KARIBU USOME HADITHI NZURI ZA KUSISIMUA

SIMULIZI: Penzi La Mfungwa sehemu Ya Ishirini (20)

simulizi ya penzi la mfungwa
"Naam! Hicho ndicho nilichokua nataka", alisema yule Askari aliyempatia Zabroni hirizi. Wakati huo sasa tayari wanaume hao walikuwa wameanza kupigana. 

Bluyner alijitahidi kurusha ngumi na mateke kwa kasi ya ajabu ila mtukutu Zabroni aliweza kuyakwepa yote,hata moja halikumpata. Bluyner alishangaa sana,alishusha pumzi kwa kasi kisha akaanza upya lakini bado mambo yalikwenda mlama. 

Hivyo akajikuta anachoka bila kupenyeza ngumi wala teke kwenye mwili wa Zabri. Zabroni baada kuona tayari Bluyner kawa mchovu,kalainika kama mrenda.
"Umechoka, sasa ngoja nikuadabishe mwana hidhaya mkubwa wewe", aliongea kwa hasira Zabroni na ndipo alipoanza kurudisha mapigo,hakutaka kuutumia mkono uliokuwa na hirizi. 

Alitumi mkono mwingine ila pindi Bluyner alipojaribu kujihami kuzuia ngumi zake, ndipo aliutumia huo mkono ambao ulionyesha kuwa na nguvu nyingi kwani ilimpelekea kumtegua mkono Bluyner. 

Mayowe ya maumivu aliyapasa Bluyner huku akiwa ameushika mkono wake ulioteguka,papo hapo riasi mbili tatu zilipigwa angani. Amri ikatolewa wafungwa wote wapande magari warudi Gerezani,kupitia nafasi hiyo Zabroni alitoweka akipitia kwenye msitu mdogo uliokuwepo jirani na maeneo hayo. 

Askari walipomuona akikimbia walimpiga risasi kama njugu lakini bahati mbaya hazikufanikiwa kumkuta,na hivyo Zabroni akawa ametoroka jela kupitia mazingira hayo ya kutatanisha yakisababishwa na hao Askari waliopewa jukumu la kuwalinda na kuwasimamia kwani uzembe walioufanya ni kuruhusu wafungwa wapigane.

Siku zote wahenga wanasema kwamba ng'ombe wa masikini hazai, akizaa basi huzaa dume. Ndivyo msemo huo ulipojizihirisha kwa Afande Veronica, kwani wakati Zabroni anatoroka jela,kwingineko Veronica nae alikuwa akimalizia hatua ya mwisho ya uhamisho wakuhamia kikazi ndani ya jiji la Dar es salaam asijue kwamba tayari yule mtu aliyemtia hatiani kwa kumdanganya na penzi la uongo hayupo tena jela,yupo huru ingawa haijafahamika wapi ataibukia lakini pia haijulikana style gani atakayo kuja mtaani.


Upande mwingine,taarifa ya kutoroka kwa mfungwa Zabroni, hatimaye ilimfikia mkuu wa gereza. Mkuu huyo alichanganyikiwa baada kupata hiyo taarifa,aliwaita wasaidizi wake kisha akawatangazia dau nono kwa yoyote atakae mkamata ama kufahamu mahali alipo huyo mtu mtukutuku Zabroni. Na moja ya Askari waliopewa dili hilo alikuwemo Afande Jimmy,ilihari huku mtaani nako Zabroni aliamuwa kujikita katika kazi ya kuzoa takataka akiwa na dhumuni la kutafuta nauli ili arudi kijijini kwao akalipe kisasi kwa Veronica pia na Bruno kisha akafungwe kihalari.

Zabroni ilibidi ajichakaze sehemu mbali mbali za mwili wake wakati huku akiwa katika mavazi yaliyoraruka raruka kila sehemu kiasi kwamba ilikuwa vigumu kumtambua,baada kuwa katika hali hiyo alianza kazi yake ya kuzoa takataka,moyoni akiamini kwamba iwe isiwe lazima atakuwa anatafutwa. Kwahiyo kazi hiyo aliamini pia itamfanya awe katika mazingira salama pasipo kusumbuliwa.


