KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Tisa (09)

simulizi ya penzi la mfungwa
Zabroni alipotea baada kufanya unyama ule,alimuacha mama mjamzito tumbo lake likibubujika damu baada kutolewa vijusi vilivyokuwemo kwenye tumbo hilo,ulikuwa ni unyama ulio pitiliza kipimo kiasi kwamba binadamu mwenye roho nyepesi hawezi kufanya hicho kitendo.

Upande wa pili yule jamaa alipo maliza mikakati yake alianza safari kumfuata mkewe huku moyoni akiwa na hofu kwani mapigo ya moyo wake kuna muda yalikuwa yakimuenda mbio pia wasiwasi nao ukimtawala kila mara,alijiuliza maswali kuhusu hali hiyo ambayo ningeni kabisa kuwahi kumtokea. 

Lakini jamaa huyo alipiga moyo konde kisha akaanza safari,kabla hajakimaliza kijiji ghafla akasikia mzee mmoja akimshuhudia mzee mwenzake kitu alichokiona huko porini. Mzee huyo alisema "Ama hakika tunako elekea sasa hii dunia imefika mwisho"

"Kwanini tena mzee mwenzangu? ..

"Dah huwezi amini nimekuta mama mmoja pori lile la miti mingi kapasuliwa tumbo,vile vitoto sasa vimetundikwa juu kama mishikaki " alijibu huyo mzee huku akifatia na sikitiko.

"Lahaulla..Mungu tutazame waja wako sisi mmmmh ", alisikika mzee msimuliwa akisema maneno hayo kwa sikitiko, na wakati wanasemazana hayo, kijana yule mwenye mke aliyetumbuliwa tumbo alistuka bila kupoteza muda alitimua mbio kuelekea huko ili akatazame kama ni mkewe ndio kafanyiwa hicho kitendo. Alipofika alimkuta ni mkewe kauliwa kikatili, hakika alilia sana hasa hasa alipovitazama vijusi vile vilivyo ning'inizwa juu kwenye mti kama mshikaki. Hali hiyo ilimpelekea kudata, uchungu wa kufiwa na mkewe aliyempenda kwa dhati ulimfanya kuwa kichaa. 

Dhambi na dumu nzito ikazidi kutanda juu ya kijana Zabroni,alifanya hayo akiamini kwamba analipa kisasi juu ya kifo cha wazazi wake. Habari ya hayo mauaji ilisambaa kila kona,na kila aliyeipata alihuzunika huku baadhi yao wakijiuliza ni roho gani aliyonayo muuwaji huyo?. Majibu alikosa,na baadhi ya watu kutoka vijiji vya jirani walitamani japo kwa dakika sifuri wamtie machoni mtukutu huyo. Na mara baada ya kufanya mauaji hayo,alitulia kwa takribani wiki mbili. 

Wanakijiji walipata ahueni wakiamini kuwa huwenda Zabro kauliwa kutoka na dhambi zake,lakini imani hiyo punde ilitoweka baada kuchomwa nyumba nyingine usiku wa manane. Na hapo ndipo hofu ilipo rudia kutanda kunako mioyo yao. Kwa kuamini hilo,mzee Fungafunga ambaye ndio chanzo hasa ya matatizo hayo aliingiwa na hofu aliamini kuwa muda wowote naye zamu yake itafika. Na wakati huyo mzee akiamini hilo jambo kutendeka muda wowote, upande wa pili kijiji jirani. 

Kijiji ambacho kilionekana kuchangamka kulingana na mishe mishe zake,lilionekna kundi la vijana wakicheza kamali. Kamali hiyo kimuonekano ilikuwa ya mazingaombwe. Unapewa lingi ndogo unailipia pesa kisha unaambiwa uchague mahala pakuirusha kwenye mazaga zaga waliyosambaza. Palikuwa na pesa zaidi ya ile unayoliyolipia lingi, vile vile palikuwa na juisi soda na mazaga zaga mengine ambayo ukiirushe ile lingi iwezekanike kuvivaa. 

Mchezo huo uliandelea kwa vijana wa pale,wengi walikosa kiasi kwamba baadhi yao iliwapelekea kununua lingi nyingi wakiamini kuwa huwenda wakafanikiwa. Lakini mambo bado yaliendelea kuwa vile vile bado waliangukia pua,wenye moyo mwepesi waliondoka zao huku wenye roho ngumu wakizidi kukomaa.

Na wakati kamali hiyo inaendelea,ghafla walionekana vijana wawili wakiwa na mabegi yao mgongoni. Vijana hao wa makamo walionekana ni wageni katika hicho kijiji,kwani nyuso zao zahili shahili zilionyesha. Walipokuwa katika pitapita yao waliuona mchezo ule wa kamali uliokuwa unaendelea. 

Kijana mmoja ambaye aliitwa Madebe alimshika bega mwenzake kisha akasema "Bruno,pesa imetuishia. Kiukweli iliyobaki haitoshi halafu istoshe bado tunasafari ndefu. Vipi tufanyeje?..",alisema Madebe huku akikodolea macho upande ule uliojaa watu wacheza kamali pamoja na watazamaji.

