeje dah"
"Daah hapo sasa nimekuelewa "
"Ndio hivyo we unadhani yule kibaka angekimbia na hela zote zile ingekuaje?.."
"Mmh ndio siku ile nilipokutuma ukanitolee pesa Bank?.."
"Ndio siku hiyo hiyo"
"Laah! Mungu wangu, enhe huyo mtu aliyekusaidia ulimpa hata ya maji?."
"Hapana sijampa lakini usijali ant. Siku zote milima haikutani ila binadam hukutana. Nina uhakika ipo siku nitakutana naye nitampa japo kidogo ili akafanyie mambo yake.."
"Huo ndio uugwana mwanangu sawa?.."
"Sawa ant"
"Ulimuuliza jina lake?.."
"Ndio kaniambia anaitwa Mr Rasi"
"Anhaa sawa hapo nadhani itakuwa rahisi sana kumfahamu pindi mtako kutana. Haya chai tayari sijui utakunywa ama utawangojea Wenzako"
"Ngoja niwasubiri tu,kwani wameenda wapi? "
"Angel kaenda kwa rafiki yake mara moja, Gift naye sijui kaenda wapi. 

Maana anatembea sana siku hizi"
"Doh basi ngoja ninywe, sijui watarudi muda gani"
Baada ya maongezi hayo,shangazi yake Tina alifurahi sana kumuona Tina akiwa katika hali ya furaha. 

Kwani Tina alipofikishiwa taarifa ya kuhusu kifo cha wazazi wake alijikuta muda wote akiwa mnyonge hana furaha,kiasi kwamba hatakama umchekeshe namna gani abadani hacheki zaidi ya kuachia tabasamu kidogo na kisha kurudi katika hali yake ya ukiwa. 

Lakini siku hiyo Tina alionekana kuwa katika hali tofauti kabisa kitu ambacho kilimfanya shangazi yake kufurahi akiamini kwamba tayari binti huyo anaanza kusahau yaliyopita.

Kwingineko ule ugomvi wa Zabroni na Bluyner uliingiliwa kati na askari ambao waliwaamulia,haikuwa kazi nyepesi ila walifanikiwa. Bluyner alionekana kumkunjia uso Zabroni ilihari Zabro naye akionekana kumkunjia uso Bluyner ingawa tayari muda huo Zabrini alikuwa akivuja damu puani na mdomoni,alizidiwa nguvu na ujanja katika hilo pambano. Na endapo kama askari wasinge ingiliaa kati basi Zabroni angekiona cha mtema kuni.

Siku hiyo Zabroni hata uji hakunywa,moyo wake ulikuwa umefura hasira. Mawazo mfurulizo yalilindima kichwani mwake huku damu kama maji ikimtoka puani,hivyo punde si punde alizidiwa akaanguka chini akapoteza fahamu. Alizinduka akiwa Hospital akiwa ametundikiwa dripu ya damu na maji,mkononi akiwa amevishwa pingu huku kando kando yake amesimamiwa na askari mkononi akiwa na bunduki. Askari huyo alikuwa mzee wa makamo. 

Zabroni akastuka kujikuta katika mazingira hayo kwa sauti ya chini akamuuliza Askari huyo aliyepewa jukumu la kumlinda"Nimefikaje mahali hapa?.."

Askari huyo aiimtazama Zabroni,hakika alitia huruma. Akajibu "Baada ya ule ugomvi ulitokwa damu nyingi iliyokupelea kupoteza fahamu ndio maana upo mahali hapa unapatiwa huduma",Mara baada kujibiwa hivyo alinyamanza kidogo kisha akarudia kusema "Sawa asante kwa jibu lako lakini naomba kufahamu kwanini huyu mtu anafanya matendo kama haya halafu mnachukulia kawaida? Je, ikowapi haki ya mfungwa kama kunamanyanyaso kama haya",Hapo huyo Askari hakumjibu Zabroni bali alikumbuka siku kadhaa zilizopita jinsi Bluyner alivyomtishia kumpiga. Ukweli Bluyner alionekana kuwa tishio kwa wafungwa wenzake hata na Askari baadhi pia.

"Loh huyu binadam sijui anaroho gani, kiukweli hata mimi tabia yake nimeichoka. Nafikiri siku nikihamishwa hapa nitafurahi sana ",alijibiwa Zabroni na askari baada kukumbuka jinsi alivyonusurika kupigwa na Bluyner.

"Upo tayari kuona mtu huyu anaibishwa?..",alihoji Zabroni.
"Unamaana gani?.
"Maana yangu ni kwamba huyu mtu nimuadabishe"
"Acha utani,umenusirika kifo halafu leo hii umuadabishe?..", alijibu Askari huyo huku akimtazama kwa jicho la huba mtukutu Zabroni. Zabroni akakaa kimya kidogo kisha akasema.

"Ndio kila kitu kinawezakana ila kama utanisaidia jambo moja"
"Jambo gani?..", aliuliza Askari huku akimkodolea macho Zabroni. Zabroni akajibu "Wakati rasmi nakabidhiwa jezi za gerezani nilivuliwa hirizi yangu,ambayo ndio kila kitu kwangu kujihami na maadau. Sidhani kama itakuwa imetupwa,naimani itakuwa imehifadhiwa tu"
"Enhe kwahiyo? .."

"Naomba ufanye juu chini ukanichukulie kisha unikabidhi tafadhali sana",alijibu Zabroni safari hiyo akiongea huku machozi yakimtoka. Askari huyo aliyemsimama kiukweli alimuonea huruma. Akamwambia "Je, unauhakika utaweza? Nipotayari kukuletea hicho kitu chako"
"Nitaweza asilimia mia moja"
"Sawa ",alijibu Askari huyo aliyepewa jukumu la kumrinda mfungwa Zabroni wakati huo anafanyiwa matibabu.

Baada ya siku nne Zabloni tayari alionekana kuwa sawa kiafya kimwili na akili pia,siku hiyo anarudi jela ilikuwa shagwe na vifijo kutoka kwa wafungwa wenzake. Pole kwa wingi zilimfikia Zabroni kwa yaliyomkumba huku wengine wakimsifu kwa kuamua kujitosa kupigana na nyampala Bluyner kijana ambaye ni tishio kwa kila mfungwa. 

Kitendo alichokifanya Zabroni kilikuwa cha kishujaa sababu tangu jamaa huyo ahukumiwe jela hakuna mfungwa hata mmoja aliyejaribu kukabiliana naye lakini Zabro alithubutu japo alichezea kichapo. "Zabro...Zabro..Zablo..Zabrooooni",Ni shangwe zilizokuwa zikitoka kwa wafungwa ambao walionyesha kufurahishwa na ujio wa Zabroni. 

Zabroni alibaki kusimama huku akiachia tabasamu pana,alipogusa upande bega lake alipofunga hirizi yake mkono wa kulia akagundua hirizi ipo. Haraka sana akatazama upande wa kushoto umbao walionekana Askari magereza wanne akiwemo na yule aliyemsaidia kumpatia hirizi,Askari huyo akamnyooshea Zabroni dole gumba akimanisha ishara kuwa mambo ni safi. 

Naye Zabroni akajibu kwa kuitikia kwa kichwa kisha akajiunga na wafungwa wenzake,wakati huo moyoni akijisemea "Veronica Veronica Zabroni nakuja kuifanyia upasuaji sehemu hiyo iliyopoteza nguvu zangu sababu hicho ndio chanzo cha haya yote "

ITAENDELEA

Powered by Blogger.