Siku moja Zabroni akiwa amechoka mchana jua kali maeneo ya Kinondoni, kando ya barabara alijalaza huku akitazama magari jinsi yanavyopisha kwa kasi na kusimama kusubiri taa ya kijani iwake. 

Mara ghafla mbele yake ikasimama gari ndogo aina ya RAV4,gari hiyo iliegesha pembeni kisha akatelemka Binti mrembo sana. Binti huyo alizipiga hatua mpaka mahali alipo simama mwanamke mmoja hivi wa makamo ambapo wawili hao walisalimiana huku wa kicheka, walionekana ni watu ambao hawajaonama muda mrefu sana. 

Walifurahi sana wakati huo huo Zabroni pale alipokuwa kajilaza alinyanyuka baada kuona kama binti huyo amemfananisha. Hivyo alistuka sana aliamua kusimama ili ajilizishe kama yule anayemfahamu au la!
___________

Zabroni alizidi kumsogelea yule binti ambaye kwa upande wake alikuwa amemfananisha lakini kabla hajamkaribia, binti yule aliambaa kuzipiga hatua kurudi kwenye gari lake. Hivyo Zabroni akawa hajamfahamu vizuri ila alistuka kusikia yule mama aliyekuwa akisalimia na yule binti akisema "Naona mambo sio mabaya Veronica,umerudi mjini sasa utazidi kunenepa", alisema hivyo mama huyo huku akicheka, yule binti aliyetajwa kwa jina Veronica aliposikia maneno hayo aligeuka ili amjibu. 

Alipo geuka alijibu akianza kwa kicheko "Ndio maana yake mama Lina", kumbe wakati Veronica anamjibu mama huyo mama ambaye alimfahamu kwa kujina la binti yake atwae Lina,Zabroni akapata kumuona usoni baada hapo awali kumpa mgongo. "Alaah! Kumbe upo huku kwa sasa! Sawa sawa popote ulipo nitakupinda tu",alijisema Zabroni baada kugundua kuwa yule binti aliyekuwa akimfananisha ndio mwenyewe Veronica. 

Tayari ile ahadi aliyoahidiwa Veronica pindi atakapo mkamata Zabroni ilitimia uhamisho wa ulikuwa umeshakamilrika,na siku hiyo alikuwa yupo katika matembezi yake kabla hajaanza kazi. Kupitia dili lile la kumkamatisha mtukutu Zabroni alipata pesa nyingi mno, alinunua gari lake pia alinunua nyumba maeneo ya Masaki jijini Dar es salaam. Maisha ya kamanda Veronica yakawa mazuri sana kwani akaunti yake benki nayo ilisheheni pesa ya kutosha,alikula na kuvaa atakavyo mwenyewe.

Veronica alipanda kwenye gari kisha akaondoka zake,huku nyuma Zabroni akibaki kumsindikiza kwa macho na mwishowe akatikisa kichwa ishara ya kukubali jambo fulani ilihari tabasamu bashasha nalo likitawala kinywani mwake mithiri ya Simba aliyemuona Swala. Kitendo hicho cha Zabroni kumkodolea macho Veronica mpaka anaondoka mahali hapo kilimshangaza mama Lina,mama yule aliyekuwa akiongea na Veronica. 

Kwa mashaka akAmuuliza Zabroni "Kulikoni mbona unamtazama sana yule dada,unamfahamu?..",Zabroni aliposikia sauti hiyi,aligeuka akaacha kutazama kule barabarani akamtazama mama Lina aliyemsemesha. Alicheka kidogo kisha akajibu huku aking'am ng'am usoni mwake "Ndio namfahamu,yule si Veronica? .."


"Ndio yeye,kwa sasa ni polisi. Amehamishwa sijui kutoka sehemu gani huko ila kwa sasa yupo hapahapa mjini" ,aliongeza mama Lina. Zabroni aliposikia maneno hayo aliachia tabasamu bashasha kisha akajibu "Alaah! Jambo nzuri sana,unajua yule binti nimesoma naye kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari. 

Lakini mwenzangu akaendelea,mimi nikaishia njiani yote ikiwa changamoto ya maisha. Na sasa nazoa takataka." ,akacheka kidogo akakaa kimya.

