KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Nane (08)

Mpiga mbiyu alipo sikia sauti hiyo alitimua mbio huku akipiga kelele,watu waliokuwa wanaishi jirani na eneo hilo walikurupuka na kutoka nje ili kuja kushuhudia nini hasa kilicho mkuta mpiga mbiyu huyo. Walipigwa na butwaa baada kuuona mwili ukining'inia juu kwenye mti huku damu zikivujia kwenye shingo, walipo mtazama vizuri waligundua kuwa mtu yule ni mzee Baluguza.

Walichoka sana,pumzi walishusha,hofu nayo ikiendelea kutanda mioyoni mwao ilihali upande wa pili mpiga mbiyu wa kijiji alikuwa akiendelea kukimbia kuelekea kwa Mwenyekiti,alipo fika akasema "Mwenyekiti,kama kijiji kuchafuka basi hiki kijiji tayari kimechafuka haswaa. 

Unahabari kama mzee Baluguza kanyongwa kwenye mti ule tunapo fanyia mkutano?.." alisema mpiga mbiyu huku akihema mithiri ya faru aliyekuwa akiukimbia mtutu wa bunduki ili usimzuru. Mwenyekiti pamoja na watu wengine ambao tayari walikuwa wamefika nyumbani hapo kwake kila mmoja alipigwa na butwaa kiaina yake,bila kupoteza muda walinyanyuka wakaenda kushuhudia.

Upande mwingine,asubuhi hiyo na mapema mama Tina ambaye ndio mke wa mzee Fungafunga alimuita binti yake ili aseme naye jambo kabla hajaelekea msibani. "Tina mwanangu"

"Abee mama" Tina aliitikia huku akijikusanya vizuri kutoka kitandani ili aweze kumsikiliza mama yake. Mama Tina aliongeza kusema "Umeamkaje?.."

"Nimeamka salama,shikamoo"

simulizi ya penzi la mfungwa
"Malakhabaaa,Tina leo mimi nataka kusema na wewe. Nakumbuka uliwahi kuniambia kuwa unamchumba hapa kijijini, na mchumba mwenyewe ni yule kijana mtukutuku. Si ndio? Hivi Tina,uzuri wako huo unaweza kuolewa na yule kijana ambaye hana hata chembe ya huruma? Tazama mauaji anayo yafanya kwa kuchoma nyumba za watu,wakubwa kwa wadogo wanakufa. 

Kiukweli mimi kama mama yako sitaki yule kijana awe mkwe wangu ", aliongea mama Tina wakati huo Tina alikuwa amejiinamia. Tina alikaa kimya ila mwishowe akajibu "Sawa mama nimekuelewa lakini tatizo sio mimi bali ni moyo,moyo wangu umempenda Zabroni mama nitafanyaje mimi", jibu la Tina, halikumfurahisha mama yake, ghafla akakunja uso na kisha akamuuliza kwa sauti kali "Kati ya mimi na Zabloni ni nani bora?..", 

kabla Tina hajamjibu mama yake,Ghafla mlango uligongwa kisha ikasikika sauti ya mzee Fungafunga ikisema "Mama Tina na mwanao hebu njooni hapa mara moja" Tina akavaa nguo haraka haraka akatii wito. 

"Jamani mnahabari lakini? Mzee Baluguza kauwawa", "We unasema kweli?..", mama Tina pamoja na binti walistuka kusikia taarifa hiyo,punde si punde akamtazama mwanaye kisha akamwambia "Unaona? Haya sasa nambie sisi wazazi wako tunaweza kuwa na mkwe muuwaji kama yule? Loh! Yule sio ameingiliwa na shetani, Zabroni ni shetani"

"Tina..Tina...Tina. yani nikikufuma upo na yule mtu? Hiyo pua kama kinu nitaing'oa pumbafu toka mbele yangu mwanahidhaya mkubwa wewe", alidakia mzee mzee Fungafunga, aliongea kwa sauti kali juu ya suala la binti yake kuwa na mahusiano na kijana Zabroni. Haraka sana Tina akarudi chumbani kwake huku akilia,aliona wazazi wake wanamkosesha amani ya moyo maana kupenda sio mchezo.