"Doh ni kweli kaka,lakini unadhani tutafanyaje sasa"

"Hivi ile hirizi ipo humo kwenye begi?.." alihoji Madebe.

"Ndio ipo" alijibu Bruno.

"Sawa hebu nipe tusogee pale Kwenye kamali,unajua huu mchezo wanatia kiini macho,kwahiyo kwa kuwa wao wanafanya ujinga acha na sisi tufanye upumbavu", alisema Madebe. Bruno akaangua kicheko huku akifungua zipu ili ampe kaka yake hirizi. 

Alipo mkabidhi, Madebe aliivaa kisha akasogea eneo lile, alilipia lingi. Safari ya kwanza aliirusha kwenye pesa,akawfanikiwa. Akarudia kurusha kwenye pesa lingi ya pili,nayo vile vile akifanikiwa. Hapo sasa taita akaona Madebe anawaumbua,upesi alimuita kando kisha akasema "Ndugu naomba tusihalibiane kazi,nina familia inanitegemea sawa. 

Kwahiyo naomba upotee hapa mara moja kabla hatujahalibiana siku" Taita kiongozi wa kamali ile aliongea kwa sauti ya kunong'ona huku uso wake akiwa ameukunja. Madebe alipo ambiwa maneno hayo hakutaka kubishana naye,alimuita mdogo wake kisha wakaondoka zao wakati huo nyuma yao wakimuacha Taita anawasindikiza kwa macho.

Madebe na Brruno tayari walikuwa na pesa ya kuanzia huko wanako elekea, walikwenda kwenye mgahawa kula chakula kabla hawajaendelea na safari ya kuelekea kijiji kilw kinacho endelea maafa kwa niaba ya kutafuta vibarua ikiwa kama njia ya utafutaji wa pesa. Walanguzi. 

Wawili hao walipokuwa mgahawani, ghafla akaingia Zabroni . Hakutaka kuongea na mtu zaidi aliketi kisha akaagiza chakula akala, alipomaliza akaondoka zake bila kulipa. Hiyo ndio ilikuwa tabia yake sasa baada kujiona ni tishio kila pande. 

Ni tabia ambayo iliwakera mama ntilie wa kijiji kile lakini kutokana sifa mbaya na yakutisha aliyokuwa nayo Zabroni,mama ntilie hao walimuogopa sana kwa maana hiyo hata pesa ya chakula walikuwa hawamdai. Ila siku hiyo ilikuwa siku tofauti kidogo kwa mama ntilie huyo,alisikika akisema kwa jazba "Mijitu mingine bwana. Akha yanakera sio siri "

"Kwanini mama?..",alihoji Madebe baada kusikia mama huyo akilalama.

"Yani we acha tu,huyu jamaa hafai hata kidogo. Anachoma nyumba za watu anauwa bila hatia yani sijui anaroho gani huyu mtu. Ubabe na yeye na na ubabe sijui kwanini serikali inaendelea kumuangalia. ", Madebe na Bruno walistuka kusikia habari hiyo, ni habari ambayo iliwacha midomo wazi Kiukweli.

"Kwahiyo unataka kusema kashindikanika?..", kwa taharuki Bruno aliuliza.

"Kabisa hawezekaniki,anatumia dawa"

"Daah poleni sana", alimaliza kwa kusema hivyo Madebe kisha wakalipia chakula walicho kula wakaendelea na safari yao. Walitumia saa moja na nusu kufika,walipofika walipigwa na butwaa baada kukuta nyumba zikiwa majivu huku nyinginezo zikisalia kuta. Vilio kila kona kijijini hapo,Madebe akamgeukia Bruno kisha akasema "Hii hali inatisha sana, na bila shaka huyu ndio yule mshenzi tuliye ambiwa na mama ntilie..."

"Kweli kabisa kaka, je tuchukue hatua gani sasa maana hii hali yatisha ujue" alijibu Bruno huku akiangaza kila kona ya kijiji.

"Daah! Nafikiri ni kupambana naye tu hakuna namna"

"Je, tutampataje?.." ,Madebe aliingiza mkono mfukoni akatoa kitambaa cheusi chenye fundo akafungua fundo ambalo lilikuwa na unga mweusi. Unga huo aliupakaza kwenye kiganja kisha akasema "Tazama kiganjani kwangu ", Bruno akatazama alimuona Zabroni akiwa kwenye makaburi mawili,makaburi ya mama na baba yake. "Umeona? Huyu jamaa hapa ndio makazi yake. Sasa mdogo wangu lazima tule nage sahani moja..tuombe kwanza kibali cha kuishi kijijini hapa kisha tufanye kazi yetu kwa utulivu", aliongea Madebe,kijana aliyetunikiwa miradhi ya ndagu kutoka kwa marehemu babu yake.

INAENDELEA

Powered by Blogger.