"Ni kweli,ila siku zote soma upate kuelimika na sio kupata kazi. Kupata kazi ni tokeo sio tegemezi,wapo watu wamesoma sana lakini hawajapata kazi. Tusiende mbali, mimi nina mwanangu anaitwa Lina. Mwanangu kasoma mpaka chuo kikuu kamaliza lakini hana kazi"

"Umeona sasa? Ndio maana mimi nimeamua kujiajiri ila asikate tamaa. Acha nipambane na kazi yangu ya kuzoa takataka." kwisha kusema hayo Zabroni akaangua kicheko kwa mara nyingine tena kisha akaondoka zake.


Upande wa pili ndani ya Sophie Hotel alionekana Karani akiwa ameketi meza moja na Mr Rasi ama waweza kumuita Bruno,walikuwa wameketi huku mbele yao pakiwa na meza iliyosheheni vinywaji vya aina mbali mbali. Karani alikunywa bunda moja ya bia,akahoa kidogo kisha akasema "Kijana,kwanza nashukuru sana kwa kutii ombi langu la kukubali kuketi mahali hapa mimi na wewe"

"Aah asante sana mzee, heshima yako",alijibu Mr Rasi. Karani akaendelea kusema. "Nadhani bado hujafahamu fika nia na madhumuni ya kukuita mahali hapa,lakini ukweli ni kwamba nimevutiwa na uwezo wako wa kupigana. Hivyo basi kama hutojali naomba uwe moja ya wapiganaji wangu ili upige pesa,na kila pambano ukishinda utapata kiasi cha pesa milioni mia mbili", Karan alisema kisha akanywa maji yaliyokuwa kwenye grasi kuchamba koo. 

Mr Rasi kijana Bruno anayesakwa na serikali kila mahali kama shilingi,aliona katu hilo dili hawezi kuliacha kizembe. Upesi alikubali. "Sawa nipo tayari ila kabla sijasaini nataka kujua vipi serikali inaifahamu namna gani hii biashara", aliongea Mr Rasi. Karan akaangua kicheko cha madaha kisha akajibu "Kijana shaka ondoa kabisa, hii biashara inapesa ndefu sana. 

Kwa maana hiyo basi tunashirikiana vema na baadhi ya viongozi wa nyanda za juu, hawa nao ni warafi wa fedha tu. Chama chetu kila mwisho wa mwaka tunakutana na kuchangishana kisha fedha tunawapa hawa warafi ambapo nao kimya kimya wanatufanya tunazidi kuvuna pesa mjini ", Karan akamaliza kwa kicheko.

" Kwahiyo hofu ondoa kabisa ", akaongeza kusema Karan.
" Sawa hakuna shida, leta mkataba nisaini ", aliongea Mr Rasi. Haraka sana ililetwa kalamu na makaratasi yaliyojiorodhesha kanuni na taratibu ya mkataba husika,Mr Rasi akamwaga wino wakati huo akiwa hajui kama adui yake kwa sasa yupo huru.

Baada hilo zoezi kukamilika Mr Rasi aliambiwa aondoke nyumbani akajiandae kwa niaba ya kuhamia kwenye makazi mapya huku akiahidiwa kununuliwa gari pindi atakapo shinda mpambano wa kwanza waliomuandalia. Nje ya hiyo Hotel alionekana Tina akiwa amemngojea Mr Rasi,Tina na Mr Rasi tayari walikuwa katika mahusiano baridi kwani tangu siku ile Mr Rasi amsaidie kumpokonya yule kibaka aliyemuibia mkoba,Tina akawa ametokea kumpenda. 

Na hata siku ya pili Tina alipomuona Mr Rasi akipigana na wale vijana saba moyo wake ukatotokea kumpenda zaidi. 

Si yeye tu bali hata shangazi yake naye alimkubali Mr Rasi kwani siku hiyo naye alikuwepo,hivyo kupitia hayo matukio mawili tofauti Tina na shangazi yake wakaweka ukaribu zaidi huku shangazi mtu akimshawishi Tina kuweka ukaribu zaidi na kijana huyo ambaye alionekana shupavu na mkakamavu. Si mwingine ni Bruno ama Mr Rasi.