Wakati hayo yanajili nyumbani kwa mzee Fungafunga, kwingineko vijana wa kijiji wenye hasira kali walishika siraha mbali mbali kisha wakaelekea nyumbani anapoishi Zabroni,kwa dhumuni la kumuuwa kabisa. Ukweli vijana hao walijitoa muhanga kwani ni rahisi sana mwanamke kuruka tikitaka kuliko kumuuwa mtukutu Zabroni, ila walipofika hawakumkuta zaidi walichoma nyumba huku wakijizatiti kwamba lazima na wao walipe kisasi kwani wamechoka kuwa wanyonge. 

Jioni Zabroni aliporudi kutoka shamba alistaajabu kuona nyumba yake ikiwa imeteketezwa na moto. Hapo sasa hasira zikampanda zaidi ya! Ilihari baadhi ya wanakijiji walipo gundua kwamba Zabroni kachomewa nyumba haraka sana walihama kijiji kwani waliamini kijana huyo hatomuacha mtu salama abadani. Na wale wasio kuwa na pa kwenda waliomba Mungu tu ili kijana huyo asifanye kitu chochote kibaya,ukweli kijiweni sasa pakawa hapakaliki. Watu waliogopa kulala majumbani mwao,walilala nje kama mateja wa Kariakoo. 

Yote hayo kuogopa kufia ndani na familia zao,ukweli Zabroni alitishia maisha ya watu yote hayo akifanya ikiwa kama kulipa kisasi juu ya kifo cha wazazi wake waliokufa kwa pamoja wakiuliwa na mzee Fungafunga aliyechoma nyumba huku msibani napo wakijitokeza wanakijiji wachache,wengi hawakujitokeza kwa madai kwamba wazazi wake hawana utu wala ushirikiano na wanakijiji wenzake. Uzushi huo ulitokea baada mmoja wa mwanakijiji kunyimwa kibarua cha kulima na mzee Ndalo. Baba yake Zabroni. 

Kwani marehemu mzee Ndalo alikuwa na mashamba mengi ila ilikuwa nadra kutoa vibarua kwa walima kwa mikono,aliingiza Trekta lakini baada mkewe kuugua ugonjwa wa kupooza alijikuta akifirisika kila leo,akihangaika huku na kule kutafuta tiba. Mwishowe aliishiwa kabisa,na ndipo ilimbidi akope fedha ambayo mwishowe ilimghalimu.

"Mmmh", siku moja aliguna Zabroni, ilikuwa yapata usiku wa saa mbili muda huo alikuwa katika matembezi yake huku akitafuta nyumba ya kuchoma usiku huo,ghafla alisikia bwana mmoja akijinasibu kwa mkewe kwamba yeye ndio shujaa aliyefyatua njiti ya kibiriti kuunguza nyumba ya Zabroni.

"Huwezi amini mke wangu, karibia wote waliogopa ila mimi nikasema hebu nipeni kibiriti hapa. Wakanikabidhi, nami upesi sikutaka kupepesa macho. Nikakiwasha", aliongeza kujisemea maneno hayo tena kwa mbwembwe zote mbele ya mkewe.

"Mmh lakini wewe jiangalie isije kuwa balaa bwana", alijibu mke wa huyo jamaa. Jamaa akajitutumua halafu akaongeza kusema "Hakuna balaa hapa mke wangu,ila naomba kesho uende kwa shangazi nilisha andaa kila kitu,tutaishi huko utajifungua salama kabisa bila hofu yoyote"

"Anhaa sawa! Na namuomba Mungu nizae mtoto wa kike sitaki wa kiume asije akawa kama hili jitu linalo uwa watu hovyo hivyo", alisema mke wa jamaa huy. Jamaa alicheka kidogo kisha akajibu "Haya bwana,kwahiyo kesho asubuhi mapema anza safari. Mimi nitakuja jioni kwa sababu kuna shamba nitaenda kuliuza ili tupate Fedha za kutumia siku mbili tatu hizi"

"Sawa mume wangu nimekuelewa", walipo kwisha kusema hayo mke na mume walirudi ndani kulala,wasijue kuwa ni kosa kubwa walilofanya hawakujua kwamba Zabroni yote waliyoongea alikuwa akiyasikia. 

Na punde si punde alikatiza eneo hilo huku Moyoni akijisemea "Naam! ukila tambua ipo siku zote na wewe utaliwa.. Ngoja nitakukomesha", kwisha kusema hayo ajabu macho yake yaliwaka kama macho ya simba kisha akapotea ikasalia sauti ya mtoto mchanga akilia ambayo nayo haikudumu ikatoweka. 