Kipindi wawili hao Mr Rasi na Tina walipokuwa wameweka ukaribu wao, yeye Mr Rasi hakuwa na sehemu maalumu ya kulala. 

Shida hiyo Tina aliifikisha kwa shangazi yake,shangazi yake alisikitika sana akamtaka Mr Rasi aishi nyumbani kwake. Mr Rasi hakulipinga hilo suala ingawa umakini bado aliuzatiti ili asigundulike. Hivyo siku hiyo baada kutia saini ilikuwa siku ya furaha sana kwake ingawa ilikuwa siku ya huzuni kwa watoto wa shangazi yake Tina pia akuwemo na shangazi mtu lakini vile vile kwa Tina kwa maana ilimbidi Mr Rasi ahame hapo nyumbani akaishi kwenye nyumba mpya aliyopewa. Walimzoea.


Siku zilisogea,ila bado uhusiano kati ya Bruno na Tina ukizidi kudumu. Kiasi kwamba Tina alimsahau kabisa Zabroni, hasa akikumbuka mambo aliyokuwa akiyafanya,moyo wala macho yake hayatamani abadani kumuona. 

Akaona kujiweka kwa Bruno Mr Rasi, ndio sehemu salama pakuweza kutuliza moyo wake asijue kwamba Mr Rasi na Zabroni ni maadui kama maji na moto.
Hatimaye siku ya pambano la Mr Rasi iliwadia, matajiri walishindana kutaja dau huku kando kando watazamaji wakishangilia. 

Siku zote Karan aliaminika kutokuwa na wapambanaji wazuri kwahiyo kupita imani hiyo,yule tajari mwenzake alikuwa akitaja dau nono akijua kabisa Karani hana watu wa kupigana na watu wake.
"Milion arobaini na tano" alitaja dau Karani,mwenzake akajibu
"Milioni stini"
"Milioni stini na tano"
"Milion sabini na tano"
Million themanini"
"Milioni tisini"
"Milioni tisini na tano"
"Million miamoja"
"Mr acha vijana wathibitishe kile tulicho kinadi hapa kwenye kadamnasi ya watu",alifunga mjadala Karani kisha akakuja namba nne kwenye kiti alichokalia huku akiiweka sawa miwani aliyovaa. 

Mpinzani wa Mr Rasi ndio alikuwa wa kwanza kuingia ulingoni,shangwe zililipuka za kumshangilia huyo jamaa aliyeonekana kuwa na mwili wa mazoezi. Kwa madaha jamaa huyo alizungusha shingo yake aliipeleka kulia na kushoto kitendo kilicho pelekea watu kuzidi kupiga mayowe ilihari upande wa pili alionekana Mr Rasi naye akiingia ulingoni.

 Mr Rasi alitambua fika kuwa anafatiliwa sana,kwahiyo ili asiumbuke mahali hapo alizilaza rasta zake mbele na nyuma pia pembeni. Kufanya hivyo ni vigumu sana kumtambua. Kama ilivyo ada,nderemo na vifijo vilisikika wakimshangilia Mr Rasi. Mpambanaji mpya kabisa mbele ya watazamaji. 

Yule tajiri aliyekuwa akitaja dau nono mara mbili ya Karani,alistuka kumuona Rasi. Akavua miwani yake ili apate kumuona, alitaharuki ikiwa wakati huo huo alionekana Zabroni akajongea sehemu hiyo kutazama pambano huku akiwa katika mavazi yake ya kuzolea takataka. Naye pia alijiweka katika hiyo hali ili kukwepa mkono wa dola,kwani tangu atoroke jela uliundwa mkakati wa kumsaka mahala popote pale alipo. 

Hivyo kujiweka namna hiyo kulimfanya asigundulike,angeliweza kujiweka kivyovyote vile lakini aliamua kuwa mzoa takataka ili apate nauli ya kurudi kijijini akalipe kisasi kwa Afande Veronica pamoja na Bruno ambaye ni Mr Rasi.

 Lakini baadaye akaja kugundua kuwa tayari Veronica yupo ndani ya jiji,ila hakuweza kuacha kusaka pesa kwa niaba ya nauli kupitia hiyo kazi kwa sababu alijua kuwa huko kijijini bado kuna adui yake mmoja ambaye ni Mr Rasi na hata asijue kwamba hata Mr Rasi naye yupo jijini kama ilivyo Veronica, zaidi mahali hapo alipokuwa akijongea ndipo yupo huyo Bruno ama Mr Rasi.


Wakati kijana Zabroni anasogea eneo hilo kutazama ndondi za Mr Rasi,upande wa pili nako eneo hilo hilo ilikuja gari ndogo aina ya Hilux. Gari hiyo ilipaki kando kidogo ya uma wa watu waliokuwa wakishuhudia mpambano,kisha akatoka ndani binti mrembo ambaye si mwingine ni Tina. 

Tina alikuja mahali hapo kutazama jinsi mpenzi wake anavyopigana,watu baadhi walipomuona Tina walimkodolea macho. Kwani Tina alikuwa amependeza sana sana siku hiyo,kiasi kwamba aliweza kumvutia kila mtu. K

ipindi Tina anafika hapo Mr Rasi alikuwa anachezea ngumi za kila sehemu ya mwili wake kana kwamba jamaa aliyekuwa akipigana nae alionekana kumzidi ubavu,lakini baada Mr Rasi kusikia sauti ya Tina ikisema "Rasi,sijapenda mimi" ,Hapo mr Rasi alijihisi kupata nguvu mara mbili ya awali. 

Alipigana ipasavyo mpaka akaibuka mshindi,ikawa furaha isiyo kifani kwa Karani lakini pia kwa mrembo Tina baada kuona yeye kuwa moja ya chachu ya ushindi.


Makubaliano sehemu ya kukutana yalifanyika baina ya matajiri hao,Karani na na mwenzake. Ilihari kwingineko upande ule aliosimama Zabroni alijikuta akivuta kumbukumbu siku za nyuma kipindi alipokuwa akipigana na Bruno,aliona mapigo aliyoyaona hapo ulingoni kutoka kwa Mr Rasi na yale ya Bruno yalifanana fika. 

Jambo hilo kidogo lilimtatiza Zabroni,lakini yote kwa yote hakutaka kutilia maanani na hivyo aliamuwa kuondoka zake kwani tayari mpambano ulikuwa umeshamalizika. 

Zabroni alizipiga hatua kutoka mahali hapo akazunguka upande ule ziliposimama gari za matajiri pia na gari aliyokuja nayo Tina,kabla hajazikaribia hizo gari alimuona binti aliyefanana na Tina akifunguliwa mlango na Mr Rasi. 

Zabroni alistuka,kwa sauti kuu akasema "Tinaaaaa",Tina aliposikia sauti hiyo aligeuka kutazama kule ilipotokea,hakujua mtu aliyemuita kwa maana watu walikuwa wengi sehemu hiyo. Zabroni baada kuona Tina hajamuona alinyoosha mikono,hapo Tina akawa amemuona. Haraka sana Zabroni alizipiga hatua kumsogelea. Alipo mfikia alimsalimia lakini Tina hakumjibu salamu yake,alishangaa sana Zabroni. 

Kwa taharuki akasema "Ni mimi mpenzi wako uliyeniacha kijijini", akacheka kidogo kisha akaendelea kusema "Tina inaama umenisahau? Au kwa sababu nimechafuka hivi ndio maana umeshindwa kunitambua? Amini Tina kwa sasa nipo mjini,niliamua kuachana na yale mambo niliyokuwa nikiyafanya. 

Ndio maana sikuhizi nimejikita kwenye kazi hii niliamua kukimbia kijijini baada kuona naogopwa sana",alisema Zabroni huku akiwa na tabasamu bashasha,wakati huo Tina alikuwa kimya akimsikiliza huku machozi yakimtoka. Aliyafuta kisha akamjibu "Sawa,yote tisa. Kumi. Mimi sio mpenzi wako tena. Nimepata mwingine anayejua nini maana ya mapenzi,na sio wewe mwanaume katili usiyekuwa na hata chembe ya huruma.