Usiku huo hakuchoma nyumba hata moja,waliolala ndani walifurahi sana kusikia jogoo anawika kwani waliamini tayari pamekucha salama. Alfajiri hiyo mapema mke wa yule jamaa aliyekuwa anajinadi kwa mkewe juu ya kuchoma nyumba ya Zabroni, alianza safari pole pole kwenda kijiji jirani kama walivyopanga yeye na mumewe usiku wa jana ikiwa njia ya kuyakimbia maafa yanayo endelea. 

Akiwa njiani kwenye giza totoro lililo jichanganya na ukungu kwa mbaali, mwanamke huyo mwenye ujauzito alizipiga hatua pole pole huku akihofia kukutana njiani na mtukutu Zabroni. Katika ya kijiji hicho ambacho Zabroni anafanya mabalaa na kijiji jirani palikuwa na msitu mkubwa ila sio sana,huo msitu kwa mwendo wa miguu inakubidi utatembea saa moja na dakika kumi na tano kuumaliza msitu huo wenye miti mirefu na mifupi, uoto wa asiri nao ukiunakshi vema. 

Mwanamke huyo alijawa na hofu,alikazana huku kimoyomoyo akimuomba Mungu afike salama. Lakini wakati anatembea,ghafla mbele yake alimuona mtu ni baada kuondoka ungungu ule uliokuwa umetanda,mwanamke huyo alifurahi akakazana zaidi ili kumfikia yule mtu aliyeonekana amebeba kifurushi kidogo mgongoni.

Mtu huyo alionekana mzee wa makamo, ndani ya nafsi yake akaamini kuwa ndio wale wale wanao kikimbia kijiji. Upesi akaongeza mwendo ili wawe sambamba katika safari hiyo isiyokuwa na matumaini. Alipo mfikia alimsalimia kisha akasema "Afadhali hapa naweza kuwa na amani"

"Amani gani tena mwanangu?.. ", alihoji mzee huyo huku wakiendelea kutembea.

"Mmh hujui kama kuna muuwaji anakitikisa kijiji?.." Mzee huyo alikaa kimya kidogo kisha akaongeza kusema "Nasikia hivyo ila sijawahi kumuona katika uso macho yangu, we vipi ukimuona utajua kweli? .."

"Ndio kwanini nisimjue? Yani ni kijana mdogo sana huwezi amini lakini mambo yake ni makubwa mno" alijibu.

"Doh! Ila nasikia analipa kisasi, sasa sijui ni kweli? Na hata hivyo jana nimepata habari kwamba amechomewa nyumba.."

"Ni kweli"
"Mmh waliochoma kweli ningewajua basi ningewapa mzizi wa kumtia hatiani yule kijana maana nasikia anatumia dawa na ndio maana hakamati", alisema mzee huyo,yule mwanamke aliposikia maneno hayo alihamaki kisha akasema "Kweli? Basi nadhani ningekuwa nipo na mume wangu ungempatia ili amkomeshe. Naye jana alishiriki,tena yeye ndio aliyefyatua njiti kuichoma nyumba yake. 

Lakini bahati mbaya nimemuacha kijijini kuna mambo anayeweka sawa" Mzee huyo aliposikia maneno hayo alisimama kisha akasema "Basi mimi ndio mhangwa. Naitwa Zabroni Zabroni ", sauti ilijirudia mara mbili mbili,Ghafla alibadilika akageuka Zabroni mwenyewe mtukutu kutoka kwenye hali ya uzee. Yule mwanamke alistuka akaanza kupiga mayowe akiomba masaada,lakini Zabroni hakujali kelele hizo. 

Macho yake yakabadirika, yakawa kama macho ya nyoka upesi alichomoa kisu kisha akampiga ngumi nzito mwanamke yule, naye hakuteteleka zaidi aliangua chini, akashuka naye akamtumbua tumbo mwanamke huyo mjamzito, akavitoa vijusi mapacha viwili ndani ya tumbo la huyo mwanamke kisha akavitumbua style ya mshikaki,akavining'iniza juu kwenye mti ambao kila mpita njia akipita lazima avione vijusi hivyo,ambavyo ndio kwanza vilikuwa vikikaribia kuwa katika hali ya kuitwa mtoto.. 

Zabroni baada kufanya kitendo hicho cha kutisha akapotea kwa kishindo kikubwa ambacho kilimpelekea nyasi mbichi kukauka!





ITAENDELEA

Powered by Blogger.