 Wako wapi wazazi wangu? Wewe ndio muhusika wa vifo vyao. Je, unadhani kwa jereha hili unaweza kuniponya? Hebu achana na mimi bwana." aliongea Tina huku machozi yakimtoka. Muda huo huo Mr Rasi alitoka ndani ya gari akazunguka ule upande aliosimama Tina akiwa anaongea na Zabroni. 

Alipofika alitaharuki kisha akamuuliza Tina "Tina,kulikoni kwani kuna nini?..",Tina hakujibu aliishia kumtazama Zabroni kwa hasira kali. Ukweli ni kwamba hata Mr Rasi hakuweza kumtambua Zabroni kwani wakati Rasi anamuuliza Tina swali hilo,Zabroni yeye aliinamisha uso wake. Ni kitendo ambacho kilimuwe ngumu Mr Rasi kumjua yule mtu anayezungumza na Tina.


"Hapana mpenzi hakuna kitu ila..",kabla Tina hajamalizia jibu lake, mara ghafla Mr Rasi alimkatisha kwa kusema "Ila nini? Unajua tunasubiliwa sisi? Wenzangu wote wapo tayari,sasa naona wewe umesimama nje muda mrefu tu hata unachokifanya hekieleweki", alifoka Mr Rasi kwa hasira. 

Tina alijua kuwa mpenzi wake kakasirika,hivyo alimsogelea kisha akamkumbatia mbele ya Zabroni halafu akasema "Tazama we mwenda wazimu, Tina sio mali yako tena. Huyu ndio mpenzi wangu kwa sasa,kwahiyo itapendeza kama utaniita shemeji popote pale utakapo niona. 

Lakini tofauti na hivyo utahatarisha maisha yako mwanahidhaya mkubwa wewe ", aliongeza kusema hivyo Tina kisha akaingia ndani ya gari,gari likawashwa wakaondoka zao huku nyuma wakimuacha Zabroni asiamini kile kilicho tokea. Moyoni akawa anajiuliza "Hivi ni kweli au ni fikra zangu tu?.." wakati Zabroni akiwa katika hali hiyo ya kutoamini kile alichokiona,upande mwingine nako ndani ya gari Mr Rasi akiwa na Tina walikuwa wakipiga zogo huku Tina akimsifu mpenzi wake kwa kuibuka kidedea. 

Lakini baada ya sifa hizo,Mr Rasi alimuuliza Tina juu ya mtu yule aliyekuwa akiongea naye "Tina kwani yule nani uliyekuwa ukiongea naye?" ,Tina mara baada kuulizwa swali hilo alikaa kimya ila baadaye kidogo alijibu "Nadhani unakumbuka sikuile nilipokwambia kuhusu matendo machafu aliyokuwa akiyafanya mpenzi wangu wa kwanza"

"Nani yule aliyekuwa anachoma nyumba hovyo? ..",alirudia kuhoji Mr Rasi huku akionekana kustuka. Tina akajibu "Huyo huyo,anaitwa Zabroni. Ndio nilikuwa naongea naye,hivyo ilikudhihilisha kwamba simtaki tena nikaamua kukutambulisha kwake kwamba wewe ndio mpenzi wangu. 

Ukweli Rasi,namchukia sana yule mwanaume kwani nafahamu yeye ndiye aliyewaua wazazi wangu. Sitaki na sitotaka kumuona tena mbele yangu" Tina alilia, wakati huo huo Mr Rasi alikanyaga breki kwa nguvu kiasi kwamba matairi ya gari yalitoa harufu. 

Papo hapo aligeuza gari kurudi kule alipotoka huku moyoni akijisemea "Huyu ndio niliyekuwa namsaka kwa muda mrefu,ngoja nikamalizane naye mapema kabla hajatoweka ndani ya hili jiji",alijisemea hivyo Mr Rasi ilihari muda huo Tina alikuwa ameshanyamanza amebaki sasa kushangaa namna Mr Rasi anavyo endesha gari kwa fujo kumfuata Zabroni. 

Kwani naye alitoka rumande ili amuue Zabroni kama njia ya kulipiza kisasi,ilihali Zabroni naye vile vile alitoroka jela ili amuue Mr Rasi ikiwa kama njia ya kulipiza kisasi.

INAENDELEA

Powered by Blogger.